Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

Niliona unanyemelea Katheu wewe mzee dotcom . Niskize Mbiti

20,873 views • 2 months ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

Baba kwa unyenyekevu mkubwa niseme nimesikitika kukusikiliza. Kwanza sikuamini kama ni wewe, maana hatujakuzoea hivi. Kwa miaka yote tangu ukiwa Mkuu wa Kanisa, umekua mtu imara, unayesimamia haki na usiyejihusisha na ushabiki wa kisiasa. Ulisimamia Kanisa vema na kutetea haki za watu katika nyakati ngumu za utawala wa awamu ya 5. Ni kweli awamu ya 6 ilianza vizuri tukashuhudia wafungwa wa kisiasa wakiachiwa huru, viongozi waliokimbia nchi wakikaribishwa kurudi, na mikutano ya kisiasa ikiruhusiwa. Kwahiyo ulikua na haki ya kumsifu Samia mwanzoni mwa utawala wake. Hata sisi tulisema mama anaupiga mwingi. Mimi ndiye mwasisi wa kauli hiyo. Lakini kwa sasa mambo yameharibika baba. Kuna matukio mengi yanayotishia haki na uhuru wa watu. Watu wanaripotiwa kutekwa na kupotea. Kipindi cha Magufuli ulisimama na kulaani vitendo hivyo, lakini kwa sasa hatujakusikia. Naomba nikukumbushe jirani yako hapo Kibosho Kindi, Deus Soka anadaiwa kutekwa pamoja marafiki zake wawili (Mbise na Mlay) maeneo ya Yombo Buza. Zaidi ya siku 70 sasa hawajulikani kama wapo hai au wameuawa. Hatujasikia ukikemea kama ulivyokemea awamu iliyopita. Lakini Deus na wenzake ni tone dogo la maji katika bahari iliyochafuka. TLS walitoa orodha ya watu 82 waliodaiwa kutekwa kwa mwaka huu. Yani kuanzia January hadi leo kuna roho 82 za watanzania wenzetu ziko mateka. Hivi hili halijakushtua Baba Askofu? Mbona hukulisemea? Yani watu 82 wanapotea kama kuku na Kanisa lipo kimya? Anyway tuseme hiyo list ya TLS hukuisikia. Je hata la mzee Kibao kushushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili hukusikia pia? Mbona hukukemea hata hilo? Halafu leo unasimama kupigia debe serikali hii iliyoshindwa kutuambia roho za watanzania wenzetu 82 zilipo? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata wauaji wa mzee Kibao, wakati walimchukua mchana kweupe? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata waliomteka Sativa. Baba kwa unyenyekevu nikuambie ukweli ambao wengi wataogopa kukuambia. Umetukosea watanzania, na umelikosea Kanisa. Kauli hizi zilipaswa kutolewa Katibu mwenezi wa CCM sio wewe. Umejenga heshima kubwa kwa miaka mingi. Kosa hili dogo linaweza kuharibu mengi mazuri uliyofanya nyuma. Jikosoe, Jirudi, Jisahihishe.!

MalisaGJ

56,688 views • 1 year ago