Video wird geladen...

Video konnte nicht geladen werden

Zur Startseite

13,879 Aufrufe • vor 13 Tagen •via X (Twitter)

0 Kommentare

Keine Kommentare verfügbar

Kommentare vom Original-Post werden hier angezeigt

Ähnliche Videos

Mchungaji Peter Saimon Msigwa aliyeambatana na Katibu wa Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi kwenye ziara ya kikazi Mkoani Lindi, amebainisha kuwa Chadema imepoteza mwelekeo wa kisiasa na kushindwa kuwa na hoja zenye kugusa maisha ya wananchi, Akisisitiza umuhimu wa kujivunia serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na namna ambavyo imefanikiwa kushughulika na changamoto za wananchi sambamba na kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali. "Nilikuwa kiongozi wa mikoa mitano ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na ninaamini ukitaka kujua habari za maji kati ya Sungura na mamba, Mamba ndiye atakusimulia habari za kwenye maji. Chama kile kimepoteza mwelekeo ni chama ambacho kipo kama chombo kilichopoteza mwelekeo angani na hakijui kinapoenda kutua ni wapi kwahiyo tusipoteze muda kung'ang'ania safari ya fisi kufuata mkono wa binadamu kisa tu unaning'inia kwamba utadondoka wakati hautadondoka." Amesema Mch. Msigwa. "Ndugu zangu wakija hapa wanasema serikali ya CCM haijafanya kitu, ni kwasababu ni vipofu tu kama nlivyokuwa mimi kabla ya kushushiwa nuru kwahiyo na wale nao wanahitaji nuru. Mimi nimekuja kwenu kama rafiki yenu, kama Mamba niliyetoka kwenye maji, vyama vile vimepoteza mwelekeo, vimepoteza touch, vimepoteza energy, wanaruka ruka kushoto na kulia hawajui waende wapi na ndio maana wakija kwenu hawazungumzi changamoto zenu wanazungumza namna ya kuingia madarakani tu." Mch. Msigwa akizungumzia hatua za maendeleo zilizopigwa kwenye miaka miaka minne ya Rais Samia na namna ambavyo zimekuwa chachu ya ustawi wa Wananchi, ameelez kuwa ujenzi wa shule kwenye maeneo mbalimbali nchi zimesaidia kuondoa ujinga, maboresho kwenye mifumo ya matibabu imesaidia kuwa na jamii yenye afya bora, huku miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege na uzalishaji wa umeme kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere vikisaidia katika kusisimua shughuli za uzalishaji na hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na la Taifa kwa ujumla.

Jambo TV

17,800 Aufrufe • vor 1 Jahr