正在加载视频...

视频加载失败

NOAH SADIKI, FROM DR CONGO

83,123 次观看 • 8 个月前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

Documentary ya "Congo, Thrill of the River", raia wa DR Congo wakisafiri kutoka Kisangani kwenda Kinsasha katika Mto Congo kwa kutumia usafiri uliotengenezwa kwa kutumia magogo 220. Vita, ukoloni, utumwa, ufisadi yamebadilisha taifa hili ambalo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi duniani, sasa limekuwa masikini zaidi. DR Congo imebarikiwa kila aina ya madini. DR Congo nchi tajiri zaidi duniani kwa maliasili, rasilimali na malighafi. Madini mengi ghafi hayajatumika yenye thamani ya hadi takriban $24 trilioni. Huu ni uchumi wa USA na Ulaya kwa pamoja. Kuna aina zaidi ya aina 1,100 za madini katika ardhi ya nchi ya DR Congo. Amana hizi ni pamoja na akiba kubwa zaidi ya madini ya coltan na kiasi kikubwa cha madini ya kobalti ardhini. 80% ya ardhi ya DR Congo inafaa kwa kilimo. DR Congo ina eneo sawa na Ulaya Magharibi. Ulaya Magharibi ni England, France, Germany, Italy, Netherlands, Spain, Portugal, Belgium, Austria.. etc. DR Congo ina hazina ya 10% ya hifadhi ya shaba Duniani. 30% ya cobalt ya Dunia. DR Congo inazalisha 80% ya madini ya coltan yanayotumika kutengeneza simu, ipods, sumaku, Jet engine. DR Congo inazalisha madini ya Uranium. Vita ya pili ya Dunia, Marekani alipiga miji miwili ya Japan (Hiroshima na Nagasaki) kwa mabomu ya atomic. Mabomu yalitengenezwa na madini ya Uranium. DR Congo inamiliki ardhi ambayo inatoa madini ya almasi, dhahabu, bauxite, graphite, fedha, zinki. Pia wanayo madini ya lead ambayo yanatumika kutengeneza risasi na mabomu. DR Congo ina ardhi yenye mafuta. Kuna misitu yenye miti mikubwa. Wanyama, vivutio vya watalii katika milima ya Virunga na Ituri. Mito na mabonde yenye unyevu na rutuba. Maziwa na bahari. Mto Congo ni mto wa pili kwa ukubwa Duniani. Ndani ya mto Congo kuna maporomoko (Inga Water Falls) ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa kusambazwa Afrika na Ulaya kwa wakati mmoja.. DR Congo yenye raia 75 milioni, 80% ya raia, sawa na 60 milioni wanaishi chini ya kipato cha dola moja (Sh2,500). Wananchi ni maskini. Serikali imeshindwa kutengeneza miundombinu. Wageni kutoka nje ya DR Congo wamevamia ardhi na kuifanya uwanja wa mapigano na mavuno ya rasilimali za watu wa Congo. Watu wa DR Congo wamebaki kuwa maskini wa kutupwa. Wageni wamesababisha machafuko, wamevuruga utaratibu wote wa uchumi, wameiba mali nyingi za nchi ya DR Congo. Wananchi wa DR Congo wamekimbia makazi yao sasa ni wakimbizi. Machafuko yanaifanya DR Congo kuwa nchi tajiri kwa rasilimali Duniani lakini taifa maskini zaidi Afrika wakati mataifa ya magharibi yakiendelea kunufaika na vita ndani ya DR Congo. Raia maskini. Wanaosababisha vita DR Congo ni mabeberu wanaoleta silaha za kivita na misaada ya kijeshi wao wanachimba madini. Tuwaambie Acheni kupora mali ya DRC! Ondoeni mikono yenu DRC! Link ya Documentary yote 👉🏾

Martin Maranja Masese

41,003 次观看 • 1 年前