正在加载视频...

视频加载失败

Pambaneni Mpate katiba Mpya

12,467 次观看 • 9 天前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

VIDEO: Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza amedai kuwa kuna tafsiri mbili zinazopingana za hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyoitoa hivi karibuni ya kuwataka Watanzania wapambane kupata katiba mpya. Amesema tafsiri ya kwanza ni ya baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaompinga Nchimbi wakidai kuwa anajitafutia sifa, na pili ni wale wanaona kauli hiyo kama himizo la heri la kuongeza juhudi za kupata katiba hiyo. Akizungumza na televisheni mtandao ya Pekuzi, Bagonza anaona upinzani dhidi ya Dkt. Nchimbi ndani ya CCM unaonesha kuwa hakuna nia ya dhati ya kuleta katiba mpya. Aidha Bagonza ameendelea kuhoji mantiki ya kuambiwa ‘pambaneni’ ikiwa Rais anaitaka katiba na ilani ya CCM imeshaahidi jambo hilo akisema kuwa ikiwa itabidi kupambana, basi watu watapambana na CCM yenyewe ambayo baadhi ya watu wake wanatafsiriwa kuzuia mchakato huo. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Julai 24, 2025 jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi aliwataka watanzania kuongeza juhudi kupambania katiba mpya wakati huu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya kuitaka katiba hiyo mpya. "Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", alisema Dkt. Nchimbi. Aidha, Dkt. Nchimbi alieleza kwamba, kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Kamati ya kuandika ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) 2025, Tume ya Haki Jinai aliyounda Rais Samia pamoja na ripoti ya Tume ya uchunguzi ya Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi (2025), moja ya mambo wananchi wanayataka ni Katiba Mpya huku ikipendekezwa kupatikana kufikia mwaka 2028 ili itumike mwaka 2029.

Jambo TV

26,168 次观看 • 1 个月前