Video wird geladen...

Video konnte nicht geladen werden

Zur Startseite

'Prophetess' wa huko Kanisa ya Kanyari...

218,088 Aufrufe • vor 1 Monat •via X (Twitter)

0 Kommentare

Keine Kommentare verfügbar

Kommentare vom Original-Post werden hier angezeigt

Ähnliche Videos

Muumini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, Mwalimu Ludovick Joseph, amesisitiza kuwa Kanisa hilo halikuitwa kuwa mshirika wa chama chochote cha kisiasa, wala msemaji wa serikali huku abainisha kuwa Kanisa limepewa wito wa kuokoa watu, kuhubiri Injili na kutangaza habari ya wokovu, na si kushirikiana na vyama vya siasa au mamlaka za kidunia. Akielezea msimamo wa Kanisa, Mwalimu Ludovick amekumbusha mafundisho ya Yesu Kristo katika Injili ya Yohana 18:36 inayosema “Ufalme wangu si wa dunia hii.” Akifafanua zaidi amesema, kauli hiyo inathibitisha haja ya Kanisa kutenganishwa na masuala ya kisiasa ya kidunia na kushikilia wito wake wa kiroho. Mwalimu Ludovick ameonya kuwa kujiingiza kwa Kanisa katika siasa za vyama kunapelekea mgawanyiko miongoni mwa waumini, kupoteza mamlaka ya kimaadili ya Kanisa na kuhatarisha umoja wa waumini, Kanisa lenyewe na Taifa. Amesisitiza kuwa viongozi wa Kanisa wanapaswa kuepuka kutumia lugha zinazofanana na za vyama vya siasa (political rhetoric) ili kudumisha heshima na uadilifu wa Kanisa. Aidha, amebainisha kuwa mamlaka ya kiroho inapaswa kutumika kama huduma, si utawala. Kanisa linapaswa kusimama katika ukweli na misingi ya maadili, huku waumini wakiendeleza wito wake wa kiroho bila kuathiriwa na mitazamo ya kisiasa. Vilevile Mwalimu Ludovick amehimiza waumini kulinda heshima, haki na umoja wa Kanisa, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila muumini kulinda wito wa kiinjilishaji na kuhakikisha Kanisa linaendelea kuwa sauti ya dhamiri ya jamii.

ROYAL TELEVISION

12,901 Aufrufe • vor 5 Monaten