Загрузка видео...

Не удалось загрузить видео

На главную

Sedapnyeee ommm

20,041 просмотров • 1 год назад •via X (Twitter)

Комментарии: 0

Нет доступных комментариев

Здесь появятся комментарии из оригинального поста

Похожие видео

VIDEO: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa na nia ya kuleta vita nchini. Akizungumza na Wananchi wa Dodoma leo Desemba 11, 2025, Waziri Mkuu amesema mijadala ya watu hao baada ya tarehe 9 Desemba ilionyesha wazi malengo yao ya kufanikisha ajenda zisizo salama, jambo ambalo linahofiwa kuathiri amani ya taifa. Amesema kuwa baadhi ya watu hao walikuwa na mambo yao yaliyofichika na walijaribu kutumia vikwazo mbalimbali kama kisingizio cha kufanikisha mpango wao. “Wana mambo yao mengine yaliyojificha, mkitaka kujua wana mambo yao, sikilizeni mijadala yao baada ya jana, hawakuwa wanaongelea maandamano, walikuwa wanasema hii ni vita, tupo vitani tuendelee na vita, hawa ni watu wanataka kutuletea vita nchini kwetu, na hili si jambo geni, hivi ndivyo wanavyofanyaga kwenye nchi zinazopata rasilimali. Fuatilieni nchi za Afrika zenye rasilimali zilizopigana wenyewe kwa wenyewe walianzaje, ni hivi hivi,” alieleza. Akiendelea, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania kudumisha amani ya nchi, akibainisha kuwa amekuwa akifuatilia kwa karibu mienendo ya watu wenye ajenda zisizo salama. “Wale wanaoelekeza vitu vingine vingine, hawatupeleki mahali pazuri, mimi nimefuatilia sana, na nimekuwa nikiwaambia kila eneo ninakopita, ninaujua mpango wao wote, hivi vingine vyote hivi walikuwa wanatafuta kisingizio cha kupitisha ajenda yao,” alisema Dkt. Mwigulu Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza Wananchi kwa kuchagua amani katika siku ya Desemba 9, akisema: “Juzi tarehe 9, kulikuwepo na vimaneno maneno vingi sana kwenye mitandao, ninyi Watanzania mkachagua amani, hongereni sana. Niliona baadhi ya watu wakinitumia meseji za kupongeza serikali, mimi niwaambieni, Mheshimiwa Rais anasema hizi pongezi ni za Watanzania wote hongereni sana. Mmechagua amani, mmechagua kuilinda nchi yenu, mmechagua kuhakikisha nchi yenyu iko na amani na iko salama, hongereni sana.”

Jambo TV

37,703 просмотров • 10 месяцев назад