正在加载视频...

视频加载失败

58,686 次观看 • 8 个月前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

UTANI WA MAKONDA KWA MAKAMU WA RAIS KUHUSU YANGA Leo February 11 2025 Katika Mkutano wa juhudi za kuimarisha utoaji wa huduma za umma kwa njia za kidijitali, mkutano wa tano wa Serikali Mtandao Umeanza Leo jijini Arusha, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wataalamu wa TEHAMA na wadau wa maendeleo. Mgeni rasmi katika mkutano huu ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Pia amegusia Mipango na maandalizi ya Siku ya wanawake Dunia ambayo inafanyika Kitaifa Mkoani humo "Sherehe ya Siku ya Wanawake Kitaifa Arusha tunafanya kitu cha tofauti. Kutakuwa na michezo kama mpira wa miguu, ukiwahusisha wachezaji wa kike kutoka timu za Simba Queens, Yanga Queens, JKT Queens na Fountain Gate FC. Hii ni sehemu ya juhudi za kukuza vipaji vya wanawake katika sekta ya michezo na kuwawezesha kwa njia mbalimbali." Maadhimisho haya yanatarajiwa kuwavutia washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, huku yakiwa na lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuwatambua wanawake kwa mchango wao katika maendeleo ya taifa. Mkutano wa Serikali Mtandao unaendelea, ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa, ikiwemo ubunifu katika utoaji wa huduma za umma kupitia mifumo ya kidijitali.

HABARIMPYA TV

44,794 次观看 • 1 年前