Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

216,412 views • 2 months ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

Veronica Lefunya, mkazi wa Hanang, Manyara akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan msaada katika masuala sita ambayo ameyafafanua vizuri zaidi. Kwa kuzingatia maswali yake kwa Rais, nitaongeza mfano wa Philippines, katika kilimo, kwa kuwa wakazi wa Hanang ni wakulima kwa kiasi kikubwa. Serikali ya Philippines imetoa 12.7 billion pesos (Sh.575 bilioni) msaada wa kifedha kwa wakulima wapatao milioni 2.3 wa mpunga nchini Ufilipino. RFFA, imebaini wakulima wadogo wa mpunga milioni 2.3 waliosajiliwa katika Mfumo wa Usajili wa Sekta za Msingi katika Kilimo (RSBSA) kufikia Juni 30, 2023. Serikali ya Philippines imetoa kiasi hicho cha fedha ili kuwasaidia wakulima wa mpunga katika kukabiliana na El Niño na gharama kubwa za uzalishaji. Wakulima wa mpunga katika nchi ya Philippines wanaolima chini ya hekta mbili za ardhi watapokea peso (php) 5,000 kila mmoja, hii ni Sh. 226,068. Fedha hizo zitatoka katika mfuko wa ziada wa ushuru (excess tariff collections) kutokana na uagizaji wa mchele mwaka 2022. Hii ni taarifa kutoka ofisi ya Rais Pesos 700 milioni (Sh. 31.60 bilioni) nyingine kutoka kwa ushuru wa mchele, zimetengwa kwa usambazaji kwa wakulima 78,000 nchini Philippines. Wakulima 78,000 chini ya mpango wa ruzuku ya fedha wa idara ya ustawi wa jamii (Department of Social Welfare and Development - DSWD) Huu ni Mpango wa Msaada wa Kifedha kwa Wakulima wa Mpunga (Rice Farmers Financial Assistance - RFFA). Tanzania sijui kama upo mpango huo. Mpango huu ni katika azma ya kuwasaidia wakulima wadogo wa mpunga kuendeleza tija yao kutokana na baadhi ya changamoto za kilimo nchini. RFFA ni usaidizi wa kifedha usio na masharti kwa wakulima wanaolima chini ya hekta mbili za ardhi kama inavyoidhinishwa chini ya sheria za Philippines Sheria hizo zinazounda na kulinda RFFA ni; Sheria ya Jamhuri (RA) Na. 11598, na Sheria ya Usaidizi wa Fedha kwa Wakulima wa Philipines ya 2021. Bei ya juu sana ya mchele imeongeza mfumuko wa bei za bidhaa nchini Philippines mwezi Agosti 2023, Rais Ferdinand Marcos akaleta mpango kazi wake. Kupunguza bei ya nafaka na kutoa msaada wa pesa taslimu kwa wauzaji reja reja wa mchele na wamiliki wa maduka madogo walioathiriwa na punguzo hilo. Nawakumbusha, RFFA ya Philippines siyo baada ya El Niño, hapan, ni fedha ambazo zimetolewa na Serikali kukabiliana na changamoto ya El Niño, baadae. Hoja ya msingi ya Bi. Veronica Lefunya inaweza kupata ufumbuzi kupitia mfano huu wa Philippines. Serikali itengee mfuko kuwasaidi wakulima Hanang Ni msimu wa kilimo Hanang. Watu wamepoteza fedha za kukodi mashamba. Wenye mashamba yameharibika vibaya. Serikali iwajibike kuwasaidia. Kilimo kinaweza kuwasaidia wananchi wa Hanang kupata chakula na fedha za kujikimu na hata kuanza kujenga makazi yao yaliyoharibika vibaya sana. MMM, Martin maranja Masese

Martin Maranja Masese

85,571 views • 2 years ago

Rais Samia Suluhu shikamoo. Umeibua mjadala mzuri na tutajadili pamoja. Nashauri wasaidizi wako wakufikishie sehemu ya maoni yangu katika mjadala huu ulioibua Ughaibuni. Kwa kutumia tafsiri yako ya umaskini, hatutakuwa na mjadala sahihi. Tafsiri ya utajiri haiwezi kuwa tu na uwezo wa kupata chakula na matunda. Hapana. Hata kazi ta Umoja wa Mataifa katika Kutokomeza Umasikini inahusishwa na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Wameyataja na kuyainisha malengo 17. Baadhi ya malengo ni; 1. Kutokomeza Umaskini 2. Kukomesha Njaa 3. Afya Njema na ustawi 4. Elimu bora 5. Usawa na jinsia 6. Maji Salama na Usafi. Lazima tutoe tafsiri ya umaskini kwa kutumia tafsiri za viwango vya Umskini vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa. Na hapo tutakuwa na mjadala mzuri. Mwaka 1998, Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha Taarifa kuhusu Umaskini (statement on poverty) ilitiwa saini na wakuu wa mashirika yote ya UN. Kimsingi, umaskini ni kunyimwa chaguo na fursa, ukiukaji wa utu wa binadamu . Inamaanisha ukosefu wa msingi. uwezo wa kushiriki kikamilifu katika jamii. Kutokuwa na chakula kulisha familia, kutokuwa na shule, zahanati ya kwenda, kutokuwa na ardhi ya kulima chakula cha mtu au kazi ili kujipatia riziki, Uwezekano wa kukabiliwa na vurugu, na mara nyingi inamaanisha kuishi kwenye mazingira ya pembezoni au tete, bila kupata maji safi na salama au vyoo. Sasa tunaweza kujadili kwa kuzingatia tafsiri hiyo ya Umoja wa mataifa (UN) kuhusu Umaskini ambayo ilitiwa saini na wakuu wa mashirika yote ya UN. Tanzaniani inazo rasilimali nyingi lakini wananchi wake ni maskini wa kutupwa. Rasilimali walizonazo haziwanufaishi kabisa na zinatumiwa hovyo. Pamoja na mikakati mingi ya kutokomeza umaskini, bado umaskini umeendelea kuwa adui wa Taifa. Viongozi wengi kama siyo wote siyo waaminifu. Hata Wanaokiuka maadili na ukosefu wa uaminifu hawachukuliwi hatua za kisheria. Wanahamishwa kutoka eneo moja la kazi na kwenda eneo lingine. Kuna ukosefu mkubwa sana wa maadili kwa watumishi na viongozi wa umma. Wamejitajirisha kupitia mali za umma. Wanao utajiri wa kutisha. Wamejitajirisha kupitia nafasi zao katika utumishiwa huo wa umma, vyanzo vyao havieleweki. Watanzani wengi wanamiliki umasikini wa kutisha sana. Tanzania ina jumla la eneo ukubwa wa 947,303 km² (30th Duniani). Eneo lenye maji 6.4%. 93.6% ni eneo la nchi kavu. 45% ya ardhi yote inafaa kwa kilimo. Eneo ambalo limetumika kwa ajili ya kilimo halijafika hata 30%. Kwanini kama ncji sasa tusiwekeze katika kilimo chenye tija na tukatafute kodi nyingi? Ardhi ya Kilimo (% ya eneo la ardhi) Tanzania ilikuwa 44.62% kufikia 2020, kulingana na ukusanyaji wa viashiria vya maendeleo vya Benki ya Dunia, Viashiria vilivyokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo vinatambulika na Benki ya Dunia (World Bank) hadi kufikia kipindi cha kuanzia Januari 2023 Kufikia ¼ ya nne ya mwaka 2021 (Q4 2021), shughuli za kilimo zilichangia karibu 30% ya Pato la Taifa la Tanzania (GDP). Ni karibu nusu ya pato lote la Taifa. Mwaka 2020, ilifikia 26.9%. Kilimo ni moja ya sekta kuu za kiuchumi Tanzania. Tangu 2012, mchango wake katika uchumi wa nchi umebaki juu ya 25%. Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Wananchi vijijini hawafanyi uzalishaji. Hii ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Zaidi ya nchi 80 Duniani huzalisha ngano duniani kote, uzalishaji mkubwa wa ngano duniani unatoka katika nchi chache tu ambazo haziwezi kuzidi nchi 10. Kulingana na takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Tanzania haipo katika orodha hiyo. Watawala wameshindwa kabisa kufikiri. Tanzania inanunua zaidi ya tani 1,000,000 za ngano kutoka nje. Hivyo kwa mwaka Tanzania inatumia zaidi ya Sh1.3 trilioni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi. Sekta ya kilimo ni msingi wa Uchumi Tanzania. 65.5% ya watanzania wameajiriwa kwenye kilimo au wanategemea kilimo kwa kipato chao cha kila siku,. 100% ya chakula inategemewa kutoka sekta ya kilimo. Kilimo kinachangia 29.1% ya pato la taifa (GDP), karibia ⅓ ya thamani ya shughuli za Uchumi. Nimeshauri sana, wezesheni vijana eneo la fedha na masoko, vijana wafanye uzalishaji. Fungamanisha sekta ya kilimo na viwanda ili kutegemeana kisekta Wekezeni katika kilimo chenye tija, tumieni kilimo kama fursa ya kutuvusha kufika mnapotaka, kodi nyingi hazitotufikisha tunapohitaji kufika kama taifa. Mtatuumiza tu. Fursa ya soko ipo sana Duniani. Hali ya mahitaji ya chakula Duniani mwaka 2020 takribani watu milioni 811 walikuwa hawana lishe bora China ni mzalishaji mkubwa zaidi wa ngano Duniani, imetoa zaidi ya tani bilioni 2.4 za ngano katika miaka 20 iliyopita, na hii ni karibu 17% ya jumla ya uzalishaji. Nchi ya pili Duniani kwa uzalishaji wa ngano ni India. Katika miongo miwili, India imetoa 12.5% ​​ya ngano yote ya Duniani. Hawa ni wauzaji wakubwa wa ngano. Kama ilivyo kwa China, India pia inahifadhi ngano yake nyingi ndani kwa mahitaji makubwa ya chakula ndani ya nchi zao. Nchi ya India ina wakazi 1.4 bilioni. Katika orodha hii, Ukraine anashika nafasi ya 10, katika miongo 2 iliyopita wamezalisha tani milioni 433 za ngano, karibu 3.1% ya jumla ya uzalishaji Russia, nchi ya tatu Duniani kwa uzalishaji wa ngano, ni muuzaji mkubwa wa ngano kimataifa. Pia, Russia kama zilivyo China na India wanahifadhi ngano yao. Russia ilisafirisha ngano yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 7.3 kwa 2021, ikichukua takribani 13.1% ya jumla ya mauzo ya ngano mwaka huo Duniani. Kulingana na takwimu za Idara ya Kilimo ya Marekani (US Department of Agriculture), Ukraine ilikuwa nchi ya 7 kwa uzalishaji wa ngano Duniani kufikia 2021. Ukraine 2021/22 ikizalisha tani milioni 33. Australia, Marekani, Russia, India na China ndizo zilizozalisha zaidi. Ukraine ni ndogo sana kwa Tanzania. Takribani 80% ya uzalishaji wa kilimo Tanzania unatokana na wakulima wadogo, wanategemea kilimo cha mikono na uzalishaji kutegemea mvua. Kilimo cha mikono na uzalishaji wa kutegemea mvua huwafanya kuwa katika hatari ya majanga ya mabadiliko ya hali ya hewa. Wizara ya kilimo ipo? Kilimo, ni tegemeo kuu la maisha kwa takribani 70% ya kaya za Tanzania, kilimo kinakuwa taratibu sana. Sekta ya kilimo, inaundwa na wakulima wadogo. Sekta ya kilimo haijanufaika na kasi sawa na sekta nyingine na inahitaji uwekezaji na kisasa. Vijana wanachangia 30% ya nguvu kazi, hasa katika kilimo. Umaskini umeenea vijijini, makazi ya zaidi ya 70% ya watu ambao ni maskini. Ukweli, ukuaji wa uchumi umeshuka hadi kwa watu maskini wa Tanzania. 70% ya Watanzania wanaendelea kuishi chini ya $2.00 kwa siku. Tanzania inayo 45% ya ardhi ambayo inafaa kwa kilimo na 30% ya matumizi hayajafikiwa. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi kukua, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo ambacho kimetoa ajira kwa watanzania karibu 70%, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania. Hatari. Hapa unapiga ramli kutafuta mchawi? Tunapaswa kujiuliza wenzetu wamefanya uchawi gani kuwa na maendeleo? Mchawi ni SERIKALI ya CCM. Kwa mujibu wa wataalamu wa Uchumi, ili kupunguza umasikini Tanzania, sekta ya kilimo inapaswa kukua kwa zaidi ya 8% angalau kwa miaka 3 mfululizo, Na wataalam hao wa uchumi kwa tafiti wanasisitiza kwamba ukuaji huo wa sekta uendelee kukua kwa wastani wa 6% kwa muda miaka 10 mfululizo. Watawala awamu zote na hata waliopo madarakani wameshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Wamechoka. Wapumzishwe. Nitawapa ushauri! Serikali kupitia wizara ya kilimo inawajibika kujenga mnyororo wa thamani. Mnyororo unaojumuisha zaidi na ustahimilivu wa bidhaa za kipaumbele, Serikali yenye kutumia ubongo lazima ihangaike na masuala yanayowahusu wananchi walio wengi, na hapa Tanzania watu hao (walio wengi) ni Wakulima. Hivyo basi, kipimo kikuu cha kuondoa umasikini wa Watanzania ni kuondoa umasikini wa wakulima. Wakulima wa Tanzania wametelekezwa kabisa. Mnyororo ujengwe katika bidhaa zinazosukumwa na upanuzi endelevu wa upatikanaji wa masoko na huduma za kifedha na kuhakikisha sekta binafsi inajitegemea; Serikali kupitia wizara ya kilimo katika utaratibu wa kibajeti kuboresha teknolojia zinazostahimili hali ya hewa zinazoongeza tija katika mazao ya kipaumbele, Mifugo na bidhaa za uvuvi; Tanzania kama nchi nyingine, inakumbwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Serikali iwekeze katika teknolojia ya kilimo. Serikali ihusike katika kuimarisha utawala bora wa ardhi, na kuwezesha uwekezaji wa umma na uwekezaji binafsi katika kilimo. BBT ni failed project. Wananchi wapewe fursa na wawezeshwe mitaji na pembejeo ili wazalishe na serikali iwatafutie masoko ya bidhaa. Wazalishe mazao ya chakulana biashara. Ni wajibu wa Serikali ambao wanaukwepa. Serikali hii naelewa haiwezi kuleta tena tija kwa muda mfupi sana uliobaki. CCM mnahitaji miaka 100 kutekeleza. Matendo ya Serikali yako yanaonyesha tofauti, Serikali haiwajali wanyonge, inapuuza uchumi wa 65.5% ya hao watu ambao unawaita siyo maskini. Ni vigumu kuondoa umasikini mkiendelea kuwadharau wakulima. Kilimo ni sekta ya msingi, ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti. Lakini itafaa nini ikiwa umaskini wa watanzania ni fursa ya kisiasa kwa watawala wa CCM nyakati zote? Wanautumia umaskini kama fimbo ya kuwachapia. Suluhisho ni moja tu. Ni kubadili mfumo mzima wa Serikali na kuweka kizazi kitakacho-chukia rushwa, wizi, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka. MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.

Martin Maranja Masese

38,634 views • 1 year ago