Загрузка видео...

Не удалось загрузить видео

На главную

Wanaume Wa Sinza..!

16,049 просмотров • 1 день назад •via X (Twitter)

Комментарии: 0

Нет доступных комментариев

Здесь появятся комментарии из оригинального поста

Похожие видео

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dkt.Dorothy Gwajima amesema wataomba kupitisha siku ya Wanaume Duniani Inayoadhimishwa kila mwaka Novemba 19 kuwa rasmi na sio kuwa kama ilivyo kwa sasa. Hayo ameyasema leo katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Wilayani Bukombe Mkoani Geita ambapo kwa kanda ya ziwa yameazimishwa Mkoani humo huku Mgeni rasmi akiwa Waziri Dkt.Dorothy Gwajima ambapo amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewanyanyua Wanawake kutoka hatua moja kwenda nyingine. “Kama wewe halijakufika Jambo hili la Mafanikio fungua masikio sasa funguo macho sasa ungana na risala hii na risala za kanda zote sita amua sasa uungane nasi pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwanyanyua Wanawake kutoka hatua moja kwenda nyingine ,” Dkt.Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii. “Wanaume wananiangalia nawaona wanasema na sisi je ? Ndugu wapendwa Wanaume na nyinyi mpo ngoja niwambie kwenye sera yetu ya maendeleo jinsia na Wanawake tumewaingiza Wanaume na sera hiyo ni mpya imetolewa toleo la mwaka 2023 Dkt.Samia Suluhu Hassan akasema hatutaweza kuendelea mbele Wanawake kama Wanaume huku hawajaelewa hii dhana wanaturudisha nyuma , “ Dkt.Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii. “Lakini tukafungamanisha na hao Wanaume wenyewe kwenye hii sera niliyoisema na wao jambo lao huwa ni novemba 19 Wanaume mpo mwanzo nilisema mpo wakasema tuko jikoni tukakosha vyombo sasa mimi nasema mpo na mpo kwenye sera kabisa maswala ya ushirikishwaji Wanaume ili waendelee lengo la kumwendeleza Mwanamke ni pamoja na kumwendeleza Mtoto wao wa kike na sio Mke wao tuu hatuongelei habari ya Mkeo tuu tunaongelea na Binti yako huyo uliyemuweka nyumbani , “ Dkt.Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii. #MillardAyoUPDATES

millardayo

23,062 просмотров • 1 год назад