Загрузка видео...

Не удалось загрузить видео

На главную

Wanawake ni Tiba na ni Dhara 😊

11,620 просмотров • 1 год назад •via X (Twitter)

Комментарии: 1

Фото профиля Abdallah Mkindi
Abdallah Mkindi1 год назад

huyu madam leila mungu akupe umri mrefuu katka hii dunia na kizazi chako unaongea vitu kuntuuu sna

Похожие видео

VIDEO: Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Zainab Abdallah, ametoa wito mzito kwa wanawake kote nchini kuhakikisha wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ni jambo la aibu kwa wanawake kushindwa kusimama pamoja na mwanamke mwenzao ambaye ametengeneza fursa nyingi kwa Taifa na hasa kwa wanawake. Akizungumza Jumapili hii katika Kongamano la Mabinti na Wanawake wa Mkoa wa Tanga lililofanyika kwenye Ukumbi wa Naivera jijini humo, Zainab amesema ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya watu wakiendelea kulalamika licha ya serikali ya awamu ya sita kutekeleza kwa vitendo mambo waliyokuwa wakiyapigania. "Yapo maneno yaliyosemwa huko nyuma kwamba nchi imefungwa, viongozi hawaruhusiwi kwenda nje kuimarisha diplomasia – lakini mama Samia ameingia, akafungua milango ya diplomasia. Wakaja tena wakasema hakuna uhuru wa vyombo vya habari, lakini Rais Samia akaweka mazingira ya uhuru wa kuzungumza. Sasa hayo yote yamefanyika, bado wanalalamika. Hakuna kitu kibaya kama mwanadamu kutokujua unachokitaka," amesema Zainab. Amewataka wanawake wa Kitanzania kuonesha mshikamano wa kweli kwa Rais Samia kwa vitendo, kwa kueneza ujumbe chanya, kujitokeza katika nafasi mbalimbali na kuonesha kuwa wanathamini jitihada za kiongozi wa kwanza mwanamke nchini. "Mimi nawaomba wanawake wenzangu tumuunge mkono Mama Samia. Ni aibu na ni fedheha kwa wanawake sisi kushindwa kumuunga mkono mwanamke mwenzetu ambaye anatuwakilisha na kutufungulia milango ya maendeleo," ameongeza. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Mwanamke na Uongozi chini ya Mkurugenzi wake Bi. Shamira Mshangama Shamira Mshangama , likiwa na lengo la kutafakari mchango wa Rais Samia kwa wanawake na mabinti katika miaka minne ya uongozi wake, sambamba na kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa Lailah Ngozi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, huku likihudhuriwa na wanawake na viongozi wa kada mbalimbali kutoka mkoa wa Tanga.

Jambo TV

17,730 просмотров • 1 год назад