正在加载视频...

视频加载失败

Watekaji na wauaji wanajulikana

36,532 次观看 • 11 天前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

Nimesikiliza maelezo yote ya muhudumu wa Rovennpec Resort, Kiluvya, Dar es Salaam akieleza tukio zima la jaribio la kumteka ndugu Deogratius Tarimo. Niwapongeze Rovennpec Resort kwa kuruhusu wanahabari kufika katika hoteli na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wao. Ni uungwana. Pia, kukubali kuachia footages za CCTV cameras siku ya tukio hilo, ni ujasiri na hakika, hakuna kitu wapigania haki tunaweza kuwalipa. Mmetenda mema. Watekaji hao walipofika Rovennpec Resort na kuanza kumdhibiti ndugu Deogratius Tarimo, walijitambulisha ni askari - polisi kutoka kituo cha Polisi Oysterbay. Watu waliomteka Boniface Jacob pale katika mgahawa wa Golden Fork pia walijitambulisha ni askari - polisi kutoka kituo cha polisi Oysterbay. Walivaa kiraia tu. Watu waliomteka Edgar Edson Mwakabela (SATIVA) alipotekwa eneo la Korogwe, watekaji walimchukua na kumpeleka karakana za kituo cha Polisi - Oysterbay. Nafikiri, Jeshi la Polisi litueleze kinaga-ubaga, kwanini hawa watekaji wakati wote wanataja au kuhusisha kituo cha Polisi - Oysterbay katika matukio ya utekaji? Kwa kuwa Polisi wanasema hawahusiki na masuala ya utekaji na wamekana watekaji, kwanini watekaji wakamatwe na kuhojiwa kwa kuchafua Jeshi la Polisi? Jeshi la Polisi kuendelea kuwa kimya na kuwaacha watekaji waendelee kutamba bila kukamatwa, wanatoa tafsiri hasi kwa jamii ya watu waliostaarabika. Au tukubaliane, watekaji wanelishinda nguvu jeahi la Polisi na Jeshi la polisi limekubali kuwaacha watekaji waendeshe oparesheni zao za kuteka na kuua? NB; matukio hayo matatu yametokea katika maeneo tofauti ya wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam na kituo cha Polisi Oysterbay kimetajwa. WHY?

Martin Maranja Masese

68,572 次观看 • 1 年前