HABARIMPYA TV's banner
HABARIMPYA TV's profile picture

HABARIMPYA TV

@HabarimpyaTv129,715 subscribers

News Updates 24 hours,.

Shorts

Matokeo bado hayajatangazwa ila Godbless Lema anashangilia,.✌️

Matokeo bado hayajatangazwa ila Godbless Lema anashangilia,.✌️

61,756 views

Mzee anautaka Ubunge kwa hali na mali 😂😂🙌

Mzee anautaka Ubunge kwa hali na mali 😂😂🙌

14,416 views

Videos

HabarimpyaTv's profile picture

Wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga wamemtaka Mbunge wao, January Makamba, kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kushindwa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni. Wakizungumza na wanahabari leo, Aprili 2, 2025, jijini Dar es Salaam, wananchi hao wamesema kuwa licha ya kumpa kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu ujao, hawako tayari kumpigia kura tena Makamba kwa nafasi ya ubunge. Changamoto Zinazowakabili Wananchi 👇👇 Miongoni mwa matatizo waliyoeleza ni hali mbaya ya miundombinu, hasa barabara, ambayo imeathiri sekta ya kilimo. Bw. Eric Edward kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amesema walitarajia Makamba kutatua changamoto ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa chai, lakini hali imeendelea kuwa mbaya. “Kiwanda cha Mponde kilianza kwa nguvu lakini sasa thamani ya chai imeshuka. Wakulima wanahangaika kusafirisha mazao kwa bajaji kwenye barabara mbovu,” alisema Edward. Naye Elias Kamute alizungumzia tatizo la maji, akisema: “Bumbuli ina maji mengi, lakini hadi leo tunapata mgao. Ahadi zimekuwa nyingi, lakini utekelezaji hakuna kwa zaidi ya miaka 15.” Kwa upande wake, Khalid Kijazi alisema Makamba hana uhusiano wa karibu na wananchi wa Bumbuli, akidai kuwa “Ni kama mtalii wa nje na Dar es Salaam badala ya kushughulikia changamoto za jimbo lake.” “Tunahitaji kiongozi mpya kwa sababu Makamba ameshindwa kutimiza wajibu wake,” alisema Ayubu Radhid, akieleza jinsi miundombinu mibovu imeathiri wakulima wa eneo hilo. Merry Gendo naye alieleza kusikitishwa na kutotimizwa kwa ahadi za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, huku akidai Makamba aliwahi kusema “Wananchi wa Bumbuli hawahitaji maendeleo bali pesa za dagaa.” Katika sekta ya afya, Iddy Amiri alisema huduma duni za matibabu na uhaba wa madaktari ni matatizo makubwa, huku elimu nayo ikidorora kutokana na ukosefu wa walimu na miundombinu duni. “Makamba aliahidi kuboresha elimu, lakini hakuna kilichotekelezwa. Tunahitaji mbunge mpya atakayeleta maendeleo ya kweli,” alisema. Wananchi hao wamesisitiza kuwa ni wakati wa mabadiliko, wakimtaka January Makamba kuachia ngazi ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwatumikia kwa ufanisi.

HABARIMPYA TV

151,142 views • 1 year ago

HabarimpyaTv's profile picture

Kijana dereva wa bodaboda anayefahamika kwa jina la Brown Anthony ameibua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi baada ya kufanikiwa kusafiri kutoka jijini Mbeya hadi Dar es Salaam kwa kutumia pikipiki aina ya Boxer 150 HD yenye namba ya usajili MC 473 FKT, ndani ya saa 10, safari iliyoanzia kwenye ubishani wa kawaida na kuhitimishwa kwa ushindi wa kihistoria. Ubishani huo ulianza tarehe 14 Januari 2026 kati ya Brown Anthony na bodaboda mwenzake Alex Ndile, ambapo walitofautiana kuhusu uwezekano wa kufika Dar es Salaam kwa pikipiki ndani ya muda wa masaa 13. Baada ya majadiliano makali, walikubaliana kuyaweka madai yao katika makubaliano rasmi ya kisheria. Makubaliano hayo yaliwekwa mbele ya mwanasheria Ambakisye Kibona, ambapo kila mmoja alikuwa na pikipiki yake binafsi, na pande zote zilikubaliana kuwa atakayeshindwa atalazimika kumpa mshindi pikipiki yake kama dau la makubaliano hayo. Baada ya makubaliano kukamilika, Brown Anthony alianza safari yake rasmi tarehe 15 Januari saa 11:00 asubuhi, akitokea Mbalizi jijini Mbeya, akitumia pikipiki yake kama ilivyokubaliwa katika makubaliano hayo ya kisheria. Katika safari hiyo ndefu na yenye changamoto, Brown Anthony alifanya mapumziko mara tatu kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo madogo ya pikipiki, hatua iliyomwezesha kuendelea na safari bila matatizo ya kiufundi. Hatimaye, alifanikiwa kuwasili jijini Dar es Salaam saa 9:35 alasiri siku hiyo hiyo, akitumia muda uliokuwa chini ya masharti ya makubaliano, na hivyo kuthibitisha ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Alex Ndile. Baada ya kukamilisha safari hiyo, Brown Anthony alianza safari ya kurejea Mbeya alfajiri ya saa 11 kutoka Dar es Salaam, na kufanikiwa kuingia Mbalizi jijini Mbeya jioni ya Ijumaa, Januari 16, 2026, ambapo alipokelewa kwa shangwe. Kufuatia ushindi huo, alikabidhiwa pikipiki ya ushindi, iliyokuwa mali ya Alex Ndile yenye namba ya usajili MC 695 EFE.

HABARIMPYA TV

43,584 views • 4 months ago