
HABARIMPYA TV
@HabarimpyaTv • 129,958 subscribers
News Updates 24 hours,.
Shorts
Videos

Wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga wamemtaka Mbunge wao, January Makamba, kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kushindwa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni. Wakizungumza na wanahabari leo, Aprili 2, 2025, jijini Dar es Salaam, wananchi hao wamesema kuwa licha ya kumpa kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu ujao, hawako tayari kumpigia kura tena Makamba kwa nafasi ya ubunge. Changamoto Zinazowakabili Wananchi 👇👇 Miongoni mwa matatizo waliyoeleza ni hali mbaya ya miundombinu, hasa barabara, ambayo imeathiri sekta ya kilimo. Bw. Eric Edward kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amesema walitarajia Makamba kutatua changamoto ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa chai, lakini hali imeendelea kuwa mbaya. “Kiwanda cha Mponde kilianza kwa nguvu lakini sasa thamani ya chai imeshuka. Wakulima wanahangaika kusafirisha mazao kwa bajaji kwenye barabara mbovu,” alisema Edward. Naye Elias Kamute alizungumzia tatizo la maji, akisema: “Bumbuli ina maji mengi, lakini hadi leo tunapata mgao. Ahadi zimekuwa nyingi, lakini utekelezaji hakuna kwa zaidi ya miaka 15.” Kwa upande wake, Khalid Kijazi alisema Makamba hana uhusiano wa karibu na wananchi wa Bumbuli, akidai kuwa “Ni kama mtalii wa nje na Dar es Salaam badala ya kushughulikia changamoto za jimbo lake.” “Tunahitaji kiongozi mpya kwa sababu Makamba ameshindwa kutimiza wajibu wake,” alisema Ayubu Radhid, akieleza jinsi miundombinu mibovu imeathiri wakulima wa eneo hilo. Merry Gendo naye alieleza kusikitishwa na kutotimizwa kwa ahadi za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, huku akidai Makamba aliwahi kusema “Wananchi wa Bumbuli hawahitaji maendeleo bali pesa za dagaa.” Katika sekta ya afya, Iddy Amiri alisema huduma duni za matibabu na uhaba wa madaktari ni matatizo makubwa, huku elimu nayo ikidorora kutokana na ukosefu wa walimu na miundombinu duni. “Makamba aliahidi kuboresha elimu, lakini hakuna kilichotekelezwa. Tunahitaji mbunge mpya atakayeleta maendeleo ya kweli,” alisema. Wananchi hao wamesisitiza kuwa ni wakati wa mabadiliko, wakimtaka January Makamba kuachia ngazi ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwatumikia kwa ufanisi.
HABARIMPYA TV151,148 görüntüleme • 1 yıl önce

Huyu Kiongozi ni Noma sanaa ukienda kichwa kichwa anakuvunja mbavu changa,. 🙌🙌
HABARIMPYA TV50,430 görüntüleme • 4 ay önce

Ustaz Juma na Musoma azungumzia uchapakazi wa Askari Faustin Mafwele na kutoa pongezi kwa jeshi la polisi.
HABARIMPYA TV75,813 görüntüleme • 8 ay önce

Kenge kaingia kwenye 18 za mlavichwa ni ameliwa kama Mpumbavu,.🙌🙌
HABARIMPYA TV118,379 görüntüleme • 1 yıl önce

Aliyekuwa kada wa CHADEMA Catherine Ruge Rasmi ajivua uanachama wa chama hicho.
HABARIMPYA TV113,078 görüntüleme • 1 yıl önce

Inaelezwa kuwa haya ndio maneno yaliyomponza Msemaji wa Yanga na kupelekea akamatwe na jeshi la Polisi,.
HABARIMPYA TV110,857 görüntüleme • 1 yıl önce

Mwenyekiti wa taasisi ya Samia Us, Geoffrey Kiliba ambaye pia ni Mwanafunzi wa chuo cha DIT akiambatana na wanafunzi wenzake wamepinga vikali kauli iliyoasisiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) isimayo 'no reform no election wakidai kauli hiyo ni mtazamo binafsi wa Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu
HABARIMPYA TV121,918 görüntüleme • 1 yıl önce

Salum Mwalimu: Leo tunaondoka CHADEMA na wasidhani tuko pekeyetu kuna kundi kubwa linafuata
HABARIMPYA TV96,282 görüntüleme • 1 yıl önce

Tuende mbele turudi nyuma huyu Dogo Amemtania sana Mama wa Taifa, inabidi akamatwe 😂😂🙌 (Jokes)
HABARIMPYA TV107,356 görüntüleme • 1 yıl önce