
John Heche
@HecheJohn • 805,431 subscribers
Vice Chairman Chadema Tanganyika, former Member of Parliament for Tarime rural constituency, a reformer.
Shorts
Videos

Huyu Bwana Kombo anazidi kuthibitisha kwamba waliua watu bila sababu ya msingi… Chande alisema kulikua na training na silaha , kombo anasema mawe!!! anasema ukimlembea jiwe polisi, anatakiwa kukupiga risasi.. Je Bwana Kombo yule mama Mtanganyika pale Arusha, Video yake Inaonekana anakimbia , akapigwa risasi mgongoni, alilemba jiwe kwa nani? Watu wameuwawa wakiwa nje ya Mageti ya nyumba zao, wengine kwenye sebule , kuna vijana Mwanza mmeaua wakiwa wanaangali Mpira… Unasema tumeheal!!!! Hamtaweza kufukia mauaji ya kutisha mliyofanya ili mjitangaze kwenye uchaguzi ambao haukuwepo… wote mnakula pesa za damu na dunia haitakaa kimya.
John Heche66,893 Aufrufe • vor 11 Tagen

Mwigulu unasemaje sasa kuhusu hili? Anaehujumu serikali ni nani? Serikali dhalimu hii iliyojaaa damu, inatesa mamilioni ya Watanzania kuanzia Mtwara mpaka Tarime toka Tarime mpaka Kigoma kutoka Kigoma mpaka Songea, Tunduma mpka Dar.. Kila kona ya Nchi hii watu wanalia kama sio kubambikiziwa kesi na polisi, ndugu zao wametekwa au wameuwawa na vyombo vya dola . Huyu mama anahitaji kulipwa nini ili aandamane kudai haki ya mtoto wake kutekwa. Watoto wa huyo kijana au wa Soka, Mdude au polepole, watoto wa Chonchoryo au Sinda, watoto wa Tall au Kipanya wakikua wataacha watoto wenu waishi kwa Amani? Mnajenga sumu ya hatari mno kwenye mioyo ya Watanzania, bahati mbaya nashindwa kuona tatizo hili na kulitatua bado mnatumia ubabe na kiburi… Fikiria huyo angekua mama yako! Utaratibu wa polisi kukamata watu upo kisheria. Kwanini polisi wanateka Watanzania? Kila mtu ambae mtoto wake au ndugu yake amechukuliwa story zinafanana kwamba watekaji walijitambulisha kwamba wao ni polisi. Jambo kubwa kama hili, Watuhumiwa ni polisi alafu unasema polisi ndio wafuatilie!hivi mnawaonaje Watanzania? Watanzania hawatakubali kuishi kwa hofu kwasababu ya kagenge kadogo ka wauaji na wanyonya damu.
John Heche31,735 Aufrufe • vor 6 Tagen

Jana nilipokwenda kuhuduria Kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Chaso. Walitumwa baadhi ya vijana kutoka UVCCM, kwa kulipwa vifedha kidogo… Sina tatizo na vijana hata kama ni wa ccm kuhudhuria na kusikiliza sera, misimamo na hoja zetu. Lakini huyu kijana, watu wetu walipomgundua na kumhoji alisema alikua ameambiwa kwamba tukianza kuzungumza kuhusu ripoti ya Chande wazomee.. Lakini pia wafanye fujo na kutoka ukumbuni, ionekane vijana hawakutusikiliza. Kwenye simu yake alikua anawasiliana na mtu anaitwa Shangwe Mtei ambae ni kiongozi wa Uvccm. Huyu Shangwe akawa anamhakikishia kwamba hata kama wako wachache wafanye fujo kwasababu OCD alikuwepo nao pale. Ghafla huyu kijana akiwa anahojiwa na watu wetu kwanini yuko pale na nia yake ni ipi, Magari mawili ya polisi yalikuja pale kitendo kinachoonesha kwamba tukio hili lilikua limepangwa kwa ushirikiano huo. Huyu kijana alikua ametumiwa muamala wa sh 50,000 kwa madai yake walitumiwa wote na wenzake, na walipatwa hofu na kutokufanya fujo kwasababu vijana wa Chaso walikua wengi zaidi na pia ulinzi ulikua imara.. Fikiria kwamba huyu ni kijana wa chuo kikuu ana fikra na mawazo ya kutumwa na kulipwa sh 50 elfu!! Tuna safari ndefu kama Nchi Lakini lazima tufike.. Asante watu wetu wa ulinzi kwa kazi nzuri.
John Heche63,031 Aufrufe • vor 1 Monat

Kenya itazidi kutuacha mbali mno kwa kila kitu… Chanzo cha ufisadi, wizi na ujambazi wa mali za umma ni usiri wa mikataba na makubaliano. Kuna ujambazi mkubwa kwenye mikataba ya bandari zetu kupewa Waarabu, viwanja vya ndege, misitu kwa Oman, gesi yetu, dhahabu zetu ikiwemo mkataba mpya wa Sengerema Nyanzaga, huu mgodi utakua mkubwa kuliko yote Nchini..kuna mikataba ya mbuga za wanayama, mikataba ya nickel na cobalts kule Kabanga. Kuna mkataba wa uranium na Urusi kule Namtumbo.. Tunaweza kutaja maelfu ya mikataba ambayo inafanywa siri ya hawa mafisadi wasio na huruma na Watanzania. Mkataba wa ujenzi wa SGR ya Tanzania ni uchafu mkubwa, kuna kipande kimejengwa kwa usd milioni 3.9 kwa kilometa na kingine kinajengwa kwa usd milioni 5.5 kwa kilometa bila ushindani. Mikataba ya manunuzi ya mabehewa ya hovyo. Mikataba ya ujenzi wa barabara takataka ambazo zinabomoka siku ya pili baada ya kukabidhiwa, mikabata ya wizi ya BRT Dar, ununuzi na ujenzi wa Meli Mwanza. Katiba ya Kenya inawapa Wakenya fursa ya kuona huo uchafu na kuchukua hatua. Ndio maana Watanzania lazima tupiganie Katiba mpya ili tukomeshe huu ushenzi unaotutesa na kutuacha masikini kwa miaka mingi. Tunataka katiba mpya sasa.
John Heche14,142 Aufrufe • vor 14 Tagen

Dunia inajua ripoti ya Chande ni uongo wa kusafisha watuhumiwa.
John Heche34,723 Aufrufe • vor 1 Monat

Ukitaka kujua aina ya watu wanaojiita watawala na level ya fikra zao na uwezo wao, Msikilize huyu bwana Ulega!!!! Yaani una Nchi yenye kilometa za mraba 945,000. Nchi pekee yenye Tanzanite duniani, Nchi pekee yenye mbuga kubwa kuliko zote Duniani, Serengeti, Ngorongoro nk. Nchi ya tatu kwa wingi wa dhahabu duniani, Nchi yenye mlima Kilimanjaro, makaa ya mawe, almasi, Victoria gesi na kila kitu. Miaka 65 ya Uhuru una mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 182,000 lakini kwa miaka 65 hiyo mmejenga barabara 16,000 tu! Yaani ni sawa na 9%. Tena barabara zenyewe hizi zimejaa mashimo kama ubao wa kuchezea bao!!! Hakuna barabara hata moja ambayo ni nzima … Anzia Tunduma Dar, Mwanza Dar , Kigoma Dar, Babati to Singida, Tabora Manyoni Yaani ni takataka… Barabara zenyewe finyu zisizowezesha hata kupishana wala kwenda km 120 kwa saa.. Barabara haina ubora inajengwa leo kabla hata mkandarasi kuondoka site imeishajaa mashimo.. Kama Imewachukua miaka 65 kujenga barabara za lami mbovu asimilia 9 ya Barabara zilizopo… maana yake wanahitaji miaka 130 kufikisha asimilia 18 ya Barabara zilizopo… achilia Mbali maeneo ambayo hayajaingizwa kwenye kanzi data ya Barabara zilizopo na zitakazofunguliwa …. Alafu bila aibu anajitokeza kusema uongo kwamba tuna mtandao mrefu wa barabara za lami kuliko Kenya!!! Hivi hawa watu hawaoni aibu? Kenya ina mtandao wa barabara za lami kilometa 25,411 sisi 16,700 kama alivyodai… Lakini factor ya pili ukubwa wa Nchi ya Kenya ni km za mraba 582,650 sisi 945,000. Kenya hawana dhahabu kama sisi, hawana tanzanite, hawana makaa ya mawe na chuma, hawana Serengeti is ala Ngorongoro kama sisi.. Yaani kwa hiki anachokisema Ulega, tukibaki chini ya huu Utawala dhalimu wa ccm tunahitaji miaka 600 ili kumaliza mtandao wote. Hapo kuna barabara kibao za mitaa na maeneo ambayo hayajapimwa mpaka sasa ambazo hazijajumlishwa hapo! Shame on you.
John Heche37,633 Aufrufe • vor 1 Monat

Hakuna mtu huwa anajisahau haraka kama Nape… Bahati nzuri nilikua nae bungeni wakati Magufuli ameshughulika nae, alikua anatia huruma sana .. leo kasogea kwenye meza ya chakula ameshiba na anawatapikia Watanzania. Kitu kimoja ninamshukuru kwamba amesema ukweli kuwa, Nchi hii hakuna uchaguzi. Kinachonishangaza ni kwamba, inawezekanaje Watanzania wakakubali dharau, Matusi na kejeli ya kiwango hiki…
John Heche371,898 Aufrufe • vor 1 Jahr

Wakenya wanajua rais ni mtumishi wa umma sio Mfalme wala Mtume.. Wakenya wana katiba na sheria bora na wanaziheshimu, wanajua kukosoa serikali au kumkosoa rais sio kosa na sio kosa la kufanya utekwe , kuuwawa au kupotezwa. Kama kiongozi anasema wazi kwamba kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake!!! Vipi mama kijijini ambae yeye hana kamba wala urefu wa kula? Watanzania tusikubali.
John Heche23,927 Aufrufe • vor 1 Monat

Barabara ya Morogoro kutoka Dar inawezekana ndio Barabara kubwa na namba moja katika Nchi hii… Hii ni Barabara inayobeba uchumi wa Nchi hii, Magari yote kutoka Dar kwenda Mikoa ya Kaskazini, Magari yote yanayotoka Dar kwenda Mikoa ya Nyanda za juu kusini na Nje ya Nchi Zambia, Congo na kusini zaidi.. Magari yanayotoka Dar kwenda Mikoa ya kati, Dodoma, Singida Magari yanayokwenda Kanda ya ziwa na nje ya Nchi Rwanda, Burundi na Uganda.. Magari yanayokwenda Magharibi Kigoma, Tabora na hata Katavi .. Miaka 65 ni vibarabara viwili tena vimejaa mashimo tupu.. ikitokea breakdown magari yanasimama masaa manne, matatu kila siku. Sijawahi kupita hata nisikute mkwamo, watu wanateseka, uchumi unaharika na hakuna suluhu… pesa zinaibiwa na nyingine zinachezewa kuhujumu Chadema na kumnyanyasa kiongozi wetu Lissu badala ya kuhudumia wananchi.. Safari ya Morogoro - Dar km 180 inapaswa kuwa saa moja na dakika 20 tu… lakini mtu anasafiri masaa matano mpaka sita!!! Utajenga uchumi gani? Nchi gani makini itapitisha mzigo kwenye bandari ambayo hakuna hata miundombinu ya kusafirisha mizigo yao kwa mda.. Shame on you ccm.
John Heche45,240 Aufrufe • vor 2 Monaten

Mauaji ya makusudi, yaliyofanywa kwa Watanzania na watu wanaopaswa kuwalinda… Baadae wanatumia tume ya Chande kama dekio la kuwasafisha, kuficha uchafu na uozo huu hautakubalika… Dunia inajua na inafuatilia, lazima haki itendeke. Tume huru ya kuchunguza na kubaini ukweli.
John Heche20,656 Aufrufe • vor 1 Monat

Mabeberu wanatuonea wivu hii ni Barabara yetu bora kabisa… kutoka Babati to Singida.
John Heche59,646 Aufrufe • vor 3 Monaten

Tume ya Jaji Chande iliundwa kuficha uovu na kusafisha wauaji.
John Heche17,477 Aufrufe • vor 1 Monat

Asante baba Askofu, Nchi hii ni yetu sote tusikilizane , tusonge mbele
John Heche134,987 Aufrufe • vor 1 Jahr

Kwa ukatili kama huu na mauaji ambayo mmefanya kwa Watanzania leo mnasema mtaongoza? Mnataka kumuongoza Nani? Mnazungumza eti maendeleo ya nini? Kwaajili ya nani kama mmeua watanzania na kuwatesa hivi? Maji, umeme, Barabara au kitu chochote bila binadamu kuwepo vina maana gani? Hili jeshi la polisi wanafundishwa nini huko kwenye vyuo vyao? Kuwa katili? Said Mwema kwenye kitabu chake aliandika kuhusu huu ukatili, Tume ya haki jinai ya Samia imeandika kwamba hili jeshi linapaswa kufumuliwa kwasababu lina element za kikoloni, baada ya haya nani tena anaweza kuwa na imani na jeshi hili? Nani anaweza kubisha. Lazima tutabadili namna ya utendaji wa jeshi la polisi. Madaraka ya damu hayatasimama kwenye Nchi yetu.
John Heche73,656 Aufrufe • vor 6 Monaten

Ukitaka kujua hakuna Nchi Sikiliza mambo kama haya. Watu walikua wnashangaa kwanini Bashite anaendesha gari mabilioni na misafara ya kutisha. Watu walikua wanashangaa kwanini anaapa hata kudhuru au kuumiza watu aliosema “wanacheza na Urais wa mama” Ukisikia wanasema tutamlinda kwa gharama yoyote unaelewa nini? Wataua. Watadhuru kumlinda ili na yeye awalinde katika uchafu huu.. you scratch my back i scratch yours. Watu wanasema na kusikia utajiri mkubwa wa ghafla wa bwana Gerson, akiongea kwa kufoka kana kwamba Nchi ni yake.. kiburi kinatoka huku. Yaani uwanja ulikadiriwa ujengwe kwa Tsh bilioni 187 alafu mkataba ukasainiwa wa Tsh bilioni 338!!!! Alafu mzabuni alipatikana bila kushindanishwa au tenda kutangazwa!!!! Sijui Kama wengi tunaelewa maana ya hili jambo. Tenda ikitangazwa makampuni ya ujenzi yakashindana bei ingekua chini zaidi, licha ya kwamba sheria ya manunuzi inakataza kutoa tenda bila ushindani, mtu mmoja au kikundi cha watu wachache wakaamua kuipa kampuni moja hiyo kazi bila ushindani!!! Hakuna anaejua kama kweli ni kampuni au ni wao wamechukua vibarua wanawalipa per day au ni kampuni ya mmoja wao ya mfukoni. Yaani bei mara mbili ya ile iliyokadiriwa!!! Watanzania wanakufa mafuriko, hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna shule bora wala hospital! Watu wanachezea fedha za wananchi kiasi hiki!!! Morocco imejanga viwanja vya kisasa na vyenye ubora wa Kimataifa, viwanja hivyo vimetumika kwenye Afcon 2025 na vitatumika kwenye Kombe la dunia 2030. Bei ya chini kuliko hicho cha mafisadi na bora zaidi. 1.Khouribga stadium billioni 150 2.Stade Municipal de Nador & Shabiba Bilioni 200 3.Prince Moulay Abdellah Stadium USD 75 m sawa na bilioni 187. Unaweza kutaja na vingine na vingine kwa mamia. Huu ni ujambazi kwa Nchi yetu, na vijana mpo hamna kazi, ajira wala matumaini mnasema tunamuachia Mungu!!!! Ukijiari iwe shamba au hata kwenye mtandao wanakuja kuchukua fedha yako kama kodi, ukinunua gari au bodaboda kodi ni mara mbili ya kununulia.. alafu pesa inachezewa hivi.
John Heche23,303 Aufrufe • vor 2 Monaten
