
John Heche
@HecheJohn • 807,414 subscribers
Vice Chairman Chadema Tanganyika, former Member of Parliament for Tarime rural constituency, a reformer.
Shorts
Videos

Nilikuwepo bungeni wakati mwenyekiti anayasema haya.. Polepole alikuwepo na alikua Mwenezi wa ccm kama huyu kijana Kihongosi wa sasa.. alikua chini ya Magufuli na aliamini haya yatawakuta Chadema tu. Nyie mnaotumika kudhuru kuumiza na kutesa watu. Your time will come. Acheni upuuzi huo mara moja. Rais sio Mungu lazima atasemwa na atakosolewa.
John Heche35,985 views • 5 days ago

Hii ni picha ya CCTV ya watu waliokuja kunifuatilia nyumbani kwangu. Wameulizia nyumba yangu, na baadae wakaondoka bila hata kutaka kuingia au kueleza kwanini wanatafuta nyumba yangu. Tumefuatilia hiyo gari na kugundua kwamba namba za usajili inazotumia sio namba halisi.. Namba hizo T318 EQJ ni namba zilizosajiliwa kwa magari ya kulima barabara sio namba za Land Cruiser hardtop hiyo. Polisi wanapaswa kutuambia hao ni kina nani na nia yao hasa ni ipi kwangu. Hatutakubali kuishi kwa hofu kwenye Nchi yetu. Mambo ya aina hii yanaweza kuingiza Nchi kwenye hatari kubwa sana . Watanzania sisi tutafanya kazi yenu bila hofu, msikubali kuona viongozi wenu wanatishiwa.
John Heche169,105 views • 27 days ago

Tanzania ya Mwalimu Nyerere iliyotoa watu na mali kupigania uhuru wa Afrika. Tanzania iliyotoa ardhi yake kuweka vituo vya mafunzo wa wapigania Uhuru kwenye bara la Afrika. Tanzania iliyosifika kwa kupigania haki za binadamu. Leo Tanzania ndio inatajwa kwa kutoa mercenary kwenda kuvuruga chaguzi kwenye Nchi za watu wengine!!! What a shame!!
John Heche62,893 views • 10 days ago

Kila mtu asikilize simulizi hii mpaka mwisho. Kwenye Utawala huu maisha ya mtu hayana thamani yoyote tena, kwao mtu ni sawa na kuku au mbuzi tu… Nafikiri hata kuku na mbuzi mmiliki wake huwa anawathamini kuliko serikali hii inavyowathamini Watanzania. Tumesema tena na tena hakuna aliesalama kwenye Utawala kama huu. Kila siku tunasikia habari za polisi kuua raia kwenye vituo, kujichukulia sheria kupiga watu na kuwaacha na ulemavu wa kudumu, kujichukulia mali za watu ikiwemo simu na fedha.. Huu sasa ni utamaduni unaozoelekeza na inageuka kuwa tabia… Tabia ikiishaota mizizi ni ngumu mno kubadilisha.. imefikia Mpaka kwa jeshi usu kama hao wa wanyamapori. Kama umemkamata mtu, ana kosa, hajaleta shida yuko chini ya ulinzi. Kwanini ufanye haya yote? Kwanini umtese binadamu mwenzako kuliko mnyama? Unamvua nguo zote, unamlaza kwenye miba!!! Unampiga mpaka anakufa? Kwanini? Mara kadhaa watu wanasema wamelawitiwa wakiwemo wale raia wa Kenya na Uganda!!!! Hii Nchi Inakwenda wapi? Tusinyamazie uovu. BBC News Swahili @jambo_online_tv GlobalNetTVChannel @mwananchi_official Tanganyika Law Society(TLS)
John Heche68,386 views • 12 days ago
3:17
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Genge dogo linatesa mamilioni ya Watanzania, kuwajaza hofu na kuwatisha. Djumbe wa Chadema alikamatwa na watu waliokuwa na pingu akateswa na Mungu akamuokoa. Mzee Ally Kibao alishushwa kwenye gari watu wakiwa wanaona mchana kweupe. Deus Soka alipigiwa simu na askari wanaofahamika kwa majina na ushahidi wa maneno yake mwenyewe upo. Madai ya familia ya Polepole kuhusu watu waliomteka na kuacha damu nyingi zikiwa zimemwagika kwake. Mke wa Mdude anasema wazi kwamba watu waliokwenda kwake walijitambulisha kama ni polisi na wakamchukua wakaacha damu zimetapakaa kwake. Maelfu ya watu waliotekwa kufungwa vitambaa na kupewa mateso mabaya, kushinikizwa kukiri uongo au kuumizwa vibaya sana wote wanataja polisi au watu waliojitambulisha kwamba wanatoka kwenye vyombo vya dola. Leo bwana Kazungu kada wa CCM kwa kukosoa mwenendo wa chama chao, anapigwa, anafungwa macho, anadhalilishwa utu wake, anafungwa pingu kama Djumbe na wengine wengi. 1. Tunajua pingu Nchi hii ziko mikononi mwa vyombo vya dola, polisi, Magereza na vyombo vingine. 2. Tunajua vyombo vinavyoweza kushusha mtu kwenye gari na kuondoka nae mchana kweupe ni vyombo vya usalama. 3. Tunajua magari yanayotumia namba zisizo halisi, namba zinazobadilishwa kila wakati ni za serikali tena kinyume cha sharia. Wanaofanya haya mambo wajue jambo moja tu. Siku sio nyingi watalipia uovu huu, Mnaweza kulindwa leo na Utawala huu wa mauaji, lakini kesho inakuja kwa kasi.. Hawa wanaokulinda hawatakua na nguvu ya kukulinda tena. Kwenu Watanzania: sababu za wazee wetu kupigania Uhuru hazikua barabara zilikua Uhuru .. Leo mtu anapoteswa na kuambiwa asiseme na akisema atakuawawa maana yake hatuko huru tena. Tusikubali ujinga kama huu.
John Heche28,162 views • 7 days ago

“Emancipate yourselves from mental slavery None but ourselves can free our minds Have no fear for atomic energy ‘Cause none of them can stop the time How long shall they kill our prophets While we stand aside and look? Some say it’s just a part to fit We’ve got to fulfill the book” Bob Marley.
John Heche28,345 views • 7 days ago

Nimekusikia Mzee wangu. Hakuna kuogopa, tusonge mbele. Asanteni wazee wangu wa Simiyu.
John Heche58,341 views • 25 days ago

Kabla ya Uhuru kulikua na serikali ya wakoloni.. Serikali ile iliiamini kwamba ilikua halali na ilikua na kila haki kwenye Nchi yetu. Kitendo cha Mwalimu kudai Uhuru mbele ya serikali iliyoamini kwamba na yenyewe ni halali alitakiwa afunguliwe kesi ya ugaidi kama sasa serikali ya ccm inavyofungulia watu kesi za ugaidi kwa kudai uchaguzi huru na siasa za kuheshimiana. Kwahiyo gaidi namba moja kwenye Nchi hii aliapaswa kuwa Mwalimu Nyerere. Serikali hii inaua na kuteka watu, inaiba uchaguzi watu wakihoji kuhusu hilo inawafungulia kesi za ugaidi na uhaini. Hilo halitawezekana, kelele itakua kubwa kila siku Mpaka uhuru utakapopatikana. Pole sana ndugu yangu China Wa China.
John Heche21,741 views • 9 days ago

Agenda ya kufunika wizi mkubwa kwenye sketa ya mafuta.. Watanzania msikubali. Tunataka kujua kwanini Vitol ametuuzia mafuta kwa usd 260 sawa sh 689,000. Wakati huo huo anawauzia Uganda mafuta hayo hayo kwa USD 83 sawa na sh 212,000 Msumbiji usd 90 sawa na 238,500. Hawa watu wanaoitwa NAMARO na TPDC wamehusikaje kwenye huu ufisadi wa kufilisi Nchi. Huu ni uhujumu uchumi mkubwa kuwahi kutokea katika Nchi hii. Kuna zaidi ya 1.2 trilioni imeibiwa katika mafuta. Katibu mkuu wa Nishati bwana Mataragio alisema tuna mafuta ya kutumia miezi mitatu. Watanzania tusikubali huu wizi.
John Heche69,738 views • 1 month ago

Huu ni uthibitisho mwingine kwamba Nchi hii inaongozwa na dola la kipolisi (police state) kisingizio kwamba kuna mihimili mitatu ya dola ni uongo. Kitendo cha mahakama ya kiraia kuwa inasimamiwa na polisi, na kila mara polisi wanapanga utaratibu, wanapiga watu na kumamata wengine ndani ya viungavya mahakama. Chombo kilichopaswa kuwa kimbilio la wananchi pale wanaponyanyaswa na polisi, chombo ambacho kila mtu alipaswa kujiona ana haki sawa na atatendewa haki kwa mujibu wa sheria, chombo hicho kinapogeuzwa kuwa kama vituo vya polisi, watu wanapigwa, wanasukumwa, wanaonewa, wanapewa amri zisizo za kisheria Mwananchi atapata wapi haki? Polisi waliokushitaki wanapokuja kusema hata namna ha wewe kusema mahakamani!!!! Kitendo cha polisi kutupiga na kututishia ndani ya viunga vya mahakama ni kitendo cha aibu kwa muhimili wetu wa mahakama. Nitamuandikia barua Jaji mkuu sio kwasababu naamini hayajui haya, ila kuweka kumbukumbu sahihi na rasmi. Mahakama iko chini ya Jaji mkuu sio chini ya IGP.
John Heche28,661 views • 15 days ago

Katika Nchi ambayo uhusiano wa serikali na wananchi ni wa kikatiba. Uhusiano wa Mwananchi kama muajiri na serikali kama muajiriwa huwezi kuona upuuzi kama huu. Nchi hii wananachi wanachukuliwa kama watumwa na watawala kama watwana au wamiliki wa watumwa. Nimeona utetezi wa jeshi la polisi kwenye upuuzi huu, inathibitisha kiwango cha dharau walichonacho hawa watu dhidi ya raia. Mwananchi huyu masikini amelima alizeti imekaa shambani miezi minne, mbegu amenunua mwenyewe, pengine kwa jembe la mkono na mvua kidogo akavuna. Hapo ilipo hiyo alizeti kuanzia mbegu imelipiwa kodi, akivuna tu kodi… huko anakopeleka kuna Mageti ya mazao kila kona.. Baada ya kuuza akinunua sukari kuna kodi , kiberiti, Sabuni na chumvi vyote kodi za kulipa askari huyo mshahara. Hata kama huyo bwana amekosea: Sheria gani inampa mamlaka askari kuchukua mzigo wake na kutupa mtaroni? PGO namba ngapi inamwambia askari mtu akifanya kosa kama hilo unaharibu mali yake kwa kuirusha kwenye mtaro unaopitisha maji machafu tena mzigo wa chakula? Kwanini usimkamate na kufuata utaratibu wa kisheria? Kwa utetezi huu wa polisi kwa askari hao ni uthibitisho wa namna serikali hii ya kidkteta inavyowaona wananchi… Haishangazi kama waliua mamia kwa maelfu ya watu na wanaona ni kawaida itakua kutupa mzigo mtaroni? Watanzania mnapaswa kubadilika wale mnaofikiri hayawahusu kwasababu nyie sio huyo bwana, watawafikia kwa njia nyingine. Kama alivyowahi kusema Martin Luther king kwa watu weusi kule Marekani. “We must learn to live together as brothers or perish together as fools“ Lazima tujifunze kuishi pamoja kama ndugu, kwa kuteteana, kusaidia na kulindana au tuangamie pamoja kama wajinga.
John Heche35,167 views • 20 days ago

Vitol yuko na nani? Nani wamempa tenda ambayo Watanzania wanauziwa mafuta kwa usd 200-260 wakati Uganda anauziwa usd 83 na Msumbiji anauziwa usd 90. Hawa Namaro waliosajiliwa Dubai mwaka 2023 ni kina nani? Wana uhusiano gani na wizi huu mkubwa unaoumiza Watanzania. Vyombo vya habari Tanzania kwanini hamfuatilii na kuandika huu ujambazi unaongamiza Nchi kwenye wizi wa mafuta.. TPDC kwanini hawakutoa tenda shindanishi katika suala kubwa kama hili la mafuta.
John Heche46,127 views • 1 month ago

We must learn to live together as brothers or we perish together as fools. Binadamu yeyote ambae hawezi kukemea vitendo vya kihuni vya watu kutekwa na kupotezwa hafai kuwa binadamu.. Eneo la Tarime watu zaidi ya 25 wametekwa na kupoteza ndani ya kipindi cha mwaka moja tu. Anaetaka tunyamazie uhuni kama huu atafute kazi nyingi e ya kufanya. Tunataka kujua ndugu zetu walipo.
John Heche21,997 views • 18 days ago

Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara.. Maneno muhimu kutoka kwako: Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari? Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika. Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika. Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko? 1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar? 2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu, Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika? Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara? Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar? Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya…. Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu? Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao. Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
John Heche58,494 views • 2 months ago

Huyu Bwana Kombo anazidi kuthibitisha kwamba waliua watu bila sababu ya msingi… Chande alisema kulikua na training na silaha , kombo anasema mawe!!! anasema ukimlembea jiwe polisi, anatakiwa kukupiga risasi.. Je Bwana Kombo yule mama Mtanganyika pale Arusha, Video yake Inaonekana anakimbia , akapigwa risasi mgongoni, alilemba jiwe kwa nani? Watu wameuwawa wakiwa nje ya Mageti ya nyumba zao, wengine kwenye sebule , kuna vijana Mwanza mmeaua wakiwa wanaangali Mpira… Unasema tumeheal!!!! Hamtaweza kufukia mauaji ya kutisha mliyofanya ili mjitangaze kwenye uchaguzi ambao haukuwepo… wote mnakula pesa za damu na dunia haitakaa kimya.
John Heche67,504 views • 3 months ago

Internet never forgets, hawa wajinga wote wanaonuka damu za watu… iko siku watajibu .
John Heche44,327 views • 2 months ago