
Hussein M Bashe
@HusseinBashe • 563,096 subscribers
Former Minister of Agriculture 🇹🇿 | MP - Nzega Urban Constituency | Farmer | Politician #TanzaniaKwanza
Shorts
Videos

Nimetoa Kauli yangu kuhusu Bei elekezi ya sukari kwa makampuni ya uzalishaji wa sukari nchi. Ni nia yetu ya dhati Kama serikali inayoongozwa na kanuni za kiuchumi kuyalinda makampuni ya uzalishaji sukari na kuwalinda walaji (watanzania). Tunao mfumo rafiki na thabiti wa upangaji bei na tumekuwa na stability ya bei ya sukari hadi mwanzoni mwa mwezi Desemba kabla ya kutokea changamoto za mvua. Nimewaeleza wazi kuwa bei ya sukari haiwezi kupangwa kwa gharama ya Mlaji (Mtanzania) na kama wana changamoto yoyote milango ya Wizara iko wazi waje tujadiliane na waache mara moja tabia kuzunguka na kutafuta njia za mkato mkato (lobbing). Wazalishaji wa sukari wanatambua tumekuwa tukifanya majadiliano ya bei, kama tunavyofanya majadiliano ya kuwapa misamaha ya kikodi au makadirio ya uzalishaji na uhitaji wa sukari nchini. Msimamo wa serikali wa bei elekezi ya sukari unatumbua uwepo wa nafuu za kikodi wanazopatiwa makampuni ya Sukari nchini. Tutaendelea kuilinda sekta ndogo ya Sukari kwa kuwa ni muhimu katika uchumi wetu na nasisitiza anaeona kuna jambo la kujadili basi afike wizarani tutajadiliana kushauriana.
Hussein M Bashe165,112 görüntüleme • 2 yıl önce

Taarifa: Kutokana na ukame unaoikumba nchi ya Zambia, nchi hiyo imeingia makubaliano na Tanzania kununua tani 650,000 za mahindi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi milioni saba wa taifa hilo. Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane na utaiingizia Tanzania dola milioni 250 sawa na Sh650 bilioni. Mahindi hayo yatakayosafirishwa kwenda Zambia yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo kwa kituo cha Songwe mahindi tani 55,000, Makambako tani 75,000, Sumbawanga tani 250,000 na Songea tani 270,000. Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NFRA Dk Andrew Komba pamoja na Mratibu wa Maafa kitaifa nchini Zambia Dk Gabriel Pollen, wakishuhudiwa na mimi kama Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo Zambia Reuben Phiri.
Hussein M Bashe126,725 görüntüleme • 1 yıl önce

Salaam Ndugu Zangu, Ningependa kutoa ufafanuzi wa kauli yangu iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 22.02.2024. Kama Waziri wa Kilimo, nilitoa maelezo juu ya hali ya upungufu wa Sukari nchini, na muda wa usambazaji tunaotarajia wa shehena inayofuata ya sukari. Nilisisitiza kuwa kutokana na usambazaji huu na hatua tulizochukua, tutarajie hadi kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan hali itakua nzuri. Rejeo hili lilikusudiwa kuwa kiashiria cha MUDA kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha KIDINI. Mara kadhaa nimesisitiza kwa kutaja vipindi vyote viwili Kwaresma na Ramadhani vina tukabili hapo mbeleni na kuwa tunajitahidi kama Serikali na azma yetu ya kutaka kutatua hii changamoto kabla ya hivi vipindi kufika na ndio maana tulianza kutoa vibali tangu mwezi wa 12, 2023. Tuendelee kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo na usalama wa chakula nchini.
Hussein M Bashe140,348 görüntüleme • 2 yıl önce

Mwaka 2019/2020, tulikutana na mkulima Iringa Vijijini jina lake David Alexander - aliyekuwa ameanzisha kilimo cha tunda la apple lakini alikwama kutokana na ukosefu wa umeme. Nilimfikishia Waziri wa Nishati changamoto hiyo na gharama za kupeleka umeme zilipunguzwa kutoka milioni 300 hadi milioni 90, kupitia mpango wa REA. Kwa ushirikiano na viongozi wa mikoa na wilaya, tulimsaidia kupata aina bora za apple na kisha kugharamia usambazaji wa miche. Leo, ameanzisha cluster inayozalisha zaidi ya tani 100 kwa msimu, na kilimo hicho sasa kimeenea Njombe, Dodoma, Kagera, na Mwanza. Ameanzisha pia bidhaa kama juisi ya apple na guide apples. Haya ni matokeo ya Serikali kuamua kuamini ndoto ya mkulima mmoja na kuwekeza katika ndoto yenye matumaini makubwa. Tunaamini Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa apple barani Afrika.
Hussein M Bashe59,801 görüntüleme • 1 yıl önce

📍Tazengwa - Nzega Kila nikiwa Nzega hapa ndio sehemu ambayo hunipa tumaini langu la kesho. Niliwahi kuwapa story humu kuwa Mwaka 1993 nikiwa kidato cha 3 Marehemu Mzee MWANIKOLONGO aliniuzia ekari 6 na ndipo nililima shamba langu la kwanza la mpunga kwa mbegu nilizopewa na Marehemu Mzee Nduju na hapa ndipo nilijenga zizi langu la kwanza la MASANZU na kuweka Ng’ombe za kwanza 6 za kufuga nilizonunua Mnada wa Ushirika nikiwa na kaka yangu Marehem Vumilia Ng’hwani. Huyu ni MIMI na haya ni Maisha yangu ya kila siku nikiwa Nzega hapa lazima nifyeke nikiwa sipo Nzega lazima nipige simu kujua wameamka vipi. Allah kamuelezea Ng’ombe katika Qur-aan kaelezea ardhi na manufaa yake. Jumaa Mubaraak Surah An-Nahl (16:5-7) “And the cattle He has created for you; in them is warmth and [numerous] benefits, and from them you eat.” (Surah An-Nahl 16:5) Surah Al-Mu’minun (23:21) “And indeed, for you in grazing livestock is a lesson. We give you drink from what is in their bellies…” Ya Allah Barik 🙏🏾
Hussein M Bashe35,030 görüntüleme • 8 ay önce

Kilimo kimenoga na Vijana wanakamata fursa. Nilifurahi sana kukutana na huyu Kijana Jacob wakati napita kwenye Ziara Mkoani Ruvuma. Niliona shamba lake nikashawishika kusimama na kumpongeza kwa kazi nzuri. #Agenda1030 Kilimo ni Fursa. Kilimo ni biashara. Kongole kwa vijana wote waliojikita kwenye Kilimo, popote ulipo, Kongole Sana. #Agenda1030
Hussein M Bashe63,177 görüntüleme • 1 yıl önce

Hii ndio hali ambayo wafanyabiashara wetu wako nayo baada ya Serikali ya Malawi kuzuia mazao kuingia nchini kwao. Kuvumilia hili kama Serikali inayohangaika na sekta ya kilimo ni ngumu. Nafahamu kumekua na maoni mbali mbali lakini naomba niendelee kusisitiza kuwa hadi Jumatano hii inayokuja, kama Serikali za Malawi na Afrika Kusini hazitobadilisha maamuzi na kutufungulia masoko basi na sisi Tanzania tutaendelea na hatua za kusitisha usafirshaji na biashara za bidhaa za kilimo na nchi hizi 2.
Hussein M Bashe42,595 görüntüleme • 1 yıl önce

Tarehe 28.04.2025 tunaenda kuweka historia na kuishi msemo wa ‘from words to reality’. Nilianza kuongelea Ushirika miaka 6 iiliyopita na miaka 3 iliyopita rasmi nilitangaza azma ya Wizara ya Kilimo kusimamia uanzishwaji wa Benki ya ya Kitaifa ya Ushirika. Miaka 3 baadae, Mhe Rais Dk. Samia Suluhu atakua mgeni rasmi na kuzindua Benki hii. Safari ya Coop Bank Tanzania imekuwa ya kipeke, kutoka kuwa ndoto hadi kuwa taasisi ya kifedha inayomilikiwa na wanachama wa ushirika kwa % kubwa. Tungeweza kuishia njiani, lakini Serikali ya Awamu ya 6 iliona umuhimu wa kuwa na benki hii kama moja ya tatuzi la upatikanaji wa mikopo ya fedha na pembejeo. Uwekezaji huu unaenda kuchangia kuleta yale mapinduzi tuliyodhamiria kwenye #Agenda1030 Kazi na Utu #TunasongaMbele #SafariYaCoopBank #UzinduziBenkiYaUshirika #UshirikaNiNguvu #UzinduziCoopBank #SamiaSuluhu #Dodoma #BenkiYaUshirika
Hussein M Bashe28,667 görüntüleme • 1 yıl önce

A modern Research Centre IITA , kituo hichi ni cha kisasa cha kufanya utafiti na miaka michache ijayo tutakua na vituo vya aina hii kikanda ,Rehabilitation ya Mlingano inaendelea ,na karibuni tutakua na Horti tengeru tissue culture investment and Mar Bioscience Lab Mdogo mdogo tunabadilisha kilimo nchini na tuifa litafika tunakotamani, tunapiga hatua katika Agenda 10/30 Inshallah.
Hussein M Bashe46,253 görüntüleme • 2 yıl önce

Mwaka 2019 mwezi wa kumi, alikuja ofisini kwangu Dada Fatma Mwasa ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Pamoja na Mzee Mwilima, kunielezea kukwama kwao kwa mradi waliokua wameanza kuutekeleza katika mkoa wa Kigoma. Mradi huo ulihusisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata chikichi na kuweza kupata Refined Palm Oil. Baada ya majadiliano ya muda mrefu na kuielezea Serikali juu ya changamoto waliyokuwa wanakabiliana nayo, Wizara ya Kilimo ilifanya jitihada ya kuiandikia Benki ya Kilimo Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), Leo ni miaka karibu minne, mradi huo ninashukuru sasa umekamilika na sasa umeanza uzalishaji wa mafuta ya kula ya mchikichi kwa maana ya Refined Palm Oil. Kiwanda hicho kimepata ithibati za ISO na TBS, na leo hii ndio kiwanda pekee Tanzania ambacho kinanunua chikichi ya mkulima, kinachakata na kuzalisha Crude Oil na mwisho kinafanya Refinery na kupack. Hivi sasa wameanza packaging ya lita 20 kwa lita 10, na brand yao inaitwa Wese na imeshaanza kuuza Kigoma. Wanakabiliwa na changamoto ya kuanzisha kituo cha utafiti, Serikai imeamua kupitia kituo chetu cha Kihinga watasaidiana kwenye suala la utafiti na uzalishaji wa miche. Wameomba ardhi kwa ajili ya kuwa na shamba la Serikali na kuanzisha Out-Growing scheme, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Umwagiliaji - NIRC tutashirikiana nao katika kujenga Out-growing scheme. Wataalamu wa Wizara ya Kilimo watakwenda Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa Contract Farming yaani kulima kwa mkataba na wakulima wa mkoa wa Kigoma wanaozalisha chikichi ili kiwanda hicho kiweze kupata malighafi ya mwaka mzima. Kwetu kama Taifa hii ilikua ni safari ya zaidi ya miaka minne au mitano, leo tumeanza kuzalisha chikichi wenyewe ndani ya nchi hii. Hivi karibuni vile vile tutazindua kiwanda kingine katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Kyela. Nashukuru benki za CRDB na TADB kwa kusupport mradi huu. Kiwanda hiki hata mkopo waliokopa benki wanalipa vizuri. Tunashukuru Mungu this is a first trial kwa nchi yetu, Ni Hatua inatupa mafundisho makubwa kwenye uwekezaji wa eneo hili. Kazi Iendelee
Hussein M Bashe37,785 görüntüleme • 1 yıl önce

Salaam Ndugu zangu. Nafarijika kuwataarifu sukari imeanza kuingia mtaani na LEO sukari iliyoletwa na kampunj ya KILOMBERO SUGAR ambaye ni mmoja ya ya wazalishaji nchini imeanza kusambazwa kama anavyoeleza Bwana Fimbo Butalla hapa,Sales manager wa Kilombero Sugar Company. Nafahamu changamoto iliyopo ya bei bado ipo na kuna maeneo wafanyabiashara hawafuati bei elekezi. Wapo tulio wakamata na baadhi tumeanza mchakato wa kuwafutia uwakala. Tutaipitia upya sheria na mfumo mzima wa uuzaji na uzalishaj wa sukari toka kiwandani mpaka kwa mlaji na hivi sasa tumewataka wazalishaji kuhakikisha wanafungua Depot mikoani wao wenyewe na kuondoa UHODHI wa Distributor wachache Tutaipitia sheria upya ya uzalishaji wa sukari ili kuweka mazingira BORA ya kuwalinda walaji na wazalishaji kwa pamoja na ushindani ulo wahaki kwa WOTE . Niwahakikishie hali hii haitajirudia TENA hivi sasa tunapitia mfumo wote wa uzalishaji wa kisheria na kibiashara ili kumlinda mlaji. Tunawajibika kulinda Mzalishaji na pia kumlinda MLAJI na nimeziomba mamlaka za mikoa kufuatilia hili na nimeagiza kila kampuni itangaze mawakala wake kwenye Magazeti ili Umma upate kuwafahamu. Naendelea kuwaomba Watanzania utulivu, Serikali imechukua hatua na Bodi ya sukari itaendelea kusimamia mchakato huu ili kudhibiti wanaojinufaisha na Upungufu huu. Tutaendelea kutoa taarifa zaidi. Sekta hii kisheria ina mfumo wa Uhodhi ambao tutaupitia upya bila kuathiri Ajira za watanzania Ninawashukuru TPA na TRA kwa ushirikiano na kutoa pruority kwa meli zote . Ninaheshimu mawazo ushauri na mijadala inayoendelea kwa wananchi kwenye swala hili nawashukuruni sana
Hussein M Bashe39,941 görüntüleme • 2 yıl önce

Wengi wanafahamu zaidi kipengele kimoja cha Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT-YIA) OfficialBBTYIA maarufu kama Block Farming, yaani Mashamba makubwa. Hata hivyo kuna miradi mingine ndani ya programu hii ikiwemo Utoaji wa mikopo ya riba nafuu (4.5%) - BBT Financing kwa vijana wenye biashara/miradi kwenye mnyororo wa thamani wa Kilimo. Kwa Mwaka wa Budget 2023/2024 kupitia Mfuko wa Pembejeo, Serikali ya Awamu ya 6 Imetoa Mikopo yenye riba nafuu (4.5%) yenye thamani ya Shilingi 950,094,520 kwa vijana 118. Programu ya OfficialBBTYIA inalenga kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo. Miradi mingine ya Programu hii ni pamoja na Mradi wa visima kwa wakulima wadogo (boreholes for small holder’s farmer) na BBT – Ugani (BBT – Agricultural Extension Enterpreneurship Scheme) 2024/2025 ni #BajetiYaWakulima #Agenda1030 #KilimoNiBiashara
Hussein M Bashe29,779 görüntüleme • 2 yıl önce

📍 Kigoma Tumekabidhi kwa Mkandarasi mradi wa umwagiliaji wa ukubwa wa Ekari 7500 na Bwawa katika Bonde la LUICHE Kigoma. Mradi huu umekuwepo kwenye mipango ya Serikali kwa muda mrefu hatimae sasa umeanza kutekelezwa. Mradi huu utahusisha ujenzi wa Barabara ya urefu wa 4km kufika shambani lakini pia utahusisha ujenzi wa Barabara za ndani ya mashamba ili kuruhusu mazao ya wakulima kutoka kirahisi Huu mradi utakua na Nyumba pia ya Afisa kilimo na utahusisha pia ujenzi wa Ghala la tani elfu 4 na kiwanda cha kukoboa Mpunga Mradi mzima utagharimu zaidi ya bilioni 60 na ni mmoja kati ya miradi mikubwa katika mkoa wa Kigoma. Kazi Iendelee #Agenda1030
Hussein M Bashe22,877 görüntüleme • 1 yıl önce

Miaka minne iliyopita tulizalisha tani 30,000 tu za mbegu hapa nchini. Leo kupitia Wakala wa Mbegu Agricultural seed agency tunazalisha zaidi ya tani 60,000 mara mbili ya hapo awali. Kupitia uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ilitoa mashamba yake kwa mikataba kwa makampuni ya Kitanzania kuzalisha mbegu bora, huku ikihakikisha soko la uhakika kupitia mikataba ya kusambaza mbegu kwa wakulima. Leo, zaidi ya 60% ya mashamba yetu yanatumiwa na sekta binafsi. Tuna makampuni 23 yanayozalisha mbegu kwenye mashamba ya Serikali na kati yao, yapo yanayoendeshwa na vijana chini ya miaka 30. Tunajenga sekta binafsi imara kwa vitendo. Ahsanteni sana kwa kushiriki kwenye safari hii. Tunasonga Mbele.
Hussein M Bashe15,427 görüntüleme • 1 yıl önce