Martin Maranja Masese's banner
Martin Maranja Masese's profile picture

Martin Maranja Masese

@IAMartin_609,637 subscribers

MMM | Public Spirited | Sperm That Won The Race | Think Deep, Don’t Sink | Cogito, ergo Sum | Patria o Muerte, Venceremos |

Shorts

Kama hatuwezi kupambana na nyuki tu, tumejifungia ndani ya gari tunarekodi, tunaweza kupambana na watekaji wenye bunduki? Tunaweza kupiga na kulinda kura? Nimesikitika sana. Huyo mwanamke anaweza kuuwawa na nyuki wanaume wanarekodi tu.

310,021 views

Jana usiku saa nane, nimepata taarifa kutoka kwa watu walikuwepo Boardrom Bar, Sinza Mapambano, Dar es Salaam askari wa jeshi la polisi wamevamia na kuanza kukamata wanawake wanaojiuza Katika ubishani na walinzi wa Boardroom Bar, polisi wakafyatua risasi ambayo ilimpiga kichwani mlinzi mmoja wa Boardroom na kumuua. Hadi sasa hatujasikia taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi Katika video hizo, unamuona askari mmoja ameingia hadi ndani ya Boardroom ameshika bunduki akilenga wateja. Ni jambo la kusikitisha sana kuona jeshi la polisi likihangaika na nyege za watanzania NB; yeyote ambaye anazo taarifa kamili kuhusu tukio hili, atujulishe. Inawezekana kabisa wamiliki wa Boardroom wakataka jambo limalizike kimya kimya, lakini LAZIMA haki za huyo mlinzi zipatikane.

268,832 views

Pasta KINYAMBE fyuzi zimeharibika.

Pasta KINYAMBE fyuzi zimeharibika.

184,012 views

Baada ya msafara wa Makamu Mwenyekiti John Heche kusimamishwa eneo la Salender Bridge, Dar es Salaam akielekea Mahakama ya Kisutu, polisi walimtaka waelekee kituo cha polisi - Oysterbay. Katika video ya pili anaonekana John Heche akiwa amesukumwa na kuanguka chini.

119,765 views

Usiku wa kuamkia leo, Jumanne 13.05.2025 watu wasiojulikana wamemwaga sumu (bado haijafahamika) katika Ofisi za CHADEMA - Kanda ya Nyasa. Ofisi hii ya kanda inahudumia mikoa mitano ndani ya chama. Mkoa wa Mbeya, Mkoa wa Njombe, Mkoa wa Songwe, Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Iringa. Ofisi za CHADEMA - Kanda ya Nyasa (makutano ya watu kukusanyika kila siku - kupika chakula na kuanza kumtafuta Mdude Mpaluka Nyagali). Sumu hiyo ambayo imemwagwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa, inapalia, inaumiza pua, inaumiza kichwa, inaumiza macho na inaumiza koo. OCD - Mbeya pamoja na timu yake wamefika na kuchukua sampuli. Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji - Mbeya wamesafisha na kuondoa sumu hiyo. MaCCM yamefikia hatua hatari ya kutumia sumu kushambulia ofisi za CHADEMA. Hivi ni vitendo vya kigaidi. MaCCM yamepagawa sana.

68,801 views

Kwa leo, acha nisiongee chochote. 😇

Kwa leo, acha nisiongee chochote. 😇

85,196 views

Wakati waumini wa kanisa la Glory of Christ Church - Ufufuo na uzima linaloongozwa na @bishopgwajima lililopo Ubungo, Dar es Salaam wakiendelea kuimba wimbo “Tanzania nakupenda kwa moyo wote” Jeshi la Polisi limeendelea kuongeza nguvu kuwadhibiti waumini hao… ni saa nane usiku.

56,592 views

EZEKIA DIBOGO WENJE, baada ya sarakasi nyingi za kuhusishwa na veggies, hatimaye amejiunga na mbogamboga leo huko Chato.

37,982 views

Mzee Stephen Masato Wasira, CCM hamkudai uhuru wa Tanganyika pekee yenu. Wapo watu wengine wengi sana ambao walidai uhuru wakiwa TANU tangu TAA na ASP hadi wakiwa CCM. Kufikia 09.12.1961 Tanganyika ilikuwa na vyama vinne (4) vya siasa. Walikuwepo TANU, AMNUT, walikuwepo ANC na UTP ambayo ilianzishwa kabla ya TANU. African National Congress (ANC) iliongozwa na Alhaji Zuberi Mwinshehe Manga Mtemvu. United Tanganyika Party (UTP) iliongozwa na Edward F. Twinning. Kabla ya uhuru Z’bar walikuwepo; Z’bar Nationalist Party (ZNP), Afro-Shirazi Party (ASP), Zanzibar & Pemba People’s Party (ZPPP). Baadae Umma Party. Tanganyika na Zanzibar huru zilizaliwa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Uhuru wa Tanganyika haukuwa kazi ya TANU na ASP tu. Msijikweze. Katika harakati hizo, walikuwepo raia wenye asili ya India; Krishna Beldev, Fazelabbas Syelmanji Khambalia, Mukthar Ahmed Ayaz, Mohammed Hussein. Pia walikuwepo raia wenye asili ya kitasha; mfano, David Lead akiwa United Tanganyika Party (UTP). Pia, Roderick Neville. Walishiriki uchaguzi wa 1958. Wapo waliouwawa kwa kutofautiana na watawala. Wapo waliopotezwa. Wapo waliofungwa. Wengine walichoka na walianzisha vyama vingine vya siasa. Ni mwendawazimu pekee anaweza kutuaminisha kwamba kazi ya kutafuta uhuru wa Tanganyika ilifanywa na TANU pekee yao. Haikuwa kazi TANU pekee. Uhuru wa Tanganyika siyo mali ya CCM. Uhuru wa Tanganyika siyo hisani ya wafuasi na viongozi wa mbogamboga. Uhuru wetu siyo zawadi kutoka CCM. Uhuru wa Tanganyika ni mali yetu sote. Ipo siku MaCCM mtaondoka madarakani kama alivyoondoka FIRAUNI. MaCCM muishi mkifahamu hilo. Panakaribia. MMM, Martin Maranja Masese.

66,402 views

Viongozi na wanachama wa CHADEMA waliokamatwa katika Mahakama ya Kisutu na kupelekwa katika msitu wa Mabwepande wamepigwa na kuumizwa sana. Wengine wameteguka na kuvunjika viungo vya mwili. Kosa lao nini? Kufika mahakamani kusikiliza kesi ya Mwenyekiti Tundu Lissu.

51,172 views

Good morning Tanzania. Live & enjoy your life when alive … When gone the world moves on.

71,377 views

Mwenyekiti Tundu Antiphas Lissu amewasili ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. #TunduLissuSioMhaini

43,425 views

Hali halisi muda huu Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima lililopo Ubungo, Dar es Salaam. Polisi wamezidi kuongezeka na waumini wa kanisa hilo wanazidi kupambania haki yao ya kuabudu ambayo imeporwa baada ya Serikali kufuta usajili wa kanisa hilo

42,184 views

VERONICA MWANJALA, amesafirisha ndizi mbivu tenga 30 za Sh2,500,000. Bandarini Zanzibar, akakamatwa, akaambiwa marufuku kuingiza chakula kutoka Tanganyika. Akapigwa faini Sh50,000. Ndizi zikataifishwa, wakapelekewa wafungwa kwa amri ya Waziri wa Kilimo Z'bar Shamata Shaame Khamis

100,755 views

RCO-Mbeya na polisi wamefika nyumbani kwa Mdude Nyagali kuchukua sampuli ya damu iliyomwagika na kufanya uchunguzi. Moyo wangu umejaa hofu. Sioni mwisho mzuri katika habari hii. Hali ilivyo hadi hapo watasema wao hawahusiki kumvamia na kumteka Mdude. Hii habari inaumiza sana.

Sensitive content

42,621 views

CHADEMA tumemaliza uchaguzi katika ngazi ya mabaraza yote ya ndani ya chama. BAZECHA, BAWACHA na BAVICHA. Chaguzi zote zimekuwa mubashara (LIVE) hatua kwa hatua huko YouTube. Tunaelekea katika Mkutano Mkuu (bado siku mbili) ambao pia utakuwa LIVE katika luninga. Sisi ni CHADEMA.

45,927 views

Afisa Usalama uliyekimbia Tanzania kwenda Scotland tangu mwaka 2008 (kwa makosa yako mengi uliyofanya kwenye idara ya usalama), njia pekee ya kurudi nyumbani ni kuhakikisha CHADEMA tumeingia IKULU na kuyaondoa MaCCM. Shambulio lako lolote kwa CHADEMA ni kuhalalisha CCM kuendelea kubaki madarakani na hiyo maana yake utaendelea kuwa mkimbizi nchini Scotland, ukiishi kwa upweke. Ukiishambulia CHADEMA, unashambuliw uhuru wako. Elewa. CHADEMA wameelekeza nguvu zao miaka 32 ya harakati za kisiasa katika mapambano dhidi ya Serikali katili ya CCM inayotumia vyombo vyote vya DOLA kuzuia kazi za kisiasa za CHADEMA. Huwezi kuwapuuza na kusema ni failure. CHADEMA katika mazingira magumu, wameweza kusimamisha wagombea wao katika uchaguzi. Wameporqa uchaguzi. Kamati Kuu imeketi, imetoka na maazimio unasema maazimio hayawezi kuing’oa CCM. Sawa. BUNDUKI? Wapiganaji ndiyo ninyi ambao mmekimbilia nje ya nchi, mnaishi mkikunja nne, kazi yenu kubwa imebaki ni kukosoa CHADEMA katika kila jambo wanafanya. Hutaki maazimio hayo, unataka maazimio ya kuingia msituni? Utaweza kuwa MUASI? Kama huwezi na unang’ang’ania kubaki ULAYA, waache CHADEMA wafanye mambo yao kwa namna ambayo wao wanaona inawafaa. Kusema strategies zao (CHADEMA) ni failure, strategies zako ni zipi? Umeleta mpango kazi ukakataliwa? CHADEMA wanahitaji maafisa usalama (kama wewe) mjiunge nao, ili harakati za kuiondoa CCM madarakani zifanikiwe. Bahati mbaya sana, unechagua kuwa mkimbizi badala ya kufanya kazi takatifu ya kupambana na MaCCM. Sijakufananisha na Abu Mohammad al-Jolani (de facto leader of Syria).. nimesema Abu Mohammad al-Jolani amerejea Syria kumuondoa Bashar al-Assad. Na wewe ni wakati wa kurejea utusaidie kupambana na kuyaondoa MaCCM. Halafu, kwanini kujadili maoni yako utafsiri ni kukuziba mdomo? Maoni yako (unayoita ushauri) hayakutakiwa kujadiliwa? Unao uhuru wa kutoa maoni lakini usizuie wengine kutoa maoni katika maoni yako. Usitafute huruma. NB; Hizo porojo nyingine hazina afya kuzijadili… nitakusubiri.

44,254 views

Tundu Lissu Show; The Legal Titan. Karibuni katika ulingo wa haki, mahali herufi za sheria zinakutana na ujasiri wa mwanasheria nguli, Tundu A.M Lissu. Mahakama Kuu ya Tanzania sasa ni maabara. Leo Mahakama Kuu, anga limebadilika rangi. Ni siku ya kukatwa kwa mzizi wa fitina, hoja hazitolewi kwa sauti tu, bali kwa uzito wa vifungu vilivyopigwa msasa! TAL ameingia amejihami kwa “mabomu” ya vifungu vya Katiba na sheria. Tunaelewa, kila neno linalotoka kwake ni kama risasi ya kisheria inayolenga kiini cha hoja... Jaji na jopo lake, uso wa mbuzi, wakichuja pumba na mchele kalamu zikicheza dansi kwenye karatasi. Umati umetulia, macho yakitazama, masikio yakisikiliza. TAL anacheza na vifungu vya sheria. Anaponyanyuka, ni kama maktaba ya sheria imeamua kupiga hatua mbele ya jopo la majaji. Mashahidi wa mchongo, wanatetemeka. Ni kama daktari anayepasua jipu la kisheria bila ganzi. Hata akiwa mbele ya pazia la mahakama, haachi hatakati—anageuza chumba cha mahakama darasa la uraia. Sheria siyo mchezo wa kuigiza, lakini leo Mahakama Kuu, tunapata ‘Live Performance’ ambayo hata Hollywood wangesubiri kwanza, waone script zinavyopangwa. Huu ni mtanange unaobebwa na ushahidi, kanuni, na precedents…., Je, ushahidi wa mchongo wa Jamhuri utapenya katika TUNDU la hoja za LISSU? NEVER!

13,627 views

Awamu ya tano ufisadi wa TZS 1.5 trilioni Awamu ya sita ufisadi wa TZS 1.14 trilioni Serikali imeleta tozo wananchi wamelipa Pesa zilikusanywa TRA lakini hazionekani Kwamba zilihamishiwa wizara ya fedha Nani ametafuna pesa zetu za tozo? UFISADI. Kuna siku tutapigwa mnada

30,394 views

Kwamba mwekezaji bandarini hajapatikana? Tukubaliane, DP WORLD ni mnunuzi siyo mwekezaji? Bunge lilipitisha (bilateral contract) bungeni, mkataba umesainiwa na serikali kuhusu bandari na kwamba DPW watapewa milele Msemaji wa serikali anasema mwekezaji hajapatikana. Mnatuonaje?

47,601 views

Videos

IAMartin_'s profile picture

Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa. Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe. Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo. Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake. Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka. Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa. Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu. Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA? Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai. Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu. Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii. Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana. Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania? Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM. Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye. Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo. Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu. Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”

Martin Maranja Masese

70,947 views • 1 month ago

IAMartin_'s profile picture

Nafikiri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inahitaji kufutwa haraka na kutengenezwa ofisi mpya kwa mujibu wa sheria. Inawezekana vipi wakashindwa kutafsiri amri halali ya Mahakama (Drawn Order)? CHADEMA tulifungua shauri la nyongeza (MISCELLANEOUS CAUSE No. 12812 la 2026) katika Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sub-Registry ya Manyara iliyopo Babati. Waombaji (Applicants) ni Katibu Mkuu CHADEMA na Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA, huku wajibu maombi (Respondents) wakiwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. CHADEMA tulifungua maombi tukiomba: 1. Mahakama itoe amri ya muda (interim order) kumzuia MSAJILI kuchukua hatua yoyote hasi dhidi ya CHADEMA tukisubiri kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa maombi ya kibali cha kufungua maombi ya amri za mahakama (prerogative orders) 2. Amri nyingine yoyote au unafuu ambao Mahakama ya Haki inaweza kuona ni haki na usawa kutoa. Maombi haya yalikwenda kwa ajili ya uamuzi wa upande mmoja (ex-parte ruling) mbele ya JAJI I.C. MUGETA, ambapo mawakili wetu—Mpale Mpoki, Nyaronyo Kicheere, na Hekima Mwasipu… Walisikilizwa pekee yao bila uwepo wa wajibu maombi. Sheria inaruhusu utaratibu huu wa dharura (extreme urgency) ili kuepusha hatari ya madhara yasiyorekebishika (risk of irreparable injury). Maombi ya CHADEMA yalikubaliwa, na tarehe 25 Mei, 2026, Mahakama ilitoa amri zifuatazo zilizotiwa saini na Jaji I.C Mugeta na kuwekwa Muhuri halali: (i) Amri ya muda ya kuzuia (interim injunction) inayomzuia Msajili kuchukua hatua yoyote hasi (adverse action) dhidi ya Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kama vile kufuta usajili wa chama au kusimamisha shughuli zake. (ii) Hakuna amri yoyote kuhusu gharama za kesi. Amri hii inafanya kazi kama breki ya dharura na ngao ya kisheria. Lengo lake si kumaliza kesi, bali ni kugandisha mambo yalivyo kwa muda ili kulinda hali halisi (status quo). MSAJILI haelewi haya mambo? Hivyo, chini ya amri hizo, CHADEMA inaendelea kuwa na haki na uhalali wa kufanya shughuli zake zote mpaka mahakama itakapoamua kama itatupa kibali cha kufungua maombi ya prerogative orders. Katika maombi ya msingi, CHADEMA tunaomba amri ya Certiorari (neno la Kilatini linalomaanisha “Kujulishwa” au “Kuthibitishiwa”. Kusahihisha makosa yaliyofanywa na mamlaka za chini. Hii ni amri kuu inayotolewa na Mahakama Kuu kwenda chombo cha kiserikali au chombo kinachotenda kama nusu-mahakama (quasi-judicial body) kufuta uamuzi uliokiuka sheria za nchi. Sasa inanishangaza kumsikiliza mtu anaitwa SISTY NYAHOZA akidai barua yao mpya kwa CHADEMA ni "jambo jipya" na kwamba amri za Mahakama haziwezi kuzuia ofisi yao kufanya shughuli zake. Ikiwa Msajili au mamlaka itakaidi zuio hili na kuchukua hatua yoyote hasi dhidi ya CHADEMA kinyume na AMRI hii halali ya CHADEMA itakuwa ni dharau kwa Mahakama (Contempt of Court). Hawa watu, wanatumika vibaya, wamepachikwa tu kwenye ofisi za umma na hawawezi hata kutafsiri sheria. SISTY na MUTUNGI wanatakiwa kuitwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma hizi.

Martin Maranja Masese

16,780 views • 9 days ago

IAMartin_'s profile picture

Ndugu Madenge katika jambo hili umenisikitisha sana. Sikutegemea unaweza kuwa sehemu ya kejeli hizi. Hao wengine ni wapumbavu tu ukijumlisha na huyo Masanja (hawakunishangaza) Siyo kwamba mnachekesha, mmeonesha ujinga wenu. Mmeonesha jinsi mlivyo machawa wa watawala. Na mmejitenga na jamii kubwa ya watanzania. Mmechagua kuwa maadui wa umma. Twitter (X) mnalalamika kuhusu umeme kila siku, watu tunakwenda barabarani na mabango ya umeme mnakwenda kutukejeli? Kweli nimeamini sasa, kuwa “paid slave” ni dhambi. Unatumikishwa tu. Masanja hajaenda shule. Hakuna ubongo kichwani, anawezaje kuwapa maudhui (content) za kipunbavu hivi na mkazitumia? Au ninyi pia mmekubali kuwa wapumbavu kama yeye? Mbaya zaidi ni kwamba wote katika kundi hilo hakuna hata ambaye ana diploma au degree ya uandishi wa habari na utangazaji. Wameokotwa kijanja-kijanja na leo wanakejeli watanzania. Kama mmeshindwa kuandamana na hamtaki, maiwadhihaki wananchi hao wachache ambao wamekubali kuandamana kwa gharama zao wenyewe. Mnapata faida gani wakiacha kuandamana? Naelewa, watangazaji wa EFM hapo mnalipwa vizuri. Maumivu makubwa ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bidhaa sokoni hakuwagusi. Labda ndiyo maana mnakejeli haya maandamano. Mnakosea sana. Mtaani kuna maumivu makali. Wananchi hawana maji wala umeme. Sukari bei juu na mtaani haipo. Miundombinu ni duni na serikali inakusanya kodi. Jukwaa pekee kueleza hayo ni katika maandamano. Biashara za watu mtaani zinakufa. Mitaji yao imepotea. Media ambayo ingelitumika kufikisha ujumbe kwa serikali ndiyo inakejeli maandamano ambayo yanatumika kupaza sauti za watu mtaani. Maandamano yale yanatumika kufikisha ujumbe kwa watawala. Ukisoma mabango wananchi wameandika na kubeba kero zao, wanatembea kwa zaidi ya kilometa 20, kuziwasilisha, mnawakejeli? Mnatumika na DOLA kwa nia ovu. Mnafifisha morali ya umma kujitokeza katika maandamano ya amani ambayo yanasaidia kubeba sauti kubwa ya umma kwenda kwa watawala. Mnakosea sana. Hili ni tatizo kubwa. Kwa kuwa mmiliki wa EFM ni mwana CCM kindakindaki anatumia chombo chake cha habari kukejeli shughuli za kisiasa na maandamano ya kiraia. Huu ni UPUMBAVU. Kazi ambazo mnazifanya hapo leo EFM/ETV, Malcom X alizieleza vizuri sana mwaka 1963. “house Negro” na “field Negro.” Ninyi watangazaji wa EFM ni ‘house negro’ kwa matendo na tabia zenu hizi. House negro aliishi katika nyumba ya bwana wake - ghorofa au dari - lakini bado aliishi katika nyumba ya bwana, alivaa mabaki ya nguo za bwana wake. Alikula chakula bwana wake alikiacha mezani. House negro alijatanabaisha kila mara kwa maana ileile ambayo bwana wake alijitambulisha. House negro alijiweka katika daraja sawa na bwana wake, wakati huo ni myumwa na kijakazi. Bwana wake aliposema, “Tuna chakula kizuri,” alisema, “Ndiyo, sisi tuna chakula kingi kizuri.” Bwana wake aliposema “tuna nyumba nzuri hapa,” alisema, “Ndiyo, tuna nyumba nzuri hapa.” Bwana wake akiugua, house negro angemuuliza “Kuna nini bosi, sisi wagonjwa?”. Maumivu ya bwana wake yalikuwa maumivu yake mara mbili. Aliumia kuliko hata watoto wa bwana wake. House negro ilimuuma zaidi bwana wake kuwa mgonjwa kuliko yeye mwenyewe kuwa mgonjwa. Hawa sasa ndiyo wafanyakazi wa EFM/ETV. Hizi ni tabia zao za kitumwa, house negro. But I know, nothing you can if you’re just a paid slave. 🙏🏽 Brigedia Mtikila, MMM.

Martin Maranja Masese

456,958 views • 2 years ago