
Martin Maranja Masese
@IAMartin_ • 609,637 subscribers
MMM | Public Spirited | Sperm That Won The Race | Think Deep, Don’t Sink | Cogito, ergo Sum | Patria o Muerte, Venceremos |
Shorts
Videos

Kuporwa kwa uwanja wa michezo wa Sahara uliopo kata ya Mabibo, Ubungo—ambalo ni eneo la wazi la umma—ni uthibitisho tosha la jinsi wananchi wanavyokosa watetezi wa haki zao pale CHADEMA wanapokuwa nje ya vyombo vya maamuzi. Wananchi wa eneo hili sasa wapo hatarini kupoteza kabisa ardhi hii ya wazi ambayo wameitumia kwa miaka mingi kwa ajili ya michezo na shughuli za kijamii.
Martin Maranja Masese45,766 görüntüleme • 4 gün önce

Mchawi binadamu, paka anatumwa tu. MPEMBA ametumwa kumshambulia NAMBA MBILI wao na amembatiza jina la YUDA. Kosa lake ni kusema alipendwa sana na JIWE. Wamekasirika sana. Jamaa anasema JIWE alimtupa Brazil. Wanasema ametengwa hadi na familia ya ‘WHITE HAIR’. Eti ni kweli, wazee wa ‘Safari ya Matumaini’ mmemtenga 'Mzee wa Mustachi'? Sisi wengine tunafurahi. Kazi yetu moja tu, kuchochea kunu. Ushirika wa 'wanyonya damu' hauwezi kudumu. NB; kama wapo wengi, kwanini hakuna makofi? SIJAPENDA.
Martin Maranja Masese57,117 görüntüleme • 6 gün önce

CHADEMA sasa hivi si chama cha siasa tu, ni imani iliyozama mioyoni mwa watu! Baada ya kushiba nondo za maana kutoka kwa viongozi, wananchi wenyewe wamemwaga upendo kwa kuchangia kiasi cha TZS 5,992,255 kidogo kidogo (Tone kwa Tone), kisha burudani ya ngoma za ukombozi ikafuata. CCM ili ipate vibe kama hili, ni lazima imwage mabilioni kusomba wasanii ili kuvuta watu. #PeoplesPower #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Martin Maranja Masese93,667 görüntüleme • 20 gün önce

Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa. Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe. Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo. Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake. Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka. Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa. Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu. Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA? Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai. Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu. Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii. Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana. Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania? Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM. Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye. Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo. Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu. Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Martin Maranja Masese70,947 görüntüleme • 1 ay önce

Nafikiri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inahitaji kufutwa haraka na kutengenezwa ofisi mpya kwa mujibu wa sheria. Inawezekana vipi wakashindwa kutafsiri amri halali ya Mahakama (Drawn Order)? CHADEMA tulifungua shauri la nyongeza (MISCELLANEOUS CAUSE No. 12812 la 2026) katika Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sub-Registry ya Manyara iliyopo Babati. Waombaji (Applicants) ni Katibu Mkuu CHADEMA na Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA, huku wajibu maombi (Respondents) wakiwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. CHADEMA tulifungua maombi tukiomba: 1. Mahakama itoe amri ya muda (interim order) kumzuia MSAJILI kuchukua hatua yoyote hasi dhidi ya CHADEMA tukisubiri kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa maombi ya kibali cha kufungua maombi ya amri za mahakama (prerogative orders) 2. Amri nyingine yoyote au unafuu ambao Mahakama ya Haki inaweza kuona ni haki na usawa kutoa. Maombi haya yalikwenda kwa ajili ya uamuzi wa upande mmoja (ex-parte ruling) mbele ya JAJI I.C. MUGETA, ambapo mawakili wetu—Mpale Mpoki, Nyaronyo Kicheere, na Hekima Mwasipu… Walisikilizwa pekee yao bila uwepo wa wajibu maombi. Sheria inaruhusu utaratibu huu wa dharura (extreme urgency) ili kuepusha hatari ya madhara yasiyorekebishika (risk of irreparable injury). Maombi ya CHADEMA yalikubaliwa, na tarehe 25 Mei, 2026, Mahakama ilitoa amri zifuatazo zilizotiwa saini na Jaji I.C Mugeta na kuwekwa Muhuri halali: (i) Amri ya muda ya kuzuia (interim injunction) inayomzuia Msajili kuchukua hatua yoyote hasi (adverse action) dhidi ya Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kama vile kufuta usajili wa chama au kusimamisha shughuli zake. (ii) Hakuna amri yoyote kuhusu gharama za kesi. Amri hii inafanya kazi kama breki ya dharura na ngao ya kisheria. Lengo lake si kumaliza kesi, bali ni kugandisha mambo yalivyo kwa muda ili kulinda hali halisi (status quo). MSAJILI haelewi haya mambo? Hivyo, chini ya amri hizo, CHADEMA inaendelea kuwa na haki na uhalali wa kufanya shughuli zake zote mpaka mahakama itakapoamua kama itatupa kibali cha kufungua maombi ya prerogative orders. Katika maombi ya msingi, CHADEMA tunaomba amri ya Certiorari (neno la Kilatini linalomaanisha “Kujulishwa” au “Kuthibitishiwa”. Kusahihisha makosa yaliyofanywa na mamlaka za chini. Hii ni amri kuu inayotolewa na Mahakama Kuu kwenda chombo cha kiserikali au chombo kinachotenda kama nusu-mahakama (quasi-judicial body) kufuta uamuzi uliokiuka sheria za nchi. Sasa inanishangaza kumsikiliza mtu anaitwa SISTY NYAHOZA akidai barua yao mpya kwa CHADEMA ni "jambo jipya" na kwamba amri za Mahakama haziwezi kuzuia ofisi yao kufanya shughuli zake. Ikiwa Msajili au mamlaka itakaidi zuio hili na kuchukua hatua yoyote hasi dhidi ya CHADEMA kinyume na AMRI hii halali ya CHADEMA itakuwa ni dharau kwa Mahakama (Contempt of Court). Hawa watu, wanatumika vibaya, wamepachikwa tu kwenye ofisi za umma na hawawezi hata kutafsiri sheria. SISTY na MUTUNGI wanatakiwa kuitwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma hizi.
Martin Maranja Masese16,780 görüntüleme • 9 gün önce

Hatuweki huu upumbavu hapa kwamba tunataka huruma ya MSAJILI, hapana. Tunaweka huu UPUMBAVU hapa kuonyesha mbogamboga walivyo WAPUMBAVU. Mwenyekiti wa wanawake wa mbogamboga wote ndiyo huyu? MSAJILI atajikausha kama anaaga maiti. Huyu maza ubongo wake ameacha mochwari? Sasa angetufanya nini? Angetuua wote? Sisi tukisema haya maneno, watavumilia? Je, ana uhakika bila bunduki za DOLA hawa mbogamboga wanatuweza? Maza kama huyu, anamuweza nani? Anyways, MAVAMPAYA yanataka damu. YAMEPAGAWA.
Martin Maranja Masese29,539 görüntüleme • 20 gün önce

“RIO ATASHAWISHI SAA ZA ROLEX ZIWE NA TANZANITE” 🤣 🤲
Martin Maranja Masese19,050 görüntüleme • 16 gün önce

KATORO – GEITA. Viwanja vya SATELİTE. CHADEMA tumekusanya #ToneTone kiasi cha TZS 2,071,000. MSAJILI USITUTISHE. Huwezi kamwe kutupangia namna gani tushughulike na MaCCM. RUZUKU ya kiwaki HATUTAKI. Angusha TONE lako hapo kupitia 0744446969; Jina - CHADEMA HQ. #PeoplesPower. 👊🏾
Martin Maranja Masese26,087 görüntüleme • 23 gün önce

Viwanja vya RELINI, ARUSHA MJINI. CHADEMA tumekusanya kiasi cha TZS 2,815,000. Hadi sasa ARUSHA imevunja rekodi ya #ToneTone tangu kuanza kwa oparesheni #KatibaMpya #FreeTunduLissu. MSAJILI USITUTISHE. Huwezi kamwe kutupangia namna gani tushughulike na MaCCM. Wananchi ndiyo wataendesha CHADEMA kwa fedha zao. Angusha TONE lako kupitia 0744 44 69 69; Jina - CHADEMA HQ. #PeoplesPower. 👊🏾
Martin Maranja Masese20,125 görüntüleme • 17 gün önce

Nafikiri eneo ambalo MaCCM yanapata kichefuchefu na kutema mate mji mzima ni nyakati hizi ambazo Wananchi wenyewe wanaamua kuchangia chama chao kwa fedha zao wenyewe. TONETONE ni hisia za ndani za UMMA katika harakati za mageuzi ya kisiasa Tanzania. Asante sana DODOMA mmechangua chama chem kiaso cha TZS 3,209,200 uwanjani. Hatujahesabu katika simu ya mkononi. Dodoma wanaendelea Mishima reload yao ya TONE TONE. #PeoplesPower #NguvuYaUmma
Martin Maranja Masese16,762 görüntüleme • 15 gün önce

Kirando, Nkasi Kaskazini, Rukwa. Hii ni leo. Hakuna kiongozi wa kitaifa yeyote. Hapa alikuwepo AIDA KENANI na watu wake tu. Mnaweza kuwatoa roho wafuasi wote wa CHADEMA lakini hamuwezi kuondoa imani kwa watu. Kwa sasa, CHADEMA ni imani ya watu. CHADEMA kwetu ni lifestyle yetu.
Martin Maranja Masese39,921 görüntüleme • 1 ay önce

Hawa watu imefika hatua siyo kwamba hawajiheshimu, lakini wamepoteza utu wa binadamu. Kwa hiyo GAZA, Palestine kuna mabango ya CCM? Gaza walifanya uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025? Gaza kuna vituo vya kupiga kura vimeandikwa INEC? Gaza ndiyo watu waliobeba silaha walivaa jezi za YANGA? Gaza ndiyo wale trafiki walikuwa na silaha? Gaza ndiyo zile mochwari zilizosheheni maiti zipo? Watu wa Gaza ni weusi watupu, hakuna hata Mwarabu mmoja? Kwa hiyo katika zile video clip uliwaona waarabu na IDF mkashindwa kuwatambua hadi ikabidi muite watalaam? Gaza wanazungumza kiswahili? Gaza maiti ao wanafunika na bendera ya Tanzania? Master Tindwa aliuwawa Gaza, Palestine? Au anazungumzia ukanda wa Gaza akimaanisha Kimara? Fikiria kidogo, mtu huyu alikuwa Jaji Mkuu kwa miaka nane. Profesa?
Martin Maranja Masese34,335 görüntüleme • 1 ay önce

Viwanja vya Nyankumbu, Geita Mjini vimeongea! Zaidi ya TZS 2,559,000 zimepatikana kupitia #ToneTone. MaCCM hayataki kuamini kwamba chama cha siasa ambacho ni mali ya umma Tanzania ni CHADEMA. Angusha TONE lako hapo kupitia 0744446969; Jina - CHADEMA HQ. #PeoplesPower. 👊🏾
Martin Maranja Masese20,226 görüntüleme • 22 gün önce

Ndugu Madenge katika jambo hili umenisikitisha sana. Sikutegemea unaweza kuwa sehemu ya kejeli hizi. Hao wengine ni wapumbavu tu ukijumlisha na huyo Masanja (hawakunishangaza) Siyo kwamba mnachekesha, mmeonesha ujinga wenu. Mmeonesha jinsi mlivyo machawa wa watawala. Na mmejitenga na jamii kubwa ya watanzania. Mmechagua kuwa maadui wa umma. Twitter (X) mnalalamika kuhusu umeme kila siku, watu tunakwenda barabarani na mabango ya umeme mnakwenda kutukejeli? Kweli nimeamini sasa, kuwa “paid slave” ni dhambi. Unatumikishwa tu. Masanja hajaenda shule. Hakuna ubongo kichwani, anawezaje kuwapa maudhui (content) za kipunbavu hivi na mkazitumia? Au ninyi pia mmekubali kuwa wapumbavu kama yeye? Mbaya zaidi ni kwamba wote katika kundi hilo hakuna hata ambaye ana diploma au degree ya uandishi wa habari na utangazaji. Wameokotwa kijanja-kijanja na leo wanakejeli watanzania. Kama mmeshindwa kuandamana na hamtaki, maiwadhihaki wananchi hao wachache ambao wamekubali kuandamana kwa gharama zao wenyewe. Mnapata faida gani wakiacha kuandamana? Naelewa, watangazaji wa EFM hapo mnalipwa vizuri. Maumivu makubwa ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bidhaa sokoni hakuwagusi. Labda ndiyo maana mnakejeli haya maandamano. Mnakosea sana. Mtaani kuna maumivu makali. Wananchi hawana maji wala umeme. Sukari bei juu na mtaani haipo. Miundombinu ni duni na serikali inakusanya kodi. Jukwaa pekee kueleza hayo ni katika maandamano. Biashara za watu mtaani zinakufa. Mitaji yao imepotea. Media ambayo ingelitumika kufikisha ujumbe kwa serikali ndiyo inakejeli maandamano ambayo yanatumika kupaza sauti za watu mtaani. Maandamano yale yanatumika kufikisha ujumbe kwa watawala. Ukisoma mabango wananchi wameandika na kubeba kero zao, wanatembea kwa zaidi ya kilometa 20, kuziwasilisha, mnawakejeli? Mnatumika na DOLA kwa nia ovu. Mnafifisha morali ya umma kujitokeza katika maandamano ya amani ambayo yanasaidia kubeba sauti kubwa ya umma kwenda kwa watawala. Mnakosea sana. Hili ni tatizo kubwa. Kwa kuwa mmiliki wa EFM ni mwana CCM kindakindaki anatumia chombo chake cha habari kukejeli shughuli za kisiasa na maandamano ya kiraia. Huu ni UPUMBAVU. Kazi ambazo mnazifanya hapo leo EFM/ETV, Malcom X alizieleza vizuri sana mwaka 1963. “house Negro” na “field Negro.” Ninyi watangazaji wa EFM ni ‘house negro’ kwa matendo na tabia zenu hizi. House negro aliishi katika nyumba ya bwana wake - ghorofa au dari - lakini bado aliishi katika nyumba ya bwana, alivaa mabaki ya nguo za bwana wake. Alikula chakula bwana wake alikiacha mezani. House negro alijatanabaisha kila mara kwa maana ileile ambayo bwana wake alijitambulisha. House negro alijiweka katika daraja sawa na bwana wake, wakati huo ni myumwa na kijakazi. Bwana wake aliposema, “Tuna chakula kizuri,” alisema, “Ndiyo, sisi tuna chakula kingi kizuri.” Bwana wake aliposema “tuna nyumba nzuri hapa,” alisema, “Ndiyo, tuna nyumba nzuri hapa.” Bwana wake akiugua, house negro angemuuliza “Kuna nini bosi, sisi wagonjwa?”. Maumivu ya bwana wake yalikuwa maumivu yake mara mbili. Aliumia kuliko hata watoto wa bwana wake. House negro ilimuuma zaidi bwana wake kuwa mgonjwa kuliko yeye mwenyewe kuwa mgonjwa. Hawa sasa ndiyo wafanyakazi wa EFM/ETV. Hizi ni tabia zao za kitumwa, house negro. But I know, nothing you can if you’re just a paid slave. 🙏🏽 Brigedia Mtikila, MMM.
Martin Maranja Masese456,958 görüntüleme • 2 yıl önce

KAHAMA – Shinyanga. Makamu Mwenyekiti CHADEMA John Heche. Homeboy is cooking. Watu ni wengi kama mchanga. Massive, overflowing crowd. This is a clear demonstration of political might—unmatched and irreplaceable. IGA UFE, JARIBU UFILISIKE. 🔥#katibampya #freetundulissu
Martin Maranja Masese17,018 görüntüleme • 21 gün önce

Leo katika harakati za kushughulika na MaCCM tulikuwa na mkutano mkubwa na mzuri wa hadhara ambao umefanyika viwanja vya Soko Kuu, Arusha Mjini na kuhutubiwa na Godbless E.J. Lema na Boniface Jacob na viongozi wengine wa chama mkoa na jimbo. Pamoja na mvua iliyonyesha watu wamegoma kuondoka na wamebaki wanakula nondo tupu. Narudia kuwaeleza, CHADEMA sasa ni imani ya watu siyo tu chama cha siasa. #nguvuyaumma #peoplespower
Martin Maranja Masese22,642 görüntüleme • 1 ay önce
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Fungua kwa tahadhari; ⚠️ Picha za kutekwa na kuuawa kwa Joshua Mollel (21), mwanafunzi wa kilimo kutoka Tanzania. Serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba, Joshua Mollel aliuawa mara tu baada ya kutekwa na kundi la HAMAS mnamo tarehe 7 Oktoba 2023. Pumzika kwa amani Joshua 🙏🏽
Martin Maranja Masese368,169 görüntüleme • 2 yıl önce

Ndugu yetu Edgar Mwakabela, SIR TIVA amepatikana katika hifadhi ya Katavi. Ameteswa na ameumizwa sana. Tunaomba watu wa Katavi mtusaidie haraka sana apate msaada wa matibabu. Rais Samia Suluhu umefika huku? Tulisema hatuwezi kurudi katika zama hizi za kuwatesa wakosoaji wako.
Martin Maranja Masese290,079 görüntüleme • 1 yıl önce

Milio ya risasi za moto imesikika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo, Dar es Salaam. Watu hao waliokwenda kumkamata Askofu Josephat Gwajima wamepambana kuvamia chumba chake lakini waumini wameendelea kuzuia asichukuliwe. Waumini hao wamekwenda kufunga barabara ya Morogoro.
Martin Maranja Masese154,330 görüntüleme • 1 yıl önce

Leo, muda huu, tupo Landmark, Ubungo, Dar es Salaam katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Dar es Salaam ambao ni wanachama CHADEMA STUDENTS ORGANIZATION (CHASO), Dar es Salaam na limehutubiwa na viongozi wakuu wa CHADEMA. Kongamano maalum kwa ajili ya kuzungumza na vijana wa CHADEMA katika mustakabali wa kesho yao. Nimefurahi kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu takribani 1,000 wameujaza ukumbi na morali ya hali ya juu kabisa. CHASO ni chanzo cha fikra bora. #PeoplesPower NB; vijana hawajasombwa, hawajalipwa, hawajalazimishwa.
Martin Maranja Masese20,013 görüntüleme • 1 ay önce