Revocatus Millambo, Ph.D.'s banner
Revocatus Millambo, Ph.D.'s profile picture

Revocatus Millambo, Ph.D.

@Millambo_27,107 subscribers

I Teach Biz Owners, Entrepreneurs, Coaches and Consultants how to Build Expert Business & Sell High Ticket Offers

Videos

Millambo_'s profile picture

Hii Ndio Dhambi Aliyoifanya Niffer. Dunia inaongozwa na sheria zake. Huwezi kuzikwepa, labda utajidanganya tu. Tangu nimeanza kujifunza ujasiliamali kuna sheria moja tu ya utajiri. 📌Hii inaitwa the Law of Effection. Nayo inasema hivi kadri unavyogusa maisha ya watu wengi kwenye mfumo unaou-control kwa kujizalisha zaidi na wingi wake ndivyo unavyoingiza kipato kikubwa. Kwa msemo mwingine, kiasi cha pesa ulichonacho au usichonacho ni sawa kabisa na kiwango wa cha thamani ulichozalisha au usichozalisha. Kama hapa hujaelewa hii itakusaidia: Ukitaka kutajirirka: Gusa mamilioni ya watu, utaingiza mamilioni ya shilingi. Formula yake ni: FAIDA KAMILI = Idadi ya vitu vilivyouzwa × Faida ya kitu kimoja kichouzwa 📌Sasa tuje kwenye sakata la Niffer. Kwenye biashara kila mtu huingia kutokana na nama alivyotathimini uwezekano wa kupiga faida. Hakuna mtu anaingia kwenye biashara kizembe tu akidhani ataweza kutoboa bila kujipanga. Atakuwa hajui anachofanya. Na ndio maana biashara nyingi zinafeli. Niffer aliusoma mchezo wa soko la ndani akaona kabisa namna watu wanavyopigwa bei juu kwenye bidhaa za kawaida. Akaona fursa. Kwa waliowahi kuwagiza vitu nje wanajua kabisa gharama ya vitu vingi huwa ni cheap sana kwa masoko ya nje hasa Uchina. Vitu vingi ukiagiza mwenyewe mpaka hapa, utakuwa umeokoa pesa nyingi sana. Sasa usipoweza kuagiza utalipa gharama kwa atakayekuagizia: Atakupiga bei kwa sababu unalipia: A.Pesa yake aliyotumia kuagiza B.Muda wake aliotumia C.Risk ya kupoteza pesa So, ukienda kununua mzigo kwake kubali kubamizwa bei yoyote atakayokwekea. Na wengi tu wanapata faida kwa zaidi ya margin ya 50%. Kuna hoja ya kulipa kodi. Kuna watu wanamlalamikia Niffer kuhusu kodi. A.Wote wanalipa kodi za bidhaa zinapoingia nchini. B.Wengi wanalipa kodi za majengo ya biashara C.Wengi wanalipa kodi TRA kwa kufanya biashara Hapa sasa kuna watu mob tu hawalipi kodi na wanapush mizigo yao fresh tu. Kila mtu kimpango wake. Nimefatilia naona Niffer ana ofisi analipa kodi, lakini pia nataka kuamini analipa kodi TRA ndio maana hapoi mtandaoni. Na asingekuwa analipa kodi, asubuhi tu angeshughulikiwa. 📌Uchawi wa Niffer Uko Wapi? Unapotaka kuingia kwenye biashara yoyote kuna vitu vya kuzingatia. Jambo la muhimu zaidi ni kuwa kadri biashara inavyokuwa rahisi kwa kila mtu kufanya ndivyo inapunguza faida maana watu wengi wataingia na saturation itawahi kufika. Hizi biashara za kuagiza mizigo sasa kila mtu anafanya. Niffer alipoingia alijua kuna ushindani mkubwa kwa sababu kwa sababu tayari watu wa Kariakoo na kwingineko wameshatawala soko na wengi tu wanauza mitandaoni. Soko limeshakuwa na watu wengi. Sasa hapa akaamua kuwa tofauti na kuwa na upekee. Akaja na mbinu za ushindi. A.Bei za Kitanzania B.Kutumia mitandao ya kijamii 📌 Kuhusu Bei: Niffer aliamua kuuza bei za chini kabisa. Kwanini? Kwenye baishara kuna option nyingi za kutengeneza milioni 10. Mfano: A.Kuuza bidhaa 10,000 kwa sh. 1000 tu AU B.Kuuza bidhaa 1000 kwa sh. 10,000 Hapa Niffer akaamua kujitenga na kila mtu, akatengeneza bahari yake isiyokuwa na ushindani. Nyie uzeni 10K ili mpate faida kubwa. Na ndo kundi kubwa la watu wanaolalamika wapo kwenye bei ya 10K na kupata faida kubwa. Yeye anakomaa na 1K ili auze mara nyingi zaidi ili kuingiza zaidi. Sasa mwenye makosa nani? 📌 Kuhusu Mitandao Niffer ana wafuasi mil 1.3 Instagram na Tiktok – 221.2K Sijui kama ana akaunti zingine. Bado anapata mashavu ya kupostiwa na watu maarufu kama kina Mange. Sasa hebu tafakari. Wewe unaagiza mzigo ule ule kama wa Niffer, Unaweka store yako pale Kariakoo. Unaweka bei 10K. Ili mtu anunue mzigo kwako lazima apande mwendokasi aje dukani kwako. Hata kama ataagiza mtu, bado lazima kwa mara ya kwanza afike dukani angalau kwa sababu hakuna namna anaweza kukufikia bila kutumia miguu. Ofisi iko sehemu moja tu. Haiwezi kutokea sehemu zaidi ya moja. Kitaalam tunasema haina leverage na sio scalable. 📌Sasa dada yako Niffer. Kwenye mitandao tu ana wafuasi Mil 1.5+ Yaani bidhaa zake zinaonekana na watu zaidi ya milioni ndani na nje ya Tanzania. Halafu anakuwekea bei 1K, kumbuka wewe umeweka 10K. Bado ana store ambapo watu hufika. (Hapa kwenye store mnatoka pasu – hakuna leverage ya maana). Kwenye mitandao sasa ndipo uchawi ulipo. Anamwanga content kama zote. Akiwa Dubai, Akiwa uchina, n.k Yote ni kukupa uhakika wa bidhaa na mizigo yake. Anakupa content za wateja kufurika kwenye maduka yake. Anakupa content za watu kununua na kumaliza mzigo wote. Anakupa content za wateja kufurahia bidhaa zake. Anakupa content za wateja wengi wa mkoa kununua kwake. Anakupa content za vile kila mtu anaweka deposit ili aletewe mzigo. Anakuoa content za kuaminiwa na wamiliki wa maduka ughaibuni. Halafu huku wewe unasubiri Mwajuma atoke zake Buza apande magari mpaka hapo ili anunue. Mwenzako watu wanaweka oda wakiwa zao huko Buza, Congo, Zambia. Effect ya social media tunaichukulia kizembe sana. Kumbuka ile Law of Effection: Kutengeneza mamilioni ya pesa, gusa mamilioni ya watu. Na Niffer kapita mule mule. Na hapa ndio Niffer kawaacha vibaya sana washindani wake. Tumesahau kuwa kitu kikikubalika kwenye mitandao huwa ni ngumu kukirudisha nyuma. Mange mwenyewe anauza udaku tena kwa buku buku, hawa Wabongo ndio wanalipia kila mwezi tena kwa VPN kabisa. Imagine anapata guts za kununua stori mpaka za milioni, maana yake anatengeneza mchuzi wa maana. Mange kashinda wapi? Social media. Chapa aliyojenga. Vivyo hivyo kwa Niffer. Amejua namna ya kuwamaliza washindani wake kwa kutumia mitandao. Chapa yake pia inazidi kukua kila siku. Sasa Itakuwaje Watu wa Kariakoo? Nimesikia wengine wanataka kwenda mahakamani. Wanaenda kumshitaki kwa kusema wanauza vitu feki? Wanaenda kumshitaki kwa kuuza bei za chini? Wanaenda kumshitaki kwa kuuza mtandaoni? Wanaenda kumshitaki kwa sababu halipi kodi TRA? Wanaenda kumshitaki kwa sababu halipi kodi ya pango? Wanaenda kumshitaki kwa sababu kawadhihaki? Bado sijajua, Na nipo hapa kujifunza. Nachojua mimi huwezi kupanga bei za masoko tu kwa kila kitu. Unawezaje kweli kuamua bei za consumables? Huwezi kupanga bei ya kila kitu, angalia mfano wa sukari. Mwamba aliingia mtegoni na kuigusa bei ya tam tam. Mpaka kesho ametuachia kisanga. Kwenye soko huria haya mambo kila mtu anazalisha kwa gharama zake. Pengine serikali huingulia kati kama bidhaa zenye maslahi mapana kwenye bidhaa nyeti. Huku ndo unakuta mafuta (petrol), umeme, maji na vitu vyeti kama hivyo. Sasa Kojie ndio ya kumfanya mama aache kazi zake za kujenga nchi akae chini kupanga bei ya sabuni ambayo bado ni luxurious maana si ya lazima kwa maisha. Wagumu wanatumia Jamaa na Kwanga na ngozi ziko tu sawa. Tukisema kila mtu ambaye alikuwa na soko limeingiliwa alalamike, unadhani malalamiko yatafika wapi? Sasa watu wa media house (Radio&TV) waandamane kisa online TVs? Bongo movie waandamane kisa kina Clam na Kicheche kutesa You Tube? Wazalishaji wa energy kama Red Bull walalamike kisa kina Mo na Azam? Bajabir na JustFits yake walalamikie Baraka Maviatu kisa bei zake zipo chini? Haiwezekani. Sio rahisi kuweza kupanga bei za vitu vitumikavyo kila siku. Mimi nasema hivi: Kama huwezi kubadilika kwenye bisahara yako kufuata masoko, basi masoko yatakulazimisha kubadilika kwa nguvu. Anyway. Huu ni mtazamo wangu tu. Nipo hapa kujifunza. Mniambie wataalam wa biashara, Niffer kazingua nini kisheria ambacho watamshughulikia nacho? Au tunategemea karma na sheria za dunia? Itapendeza kutumia logic na facts zaidi kuliko hisia. Kujifunza zaidi: Follow Revocatus Millambo, Ph.D. Karibu Telegram yetu: Bure Link: "REPOST" #SIKU100ZAUHURU Millambo, 0754087177

Revocatus Millambo, Ph.D.

98,049 Aufrufe • vor 2 Jahren

Millambo_'s profile picture

Umasikini Ni Roho MChafu - Mkatae⚠️ Umewahi kusikia kuna watu ni makaburi ya pesa? Wao wakishika pesa itapotea tu. HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KIJANA KUAMINI HUWEZI KUFANIKIWA. Wenzako wanadai benki, wewe unashangaa Savimbi kujenga nyumba. Leo ni #SIKU15 Ya #SIKU100ZAUHURU Imekuwa kasumba ya vijana wengi kuona utajiri wa watu na kushangaa wakiona haiwezekani. Ni vile pengine, siasa zimefanya kuona utajiri ni rahisi kupatiknana ukiwa kwenye mfumo. Ukiona tu upo kwenye mkumbo huu, Ujue roho ya ufukara iko juu yako. Mwenyezi Mungu hakuuumba mtu masikini, Ni mazingira tu. Mazingra yametengenezwa ili watu waamini hawawezi kutoboa. Mazingira yametengenezwa ili watu wajinenee kuwa hawawezi. Mazingira yametengenezwa ili watu wakomae na wapende kuajiriwa. Mazingira yametengenezwa ili wazalishaji wawe wachache na walaji wengi zaidi. Mazingira ya sasa yanataka vijana wengi wawe machawa. Shida ni kuwa wengi hawapati kuujua ukweli kuhusu pesa na njia zake. Kwanza pesa ni nini? Maana fasili yake haifahamiki vyema. Pesa ni mkondo. Mkondo wa nini? Mkondo wa kubadilishana thamani. Sasa wewe hapo ulipo, Ni mkondo au ni kaburi? Pesa ikija, itakaa? itazalishwa? 📌 Watu wengi ni makaburi ya pesa na si mkondo. Na makaburi daima huamini mikondo hutumia njia zisizo kutengeneza pesa. Siakati, wapo baadhi. Lakini kimsingi. Watu wengi ni makaburi na wana roho za umasikini. Huamini? Jiulize, kwa miaka 3 kurudi nyuma umeingiza kiasi gani? Ulifanya nini kuzalisha na kuizungusha pesa iwe mob? Utagundua umeingiza pesa nyingi sana. Lakini hujui huwa inaenda wapi. Nishakwambia huwa inaenda wapi. Kaburini. Bila kubadili maisha yako kutoka kaburi mpaka mkondo. Utaendelea kuita watu wizi kumbe, ni roho wako tu ndo anakupagawisha. Unadhani hapo ulipo ukipatiwa 10M na mwingine akapatiwa hiyo 10M baadaya ya miezi 6 nani atakuwa na pesa? Utakuwa nayo? Jitafakari wewe ni mkondo au kaburi? 📌Kamwe huwezi tajirika kwa kuuza muda wako kuingiza kipato. Utaingiza kipato cha maana tu kama una kazi nzuri. Lakini kitu inaitwa ukwasi, hapana. Muda hauwezi kuongezeka. Piga uwa, huwezi kuzalisha zaidi ya kile unafanyia kazi. Tuseme unalipwa 500K kwa mwezi. Maana yake kwa mwaka utalipwa mara 12 tu. Huwezi kuizidisha hiyo 500K, Wala huwezi kuongeza miezi ya kufanya kazi. Maana yake, muda ni limited. Huwezi ku-scale muda. Ndio maana ni lazima kwa wafanyakazi kuwekeza na kuzalisha passive income kama kweli nia ni kuwa na uhuru wa kifedha. Tofauti na hapo ni kusitaafu na kuingia msongo tu. Ukiona mtu ana-make sana pesa, Usione wivu, usichukie, nenda kaulize, Lazima anajua kitu wewe hujui. Bila kujali unajua kazi au biashara zake. Sio wote huwa wanaweka wazi kila mishe zao. Wewe unaona anauza mayai, kumbe mwenzako ana hisa mpaka kwenye kampuni uliyoajiriwa. 📌 Sheria za dunia zinasema: You can’t attract what you attack. Huwezi kuvutia, kile unachochukia. Kama wewe hupendi mpira, huwezi kujua na siku zote utakuwa mbali. Ndo maana huwezi jikuta unapenda mpira. Vivyo hivyo kwenye pesa. Kama unachukia watu wenye ukwasi maana yake unachukia ukwasi. Na hivyo huwezi kuwa kwenye sehemu ya kujifunza kuutafuta maana unauchukia na watu wake. Yaani unawachukia wakwasi, maana yake na wewe hupendi kuwa mmoja wao. Stori inaishia hapo. Unakumbuka kipindi cha 'matajiri kuishi kama mashetani' roho za umasikini zilifurahi sana. Iko ndani sana hii roho. Kwa bahati mbaya sana, Jamii imekutengeneza kuamini huwezi kutoboa. Hiyo ipo akilini mwako na inatengenza imani zako. Kwa taarifa yako tu. Man, watu wana ukwasi hapa nje. Usiseme, hakuna pesa, sema huna pesa. Kwa hiyo watu walivyokuwa wanamuona Boi Yai kwenye katuni za mayai wakaona ni lofa. Dah, pesa huwa haiongei wala kupiga kelele, usidharau mtu - Watu wako na Pakei. Umeona yule jamaa, Arusha. Hata umri haujaenda kivile. Anaidai benki mpaka anakamata mali za benki zote ili alipwe. Ukimuangalia alivyo na umri wake, huwezi kumdhania. Ndo pesa ilivyo my friend. Haiji kwa kuangalia kadi ya chama wala dini. Ukiipatia formula yake, umeomoka. 📌 Sasa akili za vijana: - Ukiwa na ukwasi umeiba - Wao hawaamini kama huwezi kuwa na mishe na watu hawajui - Jamii imekuaminisha ili kutoboa ni lazima uwe chawa kwa wanasiasa - Umeamua kukabidhi siti ya dereva kwa wengine na wewe kuwa abiria daima. Ewe kijana. Ukajikomboe na pepo la ufukara. Ufukara ni roho, pigana daima kuishinda. Pesa ni roho, inapenda inapopendwa. Na kupendwa kwake sio kutataka tu kuwa nayo, Bali ni kuitengenezea mfereji wa kuingia, kustawi na kujizalisha zaidi. Ikawe ni siku njema kwako kutafakari na kubadilika. REPOST Wengi Wajifunze! Kujifunza Zaidi: Sogelea Telegram Yetu ya Bure: Link: #SIKU100ZAUHURU Millambo. #Tutoboewote

Revocatus Millambo, Ph.D.

23,589 Aufrufe • vor 2 Jahren

Keine weiteren Inhalte verfügbar