
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv
@OlengurumwaO • 36,913 subscribers
Human Rights Lawyer, Researcher and Policy Analyst- CEO THRDC. Regional Director East African Human Rights Institute. Defending human rights is not a crime
Videos

Mtakatifu Yuda Thadei wa Galiilaya anajulikana ulimwenguni kote kama Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana, yasiyo na matumaini, na kesi ngumu sana. Waamini hukimbilia kwake pale ambapo nguvu za kibinadamu zimefika mwisho na hakuna njia nyingine inayoonekana.
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv27,709 просмотров • 1 месяц назад

Sabato Kareem Shekh Ali - Allah azidi kukupa hekima kama za Mfalme Suleiman
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv77,934 просмотров • 7 месяцев назад

Wito wa Kuliponya Taifa Matukio ya hivi karibuni ya tarehe 29, yaliyogubikwa na maandamano na vifo vya kusikitisha, yanaonesha umuhimu wa Tanzania kutafuta maridhiano na mwafaka wa kitaifa. Ili kuponya taifa letu, viongozi wanapaswa kukiri kwa uwazi yaliyotokea ili kujenga kuaminiana na uwajibikaji. Ni wakati wa Tanzania kukaa pamoja, kukubali ukweli, na kusonga mbele kwa umoja. Hapa kuna hatua 10 muhimu za kufikia uponyaji wa kitaifa: 1.Komesha Uchochezi na Kupunguza Mvutano Pande zote zisitishe kauli na matendo ya kichochezi. Viongozi na vyombo vya usalama wazingatie kujizuia, kuheshimu haki za binadamu na kuepuka mashambulizi au lawama za moja kwa moja dhidi ya makundi ya kijamii. 2.Uchunguzi Huru Tuhimize kufanyika kwa uchunguzi huru na wa uwazi kuhusu vurugu na vifo vilivyotokea wakati wa maandamano. Hii itasaidia kubaini uwajibikaji na kuzuia matukio yajayo. Kuhimiza uwajibikaji na watuhumiwa hawapaswi kuwa sehemu ya tume ya uchunguzi. 3.Majadiliano na Usuluhishi Kuanzisha majadiliano ya kitaifa yanayoshirikisha serikali, vyama vya upinzani, makundi ya vijana, asasi za kiraia, na viongozi wa kijamii ili kushughulikia malalamiko na kutafuta mwafaka wa pamoja. 4.Hatua za Maridhiano Kuunga mkono uundwaji wa mifumo ya maridhiano ikijumuisha tume za ukweli na maridhiano au program za kijamii ili kuponya majeraha yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea hivi karibuni. 5.Marekebisho ya Uchaguzi Kutilia mkazo katika marekebisho ya muenendo wa uchaguzi, yatakayohakikisha uchaguzi huru, wa haki, na wa uwazi, na kushughulikia changamoto zilizochangia machafuko. 6.Ulinzi wa Haki za Binadamu Kutetea na kulinda uimarishaji na ulinzi wa haki za binadamu, ikiwemo haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza. Kuhakikisha waliokamatwa au kutekwa wakati wa maandamano wanapata haki na uwakilishwaji sawa wa kisheria. 7.Kuepuka Kulaumiana Viongozi wajikite kwenye kutafuta sababu za msingi za matukio badala ya kusaka wanaolaumiwa, ili kuzuia kurudiwa kwa hali kama hiyo. 8.Ushirikishwaji wa Umma Kujadiliana na wananchi kuhusu yaliyotokea ili kupata taarifa, kujenga upya kuaminiana, na kuhakikisha wananchi wanasikilizwa hasa kizazi hiki cha vijana (Gen-Z). 9.Suluhisho la Muda Mrefu Kushughulikia chanzo cha msingi cha migogoro kama kukamilisha mchakato wa katiba mpya, kupunguza matabaka ya kiuchumi, kutatua suala la kutengwa kisiasa, na kudhibiti dhuluma za kijamii. Hii itahitaji sera za kina na ushirikiano wa jamii. 10.Kuombea Taifa Kuwataka viongozi wa dini kuandaa ibada na dua za kuiombea nchi, zenye lengo la kuiongoza Tanzania kwenye uponyaji na maridhiano. Kwa kufuata hatua hizi, Tanzania inaweza kuanza kupona na kujenga mustakabali wenye utulivu, amani, na ujumuishi. Njia ya mwafaka na maridhiano ni ngumu, lakini ni muhimu kwa ustawi wa Watanzania wote. Nawaomba viongozi na wananchi watulie na kujitolea kuliponya taifa letu, kurejesha amani na utulivu. Tujiepushe kutumia dini kugawa watu au kutafuta huruma ya umma visivyo. Mungu Ibariki Tanzania, Advocate Onesmo Olengurumwa – 03/12/2025
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv59,752 просмотров • 7 месяцев назад

Serikali Mlipeni huyu mama - naombeni kujua anapatikana wapi Dr. Dorothy Gwajima
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv80,478 просмотров • 1 год назад

Ila jama mbona wanabonga sana kiswahili-usikute ni wenzetu
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv68,641 просмотров • 1 год назад

Salamu za Mwalimu Nyerere kuhusu Ngorongoro Samia Suluhu
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv35,094 просмотров • 1 год назад

Mwanaharakati kutoka Tanzania, Ndugu Julius Nyerere akiingilia mambo ya ndani ya Zambia after visiting President Kaunda in Prson na kumsaidia aachiwe baadaye. Kubwa la haraka alifanikiwa kumshawishi Rais wakati huo aruhusu Kaunda akae gereza la nyumbani huku swala lake likiendelea kujadiliwa. Kutoka maktaba
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv23,782 просмотров • 1 год назад

Wakati tunamwombea Father Kitima apone , Sala nyingi zinahitajika ili kumnusuru Ndugu Mdude Mdude Nyagali Kwa mazingira waliomchukua ni zaidi ya utekaji , tunafuatilia sana mambo ya utekaji kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Tunajiua aina ya utekaji ambayo mtu anaweza kurudi salama na aina ya utekaji ambayo mtu anapotea kabisa. Ya Mdude ni zaidi ya Utekaji - Wale walidhamiria kumpoteza pale pale nyumbani kwa mazingira ya tukio lile ni kwa vile tu walikuta familia. Bado tunasisitiza umuhimu wa vyombo huru vya uchunguzi kwa kesi ambazo vyombo vya usalama vinatuhumiwa. Tunaomba sana msimue Mdude , mrudisheni akiwa salama. Haya matukio tunapaswa kila mtanzania ayachukie, akemee na kuyakataa. Wakati huo huo nashauri kila mtu ajitahidi kuzingatia usalama wake wakati huu
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv23,827 просмотров • 1 год назад

Very unfortunate - Ni Bahati mbaya sana kwa upinzani wakati huu
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv23,146 просмотров • 1 год назад

Hapa jibu ni Katiba mpya - ndio mjue tukidai katiba mpya itatibu magonjwa mengi sana
Olaigwanani-Olengurumwa, Adv15,616 просмотров • 1 год назад