Boniface Chengula's banner
Boniface Chengula's profile picture

Boniface Chengula

@bohny_chengula119,074 subscribers

Phones & Electronics in general | iG: Chengula_iPhone.Store | 📍Mwenge ITV | ☎️0752-992667 | Not affiliated with any Brand.

Videos

bohny_chengula's profile picture

Nimeona video hii kwa niffer huko TikTok akielezea nini wafanyabiashara wafanye pale ambapo watajiri au wafanyabiashara wakubwa wanapo post bei za jumla katika page zao za mitandaoni. Kuna point mbili nataka kuzielezea. Kinachosababisha wafanyabiashara wakubwa wapost bei za jumla ntandaoni ni kukosa ethics za biashara tu, sababu bei kubwa sikuzote haiwezi kukuletea wateja wengi japo sometimes it does. Pili, uwepo wa wachina umekuja kufanya biashara kua ngumu sana, sababu kilakitu ambacho Mtanzania alikua anakifata China leo hii mchina anakileta kwa bei ndogo. Zunguka kwenye malls za Home city na malls zingine mpya ambazo mchina anuza, unakuta mafuta Mtanzania alikua anaagiza China na kuuza kwa 10k lakini ukienda kwa mall ya mchina anuza 3k, apo mbongo mwenzako si utamuona mwizi? Lakini kingine ni kwamba wauzaji wa jumla wanatakiwa wamlinde mteja wa jumla sababu yeye anakuja kwako kununua mzigo mkubwa mara kwa mara, hivo kama utapost bei za jumla mtandaoni inaonesha wewe kanuni za biashara huzijui. Hii ni kwa biashara zote sio cosmetic au furniture Au electronics pekee, kila kitu. Wafanyabiashara wengi wa leo wabinafsi, kutokujua ethics za biashara, lakini kwa wateja wanao waona watanzania wenzao wanauza vitu bei kubwa basi pia wanakosea sababu, biashara zina mambo mengi, mwingine anapewa mali kauli huko anakoagiza mzigo, mwingine alipata mzigo bei ndogo na akasafirisha bei ndogo, ko mkija sokoni bei hamuwezi wote mkafanana, lakini hili la wachina Serikali yetu ingeliangalia sana, maana miaka miwili mbele hali haitakua nzuri sana maana hali za wafanyabiashara wengi zitakua ngumu.

Boniface Chengula

118,389 次观看 • 18 天前

没有更多内容可加载