
EastAfricaTV
@eastafricatv • 2,062,968 subscribers
Official EastAfricaTV (EATV) Twitter Email: [email protected]
Shorts
Videos

#VIDEO Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, amekuwa miongoni mwa viongozi na watu mashuhuri waliofika kushuhudia tukio la kihistoria la uzinduzi wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) kinachozunduliwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan, wilayani Rufuji mkoani Pwani. #EastAfricaTV
EastAfricaTV36,931 görüntüleme • 7 gün önce

🗣️Mwanne Othman Kamby anaamini msanii akifanya kazi na SIMBA..!🦁 nyota yake inazidi kuwa kubwa. Hiyo imekuja baada ya mkongwe Angelique Kidjo kutunukiwa heshima ya Hollywood Walk of Fame,pale Los Angeles Marekani. Na Diamond Platnumz na Kidjo tayari wameshafanya wimbo wa pamoja 'Kakua' #DADAZ
EastAfricaTV40,647 görüntüleme • 10 gün önce

#HABARI Vijana 531 wanatarajiwa kuondoka nchini kwenda kufanya kazi katika Saudi Arabia, Qatar, Oman, Falme za Kiarabu (UAE), Ujerumani na Bosnia kupitia fursa za ajira za kimataifa. Wameagwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Zuhura Yunus, ambaye amesema hatua hiyo inaonyesha kuendelea kupanuka kwa masoko ya ajira kwa Watanzania. Amesema jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita zimechangia kufunguliwa kwa fursa zaidi za ajira nje ya nchi kupitia ushirikiano wa kimataifa. Pia amewataka vijana hao kuzingatia sheria za nchi wanazokwenda, kufanya kazi kwa weledi na kuitangaza vyema Tanzania. #EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV80,226 görüntüleme • 29 gün önce

#Fahamu | Msafara wa Rais wa Marekani, Donald Trump ukielekea Michigan ambapo amewasili kwa ziara ya kikazi kwenye kiwanda cha magari cha General Motors (GM). Akiwa huko, Trump alishuhudia mashindano ya magari akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa GM, Mary Barra, kabla ya kutoa hotuba iliyosisitiza umuhimu wa ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kama njia ya kulinda ajira za Wamarekani. Video | TCD Dearborn News #EastAfricaTv | #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV75,657 görüntüleme • 1 ay önce

#HABARI Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ametekeleza oparesheni ya uvamizi katika makazi ya kijana Bundala Mashiku (24) kijana aliyemuoa mwanafunzi aliyefaulu kuendelea kidato cha tano, huku akiliagiza Jeshi la Polisi kumkamata kijana huyo pamoja na Baba yake ili kujibu tuhuma zinazowakabili. #EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV71,140 görüntüleme • 1 ay önce

#VIDEO Maandamano nchini India yamechukua sura mpya baada ya mmoja wa waandamanaji kulipanda gari la polisi la maji ya kuwasha na kuligeuzia maafisa wa usalama wakati wa jitihada za kutawanya umati. Maandamano hayo yalichochewa na malalamiko kuhusu uvujaji wa mitihani ya kuingia vyuo vikuu (NEET), mfumo wa elimu pamoja na madai ya ukandamizaji wa viongozi wa upinzani na wanafunzi. Waandamanaji wanataka mageuzi katika sekta ya elimu na kujiuzulu kwa Waziri wa Elimu wa Muungano, Dharmendra Pradhan, huku polisi wakiendelea kutumia nguvu kudhibiti maandamano hayo. #EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV77,781 görüntüleme • 1 ay önce

#HABARI Madereva wa magari ya masafa marefu wameeleza kutoridhishwa na utaratibu unaowalazimu kurejea darasani kila wanapohitaji kuhuisha leseni zao za udereva, wakidai kuwa mafunzo hayo yanajirudia na yanapoteza muda ambao ungeweza kutumika katika shughuli zao za usafirishaji. Wamesema utaratibu huo unaathiri uzalishaji wao pamoja na shughuli za waajiri, hivyo wamezitaka mamlaka husika kutafuta njia mbadala zitakazorahisisha mchakato wa uhuishaji wa leseni bila kuathiri utendaji wa madereva. #EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV61,162 görüntüleme • 1 ay önce

#HABARI Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti wa CHADEMA kutoka mikoa yote nchini katika kikao kilichofanyika mkoani Dodoma. Mkutano huo umefanyika leo, Agosti 13, 2026, ukiwakutanisha viongozi wa chama kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mazungumzo hayo yalihusisha wenyeviti wote wa mikoa ya CHADEMA nchini. Taarifa haikueleza kwa kina ajenda au maamuzi yaliyofikiwa katika kikao hicho. #EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
EastAfricaTV19,627 görüntüleme • 16 gün önce

🗣Mwanza kuna sehemu kama huna Bilioni 10 hupati Kiwanja - Msanii H Baba #DADAZ
EastAfricaTV31,778 görüntüleme • 1 ay önce

#Bungeni: Akichangia Bajeti ya Wizara ya Elimu, Mbunge wa Kuteuliwa (CCM), Shamsi Vuai Nahodha ameweka mkazo kwenye uhusiano wa kile kinachofundishwa darasani na uhalisia wa maisha. Kwa urefu zaidi unaweza kuitazama kupitia YouTube channel yetu ya EastAfricaTV #EastAfricaTV #Bungeni #HainaKuchoka #EATV2025
EastAfricaTV223,766 görüntüleme • 1 yıl önce