
(---) Onesmo Mushi
@EduTalkTz • 43,577 subscribers
Power tends to corrupt, and absolute power corrupts absolutely — Lord Acton
Shorts
Videos

Mtaka ni mbegu nzuri iliyoanguka kwenye udongo mbaya. Kuna mambo hauwezi kufake, ni ama unayo au hauna. Ameuliza swali muhimu sana ambalo Mwal. Richard Mabala amekuwa akisisitiza kila mara anaposema “Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kusema iwe ikawa.” Huu “uchumi wa dola trillion moja” by 2050 unatengenezwa na human resource ipi? Mtoto anayezaliwa leo hii ana mazingira yoyote ya kumwandaa kushiriki kikamilifu kwenye uchumi, tofauti na mama yake aliyezaliwa miaka 15 - 20 iliyopita? Ni kipi haswa kilichobadilika kwenye elimu ya Tanzania ambacho unaweza kusema “hawa wa jana hakika hawakuandaliwa lakini hawa wa leo wana uhakika wa kuwa rasilimali watu?” JIBU LA MSINGI NI HAKUNA. Mazingira ni yale yale, miundombinu duni ni ile ile, tatizo la walimu ni lile lile, vifaa vya TEHAMA ni changamoto vile vile, na bajeti ni kiduchu vile vile. Tena kama haitoshi ndio kwanza tumeongeza idadi ya wanafunzi mara dufu halafu juu yake tukakopi sehemu ya sera ya elimu ya Finland na kuitumbukiza Tanzania. Mwanafunzi mzuri wa policy borrowing anaweza kutabiri with certainty kuwa tulichofanya ni mbili jumlisha mbili toa nne, haswa kwa kuzingatia uhalisia wetu wa kimiundombinu. Hoja nyingine nyeti ni hii ya KUSUBIRI KUSAIDIWA KILA KITU. Yani hata kutumia wataalam wetu kama wakina Kipanya na Mabala kututengenezea makala za kufundishia imekuwa changamoto, mpaka tusubiri “WAHISANI.” Pata picha hadithi za ucheshi wa kufundishia za Mabala, ambaye ni mtaalam wa literacy, zimekutana na katuni za Kipanya, vyote kwenye program moja. Ameuliza Mtaka, ni kipi haswa kwenye katuni ya Akili and Me kinachohitaji mtu kutoka nje?? Mwisho Mtaka akagusa panapouma. Katuni za HakiElimu kuhusu uhalisia wa mazingira ya kufundishia zilikuwa na shida gani?? Hatutaki kuambiwa ukweli kuhusu hali ya madawati mashuleni, vyoo, changamoto kubwa ya walimu na uwezo wao, pepo la lugha ya kufundishia n.k. Kila mara jamaa wakidepict uhalisia, mnasema “oohhhh wanashusha moral ya walimu; ooohhh wanamdharaulisha mwalimu; ooohhh wanaondoa utu wa wanafunzi; ooohhhh blah blah blah.” Tunapenda political correctness kiasi kwamba tupo tayari kuficha ukweli na kuacha watoto waendelee kusomea kwenye mazingira ya tabu na mateso kuliko kukabiliana na ukweli.
(---) Onesmo Mushi26,991 views • 20 days ago

Kwenye Riwaya ya Crime and Punishment, Fyodor Dostoevsky anazungumzia namna NAFSI inavyoweza kumwadhibu yule anayetenda uovu kuliko hata jela. Anasema unaweza kufake kwa tabasamu na ngonjera za hapa na pale lakini nafsi itakutandika mpaka uteme moto. Hii ni kwa muuwaji, sijui hali ipoje kwa yule ambaye analazimika kuficha siri za muuwaji na kuutetea uuwaji. A must read kwa wakati huu!!
(---) Onesmo Mushi10,316 views • 6 days ago

Tanzania kitendo cha kusema tu “hupendi nini kuhusu Rais” tayari kinatosha kukupoteza.
(---) Onesmo Mushi18,190 views • 22 days ago

Mwalimu Richard Mabala , mchukue ndugu yako mzungumze kinyumbani bhana😎.
(---) Onesmo Mushi22,685 views • 29 days ago

Ndio utapeli unaofanywa na wanasiasa wa Tanzania, kila kitu ujanja ujanja. Elimu ya juu imegeuzwa kuwa tissue paper, inapangusa upumbavu wa watawala tu. Chukulia mfano Mwigulu Nchemba. Wakati anafanya PhD pale UDSM 2012 - 2017, alikuwa pia Mbunge anayehudhuria vikao vya Bunge Dodoma, Mjumbe wa Kamati za Bunge za Bajeti, Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, Mhazini wa CCM, Naibu Waziri wa Fedha, Waziri wa Kilimo, na Waziri wa Mambo ya Ndani. Chuo Kikuu cha Daresalaam University of Doha for Science and Technology kinatuaminisha kwamba wakati Mwigulu Nchemba anatekeleza majukumu yote haya aliweza pia kupata muda wa kujiandikisha kama mwanafunzi wa PhD full time. Yani wakati anatekeleza majukumu yote haya, aliweza pia kuhudhuria vipindi vyote na kukamilisha coursework, akapata muda wa kufanya tafiti, kuchapisha makala, kuandika dissertation, halafu kama haitoshi, akamaliza yote haya ndani ya miaka mitano na kutunukiwa PhD. Unless haufahamu what it takes kufanya PhD, huu ni muujiza wa hali ya juu. Hata hivyo haishangazi kwa sababu ni UDSM hii hii ailiyompa Samia PhD ya heshima mara baada tu ya kuingia madarakani.
(---) Onesmo Mushi27,704 views • 1 month ago

Professor kama Professor😂😂😂!! Kuna wakati ni vigumu sana kujadili hoja za hawa jamaa pasipo kuzungumzia taaluma zao. Kinchi ambacho mpaka leo kinategemea mikopo na misaada kujazia bajeti nacho kinapayuka namna hii😎. Kusupply condoms tu changamoto, mpaka USAID waje😎.
(---) Onesmo Mushi18,287 views • 1 month ago

Biblia yangu inaniambia Yesu aliona kifo ni bora kuliko kutii upumbavu. Alipopata nafasi ya kukutana na Mafarisayo na Masadukayo akawachana live. Hata aliposimama mbele ya Pilato, hakumumunya maneno. Hii ya kuheshimu washenzi walioshindwa kujiheshimu wenyewe tumekuachia.
(---) Onesmo Mushi11,587 views • 19 days ago