
HabariLeo
@HabariLeo • 169,425 subscribers
Kwa habari za uhakika na kina | Sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Tanzania Standard Newspapers (TSN)
Videos

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amepinga suala la malipo ya kumuona daktari licha ya vituo vya afya kujengwa na wananchi, amesisitiza kuwa jukumu la kumlipa daktari ni la serikali ukizingatia anapokea mshahara. Imeandaliwa na Ben Shija #HabarileoUPDATES
HabariLeo220,733 görüntüleme • 2 yıl önce

MTANDAONI - Wananchi walijitokeza kwa mayowe na kutumia katapila katika juhudi za kumfukuza tembo aliyekuwa akiingia kwenye mashamba na makazi yao, lakini hali ilichukua mkondo wa kushtua baada ya tembo huyo kuparamia katapila, akionyesha ujasiri usiotarajiwa mbele ya juhudi za kumtoa eneo hilo. Imeandaliwa na Mwandishi Zaidi tembelea //habarileo.co.tz #HabarileoUPDATES
HabariLeo103,002 görüntüleme • 1 yıl önce

DAR ES SALAAM: KATIKA tukio lisilo tarajiwa na wengi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko alisimamisha hotuba kwaajili ya askari aliyemtolea amri wakati akimuongoza kwenye gwaride na kumpa anachostahili. Katika hatua nyingine, Dk. Biteko ameilekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza ili kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kuhakikisha Magereza yote yanaondokana na Nishati isiyo safi. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Machi 28, 2025 jijini Dar es salaam katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Namba 27 - 2024/2025 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA). “Magereza yote 129 yamehama katika matumizi ya kuni na sasa yanatumia nishati safi ya kupikia. Naielekeza REA ile ruzuku tunayopanga kuitoa kwa wazalishaji mbalimbali kwa ajili ya vifaa vya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia Magereza wapewe kipaumbele,” amesema Dk. Biteko. Video na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati #HabarileoUPDATES
HabariLeo89,793 görüntüleme • 1 yıl önce

DAR ES SALAAM : Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imetangaza kuwa itapiga mnada magari mbalimbali ambayo hayatumiki ikiwemo Range Rover Wagon siku ya Ijumaa Desemba 13, 2024. - Mnada huo utafanyika katika Jengo la TSN lililopo Mtaa wa Isimani Upanga, Dar es Salaam utahusisha pia pikipiki, vifaa vya TEHAMA, samani za ofisi na vifaa vingine. - Watakaohitaji kukagua vifaa hivyo vya mnada wanaruhusiwa kufanya hivyo leo na kesho katika eneo hilo la mnada na kupewa maelezo kwa kina. - Imeandaliwa na Samwel Swai Zaidi tembelea #HabarileoUPDATES
HabariLeo78,725 görüntüleme • 1 yıl önce

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa mpaka sasa ameshindwa kutofautisha kati ya kulala na kuzimia ila anaamini kuwa Mwenyezi Mungu wakati anakiumba kifo pia aliwapa wanadamu usingizi ili pindi wanapolala iwe ni mazoezi ya kukizoea kifo. RC Chalamila ameyasema hayo wakati wa Misa ya Mazishi ya Padri Timothy Maganga Nyasulu yaliyofanyika katika kituo cha Hija Pugu, jjini Dar es Salaam mapema wiki hii. Imeandaliwa na Ben Shija #HabarileoUPDATES
HabariLeo28,834 görüntüleme • 1 yıl önce

MBUNGE wa Viti Maalum (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Halima Mdee amesema kama wabunge hawata acha ubadhilifu wa pesa za Halmashauri uendelee na kupendekeza Bunge limtake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi kubaini udanganyifu, wizi au rushwa katika pesa zilizopotea. #HabarileoUPDATES #TunawezeshaVIJANA
HabariLeo22,793 görüntüleme • 3 yıl önce
Daha fazla içerik yok.