
HABARIMPYA TV
@HabarimpyaTv • 129,715 subscribers
News Updates 24 hours,.
Shorts
Videos

Huyu Kiongozi ni Noma sanaa ukienda kichwa kichwa anakuvunja mbavu changa,. 🙌🙌
HABARIMPYA TV50,288 просмотров • 3 месяцев назад

Wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga wamemtaka Mbunge wao, January Makamba, kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kushindwa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni. Wakizungumza na wanahabari leo, Aprili 2, 2025, jijini Dar es Salaam, wananchi hao wamesema kuwa licha ya kumpa kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu ujao, hawako tayari kumpigia kura tena Makamba kwa nafasi ya ubunge. Changamoto Zinazowakabili Wananchi 👇👇 Miongoni mwa matatizo waliyoeleza ni hali mbaya ya miundombinu, hasa barabara, ambayo imeathiri sekta ya kilimo. Bw. Eric Edward kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amesema walitarajia Makamba kutatua changamoto ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa chai, lakini hali imeendelea kuwa mbaya. “Kiwanda cha Mponde kilianza kwa nguvu lakini sasa thamani ya chai imeshuka. Wakulima wanahangaika kusafirisha mazao kwa bajaji kwenye barabara mbovu,” alisema Edward. Naye Elias Kamute alizungumzia tatizo la maji, akisema: “Bumbuli ina maji mengi, lakini hadi leo tunapata mgao. Ahadi zimekuwa nyingi, lakini utekelezaji hakuna kwa zaidi ya miaka 15.” Kwa upande wake, Khalid Kijazi alisema Makamba hana uhusiano wa karibu na wananchi wa Bumbuli, akidai kuwa “Ni kama mtalii wa nje na Dar es Salaam badala ya kushughulikia changamoto za jimbo lake.” “Tunahitaji kiongozi mpya kwa sababu Makamba ameshindwa kutimiza wajibu wake,” alisema Ayubu Radhid, akieleza jinsi miundombinu mibovu imeathiri wakulima wa eneo hilo. Merry Gendo naye alieleza kusikitishwa na kutotimizwa kwa ahadi za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, huku akidai Makamba aliwahi kusema “Wananchi wa Bumbuli hawahitaji maendeleo bali pesa za dagaa.” Katika sekta ya afya, Iddy Amiri alisema huduma duni za matibabu na uhaba wa madaktari ni matatizo makubwa, huku elimu nayo ikidorora kutokana na ukosefu wa walimu na miundombinu duni. “Makamba aliahidi kuboresha elimu, lakini hakuna kilichotekelezwa. Tunahitaji mbunge mpya atakayeleta maendeleo ya kweli,” alisema. Wananchi hao wamesisitiza kuwa ni wakati wa mabadiliko, wakimtaka January Makamba kuachia ngazi ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwatumikia kwa ufanisi.
HABARIMPYA TV151,142 просмотров • 1 год назад

Ustaz Juma na Musoma azungumzia uchapakazi wa Askari Faustin Mafwele na kutoa pongezi kwa jeshi la polisi.
HABARIMPYA TV75,783 просмотров • 6 месяцев назад
5:06
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Kiongozi wa Dini ya Waislamu Sheikh Mwaipopo amjia juu Rais wa Baraza la Maaaskofu wa kanisa katoliki (TEC) Askofu Dkt. Pisa kwa kutoa kauli ya kulaani na kutaka Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu aachiwe haraka, adai kauli hiyo ni kutaka kuiingilia Serikali.
HABARIMPYA TV130,277 просмотров • 1 год назад

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameibua shangwe katika Kongamano la ziwa Tanganyika baada ya kuzungumza Kifaransa kwa ufasaha, akionyesha dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda. Kongamano hilo linaendelea hadi Aprili 18, 2026 likiwakutanisha viongozi na wawekezaji kutoka nchi za ukanda huo.
HABARIMPYA TV21,881 просмотров • 1 месяц назад

Kenge kaingia kwenye 18 za mlavichwa ni ameliwa kama Mpumbavu,.🙌🙌
HABARIMPYA TV118,295 просмотров • 1 год назад

Aliyekuwa kada wa CHADEMA Catherine Ruge Rasmi ajivua uanachama wa chama hicho.
HABARIMPYA TV113,076 просмотров • 1 год назад

Mwanaume anayedhaniwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) awajibishwa na raia wenye hasira kali mkoani Arusha.
HABARIMPYA TV25,258 просмотров • 2 месяцев назад

Inaelezwa kuwa haya ndio maneno yaliyomponza Msemaji wa Yanga na kupelekea akamatwe na jeshi la Polisi,.
HABARIMPYA TV110,857 просмотров • 1 год назад

Mwenyekiti wa taasisi ya Samia Us, Geoffrey Kiliba ambaye pia ni Mwanafunzi wa chuo cha DIT akiambatana na wanafunzi wenzake wamepinga vikali kauli iliyoasisiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) isimayo 'no reform no election wakidai kauli hiyo ni mtazamo binafsi wa Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu
HABARIMPYA TV121,890 просмотров • 1 год назад

Kijana dereva wa bodaboda anayefahamika kwa jina la Brown Anthony ameibua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi baada ya kufanikiwa kusafiri kutoka jijini Mbeya hadi Dar es Salaam kwa kutumia pikipiki aina ya Boxer 150 HD yenye namba ya usajili MC 473 FKT, ndani ya saa 10, safari iliyoanzia kwenye ubishani wa kawaida na kuhitimishwa kwa ushindi wa kihistoria. Ubishani huo ulianza tarehe 14 Januari 2026 kati ya Brown Anthony na bodaboda mwenzake Alex Ndile, ambapo walitofautiana kuhusu uwezekano wa kufika Dar es Salaam kwa pikipiki ndani ya muda wa masaa 13. Baada ya majadiliano makali, walikubaliana kuyaweka madai yao katika makubaliano rasmi ya kisheria. Makubaliano hayo yaliwekwa mbele ya mwanasheria Ambakisye Kibona, ambapo kila mmoja alikuwa na pikipiki yake binafsi, na pande zote zilikubaliana kuwa atakayeshindwa atalazimika kumpa mshindi pikipiki yake kama dau la makubaliano hayo. Baada ya makubaliano kukamilika, Brown Anthony alianza safari yake rasmi tarehe 15 Januari saa 11:00 asubuhi, akitokea Mbalizi jijini Mbeya, akitumia pikipiki yake kama ilivyokubaliwa katika makubaliano hayo ya kisheria. Katika safari hiyo ndefu na yenye changamoto, Brown Anthony alifanya mapumziko mara tatu kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo madogo ya pikipiki, hatua iliyomwezesha kuendelea na safari bila matatizo ya kiufundi. Hatimaye, alifanikiwa kuwasili jijini Dar es Salaam saa 9:35 alasiri siku hiyo hiyo, akitumia muda uliokuwa chini ya masharti ya makubaliano, na hivyo kuthibitisha ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Alex Ndile. Baada ya kukamilisha safari hiyo, Brown Anthony alianza safari ya kurejea Mbeya alfajiri ya saa 11 kutoka Dar es Salaam, na kufanikiwa kuingia Mbalizi jijini Mbeya jioni ya Ijumaa, Januari 16, 2026, ambapo alipokelewa kwa shangwe. Kufuatia ushindi huo, alikabidhiwa pikipiki ya ushindi, iliyokuwa mali ya Alex Ndile yenye namba ya usajili MC 695 EFE.
HABARIMPYA TV43,584 просмотров • 4 месяцев назад