
John Heche
@HecheJohn • 806,026 subscribers
Vice Chairman Chadema Tanganyika, former Member of Parliament for Tarime rural constituency, a reformer.
Shorts
Videos

Internet never forgets, hawa wajinga wote wanaonuka damu za watu… iko siku watajibu .
John Heche43,742 views • 16 days ago

Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara.. Maneno muhimu kutoka kwako: Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari? Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika. Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika. Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko? 1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar? 2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu, Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika? Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara? Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar? Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya…. Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu? Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao. Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
John Heche58,286 views • 1 month ago

Huyu Bwana Kombo anazidi kuthibitisha kwamba waliua watu bila sababu ya msingi… Chande alisema kulikua na training na silaha , kombo anasema mawe!!! anasema ukimlembea jiwe polisi, anatakiwa kukupiga risasi.. Je Bwana Kombo yule mama Mtanganyika pale Arusha, Video yake Inaonekana anakimbia , akapigwa risasi mgongoni, alilemba jiwe kwa nani? Watu wameuwawa wakiwa nje ya Mageti ya nyumba zao, wengine kwenye sebule , kuna vijana Mwanza mmeaua wakiwa wanaangali Mpira… Unasema tumeheal!!!! Hamtaweza kufukia mauaji ya kutisha mliyofanya ili mjitangaze kwenye uchaguzi ambao haukuwepo… wote mnakula pesa za damu na dunia haitakaa kimya.
John Heche67,265 views • 1 month ago

Matamshi haya haya yakisemwa na baadhi ya watu, itakua shida kubwa sana .
John Heche33,295 views • 23 days ago

Jana nilipokwenda kuhuduria Kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Chaso. Walitumwa baadhi ya vijana kutoka UVCCM, kwa kulipwa vifedha kidogo… Sina tatizo na vijana hata kama ni wa ccm kuhudhuria na kusikiliza sera, misimamo na hoja zetu. Lakini huyu kijana, watu wetu walipomgundua na kumhoji alisema alikua ameambiwa kwamba tukianza kuzungumza kuhusu ripoti ya Chande wazomee.. Lakini pia wafanye fujo na kutoka ukumbuni, ionekane vijana hawakutusikiliza. Kwenye simu yake alikua anawasiliana na mtu anaitwa Shangwe Mtei ambae ni kiongozi wa Uvccm. Huyu Shangwe akawa anamhakikishia kwamba hata kama wako wachache wafanye fujo kwasababu OCD alikuwepo nao pale. Ghafla huyu kijana akiwa anahojiwa na watu wetu kwanini yuko pale na nia yake ni ipi, Magari mawili ya polisi yalikuja pale kitendo kinachoonesha kwamba tukio hili lilikua limepangwa kwa ushirikiano huo. Huyu kijana alikua ametumiwa muamala wa sh 50,000 kwa madai yake walitumiwa wote na wenzake, na walipatwa hofu na kutokufanya fujo kwasababu vijana wa Chaso walikua wengi zaidi na pia ulinzi ulikua imara.. Fikiria kwamba huyu ni kijana wa chuo kikuu ana fikra na mawazo ya kutumwa na kulipwa sh 50 elfu!! Tuna safari ndefu kama Nchi Lakini lazima tufike.. Asante watu wetu wa ulinzi kwa kazi nzuri.
John Heche63,178 views • 2 months ago

Mwigulu unasemaje sasa kuhusu hili? Anaehujumu serikali ni nani? Serikali dhalimu hii iliyojaaa damu, inatesa mamilioni ya Watanzania kuanzia Mtwara mpaka Tarime toka Tarime mpaka Kigoma kutoka Kigoma mpaka Songea, Tunduma mpka Dar.. Kila kona ya Nchi hii watu wanalia kama sio kubambikiziwa kesi na polisi, ndugu zao wametekwa au wameuwawa na vyombo vya dola . Huyu mama anahitaji kulipwa nini ili aandamane kudai haki ya mtoto wake kutekwa. Watoto wa huyo kijana au wa Soka, Mdude au polepole, watoto wa Chonchoryo au Sinda, watoto wa Tall au Kipanya wakikua wataacha watoto wenu waishi kwa Amani? Mnajenga sumu ya hatari mno kwenye mioyo ya Watanzania, bahati mbaya nashindwa kuona tatizo hili na kulitatua bado mnatumia ubabe na kiburi… Fikiria huyo angekua mama yako! Utaratibu wa polisi kukamata watu upo kisheria. Kwanini polisi wanateka Watanzania? Kila mtu ambae mtoto wake au ndugu yake amechukuliwa story zinafanana kwamba watekaji walijitambulisha kwamba wao ni polisi. Jambo kubwa kama hili, Watuhumiwa ni polisi alafu unasema polisi ndio wafuatilie!hivi mnawaonaje Watanzania? Watanzania hawatakubali kuishi kwa hofu kwasababu ya kagenge kadogo ka wauaji na wanyonya damu.
John Heche32,364 views • 1 month ago

Hakuna mtu huwa anajisahau haraka kama Nape… Bahati nzuri nilikua nae bungeni wakati Magufuli ameshughulika nae, alikua anatia huruma sana .. leo kasogea kwenye meza ya chakula ameshiba na anawatapikia Watanzania. Kitu kimoja ninamshukuru kwamba amesema ukweli kuwa, Nchi hii hakuna uchaguzi. Kinachonishangaza ni kwamba, inawezekanaje Watanzania wakakubali dharau, Matusi na kejeli ya kiwango hiki…
John Heche371,932 views • 2 years ago

Mbeya mmetisha sana, Asanteni sana kwa mapenzi makubwa kwa chama chetu.
John Heche11,445 views • 17 days ago

Ukitaka kujua aina ya watu wanaojiita watawala na level ya fikra zao na uwezo wao, Msikilize huyu bwana Ulega!!!! Yaani una Nchi yenye kilometa za mraba 945,000. Nchi pekee yenye Tanzanite duniani, Nchi pekee yenye mbuga kubwa kuliko zote Duniani, Serengeti, Ngorongoro nk. Nchi ya tatu kwa wingi wa dhahabu duniani, Nchi yenye mlima Kilimanjaro, makaa ya mawe, almasi, Victoria gesi na kila kitu. Miaka 65 ya Uhuru una mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 182,000 lakini kwa miaka 65 hiyo mmejenga barabara 16,000 tu! Yaani ni sawa na 9%. Tena barabara zenyewe hizi zimejaa mashimo kama ubao wa kuchezea bao!!! Hakuna barabara hata moja ambayo ni nzima … Anzia Tunduma Dar, Mwanza Dar , Kigoma Dar, Babati to Singida, Tabora Manyoni Yaani ni takataka… Barabara zenyewe finyu zisizowezesha hata kupishana wala kwenda km 120 kwa saa.. Barabara haina ubora inajengwa leo kabla hata mkandarasi kuondoka site imeishajaa mashimo.. Kama Imewachukua miaka 65 kujenga barabara za lami mbovu asimilia 9 ya Barabara zilizopo… maana yake wanahitaji miaka 130 kufikisha asimilia 18 ya Barabara zilizopo… achilia Mbali maeneo ambayo hayajaingizwa kwenye kanzi data ya Barabara zilizopo na zitakazofunguliwa …. Alafu bila aibu anajitokeza kusema uongo kwamba tuna mtandao mrefu wa barabara za lami kuliko Kenya!!! Hivi hawa watu hawaoni aibu? Kenya ina mtandao wa barabara za lami kilometa 25,411 sisi 16,700 kama alivyodai… Lakini factor ya pili ukubwa wa Nchi ya Kenya ni km za mraba 582,650 sisi 945,000. Kenya hawana dhahabu kama sisi, hawana tanzanite, hawana makaa ya mawe na chuma, hawana Serengeti is ala Ngorongoro kama sisi.. Yaani kwa hiki anachokisema Ulega, tukibaki chini ya huu Utawala dhalimu wa ccm tunahitaji miaka 600 ili kumaliza mtandao wote. Hapo kuna barabara kibao za mitaa na maeneo ambayo hayajapimwa mpaka sasa ambazo hazijajumlishwa hapo! Shame on you.
John Heche37,682 views • 2 months ago

Dunia inajua ripoti ya Chande ni uongo wa kusafisha watuhumiwa.
John Heche34,802 views • 2 months ago

Barabara ya Morogoro kutoka Dar inawezekana ndio Barabara kubwa na namba moja katika Nchi hii… Hii ni Barabara inayobeba uchumi wa Nchi hii, Magari yote kutoka Dar kwenda Mikoa ya Kaskazini, Magari yote yanayotoka Dar kwenda Mikoa ya Nyanda za juu kusini na Nje ya Nchi Zambia, Congo na kusini zaidi.. Magari yanayotoka Dar kwenda Mikoa ya kati, Dodoma, Singida Magari yanayokwenda Kanda ya ziwa na nje ya Nchi Rwanda, Burundi na Uganda.. Magari yanayokwenda Magharibi Kigoma, Tabora na hata Katavi .. Miaka 65 ni vibarabara viwili tena vimejaa mashimo tupu.. ikitokea breakdown magari yanasimama masaa manne, matatu kila siku. Sijawahi kupita hata nisikute mkwamo, watu wanateseka, uchumi unaharika na hakuna suluhu… pesa zinaibiwa na nyingine zinachezewa kuhujumu Chadema na kumnyanyasa kiongozi wetu Lissu badala ya kuhudumia wananchi.. Safari ya Morogoro - Dar km 180 inapaswa kuwa saa moja na dakika 20 tu… lakini mtu anasafiri masaa matano mpaka sita!!! Utajenga uchumi gani? Nchi gani makini itapitisha mzigo kwenye bandari ambayo hakuna hata miundombinu ya kusafirisha mizigo yao kwa mda.. Shame on you ccm.
John Heche45,262 views • 3 months ago

Mabeberu wanatuonea wivu hii ni Barabara yetu bora kabisa… kutoka Babati to Singida.
John Heche59,896 views • 5 months ago

Kwa ukatili kama huu na mauaji ambayo mmefanya kwa Watanzania leo mnasema mtaongoza? Mnataka kumuongoza Nani? Mnazungumza eti maendeleo ya nini? Kwaajili ya nani kama mmeua watanzania na kuwatesa hivi? Maji, umeme, Barabara au kitu chochote bila binadamu kuwepo vina maana gani? Hili jeshi la polisi wanafundishwa nini huko kwenye vyuo vyao? Kuwa katili? Said Mwema kwenye kitabu chake aliandika kuhusu huu ukatili, Tume ya haki jinai ya Samia imeandika kwamba hili jeshi linapaswa kufumuliwa kwasababu lina element za kikoloni, baada ya haya nani tena anaweza kuwa na imani na jeshi hili? Nani anaweza kubisha. Lazima tutabadili namna ya utendaji wa jeshi la polisi. Madaraka ya damu hayatasimama kwenye Nchi yetu.
John Heche73,678 views • 7 months ago