John Heche's banner
John Heche's profile picture

John Heche

@HecheJohn807,414 subscribers

Vice Chairman Chadema Tanganyika, former Member of Parliament for Tarime rural constituency, a reformer.

Shorts

Kwa ukatili kama huu na mauaji ambayo mmefanya kwa Watanzania leo mnasema mtaongoza? Mnataka kumuongoza Nani? Mnazungumza eti maendeleo ya nini? Kwaajili ya nani kama mmeua watanzania na kuwatesa hivi? Maji, umeme, Barabara au kitu chochote bila binadamu kuwepo vina maana gani? Hili jeshi la polisi wanafundishwa nini huko kwenye vyuo vyao? Kuwa katili? Said Mwema kwenye kitabu chake aliandika kuhusu huu ukatili, Tume ya haki jinai ya Samia imeandika kwamba hili jeshi linapaswa kufumuliwa kwasababu lina element za kikoloni, baada ya haya nani tena anaweza kuwa na imani na jeshi hili? Nani anaweza kubisha. Lazima tutabadili namna ya utendaji wa jeshi la polisi. Madaraka ya damu hayatasimama kwenye Nchi yetu.

73,711 görüntüleme

Usiku huu Mimi na wasaidizi wangu, tumeachiwa na polisi baada ya kututeka na kutushikilia kinyume cha utaratibu kwa mda mrefu. Hakuna kiwango cha udhalilishaji, vitisho wala mauji kinachoweza kuzuia kiu yetu ya kutafuta mabadiliko. Tutaipigania demokrasia kwa gharama yoyote. Nitaeleza kilichotokea leo, katika hatua za baadae. Asanteni Watanzania.

101,305 görüntüleme

Thank you champ.

Thank you champ.

61,556 görüntüleme

Tuko mkuyuni Mwanza saa nzima hakuna gari inasogea mbele wala kurudi nyuma, kujenga kadaraja hapa imechukua miaka miwili. Hali ni hii kila siku asubuhi na jioni.. watu wanateseka kama vile tumepata uhuru jana. Nchi haina uongozi kabisa ni uozo tu…

24,578 görüntüleme

Videos

Genge dogo linatesa mamilioni ya Watanzania, kuwajaza hofu na kuwatisha. Djumbe wa Chadema alikamatwa na watu waliokuwa na pingu akateswa na Mungu akamuokoa. Mzee Ally Kibao alishushwa kwenye gari watu wakiwa wanaona mchana kweupe. Deus Soka alipigiwa simu na askari wanaofahamika kwa majina na ushahidi wa maneno yake mwenyewe upo. Madai ya familia ya Polepole kuhusu watu waliomteka na kuacha damu nyingi zikiwa zimemwagika kwake. Mke wa Mdude anasema wazi kwamba watu waliokwenda kwake walijitambulisha kama ni polisi na wakamchukua wakaacha damu zimetapakaa kwake. Maelfu ya watu waliotekwa kufungwa vitambaa na kupewa mateso mabaya, kushinikizwa kukiri uongo au kuumizwa vibaya sana wote wanataja polisi au watu waliojitambulisha kwamba wanatoka kwenye vyombo vya dola. Leo bwana Kazungu kada wa CCM kwa kukosoa mwenendo wa chama chao, anapigwa, anafungwa macho, anadhalilishwa utu wake, anafungwa pingu kama Djumbe na wengine wengi. 1. Tunajua pingu Nchi hii ziko mikononi mwa vyombo vya dola, polisi, Magereza na vyombo vingine. 2. Tunajua vyombo vinavyoweza kushusha mtu kwenye gari na kuondoka nae mchana kweupe ni vyombo vya usalama. 3. Tunajua magari yanayotumia namba zisizo halisi, namba zinazobadilishwa kila wakati ni za serikali tena kinyume cha sharia. Wanaofanya haya mambo wajue jambo moja tu. Siku sio nyingi watalipia uovu huu, Mnaweza kulindwa leo na Utawala huu wa mauaji, lakini kesho inakuja kwa kasi.. Hawa wanaokulinda hawatakua na nguvu ya kukulinda tena. Kwenu Watanzania: sababu za wazee wetu kupigania Uhuru hazikua barabara zilikua Uhuru .. Leo mtu anapoteswa na kuambiwa asiseme na akisema atakuawawa maana yake hatuko huru tena. Tusikubali ujinga kama huu.
3:17

Sensitive content

This media may contain sensitive content.

HecheJohn's profile picture

28,162 görüntüleme • 7 gün önce

HecheJohn's profile picture

Katiba ndio Suluhu ya haya matatizo yote.

John Heche

22,273 görüntüleme • 8 gün önce

HecheJohn's profile picture

Katika Nchi ambayo uhusiano wa serikali na wananchi ni wa kikatiba. Uhusiano wa Mwananchi kama muajiri na serikali kama muajiriwa huwezi kuona upuuzi kama huu. Nchi hii wananachi wanachukuliwa kama watumwa na watawala kama watwana au wamiliki wa watumwa. Nimeona utetezi wa jeshi la polisi kwenye upuuzi huu, inathibitisha kiwango cha dharau walichonacho hawa watu dhidi ya raia. Mwananchi huyu masikini amelima alizeti imekaa shambani miezi minne, mbegu amenunua mwenyewe, pengine kwa jembe la mkono na mvua kidogo akavuna. Hapo ilipo hiyo alizeti kuanzia mbegu imelipiwa kodi, akivuna tu kodi… huko anakopeleka kuna Mageti ya mazao kila kona.. Baada ya kuuza akinunua sukari kuna kodi , kiberiti, Sabuni na chumvi vyote kodi za kulipa askari huyo mshahara. Hata kama huyo bwana amekosea: Sheria gani inampa mamlaka askari kuchukua mzigo wake na kutupa mtaroni? PGO namba ngapi inamwambia askari mtu akifanya kosa kama hilo unaharibu mali yake kwa kuirusha kwenye mtaro unaopitisha maji machafu tena mzigo wa chakula? Kwanini usimkamate na kufuata utaratibu wa kisheria? Kwa utetezi huu wa polisi kwa askari hao ni uthibitisho wa namna serikali hii ya kidkteta inavyowaona wananchi… Haishangazi kama waliua mamia kwa maelfu ya watu na wanaona ni kawaida itakua kutupa mzigo mtaroni? Watanzania mnapaswa kubadilika wale mnaofikiri hayawahusu kwasababu nyie sio huyo bwana, watawafikia kwa njia nyingine. Kama alivyowahi kusema Martin Luther king kwa watu weusi kule Marekani. “We must learn to live together as brothers or perish together as fools“ Lazima tujifunze kuishi pamoja kama ndugu, kwa kuteteana, kusaidia na kulindana au tuangamie pamoja kama wajinga.

John Heche

35,167 görüntüleme • 20 gün önce

HecheJohn's profile picture

Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara.. Maneno muhimu kutoka kwako: Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari? Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika. Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika. Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko? 1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar? 2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu, Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika? Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara? Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar? Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya…. Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu? Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao. Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?

John Heche

58,494 görüntüleme • 2 ay önce