
Jambo TV
@Jambotv_ • 959,421 subscribers
Independent News Source | WhatsApp+255767252999
Shorts
Videos

VIDEO: Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Rajabu Maganya, amesema mchakato wa Katiba Mpya ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2030. Maganya amesema mchakato huo hauwezi kukamilika ndani ya mwaka mmoja, lakini ameeleza kushangazwa na baadhi ya vyama vya siasa na watu wanaohamasisha wananchi kupigania Katiba Mpya kana kwamba imezuiwa. "Ni nani aliyezuia Katiba Mpya? Ni nani amesema hakutakuwa na Katiba Mpya?" amehoji Maganya, akisisitiza kuwa Serikali na CCM hazijawahi kutangaza kuwa mchakato huo hautafanyika. Maganya ametoa kauli hiyo leo, Julai 24, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la Sinza, Wilaya ya Ubungo. Kauli yake imeibua mjadala miongoni mwa Watanzania, ikitolewa siku ambayo Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, pia alizungumzia suala la Katiba Mpya wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa wanachama wa watetezi wa haki za binadamu uliofanyika leo, Julai 24, 2026.
Jambo TV109,411 Aufrufe • vor 4 Tagen

VIDEO: Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Wolfgang Pisa ameeleza kuwa hali ngumu ya kiuchumi imesababisha vijana kukumbwa na msongo wa mawazo, kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa ajili ya malengo yao, na shinikizo la kuhama nchi kutafuta fursa, jambo ambalo ni hatari ikiwa hawatatayarishwa vizuri. Akizungumza hivi karibuni kando ya Mkutano Mkuu wa 21 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) ulifanyika jijini Nairobi, Kenya, Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, amesisitiza kuwa kuna haja ya kuongea na vijana mara kwa mara kupitia njia tofautitofauti ikiwamo mitandao ya kijamii na kuwahamasisha kutumia mitandao hiyo vyema. “Wengine wahanga wa mazingira kwasababu ya uchumi, na moja ya matatizo makubwa ni mambo mawili ambapo kutokana na hizo changamoto, moja ni wanasiasa, wanasiasa wanaotumia vijana kufikisha malengo yao, lakini vijana kwasababu hawana uchaguzi mkubwa katika uchumi wakati mwingine ni aidha nijiunge au nitakufa njaa”, ameeleza Pisa.
Jambo TV19,060 Aufrufe • vor 22 Stunden

VIDEO: "Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", - Dkt. Nchimbi. Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Julai 24, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDCOALITION unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Jambo TV82,498 Aufrufe • vor 5 Tagen

VIDEO Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex jijini Dodoma ameibua kilio kuhusu kudorora kwa biashara, akieleza kuwa ukosefu wa wateja pamoja na mzunguko mdogo wa fedha umeendelea kuathiri shughuli za wafanyabiashara wengi ndani ya soko hilo. Akizungumza mbele ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo leo Julai 22, 2026, mfanyabiashara huyo amesema hali ya biashara imekuwa ngumu kwa kiwango cha kuathiri mapato ya wafanyabiashara, huku baadhi yao wakilazimika kukaa muda mrefu madukani bila kupata wateja. “Mheshimiwa, hela ziko wapi? Hela hamna. Unakaa dukani unasinzia kwasababu hakuna wateja. Mzunguko wa fedha hamna, soko limeelemewa,” amesema mfanyabiashara huyo. Akijibu hoja hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema wakati Serikali ilipojenga Soko la Machinga Complex haikutarajia ongezeko kubwa la wafanyabiashara waliokuja kufanya biashara katika eneo hilo. Amesema Serikali inaendelea na mpango wa kujenga masoko mengine katika maeneo mbalimbali ili kupanua fursa za biashara, kupunguza msongamano wa wafanyabiashara na kuweka mazingira bora zaidi ya kufanyia biashara nchini.
Jambo TV71,347 Aufrufe • vor 7 Tagen

VIDEO: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amebainisha kuwa ni vigumu kwa mtetezi wa amani kuwa adui wa haki, au mtetezi wa haki kuwa adui wa amani, kwani mambo haya mawili yanategemeana. Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDCOALITION unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 24, 2026, Dkt. Nchimbi amewahimiza Watanzania kuacha kuogopa kutamka neno haki kwa sababu maneno yanazaa matendo ya kuitekeleza haki hiyo Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kuona Tanzania ambapo kila mwananchi anajisikia fahari ya Utanzania wake, amani, na usalama akiwa ndani ya nchi yake. Amesema ingawa kuna utofauti wa itikadi za kisiasa, dini, na makabila, ni muhimu Watanzania watambuane kwa utaifa wao kwanza ili kila mmoja awe na hamu ya kuchangia maendeleo ya nchi.
Jambo TV43,748 Aufrufe • vor 5 Tagen

VIDEO: Makamu wa Rais wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kuongeza juhudi kupambania katiba mpya katika wakati huu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya kuitaka. Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa huu ni wakati sahihi kwani Rais anayefuata huenda asiitake katiba mpya(kama haijapatikana) kutokana na hii iliyopo kuwa inampa mamlaka makubwa. Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema hayo leo Julai 24, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDCOALITION unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Jambo TV38,404 Aufrufe • vor 5 Tagen

VIDEO: Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini amekiasa chama hicho kutumia vyombo vyake vya ndani kufanya uchunguzi wa tuhuma za kifedha ili kuwasafisha viongozi na kuimarisha imani ya wanachama wake. Akizungumza hivi karibuni kutokana na tuhuma za ubadhirifu dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara, John Heche ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambao wengine wamesimamishwa na uongozi wa CHADEMA kwa kuhoji suala hilo, Selasini amesisitiza kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kuwa tofauti na CCM kwa kile alichokiita kuficha mambo. Amedai kuwa upinzani unaikosoa CCM kwa kuficha mambo, hivyo ni lazima wao waoneshe mfano kwa kuwa wawazi zaidi katika taratibu zao. “Ninachosema tu ni kwamba tumemsikia Katibu Mkuu na kwasababu chama chetu ni chama cha kidemokrasia ni matumaini yangu kwamba hilo jambo litawekwa wazi zaidi kwa maana kwamba chama kina vyombo. Sasa kama kina vyombo ili kuwa-contain wanachama, kuwaleta wanachama pamoja, kuleta ule uaminifu wa pamoja ni vizuri vile vyombo vikafanya kazi yake na kazi ikiwa nzuri maana yake viongozi wanasafishika”, ameeleza Selasini”, ameeleza Selasini. Hata hivyo, akizungumza na wanahabari Julai 10, 2026, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alisema kama kuna mwanachama yeyote wa chama hicho ambaye ana taarifa zozote za malalamiko anapaswa kufuata taratibu za kikatiba za chama hicho na Zaidi akaeleza kuwa walikuwa na taarifa kuwa wale ambao wamekuwa wakitoa tuhuma dhidi ya viongozi wamekuwa wakilipwa fedha mpaka milioni mbili kwa lengo la kuchafua viongozi.
Jambo TV104,760 Aufrufe • vor 15 Tagen

VIDEO: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kumtambua mwanaharakati yeyote kwa uwezo wake wa kufikiri na kushawishi akisisitiza kuwa anatamani pia kujenga taifa ambalo watu wenye mitazamo tofauti wanaweza kukaa pamoja na kuzungumza mambo ya nchi yao kwa amani, bila kuwepo kwa uhasama au uadui. Dkt. Nchimbi ameeleza matamanio hayo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 24, 2026, Dkt. Nchimbi Aidha, ametoa wito kwa kila Mtanzania kutumia nafasi aliyonayo kurudisha umoja na mshikamano, pamoja na kusimamia haki kama msingi wa amani.
Jambo TV34,021 Aufrufe • vor 5 Tagen

VIDEO: Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kuwa watuhumiwa 36 kati ya 130 waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wamefikishwa mahakamani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania, watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu vilivyohusisha vurugu, uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani. Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya watuhumiwa walihusishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano katika kuhamasisha mikusanyiko isiyofuata sheria, kusambaza jumbe za uchochezi pamoja na kuandaa mipango ya vitendo vya uhalifu. Aidha, Jeshi la Polisi limesema ushahidi uliokusanywa unaonyesha kuwepo kwa tuhuma za kupanga na kushiriki vitendo kama vile kuchochea vurugu, kushambulia watu, kuharibu mali za umma na binafsi, pamoja na kuzuia utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya dola. Kati ya waliokamatwa, baadhi walifikishwa mahakamani katika mikoa mbalimbali, huku wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi kutokana na ushahidi unaoendelea kukusanywa. Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kulindwa nchini. Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime leo Jumapili Julai 26, 2026.
Jambo TV18,664 Aufrufe • vor 2 Tagen

VIDEO: Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amewataka vijana kuacha kulalamika na badala yake kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi, huku akieleza kusikitishwa na baadhi ya watu wanaowahamasisha vijana kutoa fedha walizonazo kuwapatia wao. Msigwa amesema hayo jana jijini Dodoma wakati alipotembelea Soko la Machinga Complex na kukutana na wafanyabiashara, ambapo alisisitiza kuwa Tanzania ina fursa nyingi zinazoweza kuwainua vijana kiuchumi ikiwa wataamua kuzitumia ipasavyo badala ya kupoteza muda katika mambo yasiyo na manufaa. "Tuwasikilize wanaotuelekeza kupata pesa, tusiwasikilize wanaotuelekeza kufanya fujo, mambo ambayo mwisho wa siku hayakupi pesa," amesema Msigwa.
Jambo TV26,549 Aufrufe • vor 6 Tagen

VIDEO: “Si walisema wanamweka Lissu ndani chama kitakufa, kimekufa? Ndiyo kinakuwa cha moto zaidi kabisa, wakimweka Heche…atakuja Chagulani, atakuja Obadi atakuja nani…yaani huu moto umeshawaka hakuna namna ya kuuzima, watamwachia kama walivyomkamata”, - Heche. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche ameeleza hayo Jumamosi, Julai 25, 2026, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusu viongozi na wanachama kadhaa wa chama hicho wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini kwa tuhuma za ugaidi ambapo pia amedai kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu ina msukumo wa kisiasa, akishangaa namna kesi hiyo inavyochukua muda mrefu kumalizika.
Jambo TV13,857 Aufrufe • vor 3 Tagen

VIDEO: Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, kimeitaka Serikali kutoa majibu juu ya mustakabali ya bei ya Tumbaku kushuka, hali ambayo imekua ikisababisha wakulima wa zao hilo kutokuona tija ya Kilimo kutokana na gharama za uzalishaji kuwa ni kubwa, tofauti na bei wanayoikuta sokoni. Maagizo hayo ya Chama yametolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba, jana Julai 24, 2026 akiongozana na Kamati ya siasa CCM Mkoa, wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani Kaliua ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa kipindi cha Miezi 6 . Nkumba, ameitaka Serikali kuona namna bora ya kuhakikisha Wakulima kujua bei ya zao hilo kabla ya kuanza kwa masoko, ili kumpa urahisi mkulima wa kujiandaa vyema na msimu mpya wa kilimo "Tumeelekeza kwamba Serikali lazima ije na majibu na baadhi ya maelekezo tunataka sasa utaratibu ubadilike, badala ya wakulima wetu kwenda sokoni wakiwa hawajui bei ya Tumbaku tunataka wajue bei " Nkumba alisema
Jambo TV13,530 Aufrufe • vor 4 Tagen

VIDEO: "Wazo hili kwa CHAUMMA la kuchangia ni geni, je, hii sio tonetone? Hii sio tonetone, huu ni mchango kwaajili ya CHAUMMA, wa tonetone wapo lakini hii ni operesheni kwaajili ya kuichangia CHAUMMA, na huwezi kusema kuchangia kumeigwa mahali fulani kwani Tanzania anayechangisha fedha ni chama kimoja tu? Mbona harusi watu wanachangia, nayo ni tonetone?”, Kigaila. Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma ((CHAUMMA), Benson Kigaila ameeleza hayo leo Julai 21, 2026 Jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuzindua kampeni mpya ya chama hicho ya "Tujenge Pamoja,Tanzania ni Sisi".
Jambo TV21,263 Aufrufe • vor 7 Tagen

"changieni chama nisiwakute nilipowaacha, tutagombana" Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akimwambia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wakili Deogratius Mahinyila leo mahakamani. Lissu ameupongeza uongozi wa chama hicho kwa kuendelea kufanya kazi bila ya uwepo wake huku akiwataka kuongeza juhudi bila kumsubiri yeye atoke gerezani.
Jambo TV17,721 Aufrufe • vor 7 Tagen

VIDEO: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameeleza kuwa amani, utulivu, na mshikamano wa taifa si mambo ya kufanyia mchezo au majadiliano kwani amani ya nchi imejengwa kwa jasho, uzalendo, damu, na hekima za waasisi wa taifa la Tanzania, hivyo serikali haitakubali mtu yeyote mwenye nia ovu aivuruge. Dkt. Mwigulu amesema hayo Jumapili, Julai 5, 2026 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya fainali za Shindano la Vijana Uchumi Challenge 2026 na utoaji wa tuzo kwa washindi, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa amani ikivunjika, mwathirika wa kwanza ni mkazi wa eneo hilo husika hivyo kila mwananchi, na hasa vijana wana wajibu wa kuilinda amani hiyo. Amedai kuwa serikali ina vyanzo sahihi vya taarifa za watu wanaoratibu vurugu akitoa mfano wa mtu mmoja aliyekamatwa na kukiri kuwa na mpango wa kushawishi vijana kufanya vurugu kwa ahadi za kulipwa. Aidha Waziri Mkuu amedai kuna mipango ya watu kutumia mabomu na silaha ili kusababisha vifo, kisha kusingizia kuwa ni Jeshi la Polisi au serikali ndiyo imehusika na mauaji hayo. Kutokana na hilo, amesema serikali itachukua hatua kali sana dhidi ya michezo hiyo ya kuvuruga amani.
Jambo TV47,317 Aufrufe • vor 23 Tagen

VIDEO: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro kimeitaka mamlaka ya chama hicho kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma za kifedha zinazomkabili Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, John Heche na kutoa majibu rasmi ili kuondoa sintofahamu miongoni mwa wanachama na wananchi wa Tanzania. Akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Julai 9, 2026, Katibu wa CHADEMA mkoani humo Barnabas Okola ameeleza kuwa viongozi wa Chadema ni binadamu na siyo malaika, na hivyo wanapaswa kuongozwa na kanuni na taratibu za chama na kwamba ikiwa tuhuma hizo ni nzito, ingekuwa vyema hata Makamu Mwenyekiti akajivua nafasi yake kwa muda ili ukweli ubainike. Okola amebainisha kuwa uvumi kwenye mitandao ya kijamii ambao umekuwa ukidai kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema amekuwa akipokea michango ya "tonetone" kutoka kwa wadau lakini haifikishi kwenye chama si wa afya kwa chama, akisisitiza kuwa jambo hili ni lazima lizungumzwe na kutolewa ufafanuzi kwa sababu lisiposemewa, linaweza kuonekana kuwa ni kweli.
Jambo TV37,193 Aufrufe • vor 20 Tagen

VIDEO: Shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tanzania Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona limeahirishwa kwa muda wa lisaa limoja (saa saba na nusu mpaka saa nane na nusu mchana) kutoa mapumziko. Leo ilikuwa ni zoezi la kuhoji maswali ya dodoso ambapo tayari Lissu amemhoji shahidi wa pili katika kesi ambaye ni Nashon Nkungu na shahidi wa tatu Paul Kisabo. Wakili Nashon Nkungu alihojiwa maswali ya dodoso (Cross Examination) na Lissu baadae akaulizwa na upande wa mjibu maombi wa kwanza mpaka wa tatu kisha maswali ya kusawazisha na wakili wao Edson Kilatu hivyo zoezi la ushahdi wake limekamilika ambapo kwa upande wa Kisabo ameulizwa maswali ya dodoso na Lissu pekee baada ya mapumziko zoezi litaendelea. Shauri hili la kikatiba na 7300/2026 limefunguliwa Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo na linasilkilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Longopa
Jambo TV15,759 Aufrufe • vor 8 Tagen

VIDEO: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani huku ikidhibiti wale ambao wanapanga kufanya matukio yoyote yatakayohatarisha usalama wa nchi. Ametoa kauli hiyo akizungumza na Makundi ya Walinzi wa amani katika jamii, Polisi jamii, Wazee, Sungusungu, Wenyeviti wa Mitaa,Mabalozi na Wenyeviti wa Vitongoji Vitongoji, Shinyanga Mjini. Pamoja na hayo ameeleza kuwa mpaka sasa hajapokea wito wowote kutoka mahakamani kutokana na uwepo wa taarifa za kuwa kuna imefunguliwa dhidi yake. “timu hiyo inayosema inanipeleka mahakamani ndiyo hiyo hiyo ilikua inapinga Mkataba wa Uwekezaji wa bandari...wameshindwa kuwapeleka mahakamani ambao wanachochea kuangamiza Taifa letu kwa kuchoma moto. Kama wana uchungu kweli na haki za Binadamu ni lini na wapi mliwasikia wanakemea vitendo hivyo hatarishi kwa uhai wa watu na Taifa?” amehoji Katambi Kauli ya Katambi inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu Mwanasiasa Dkt. Wilbroad Slaa, Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kutoa taarifa kwa umma kuwa wamefungua kesi dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuhoji juu ya katazo la mikutano ya hadhara lililotolewa na Patrobas Katambi bungeni Juni 26, 2026.
Jambo TV16,328 Aufrufe • vor 9 Tagen

VIDEO: Mchekeshaji na mtengenezaji wa maudhui mtandaoni, Gasper Joseph Kagonda amesema matumizi yake ya neno 'Malawi' kwenye maudhui yake ni lugha ya picha inayotumika kufikisha ujumbe, na si kulenga nchi yoyote moja kwa moja. Akizungumza katika mahojiano na Jambo TV, Gasper amesema maudhui yake yanayochekesha hubeba pia mafunzo na ujumbe kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Tazama mahojiano kamili kwenye Youtube yetu ya Jambo TV
Jambo TV20,748 Aufrufe • vor 14 Tagen