
Jambo TV
@Jambotv_ • 959,191 subscribers
Independent News Source | WhatsApp+255767252999
Shorts
Videos

VIDEO: Kiongozi wa Taasisi ya Asaalam Islamic Foundation Sheikh Muharram Mziwanda ameeleza kushangazwa na Kauli ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuwa kilichofanyika Oktoba 29, 2025 ilikuwa maandamano na si vurugu, uharibifu na wizi kama ilivyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, akiitaka TEC kuachana na matamko aliyodai kuwa yanachochea ghasia na hasira. Sheikh Mziwanda amebainisha hayo Jumapili Novemba 16, 2025 Jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari, akirejea kauli ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa waliowahi kueleza kuwa Oktoba 29 wangekinukisha, kufanya uasi na kuvuruga uchaguzi mkuu. Akirejea kauli ya Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, Sheikh Mziwanda amehoji lilipokuwa baraza hilo wakati kile alichokiita kauli za chuki, hasira na hamasa zilipokuwa zikitolewa na baadhi ya wanasiasa, huku pia akieleza kusikitishwa na namna ambavyo TEC hawajaeleza chochote kuhusu uharibifu na wizi wa mali za umma na za watu binafsi uliotokea hapo Oktoba 29. "Kuna wakati hadi unauliza au baraza linahusika? kwasababu mapito wanayopita TEC yanatutia mashaka. Na mimi niwazindue wananchi kwamba yale hayakuwa maandamano kwa mujibu wa waasisi wa tukio lile kwasababu wao walisema wanaenda kukinukisha. Mimi niombe hata kama viongozi wa dini tunashiriki kwenye harakati basi tuzingatie harakati zenye maslahi kwa nchi yetu." Amesema Sheikh Mziwanda. Mziwanda ameliomba Baraza la Maaskofu kusimama katika nafasi yao ya kushirikiana na serikali katika kuijenga nchi, akiwataka yale yote yanayoashiria amani waliunge mkono na yote yenye kuhatarisha amani wayakemee ikiwamo kauli zilizokuwa zikitolewa mapema za kuhamasisha na kutangaza kuhusu vurugu na ghasia hizo za Oktoba 29, 2025.
Jambo TV217,777 views • 6 months ago

VIDEO: Hapa ni Itega Jijini Dodoma nyumbani kwa marehemu Jenista Mhagama, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mkoani Ruvuma ambaye amefariki dunia leo Desemba 11, 2025 akiwa jijini humo. Tangu taarifa za msiba kutolewa, waombolezaji, viongozi wa Serikali pamoja na Wabunge mbalimbali wameendelea kufika nyumbani hapa kutoa pole na kushiriki katika shughuli za maombolezo. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu Msiba huu.
Jambo TV134,078 views • 5 months ago

VIDEO: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe Freeman Mbowe amesema uongo kuwa waliwahi kufanya mazungumzo ya iwapo anahitaji kugombea nafasi hiyo ama la ," yeye alitaka vyote awe Mwenyekiti na agombee Urais" Lissu ameyasema hayo mapema leo mchana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea nje ya Nchi
Jambo TV344,558 views • 1 year ago

VIDEO: “Tumejiwekea malengo mahususi ya kuhakikisha tunakomesha shughuli ya kujiuza kwa madada poa na makaka poa katika maeneo yote ya wilaya ya Ubungo, ni vyema na wakati ni sasa kwa jamii yetu yote kuhakikisha tunalinda maadili yetu Watanzania- DC Bomboko Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko akizungumza wakati wa operesheni ya kutokomeza biashara ya ukahaba wilayani humo.
Jambo TV461,719 views • 2 years ago

VIDEO: Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameibua madai kuwa wamebaini uwepo wa wachochezi na wanaharakati wanaolipwa ili kuvuruga amani ya nchi, akidai kwamba baadhi ya vijana wanaoishi nje ya Tanzania wamepokea dola milioni mbili (sawa na shilingi bilioni 4.5) kwa ajili ya kuchochea vurugu. Ametoa kauli hiyo akiwa katika ziara yake mkoani Arusha, leo Novemba 30, 2025 ambapo amesema uchochezi mwingi unatoka kwa watu waliopo nje ya nchi na kwamba malengo yao yamejikita kwenye rasilimali za taifa. Ameeleza kuwa juhudi za kujaribu kuwavuruga Watanzania zinatokana na rasilimali zinazogunduliwa nchini, ikiwemo uranium ambayo Tanzania sasa inakadiriwa kuwa na tani 890,000 za ujazo, na hivyo kuwa nchi ya tisa duniani na ya kwanza Afrika. “Wanalenga tupigane ili wachukue rasilimali. Tumeshuhudia hili likiharibu mataifa mengi ya Afrika,” amesema. Amani ikitoweka, hata karoti na nyanya za Ngarenanyuki haziwezi kuuzwa,” ameonya. Ametoa wito kwa Watanzania kukataa kurudishwa katika vurugu, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa kupambana na umaskini na kukuza ajira nchini.
Jambo TV139,470 views • 6 months ago

VIDEO: Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Adbul (Diamond Platnumz) ameilalamikia Serikali ya Tanzania kuwa imewekeza nguvu kubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu huku ikiudharau muziki na kuukumbuka kwenye kampeni pekee. Ameeleza hayo leo Machi 31, 2026 kwenye mahojiano maalum na kituo cha Wasafi FM akieleza kuwa muziki unapuuzwa sana na hata ushauri wa ujenzi wa Arena kaa ajili ya matukio makubwa ya kimziki haufanyiwi kazi pamoja na kwamba ni muhimu sana. "Wanaweka nguvu sana kwenye mpira ila kwenye mziki wana dharau sana mshikaji wangu sisi tunaonekana tu kwenye kampeni yani hapo tupo 'serious' ila baada ya hapo ila baada ya hapo miundombinu aaah" amesema Diamond Platnumz
Jambo TV49,289 views • 2 months ago

VIDEO: Mbunge Mteule wa Viti Maalum kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, amesema hajafurahishwa na uteuzi wake wa nafasi hiyo, akidai kuwa alinyang’anywa ushindi wa Ubunge wa Jimbo na kupewa nafasi ya ubunge wa Viti Maalum. Mligo ametoa kauli hiyo leo, Novemba 10, 2025, katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya kujisajili kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13, unaotarajiwa kuanza Novemba 11, 2025. Mligo amesema hajafurahishwa na namna alivyoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Mkoa wa Njombe, hasa katika kipindi ambacho Watanzania wanapitia hali ngumu ya Kisiasa na Kijamii. "Wakati mimi naapishwa, kuna watu Mtaani wamezika ndugu zao, watu wamekufa. Taifa liko kimya. Mimi sijafurahia kuwa Mbunge katika Bunge ambalo taifa linavuja damu,” amesema Bi. Mligo. Aidha, ameeleza kuwa ataingia Bungeni kama Mbunge wa Kitaifa mwenye dhamira ya kuwasemea Wananchi wasio na sauti, akisisitiza kuwa atapigania demokrasia, haki na utawala wa sheria, badala ya kufuata maagizo bila kuhoji.
Jambo TV129,603 views • 6 months ago

VIDEO: Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini, limelaani vikali vitendo vya uhalifu vilivyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na kuisihi serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo na vinara wa machafuko hayo. Katika tamko lililotolewa siku ya Alhamisi, viongozi wa taasisi hizo wamesema tukio hilo limeacha majonzi makubwa kutokana na vifo vya watu wasio na hatia, ulemavu wa kudumu, na uharibifu wa mali na miundombinu ya umma na binafsi. Viongozi hao wameeleza kuwa kabla ya uchaguzi mkuu, walifanya jitihada kubwa kuhimiza utunzaji wa amani, wakisisitiza kuwa kudai haki ni jambo la msingi, lakini lisifanywe kwa njia zinazohatarisha usalama wa taifa. BAKWATA imeiomba serikali kuwa na jicho la huruma kwa familia zilizopoteza ndugu zao, waliojeruhiwa au kuathirika kwa njia yoyote katika machafuko hayo, huku ikiitaka pia kuchukua hatua dhidi ya wale ‘waliowachochea vijana kujiingiza kwenye vurugu’. Aidha, tamko hilo limehimiza serikali kuzingatia suluhu na maridhiano pale inapobidi, kwa maslahi mapana ya taifa. Hata hivyo, viongozi hao wameonya kuwa maridhiano yasitumike kama zawadi kwa watu waliotenda uhalifu, wakisema vitendo vya namna hiyo havipaswi kufumbiwa macho. Aidha viongozi wa Kiislamu hao wamempongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa kishindo wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo huku wakimtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake.
Jambo TV124,656 views • 6 months ago

Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Nusrat Hanje amesema hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuia uchaguzi nakudai uchaguzi utafanyika nakuwataka watu kuacha kuwapa kiki Wanaodai wanauwezo wakudhibiti Uchaguzi ujao. Hanje ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 10,2025 bungeni Jijini Dodoma Wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2025/2026. Amesema “Hakuna mtu mwenye uwezo wa kudhibiti uchaguzi , pale CHADEMA hakuna hata wapiga kura milioni tano huwezi ukawambia Wazunguke Mikoani wakatafute saini milioni 15 , hakukuwa na haja ya kutumia nguvu nawala hawana pesa zakuzunguka kwenye mikoa kufanya Mikutano ya hadhara ,” Hanje pia ameipongeza serikali kwa udhibiti wake wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya, akiiomba kuendeleza jitihada za uthibiti wa dawa hizo kutokana na madhara yake makubwa katila kuua nguvu kazi ya Vijama wa Kitanzania.
Jambo TV204,647 views • 1 year ago

VIDEO: Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Ali Kawaida amelaani maandamano yaliyotokea Oktoba 29, ambapo amesema waliochochea maandamano hayo wako nje ya nchi na wengine sio Watanzania na wale ambao ni Watanzania hawana mpango wa kurudi nchini na wamefanya hivyo kwakuwa wamelipwa ili kuvuruga amani iliyopo Tanzania.
Jambo TV107,392 views • 6 months ago

VIDEO: Shura ya Maimamu na Viongozi wa taasisi za Kiislamu Mkoani Arusha imetoa tamko la kulaani machafuko ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe ili kurejesha na kulinda amani ya nchi. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Arusha, mlezi wa Shura hiyo, Sheikh Juma Ikusi, amesema machafuko yaliyotokea yameacha majereha na kuchafua taswira ya taifa lililojengwa kwa misingi ya umoja na mshikamano tangu enzi za waasisi wa taifa. Katika tamko hilo, Sheikh Ikusi pia alionyesha kukerwa na baadhi ya matamko kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), akidai kuwa baadhi ya kauli zao zilichochea Mazingira ya vurugu wakati wa uchaguzi. “Maaskofu wa TEC sasa wameingia katika mrengo wa kisiasa nchini? Inasikitisha sana pale ambapo maaskofu wanaomba watu kutoka nje ya nchi, ambao waliwahi kututawala na kutunyonya, waje kufanya uchunguzi,’” Sheikh Ikusi alisema Aidha, Sheikh Ikusi amesema kuwa katika dini ya Kiislamu, amani ndiyo msingi mkuu unaopewa kipaumbele zaidi kuliko haki, na hivyo amewasisitiza Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Jambo TV99,939 views • 6 months ago

VIDEO: Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi. Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili. Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue. “mama mmoja amenipigia simu eti Baba nimeambiwa hapa hospitali wameishiwa gloves wameishiwa vifaa vitakavyonisaidia mimi kujifungua wamesema nilipe 50,000/= ili nichangie kwenda kununua vitu vitakavyonisaidia kujifungua” Chalamila anasema baada ya mama huyo kutokuwa tayari kununua vifaa akamwambia aende akajifungue nyumbani “Nikamwambia Mama pole kwanza hiyo siyo haki toka nje chukua bajaji nenda zako nyumbani kamwambie mumeo achukue kisu na mikasi akusaidie kujifungua” Aidha amefafanua lengo la kumwambia hivyo ni kwa sababu sio nyakati zote vifaa vipo na pia kuna nyakati inabidi mgonjwa aangalie hali yake kwanza na namna ya kujisaidia kabla ya kulalamika.
Jambo TV211,406 views • 1 year ago

VIDEO: Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi. Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, amesema kuwa amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutumia nguvu bali kwa maridhiano na haki, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani ya nchi kwa kuhakikisha mifumo ya uchaguzi inarekebishwa ili kutoa nafasi kwa upatikanaji wa viongozi wa haki na wa kweli. “Katika hali ya kawaida, nani anaharibu amani? Anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema ‘jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi kwani mifumo ya sasa haiwezi kutupatia viongozi wa haki na kweli’?” amehoji Askofu Pisa. Akizungumza katika mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi, Askofu huyo amesema kuwa kama kurudi mezani ndiko kunakoweza kulinda amani, basi kila anayehamasisha hilo anapaswa kuungwa mkono, si kukandamizwa au kukamatwa. “Kwa maana hiyo wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti, na wengine wasikamatwe wala kusumbuliwa. Pia mihimili isiingiliwe bali itende kazi zake kwa haki,” amesisitiza. Amesema kuwa amani ni tunu adhimu inayopatikana kwa gharama kubwa, hivyo haipaswi kuchezewa, huku akisisitiza kuwa taifa linapaswa kuikataa dhana ya kuimba wimbo wa amani isiyotokana na haki. Kauli ya Askofu Pisa imekuja wakati ambapo mjadala wa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa ukitawala anga ya kisiasa nchini, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kukamatwa kwa viongozi wao wakubwa akiwamo Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu , na ukosefu wa haki katika uendeshaji wa siasa.
Jambo TV175,319 views • 1 year ago

VIDEO: UVCCM wamtumia salamu Mange Kimambi, "akirudi Nchini tutagawana mbavu zake"
Jambo TV385,469 views • 3 years ago

VIDEO: Tumefika hapa Area D jijini Dodoma, nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi. Lukuvi amefariki dunia leo asubuhi, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambako alikuwa akipatiwa matibabu kufuatia tatizo la mshtuko wa moyo. Katika mahojiano msibani hapa, Mbunge wa Jimbo la Kilolo na Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati, ameonesha masikitiko yake makubwa kufuatia msiba huu mzito.
Jambo TV39,025 views • 2 months ago

VIDEO: Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye pia ni mwanafamilia wa marehemu Mzee Edwin Mtei, amejibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa mitandaoni zikidai kuwa CHADEMA haijapewa nafasi na hadhi inayostahili katika taratibu za kumuenzi muasisi wa chama hicho kabla ya mazishi yake. Akizungumza na waandishi wa habari, Mbowe amesema anasikitishwa na taarifa hizo akizitaja kuwa ni za uongo na zenye nia ya kuuchafua msiba huo, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu wala kundi lililotengwa katika maandalizi ya mazishi ya marehemu Mzee Mtei. Mbowe amesema familia inapenda kuona mwili wa marehemu ukipumzishwa kwa amani bila malumbano yoyote, akibainisha kuwa CHADEMA imepewa nafasi kubwa katika taratibu zote kuanzia zoezi la kuuchukua mwili Mochwari hadi shughuli za kumuaga na kumuenzi marehemu. Ameongeza kuwa watu wengi waliopo msibani hapo ni wanachama na viongozi wa CHADEMA, jambo linalothibitisha kuwa chama hicho kimehusishwa kikamilifu katika kila hatua ya maandalizi ya msiba huo. “Ninasikitishwa na baadhi ya watu wanaotaka kuuchafua msiba huu kwa kutoa taarifa za uongo. Hakuna aliyebaguliwa wala kutengwa. Kila mtu amepewa nafasi ya kumuenzi Mzee Mtei,” amesema Mbowe. Mazishi ya Mzee Edwin Mtei yanatarajiwa kufanyika kesho, Jumamosi, katika makaburi ya nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha.
Jambo TV64,872 views • 4 months ago

VIDEO: Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema moja ya sababu iliyomuwezesha mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) ambaye ni yeye mwenyewe kupata ushindi wa asilimia zaidi ya 97% ni pamoja na kutokuwepo kwa upinzani mkubwa lakini pia wafuasi wa vyama vya upinzani kuipigia kura CCM. Ameyasema hayo leo Disemba 02, 2025 alipokuwa akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar Es Salaam na kueleza kuwa vyama vilivyoshiriki uchaguzi havikuwa na nguvu kubwa kama hao wapinzani wawili. "halafu wanahoji kwa nini asilimia 97% wao walikuwepo? wao hawakuwepo na wale 16(vyama 16 vilivyokuwa na wagombea Urais) waliokuwepo ni wadogo sana ambao wangetingisha CCM hawakuwepo hakukuwa na CHADEMA hakukuwa na ACT ndiyo ambao tungeenda nao" amesema Dkt. Samia
Jambo TV83,660 views • 6 months ago

VIDEO: “Kizazi chetu kina GMO nyingi sana-Genetically Modified Organism au kiswahili tungeweza kusema labda ni viumbe ambavyo vimebadilishwa vile vinasaba na kwa sababu hiyo wanaishi nje ya vinasaba vyao. Tuna GMO ambao ni mapadri, tuna GMO waamini, tuna GMO watawa, wanaishi kinyume na utofauti na kile ambacho wanapaswa kukiishi, lakini pia waamini GMO wako wengi. Siku za hivi karibuni nilisikia kina GMO wakiwa wanaandamana kwenda kwenye ofisi fulani, hao ni GMO hawa, wa ajabu kabisa, unaenda kufanya nini? Wamepoteza ule uhalisia wao ile identity, wanakubali kununuliwa ili waende kuchafua kazi ya Mungu. Ninyi tunawaomba mkapambane na hao GMO lakini hakikisheni kwanza nyinyi wenyewe sio GMO. Hakikisheni kuwa mnawarudisha katika uhalisia ili kila kitu kinachofanywa kifanywe chini ya mwamvuli wa Mungu ambaye ni mwema na mwenye haki. Wafundisheni watu hao. Katika majukumu yenu, pia mtapaswa kwa namna ya pekee sana kutoa sakramenti ya ubatizo, nendeni mkawafundishe”, Askofu Kibozi Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Wilbroad Henry Kibozi akizungumza wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya utoaji wa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa waliokuwa mafrateli 9 wa Metropolitani ya Dodoma katika Parokia ya Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mt. Paulo wa Msalaba, Alhamisi Januari 8, 2026.
Jambo TV66,457 views • 4 months ago

VIDEO: Mzee John Samwel Swai(61) mstaafu wa Jeshi la Polisi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia asiondolewe katika kambi anayoishi kwani bado hajalipwa fedha za mizigo pamoja na fedha za likizo ambazo anapaswa kulipwa. Mzee huyo alistaafu mwaka 2020 baada ya kutumikia jeshi la polisi kuanzia mwaka 1983 amedai kupewa barua na Mkuu wa Kambi za Polisi inayomtaka kuhama ndani ya siku saba kuanzia Februari 04 mpaka leo Februari 10 na endapo asipohama vitu vyake vitatolewa nje. Kupitia barua aliyopewa tarehe nne mwezi huu imesema “Umeariwa kukabidhi nyumba tajwa hapo juu, kwani umeshastaafu kazi toka 2020. Oc Barracks amekuamuru kukabidhi nyumba tajwa hapo juu kwa kuwa umestaafu kazi. Umepewa siku 07 kuanzia leo tarehe 04/02/2025 hadi 10/02/2025 uwe tayari umekabidhi nyumba hiyo, Kushindwa kutekeleza amri hii, vitu vyako vitatolewa nje, hivyo unaamriwa kuviondoa mwenyewe kabla ya kutolewa” Mzee Swai amewaomba wasaidizi wa Rais ambao Jeshi la Polisi lipo chini yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kumsaidia wakati huo serikali ikiendelea kushuhulikia malipo yao. Jambo TV imefanya jitihda za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime kwa njia ya simu lakini jitihada hazikuzaa matunda. NB: Video kamili inapatikana Youtube.
Jambo TV177,787 views • 1 year ago