Jambo TV's banner
Jambo TV's profile picture

Jambo TV

@Jambotv_959,191 subscribers

Independent News Source | WhatsApp+255767252999

Shorts

Tupate wadhamini kidogo kabla ya kwenda kula biriyani pale kwa Shilole #ShishiFood

Tupate wadhamini kidogo kabla ya kwenda kula biriyani pale kwa Shilole #ShishiFood

71,943 次观看

Videos

Jambotv_'s profile picture

VIDEO: Kiongozi wa Taasisi ya Asaalam Islamic Foundation Sheikh Muharram Mziwanda ameeleza kushangazwa na Kauli ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuwa kilichofanyika Oktoba 29, 2025 ilikuwa maandamano na si vurugu, uharibifu na wizi kama ilivyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, akiitaka TEC kuachana na matamko aliyodai kuwa yanachochea ghasia na hasira. Sheikh Mziwanda amebainisha hayo Jumapili Novemba 16, 2025 Jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari, akirejea kauli ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa waliowahi kueleza kuwa Oktoba 29 wangekinukisha, kufanya uasi na kuvuruga uchaguzi mkuu. Akirejea kauli ya Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, Sheikh Mziwanda amehoji lilipokuwa baraza hilo wakati kile alichokiita kauli za chuki, hasira na hamasa zilipokuwa zikitolewa na baadhi ya wanasiasa, huku pia akieleza kusikitishwa na namna ambavyo TEC hawajaeleza chochote kuhusu uharibifu na wizi wa mali za umma na za watu binafsi uliotokea hapo Oktoba 29. "Kuna wakati hadi unauliza au baraza linahusika? kwasababu mapito wanayopita TEC yanatutia mashaka. Na mimi niwazindue wananchi kwamba yale hayakuwa maandamano kwa mujibu wa waasisi wa tukio lile kwasababu wao walisema wanaenda kukinukisha. Mimi niombe hata kama viongozi wa dini tunashiriki kwenye harakati basi tuzingatie harakati zenye maslahi kwa nchi yetu." Amesema Sheikh Mziwanda. Mziwanda ameliomba Baraza la Maaskofu kusimama katika nafasi yao ya kushirikiana na serikali katika kuijenga nchi, akiwataka yale yote yanayoashiria amani waliunge mkono na yote yenye kuhatarisha amani wayakemee ikiwamo kauli zilizokuwa zikitolewa mapema za kuhamasisha na kutangaza kuhusu vurugu na ghasia hizo za Oktoba 29, 2025.

Jambo TV

217,777 次观看 • 6 个月前

Jambotv_'s profile picture

VIDEO: Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini, limelaani vikali vitendo vya uhalifu vilivyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na kuisihi serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo na vinara wa machafuko hayo. Katika tamko lililotolewa siku ya Alhamisi, viongozi wa taasisi hizo wamesema tukio hilo limeacha majonzi makubwa kutokana na vifo vya watu wasio na hatia, ulemavu wa kudumu, na uharibifu wa mali na miundombinu ya umma na binafsi. Viongozi hao wameeleza kuwa kabla ya uchaguzi mkuu, walifanya jitihada kubwa kuhimiza utunzaji wa amani, wakisisitiza kuwa kudai haki ni jambo la msingi, lakini lisifanywe kwa njia zinazohatarisha usalama wa taifa. BAKWATA imeiomba serikali kuwa na jicho la huruma kwa familia zilizopoteza ndugu zao, waliojeruhiwa au kuathirika kwa njia yoyote katika machafuko hayo, huku ikiitaka pia kuchukua hatua dhidi ya wale ‘waliowachochea vijana kujiingiza kwenye vurugu’. Aidha, tamko hilo limehimiza serikali kuzingatia suluhu na maridhiano pale inapobidi, kwa maslahi mapana ya taifa. Hata hivyo, viongozi hao wameonya kuwa maridhiano yasitumike kama zawadi kwa watu waliotenda uhalifu, wakisema vitendo vya namna hiyo havipaswi kufumbiwa macho. Aidha viongozi wa Kiislamu hao wamempongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa kishindo wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo huku wakimtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake.

Jambo TV

124,656 次观看 • 6 个月前

Jambotv_'s profile picture

VIDEO: Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi. Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, amesema kuwa amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutumia nguvu bali kwa maridhiano na haki, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani ya nchi kwa kuhakikisha mifumo ya uchaguzi inarekebishwa ili kutoa nafasi kwa upatikanaji wa viongozi wa haki na wa kweli. “Katika hali ya kawaida, nani anaharibu amani? Anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema ‘jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi kwani mifumo ya sasa haiwezi kutupatia viongozi wa haki na kweli’?” amehoji Askofu Pisa. Akizungumza katika mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi, Askofu huyo amesema kuwa kama kurudi mezani ndiko kunakoweza kulinda amani, basi kila anayehamasisha hilo anapaswa kuungwa mkono, si kukandamizwa au kukamatwa. “Kwa maana hiyo wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti, na wengine wasikamatwe wala kusumbuliwa. Pia mihimili isiingiliwe bali itende kazi zake kwa haki,” amesisitiza. Amesema kuwa amani ni tunu adhimu inayopatikana kwa gharama kubwa, hivyo haipaswi kuchezewa, huku akisisitiza kuwa taifa linapaswa kuikataa dhana ya kuimba wimbo wa amani isiyotokana na haki. Kauli ya Askofu Pisa imekuja wakati ambapo mjadala wa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa ukitawala anga ya kisiasa nchini, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kukamatwa kwa viongozi wao wakubwa akiwamo Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu , na ukosefu wa haki katika uendeshaji wa siasa.

Jambo TV

175,319 次观看 • 1 年前