
Jamii Forums
@JamiiForums • 1,840,856 subscribers
Inform | Engage | Empower | Digital Democracy
Shorts
Videos

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum ameyasema hayo Jumanne, Mei 26, 2026, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano ulioandaliwa na JMAT jijini Dodoma. Kauli hii inakuja siku chache baada ya Maseneta wawili wa Marekani, Jeanne Shaheen na Ted Cruz, kuwasilisha muswada katika Seneti ya Marekani uliotaka Serikali ya Marekani kufanya tathmini ya mahusiano yake na Tanzania. Zaidi tembelea #JamiiForums #Diplomasia #JFDiplomacy
Jamii Forums36,469 views • 13 days ago

DAR: Mchora Katuni ambaye pia amewahi kuwa Mtangazaji wa Redio na TV, Masoud Kipanya ametoa kauli hiyo Mei 15, 2026 akieleza mtazamo wake kuhusu Waandishi wa Habari walioshiriki kuwania nafasi za uongozi kupitia Vyama vya Siasa. Je, Uhuru wa Habari utakuwa hatiani kulingana na mgongano huo wa kimaslahi? Nini maoni yako Mdau? Zaidi bofya #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa Video: Tell A Vision
Jamii Forums33,115 views • 20 days ago

Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu aliyasema hayo katika mahojiano yaliyoruka Mei 9, 2026 na Jenerali Ulimwengu pamoja na Khalifa Said wa The Chanzo kuhusu Ripoti ya Kuchunguza Matukio ya Wakati na Baada ya Oktoba 29, 2025. Fuatilia zaidi #JamiiForums #Uwajibikaji
Jamii Forums28,579 views • 29 days ago

DAR: Ally Mkii amefungua shtaka la Madai Mahakama Kuu, akiitaka Hospitali ya Aga Khan imlipe fidia ya Tsh. Bilioni 1.2, akidai uzembe wa kimatibabu umesababisha Mtoto wake akatwe mguu alipofika hapo kutibiwa Wakili wa Ally, Pasensa Kurubone, amesema Washtakiwa ni Hospitali hiyo na Daktari aliyehusika, ambapo Mahakama imetupilia mbali pingamizi la Hospitali lililotaka shauri lisikilizwe na Mabaraza ya Waganga Upande wa Ally Mkii amesema “Tulimpeleka Aga Khan Tawi la Mbagala, Mwaka 2022, baada ya vipimo tukapelekwa Aga Khan ya Mjini, wakasema ana mvunjiko mdogo, akafungwa POP. Ikatakiwa turudi baada ya Wiki 3, hali ikawa mbaya tukarudi baada ya Wiki, ikabainika POP imebana na kushindwa kupitisha Damu” JamiiForums imewasiliana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Aga Khan, Olayce Lotha aliyesema “Suala lipo chini ya Mkurugenzi wa Tiba na Afya pamoja na Wanasheria wetu, nalielekeza kwao kwa taarifa na ufafanuzi zaidi.” Soma #JamiiForums #Accountability
Jamii Forums217,965 views • 1 year ago

SIASA: Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Mwaka huu (2024) Serikali haitapeleka Huduma ya Dawa, Mbegu wala Wanunuzi kwenye Jimbo la Kisesa kwa kuwa Mbunge wao (Luhaga Mpina) amekuwa akisema Serikali inapeleka huduma feki Bashe ameongeza kwa kusema kuwa atakwenda Kisesa kuwauliza Wananchi ili kama hayo ni mawazo yao huduma hizo zitasitishwa ili Wananchi na Mpina wasimamie suala hilo Soma #JFMatukio #Governance #JamiiForums
Jamii Forums280,848 views • 1 year ago

DAR: Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama umewatia mbaroni raia wa kigeni wenye asili ya Kichina wakiwa na kiasi cha takriban Tsh. Bilioni 6 taslimu zilizokuwa zimefichwa katika "Apartment" Namba 317, ghorofa ya tatu, Jengo la Phoenix, Mtaa wa Mazengo. Aidha, Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Doreen Kapwani amesema “Kesho (Januari 7, 2026) ufafanuzi kamili utatolewa kuhusu tukio hilo kupitia kwa Kamanda wa Polisi Kinondoni. TAKUKURU tulikuwepo na tumeshiriki.” Soma #JamiiForums #Accountability #KemeaRushwa #JFMatukio
Jamii Forums80,102 views • 5 months ago

MBEYA: Mwananchi akiuliza swali akiwa katika Mkutano kati ya Vijana na Viongozi wa Dini kuhusu Haki na Amani Ulioandaliwa na Kamati ya Dini mbali mbali (ISCEJIC) kufuatia Matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025. Mkutano ulifanyika Aprili 16, 2026 ukiongozwa na Sheikh Khamis Mataka wa BAKWATA na kuhudhuriwa na viongozi wa Dini mbalimbali akiwemo Mchungaji Modest Pesha wa CCT. Zaidi #JamiiForums #Uwajibikaji #JFMatukio
Jamii Forums24,745 views • 1 month ago

DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar limesema linawashikilia Watu 8 kwa tuhuma za tukio la Novemba 11, 2024 eneo la Kiluvya ambapo Watu kadhaa walifanya jaribio la kumteka Mfanyabiashara, Deogratius Tarimo, Mkazi wa Kibaha - Pwani Kamanda Kanda Maalum ya Polisi, Muliro J. Muliro - SACP amesema Watuhumiwa wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika Mikoa ya Dar, Songea Ruvuma na eneo la Mbingu Mlimba Morogoro, pia wamekamata gari aina ya Toyota Raum waliyoitumia wakati wa tukio ikiwa na namba T 237 EGE ambayo si halisi, ambapo uchunguzi umebaini namba halisi ni T237 ECF Amewataja waliokamatwa kuwa ni Bato Bahati Tweve (umri Miaka 32 – Bondia), Yusuph Abdallah (32), Fredrick Juma (31), Nelson Elimusa Msela (24 - Dereva Tax), Benk Daniel Mwakalebela ‘Tall’ (40), Thomas Ephraim Mwakagile ‘Baba Mage’ (45), Anitha Alfred Temba (27) na Isack Mwaifani (Bondia) Soma #JFMatukio #JamiiForums #Accountability
Jamii Forums221,697 views • 1 year ago

DAR: Dereva wa Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) ambaye jina lake halijafahamika, akiendesha kutoka kituo cha Gerezani kwenda Kimara, amedaiwa kutosimama kwenye vituo vingi vya njiani baada ya kurushiana maneno na Abiria ambao walilalamikia uendeshaji wake Mdau wa amedai licha ya Basi kujaa, Dereva aliendelea kupakia Abiria ambapo walilalamika kuwa anawaumiza kwa kufungua na kufunga milango, hali iliyoibua ubishani. Baada ya kutoka Kituo cha Magomeni Dereva hakusimama, akawapeleka Abiria wote Kituo cha Kimara Mwisho Anadai walipofika Kimara, Dereva alishuka na kuondoka na baada ya mvutano wa muda mrefu, Dereva mwingine akaamua kuchukua basi husika na kuwarejesha wale waliopitilizwa vituo Soma #JFHuduma #JFUwajibikaji #JamiiForums
Jamii Forums298,633 views • 2 years ago

DAR: Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu Soma #JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Governance #HumanRights #UchaguziMkuu2025
Jamii Forums146,528 views • 1 year ago

DAR: Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA), Abdallah Mhagama ametoa kauli hiyo Aprili 9, 2026 wakati wa mahojiano na Kituo cha Redio cha #RadioOne. Yapi maoni yako Mdau? Shiriki mjadala huu kupitia #JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma
Jamii Forums29,851 views • 1 month ago