
Jamii Forums
@JamiiForums • 1,840,694 subscribers
Inform | Engage | Empower | Digital Democracy
Shorts
Videos

DAR: Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ameyasema hayo Julai 23, 2026 alipokuwa akizungumza na Wananchi kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga wakati wa Tamasha la Kuwafikia na Kuhamasisha Jamii Dhidi ya Dawa za Kulevya, lililoanza kwa matembezi kutoka Azizi Ali hadi Mwembe Yanga. Mdau una maoni gani? Fuatilia zaidi #JamiiForums #Uwajibikaji #Utawala
Jamii Forums45,518 views • 4 days ago

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taaluma UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Enos Shija ameeleza hayo wakati akihojiwa na Kituo cha DW cha Ujerumani, Julai 24, 2026. Ikumbukwe, Julai 21, 2026, Dkt. Kaijage alipewa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Julai 8, 2026 akidaiwa kuhamasisha maandamano Julai 7, 2026, kwa sasa anakabiliwa na shtaka la ugaidi ambalo halina dhamana. Fuatilia zaidi mjadala #JamiiForums #JFMatukio
Jamii Forums32,295 views • 3 days ago

MOROGORO: Wiki iliyopita katikati ya mwezi Julai 2026, ilisambaa video ikionesha Wakazi wa Kijiji cha Kisaki wakitoa hoja mbele ya Askari wa Jeshi la Polisi wakidai kuna ndugu zao walioingia Hifadhi ya Taifa ya Nyerere wamepotea na wengine kuuliwa. Kamanda wa Polisi Mkoa, ACP Andrew Kantimbo amesema, “Uchunguzi wa awali haujabaini mauaji, wala mtu aliyejeruhiwa, kuna Watu wawili inadaiwa waliingia hifadhini, hawajarejea katika makazi yao. Wananchi watambue maeneo ya hifadhi yana wanyama wakali, wasiingie bila kufuata taratibu, uchunguzi unaendelea.” Upande wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema, “Tunashirikiana na Jeshi la Polisi, hatujawapata watu wanaodaiwa kupotea, tunatoa wito yeyote mwenye taarifa awasiliane nasi, tupo tayari kutoa ushirikiano.” Fuatilia zaidi #JamiiForums #Uwajibikaji #JFMatukio #CivilRights
Jamii Forums14,903 views • 5 days ago

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali John Jacob Mkunda ameyasema hayo wakati wa Gwaride la kuwaaga Majenerali 17 waliostaafu, lililofanyika Julai 10, 2026 katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Kikombo, jijini Dodoma. Fuatilia zaidi #JamiiForums #Utawala #Siasa Video: BM Tv
Jamii Forums27,865 views • 17 days ago

Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mwanafunzi wa Uhandisi Vifaa Tiba (Biomedical Engineering) ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika kuangalia utaratibu wa Wanachuo kutakiwa kulipia ili kupata nafasi ya mafunzo ya vitendo (field practice) katika baadhi ya taasisi kubwa akitolea mfano hospitali. Yapi maoni yako Mdau? Fuatilia Mjadala #JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji Video credit: maria_robyt
Jamii Forums31,461 views • 26 days ago

Waziri Deogratius Ndejembi ametoa maelekezo hayo, Juni 28, 2026, Ubungo jijini Dar es Salaam katika Kituo cha usimamizi wa Gridi ya Taifa ambapo ametaka kamati hiyo ishirikishe wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Fuatilia zaidi #JamiiForums #Uwajibikaji
Jamii Forums26,455 views • 29 days ago

DAR: Msanii Mkongwe wa #BongoFleva, Juma Nature kupitia ukurasa wake wa Instagram, Juni 20, 2026, alitoa wito kwa Manispaa ya Temeke kushughulikia tatizo la foleni inayosababishwa na Malori maeneo ya Mbagala akieleza kuwa hiyo ni kero kwa Wananchi wengi. Ikumbukwe kuwa kwa nyakati tofauti Wadau mbalimbali wa wamekuwa wakitoa wito hatua zichukuliwe kuhusu changamoto hiyo wakieleza inapunguza kasi ya shughuli nyingi za Kijamii na Kiuchumi. Nini maoni yako? Zaidi tembelea #JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
Jamii Forums21,378 views • 28 days ago