
Jamii Voice
@jamiivoice • 32,448 subscribers
VOICE OF JAMII
Shorts
Videos
4:17
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

HABARI: Wanaume watatu wamekutwa katika chumba kimoja eneo la Msasani, Kitongoji cha Oloresho, Kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, katika mazingira yaliyoibua mashaka miongoni mwa Wananchi. Mmoja wa Wanaume hao, aliyefahamika kwa jina la Alex Kimario, anayedaiwa kuwa dereva wa bodaboda, alishikiliwa na wananchi baada ya vijana wawili waliokuwa naye kutoroka katika eneo hilo. Baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa Alex alikuwa akiwafanyia Vijana hao wawili kitendo cha ngono kinyume na maumbile, madai ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka. Akizungumza, Alex ameeleza kuwa vijana hao walimuita ili awapeleke eneo la Kambi ya Fisi, akisema tayari alikuwa amewahi kuwapeleka sehemu mbalimbali zaidi ya mara tatu. “Hawa vijana wameniita kuwapeleka mtaa wa Kambi ya Fisi, nilivyokuja kumbe hawa vijana tabia zao sizijui. Nimeshakuja zaidi ya mara tatu nawachukua na kuwapeleka mahali wanataka,” amesema Alex. Kuhusu mafuta yaliyodaiwa kukutwa katika chumba hicho, Alex amesema ni mafuta ya kawaida ya kujipaka ambayo yanaweza kutumika katika sehemu mbalimbali za mwili. Mke wa Alex aliyefika eneo la tukio baada ya kupata taarifa amesema ameshtushwa na tukio hilo, akieleza kuwa anamfahamu mume wake kama mtu wa dini na mwimbaji wa kwaya. Balozi wa eneo hilo, Lydia Danieli, amesema analifahamu tukio hilo na kwamba baadhi ya mienendo ya vijana hao ilikuwa imewahi kuwafanya wananchi kuwa na mashaka. Jeshi la Polisi lilifika katika eneo hilo na kumchukua Alex kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.
Jamii Voice99,066 Aufrufe • vor 24 Tagen

HABARI: Hofu imetanda katika eneo la Makole jijini Dodoma baada ya dereva wa basi la kampuni ya Satco, lenye namba za usajili T308 EME, kudaiwa kutishiwa kwa silaha ya moto kufuatia ajali iliyohusisha basi hilo na gari aina ya Land Cruiser lenye namba T881 ENZ. Kwa mujibu wa mashuhuda, basi hilo lilikuwa likitokea katika Stendi Kuu ya Mabasi Dodoma kuelekea Geita, kabla ya kufika eneo la Makole ambapo inadaiwa Land Cruiser ililipita kwa upande na kusababisha magari hayo kugongana. Mashuhuda hao wameeleza kuwa baada ya magari hayo kugongana, dereva wa Land Cruiser alishuka na kufuatwa na kile kilichoelezwa kuwa bastola, kisha kumfuata dereva wa basi na kumtaka ashuke na kuingia kwenye Land Cruiser. Tukio hilo lilizua taharuki miongoni mwa wananchi waliokuwa eneo hilo, huku mazingira ya tukio yakisababisha hofu kuhusu usalama wa madereva na abiria. Hata hivyo, madai kuhusu matumizi ya silaha katika tukio hilo bado yanahitaji kuthibitishwa na mamlaka husika, huku wananchi wakitaka vyombo vya usalama kuchunguza tukio hilo na kuchukua hatua endapo itabainika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria.
Jamii Voice53,133 Aufrufe • vor 24 Tagen

HABARI: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche alipokuwa akihojiwa na @nijuzenews
Jamii Voice42,525 Aufrufe • vor 1 Monat

Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi, amemtaka Katibu Mwenezi wa CCM, Kenani Kihongosi kuachana na kumzungumzia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche kwenye mikutano yake. Sugu amesema Kihongosi hawezi kupimana ubavu na John Heche kisiasa. Ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhara Kanda ya Nyasa leo Septemba 20, 2026.
Jamii Voice22,377 Aufrufe • vor 25 Tagen

HABARI: Katibu Mkuu wa Act Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ado Shaibu, amesema kuwa Serikali inapaswa kuondoa ukimya na kueleza alipo Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Nchimbi. Ado ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Bugogwa, Mtaa wa Igomba, Ilemela, Mwanza leo tarehe 10 Septemba 2026. Ado amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa minong’ono iliyopo ambapo baadhi ya watu wanavumisha kuwa Dk. Nchimbi anashikiliwa na vyombo vya dola Ado amesema katika hilo Dk. Nchimbi mwenyewe, familia na vyombo vya dola vina wajibu wa kuihakikishia jamii kuwa Dk. Nchimbi yupo katika mikono salama. Ado amesema ACT Wazalendo itaendelea kupaza sauti kwa ajili ya watu wote wanaokandamizwa bila kujali wanatoka Chama gani kwa sababu huo ni wajibu wa kimapambano wa Chama cha siasa.
Jamii Voice15,960 Aufrufe • vor 1 Monat

HABARI: Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni Dereva wa Lori aliyefahamika kwa jina la Feisal Jabir adaiwa kuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wa kituo cha Mafuta kilichopo eneo la Kihonda Viwandani Manispaa ya Morogoro. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni Abdulaziz Mbwana ambaye msaidizi wa dereva huyo aliyeuawa ameeleza kuwa tukio hilo limetokea majira ya asubuhi baada ya dereva kuegesha gari na kwenda msikitini kuswali, baada ya kurudi ili kuendelea na safari yao ndipo yalipotokea malumbano na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta hali iliyopelekea mlinzi huyo kufyatua risasi na kumpiga akiwa ndani ya gari. Kaimu Afisa Mahusiano Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Scolastica Ndunga amekiri kupokea mwili huo ambapo ambapo amesema kuwa mwili huo ulikuwa na jeraha kichwani na kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa kidaktari kubaini undani wa jeraha hilo Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo inaeleza kuwa mtuhumiwa Hussein Idd Hussein mwenye umri wa miaka 37mlinzi wa kampuni ya Ruge Security anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Feisal Jabir Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea Septemba 9.2026 majira ya saa 12 alfajiri ambapo chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kutaka kulipwa shilingi 15,000/= gharama ya kulinda gari hilo na dereva alidaiwa kukataa na kuingia kwenye gari ndipo mtuhumiwa alipoamua kufyatua risasi kichwani na kupelekea kifo cha marehemu huyo
Jamii Voice13,456 Aufrufe • vor 1 Monat
Keine weiteren Inhalte verfügbar