Jamii Voice's banner
Jamii Voice's profile picture

Jamii Voice

@jamiivoice • 32,448 subscribers

VOICE OF JAMII

Shorts

HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limemshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa kosa la kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la kampuni ya SATCO, Said Fadhili (54). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, tukio hilo lilitokea wakati Said Fadhili alipokuwa akielekea kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies, ambapo inadaiwa Masawa alimtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola. Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Masawa. Uchunguzi wa awali uliofanywa na Polisi umebaini kuwa kitu alichokuwa nacho ni toyi (toy) na si silaha halisi kama ilivyodhaniwa awali. Polisi pia imebaini kuwa gari aina ya Land Cruiser LX70 Series lililokuwa likiendeshwa na Masawa lilikuwa na namba za usajili STM 5806, ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo ni mali ya TARURA, wakati gari hilo wakati wa tukio lilikuwa likitumia namba T 881 ENZ, inayodaiwa kuwa ni ya gari mali ya mtu mwingine. Kamanda Hyera amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kwa madereva dhidi ya kutumia namba bandia za magari, likisema kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

37,542 просмотров

HABARI: Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bukombe, SSP Harun Kasubi, amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi kumtembelea na kumfariji mwandishi mwandamizi wa Kituo cha Star TV, Makunga Peter Makunga, katika makazi yake yaliyopo Wilaya ya Bukombe, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano, utu na uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii. Katika ziara hiyo, Jeshi la Polisi limemfariji na kumkabidhi msaada wa fedha taslimu kwa ajili ya kumsaidia katika kipindi anachopitia, huku SSP Kasubi akisisitiza umuhimu wa jamii kuwa na utamaduni wa kujali, kutembeleana na kusaidiana, hususan kwa watu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali. Aidha, SSP Kasubi amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza dhana ya Polisi Jamii kwa vitendo kwa kuwafikia wananchi na makundi mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha mahusiano, mawasiliano na ushirikiano katika masuala ya usalama na ustawi wa jamii. Kwa upande mwingine, ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii ni muhimu katika kuimarisha amani, utulivu na usalama, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kudumisha utamaduni wa kujali na kusaidiana.

10,173 просмотров

Videos

HABARI: Wanaume watatu wamekutwa katika chumba kimoja eneo la Msasani, Kitongoji cha Oloresho, Kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, katika mazingira yaliyoibua mashaka miongoni mwa Wananchi. Mmoja wa Wanaume hao, aliyefahamika kwa jina la Alex Kimario, anayedaiwa kuwa dereva wa bodaboda, alishikiliwa na wananchi baada ya vijana wawili waliokuwa naye kutoroka katika eneo hilo. Baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa Alex alikuwa akiwafanyia Vijana hao wawili kitendo cha ngono kinyume na maumbile, madai ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka. Akizungumza, Alex ameeleza kuwa vijana hao walimuita ili awapeleke eneo la Kambi ya Fisi, akisema tayari alikuwa amewahi kuwapeleka sehemu mbalimbali zaidi ya mara tatu. “Hawa vijana wameniita kuwapeleka mtaa wa Kambi ya Fisi, nilivyokuja kumbe hawa vijana tabia zao sizijui. Nimeshakuja zaidi ya mara tatu nawachukua na kuwapeleka mahali wanataka,” amesema Alex. Kuhusu mafuta yaliyodaiwa kukutwa katika chumba hicho, Alex amesema ni mafuta ya kawaida ya kujipaka ambayo yanaweza kutumika katika sehemu mbalimbali za mwili. Mke wa Alex aliyefika eneo la tukio baada ya kupata taarifa amesema ameshtushwa na tukio hilo, akieleza kuwa anamfahamu mume wake kama mtu wa dini na mwimbaji wa kwaya. Balozi wa eneo hilo, Lydia Danieli, amesema analifahamu tukio hilo na kwamba baadhi ya mienendo ya vijana hao ilikuwa imewahi kuwafanya wananchi kuwa na mashaka. Jeshi la Polisi lilifika katika eneo hilo na kumchukua Alex kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.
4:17

Sensitive content

This media may contain sensitive content.

jamiivoice's profile picture

99,066 просмотров • 24 дней назад

jamiivoice's profile picture

Wasifu wa Marehemu

Jamii Voice

16,376 просмотров • 25 дней назад

jamiivoice's profile picture

HABARI: Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni Dereva wa Lori aliyefahamika kwa jina la Feisal Jabir adaiwa kuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wa kituo cha Mafuta kilichopo eneo la Kihonda Viwandani Manispaa ya Morogoro. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni Abdulaziz Mbwana ambaye msaidizi wa dereva huyo aliyeuawa ameeleza kuwa tukio hilo limetokea majira ya asubuhi baada ya dereva kuegesha gari na kwenda msikitini kuswali, baada ya kurudi ili kuendelea na safari yao ndipo yalipotokea malumbano na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta hali iliyopelekea mlinzi huyo kufyatua risasi na kumpiga akiwa ndani ya gari. Kaimu Afisa Mahusiano Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Scolastica Ndunga amekiri kupokea mwili huo ambapo ambapo amesema kuwa mwili huo ulikuwa na jeraha kichwani na kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa kidaktari kubaini undani wa jeraha hilo Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo inaeleza kuwa mtuhumiwa Hussein Idd Hussein mwenye umri wa miaka 37mlinzi wa kampuni ya Ruge Security anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Feisal Jabir Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea Septemba 9.2026 majira ya saa 12 alfajiri ambapo chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kutaka kulipwa shilingi 15,000/= gharama ya kulinda gari hilo na dereva alidaiwa kukataa na kuingia kwenye gari ndipo mtuhumiwa alipoamua kufyatua risasi kichwani na kupelekea kifo cha marehemu huyo

Jamii Voice

13,456 просмотров • 1 месяц назад

Больше нет контента для загрузки