Kigogo Media's banner
Kigogo Media's profile picture

Kigogo Media

@kigogo20141,496,684 subscribers

Official X handle of Kigogo Media I The uncensored,unfiltered and unbiased online news in East Africa I Email: [email protected]

Shorts

MBUNGE BASHUNGWA ACHA KUJIKOMBAKOMBA 📌 KWANZA nimeshangaa na pili nimestushwa sana na alichokiongea Bashungwa akiwa anahutubia wana CCM wenzake huko Karagwe. BASHUNGWA alipaswa kukaa kimya kwenye mambo mengi sana kwa sababu ni miongoni mwa mawaziri incompetent sana waliowahi kukaa kwenye uongozi wa hii nchi. BASHUNGWA amekuwa waziri kwenye wizara saba tofauti na hakuna mahali kafanya kitu cha maana na cha kukumbukwa na akaishia kufukuzwa hata huo uwaziri na kuonekana ni useless!. LEO nchi imesha move na inasonga mbele anaanza kutukumbusha sijui maujinga gani ya kilichotokea kwenye mchakato wa kufukuzwa kwa makamu wa Rais!. HAYO mambo yalishasemwa huko chamani na akina Kawaida na Dokta Migiro na tumeshazahau na tunasonga mbele!. Lakini kwa kuwa mnawashwa sana na kiti kilichoko wazi wa uwaziri wa nishati basi kila mtu anapanuapanua tu mdomo kuonhea ili mradi aonekane yupo yaani.. AU Bashungwa anadhani kwa KUJIKOMBAKOMBA huku kutamfanya awe waziri tena? Maana ni kama Bashungwa na yule mfanya biashara mpya wa mtindi mnanyemelea sana uwaziri na wanaotaxkuwa kuna siku watarudi tena kwenye baraza? KWANI mmesahau vidonda mmewapa watanzania mlipokuwa mawaziri? Halafu hivi huwa hamuwezi kuishi na kufanya maisha bila kuwa mawaziri? Maana mnahangaika kwelikweli yaani!.. ACHENI tamaa na KIJIKOMBAKOMBA fanyeni kazi ya ubunge mliyochaguliwa kuifanya na wananchi wenu haya mengine siyo lazima muwe nyie mawaziri !. Au kuna mambo mlisahau kufanya? KAMA wewe Bashungwa umekuwa waziri wa kila kitu si inatosha sasa utulie au? Mbona mnakuwa na tamaa hivi khaa au maisha bila uwaziri hayaendi? #KigogoMediaUpdates

58,667 views

Videos

kigogo2014's profile picture

TULIWAPA ANGALIZO MUDA SANA MKAWA KICHWA NGUMU NA WAJUAJI 📌 TULIWAPA angalizo muda sana kuhusu umuhimu na nguvu iko kwenye taasisi ya Urais na tukawasihi sana kuwa msimuangalie nani amekaa kwenye kiti cha urais bali tazama neno lenyewe urais. HAMKUWA wasikivu mkawa mnaendeshwa na mihemko na makasiriko mkidhani taasisi ya urais ni kitu chepesi chepesi tu na kinaweza kuchezewa na kudharauliwa WENGINE mkaanza kuleta kejeli hapa kuwa oooh Katoliki ndiyo kila kitu wanaamua nani awe nani nchi hii ba blah blha zingine za kutosha tu.. SHIDA yenu ni kuwa mlikuwa mnatazama urais kama mtu na siyo taaisis. HAYA majibu ya ukubwa na umuhimu wa taasisi ya urais haya hapa na mmeambiwa kwa kirefu nani alitaka kikao kile na walikwenda kufanya nini huko Ikulu. ACHENI kupumbazwa na kudanganywa na maneno ya wanaharakati na wapinzani waliochanganyikiwa ambao hawana agenda inayoeleweka zaidi ya kulalamika na kulaumu kila kitu.. TEC na Kitima bado mnataka kushindana na taasisi ya Urais ? Bado mnataka kufanya harakati kwenye mambo ya dini yenu? Bado mnataka kuwa mouthpiece ya CHADEMA na wahalifu wao walioko gerezani na mikesi ya ugaidi na uhaini? NAWAPA ANGALIZO tu kuwa huyu anayetoa hili tamko hapa ni Bwana Kitima kinara wa kuitukana serikali na dola na mtu aliyetumia TEC kwa muda mrefu sana kuisambulia serikali na mtu aliyefanya mambo ya hovyo sana dhidi ya Rais kwenye msiba wa Kadinali Pengo. KUWENI NA HESHIMA NA MAMLAKA MTAFIKA MBALI 📌 #KigogoMediaUpdates

Kigogo Media

26,523 views • 23 days ago

kigogo2014's profile picture

(✍🏿 na mwandishi wetu) Mwenezi wa CCM Paul Makonda anapaswa kujitafakari sana baada ya kusikia kauli hii ya Katibu Mkuu wa CCM. Kauli hii ina mwangwi mkali sana na kwa kuwa Makonda hana akili hawezi kujua kama ujumbe huu ni wa kwake na ataendelea kupuyanga tu kwa kudhani kudhalilisha viongozi wa serikali na kuwatukana ndiyo kufanya kazi kama mwenezi. Makonda anapokosoa mawaziri na wakurugenzi ajue wazi anamkosoa Rais ambaye amewateua na anahoji umakini wa Rais aliyewateuwa kama wanafanya kazi sawasawa! Narudia kitendo cha Makonda kudhalilisha wateule wa Rais ni kuwa anamdhalilisha Rais na anahoji umakini wa Rais kwenye kuteuwa watu hao!.. Kwa ukomavu wa Dokta Nchimbi kwenye siasa za CCM na kwa uzoefu alio nao nina uhakika hiki chama atakirudisha kwenye mstari na kuwa na viongozi wenye maadili na wanaojua kufanya siasa za kistaarabu na zisizo dhalilisha watumishi wa serikali kama ambavyo anafanya Makonda na wakiomtuma kufanya kazi ya kutukana watu na kuwadhalilisha. Makonda ni “project” ya watu fulani waliofanikiwa kurubuni na kudanganya mamlaka za uteuzi kuwa atawasaidia sana kwenye kampeni za uchaguzi ujao na kuthibiti makundi ya uasi ndani ya chama kwa kuwatukana na kuwadhalilisha. Kichekesho kilikuwa ni kuwa wanataka na wakitaka apatikane mtu wa version kama ya “MUSIBA MULAGA” lakini bahati mbaya sana wamepata bomu na kwa mwendo huu silioni bomu hili likiendelea kukaa muda mrefu bila kulipuka kwa kukipaka kinyesi chama kizima. Kinachoendelea ni lazima kutakuwa na malalamiko ya jumla ya viongozi ndani ya serikali juu ya uzalilishaji unaofanywa na Makonda na matendo yake ya kuvunja sheria na taratibu na kuingilia utendaji wa viongozi wa serikali na hili lazima litalazimu uteuzi wake kuangaliwa upya. CCM haiwezi kuendelea kuwa na mwenezi anayedhalilisha viongozi wa serikali kama waziri mkuu,mawaziri,wakuu wa mikoa,wakurugenzi,wakuu wa mikoa na watu wengine kwa kigezo cha kusikiliza kero. MAKONDA hana mamlaka ya kumhoji waziri yoyote kuhusu chochote ni vile tu mawaziri wetu ni waoga na wanafanya kazi kinafiki lakini Makonda ni mtu wa kumwambia AKOME KUSUMBUA WATU kwa kuwa hawaripoti kwake. Akahangaike na watu wake chamani huko na siyo serikalini. Huwezi kushauriwa wa wajinga na makanjanja wa uandishi wa habari walioko Sinza Makaburini halafu ukadhani unafanya mambo ya maana!.Lazima utakwama tu na ndicho kinachomkuta Makonda, kazungukwa na wajinga ndiyo maana anafanya ujinga kila kukicha. #KigogoMediaUpdates

Kigogo Media

23,591 views • 2 years ago

kigogo2014's profile picture

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Arusha) HII NI AIBU KUBWA!! Hakuna mtalii atakuja kurudi na kutembelea tena Serengeti kwa hali hii. Hii ndiyo highway ya kwenda Serengeti national park kilometa 10 tu kutoka Naabi Gate hali iko hivi. Hali hii inasikitisha na inafadhaisha sana Tunajiuliza hela wanazokusanya TANAPA zinakwenda wapi? Haya ndiyo mafanikio ya Royal Tour? Tunawezaje kama taifa kutumia mabilioni ya fedha kutangaza utalii na watalii wakaamini na kuanza kuja kwa wingi. lakini wanapokuja wanakutana na hali hii? Yaani tuna lengo gani? Au hizi ni zile juhudi za kikundi kile kumfelisha mheshimiwa Rais Samia kwenye mambo ya kuleta maendeleo kwenye hii nchi? Waziri wa Utalii upo? Unajua haya yanatokea? Tunajua TANAPA hela yote wanakusanya wanapeleka hazina na mlishawakataza kutumia hela mpaka muwape kibali. Hivi waziri huoni haja ya kubadilisha huu utaratibu ? Hivi kwenye baraza la mawaziri huwa mnajadili nini nyie watu? Sitaki kuandika sana lakini kaeni mkujua hakuna mtalii mwenye akili timamu atakuja kupoteza muda wake na hela kwenye hali hii. Haya mambo ndiyo maana wakenya wanatuzidi sana na watalii wanapenda kwenda Kenya kuliko kuja Tanzania kwa sababu tunashindwa kuwa siriazi na mambo madogo madogo kama haya. Kwa haya mauzauza na mateso wanayopata watalii hawa kaeni mkijua nguvu zote tulizotumia kama taifa kwanye Royal Tour ni bure na hakuna kitu tunakwenda kufaidika kwa kuwa watalii hawa watakwenda kutangaza ubovu wa barabara zaidi kuliko mazuri waliyoyaona na hii ni uzembe wa TANAPA na wizara na serikali kutokuwa makini na kutengeneza barabara hizi. Hakuna mtalii duniani anayesafiri kwenda mahali kwa ajili ya kupata shida au kuteseka. Kwa hiyo kama mmeanzisha utalii wa kuteseka kwa watalii ni bora mseme ili wajue na sisi tutawasaidia kuutangaza kwa nguvu zote! #KigogoMediaUpdates

Kigogo Media

19,938 views • 2 years ago

No more content to load