
Kigogo Media
@kigogo2014 • 1,496,558 subscribers
Official X handle of Kigogo Media I The uncensored,unfiltered and unbiased online news in East Africa I Email: [email protected]
Shorts
Videos

Semeni nyie sasa maana mimi nimeshalisema sana hili takataka Maria Sarungu halisikii📌
Kigogo Media24,592 Aufrufe • vor 19 Tagen

WANAKUSIKIA SANA ILA SASA WATAKUPITISHA? NI SAWA kujilinganisha na Magufuli na misimamo yake na ni sawa kuziishi farsafa zake kwa kuwa pengine ndiyo "role model" wako kama walivyo wanasiasa wengine wengi wa Tanzania. KUNA waliojifananisha na Nyerere na kila wakiongea wanamtaja Nyerere this Nyerere that , Nyerere wat wat LAKINI wakakumbana na dhoruba kali sana na kukutana na ngumi ya chuma na wakaishia kutupwa nje ya CCM. SWALI ni Je? Watakupitisha kwa huu umagufuli unaouamini? Wanataka mtu wa hivi? Mimi nakukupa angalizo tu kwa hali ya sasa ma siku zijazo.. YETU ni macho na 2030 siyo mbali na vumbi litaanza kutimka vibaya sana ifikapo 2027 baada ya ule mkutano mkuu 📌 #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media24,798 Aufrufe • vor 1 Monat

TULIWAPA ANGALIZO MUDA SANA MKAWA KICHWA NGUMU NA WAJUAJI 📌 TULIWAPA angalizo muda sana kuhusu umuhimu na nguvu iko kwenye taasisi ya Urais na tukawasihi sana kuwa msimuangalie nani amekaa kwenye kiti cha urais bali tazama neno lenyewe urais. HAMKUWA wasikivu mkawa mnaendeshwa na mihemko na makasiriko mkidhani taasisi ya urais ni kitu chepesi chepesi tu na kinaweza kuchezewa na kudharauliwa WENGINE mkaanza kuleta kejeli hapa kuwa oooh Katoliki ndiyo kila kitu wanaamua nani awe nani nchi hii ba blah blha zingine za kutosha tu.. SHIDA yenu ni kuwa mlikuwa mnatazama urais kama mtu na siyo taaisis. HAYA majibu ya ukubwa na umuhimu wa taasisi ya urais haya hapa na mmeambiwa kwa kirefu nani alitaka kikao kile na walikwenda kufanya nini huko Ikulu. ACHENI kupumbazwa na kudanganywa na maneno ya wanaharakati na wapinzani waliochanganyikiwa ambao hawana agenda inayoeleweka zaidi ya kulalamika na kulaumu kila kitu.. TEC na Kitima bado mnataka kushindana na taasisi ya Urais ? Bado mnataka kufanya harakati kwenye mambo ya dini yenu? Bado mnataka kuwa mouthpiece ya CHADEMA na wahalifu wao walioko gerezani na mikesi ya ugaidi na uhaini? NAWAPA ANGALIZO tu kuwa huyu anayetoa hili tamko hapa ni Bwana Kitima kinara wa kuitukana serikali na dola na mtu aliyetumia TEC kwa muda mrefu sana kuisambulia serikali na mtu aliyefanya mambo ya hovyo sana dhidi ya Rais kwenye msiba wa Kadinali Pengo. KUWENI NA HESHIMA NA MAMLAKA MTAFIKA MBALI 📌 #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media26,523 Aufrufe • vor 2 Monaten

MIZEE KAMA WARIOBA INA MCHANGO MDOGO SANA KWA TAIFA KWA NYAKATI HIZI ZA SASA..📌 INASIKITISHA sana kuona mtu mzee wa umri wa Jaji Warioba anatokwa na kauli za hovyo kama anazoziongea kila akipewa kipaza sauti. Ni hasara na aibu kwa taifa kuwa na mizee ya hivi na bado tunaendelea kuisikiliza ikiongea mambo yasiyo na maana. JAJI WARIOBA anaongelea mambo ya kufukuzwa CCM kwa Nchimbi. Kwani hakuwa anasikia sababu za kufukuzwa kwake? Hakuwa anafuatilia mienendo yake na kauli zake zikikiznana na CCM na mwenyekiti wake? Yeye alipokuwa makamu wa Rais na waziri mkuu aluwahi kikinzana na Nyerere au Mwinyi? JAJI WARIOBA ni kama amegoma kustaafu siasa na hataki kuona na kukubali kuwa "kila zama zina kitabu chake".. Yaani kila anapopewa kipaza sauti na kupanua mdomo wake lazima ataongea mambo ya kupinga na kukosoa serikali utafikiri ni mgeni wa jisni serikali inavyofanya kazi. JAJI WARIOBA anakosoa kila kitu ambacho serikali inafanya na hasa linapokuja suala la katiba.. Amekuwa anaimba kila kukicha kuhusu katiba mpya. Kwani si alimaliza kazi ya kutoa rasimu ya katiba mpya! Na bunge maalumu la katiba likafanya kazi yake na kupitisha rasimu ambayo iko tayari na inangoja kufanyiwa referendum au haya hajui? JAJI WARIOBA hajui nani waliovuruga mchakato wa kupata katiba wakati ule? Au alikuwa wapi wakati wahuni wa UKAWA waliposusia bunge la katiba na kutoka bungeni kupinga kupitishwa kwa katiba ile? Au hakuwepo alikuwa kalewa pombe anazokunywa na alipitwa na tukio lile? JAJI WARIOBA kila kitu kuhusu katiba ya Tanzania kwake ni kibaya na kila kitu anataka kiandikwe upya. Lakini huyu ni mtu ambaye alikuwa waziri mkuu na makamu wa Rais wa Tanzania. Kipindi anapewa vyeo viwili kwa mpigo na kuwa navyo yeye pekee hakuona kama katiba ilikuwa ina shida na hakuwahi kupanua mdomo wake kutaka katiba iandikwe upya au kubadilishwa kwa sababu si sawa kuwa na vyeo viwili kwa mtu mmoja.. AINA HII ya wazee ndiyo wale ambao tuliambiwa wakati fulani kuwa wanawashwawashwa sana na mambo ya serikali wakati wameshastaafu na hawataki kustaafu .. Yaani wako nje ya siasa na utumishi wa umma lakini bado wanawashwa sana na mambo yanavyofanywa na wengine. JAJI WARIOBA kama alikuwa anawashwa sana na suala la katiba mpya ya Tanzania alikuwa wapi kipindi ana madaraka na yuko serikali na kwenye CCM kusema hayo? Yaani katiba anaiona mbya kwa kuwa hayupo kwenye mfumo na kastaafu? Au katiba mbaya kwa kuwa haina manufaa kwake na watoto wake waliozoea kuhongwa vyeo vya kisiasa kwa kutumia jina la baba yao? ILIKUWA ni matarajio ya watu wengi sana kwa umri wa JAJI WARIOBA alipaswa kuwa sehemu ya wazee wa kushauri serikali na CCM na siyo kuwa mwanaharakati wa kupanuapanua mdomo kwenye mambo ya hovyo hovyo kila kukicha. NIMEMSIKIA juzi anaongelea kuwa eti 2030 tukiingia bila kuwa na katiba mpya nchi itaingia kwenye machafuko.. Hizi ndiyo kauli wanazoongea wanaharakati wenzake na watu wenye nongwa wenzake kila kukicha .. Yaani hawataki kuona Tanzania inatulia na kuwa na amani kwa vile tu wao siyo sehemu ya mfumo wa sasa. JAJI WARIOBA alipewa dhamana ya kuongoza tume ya mabadiliko ya katiba ya Tanzania. Kwa walioisoma rasimu ya Warioba ilijaa uchafu na upuuzi mwingi sana mpaka bunge la katiba lililazimika kukaa na kuandika upya baadhi ya maeneo kwa kuwa alichokifanya Jaji Warioba ilikuwa ni uchafu mtupu.. Ndiyo maana tume yake ilipomaliza kazi siku hiyo hiyo kila kitu chake kilifutwa mpaka tovuti ya tume na ofisi yake ilifungwa pale jengo la mamboya ndanoi Posta kwa sababu ya uhovyo wake. LEO Jaji Warioba anasimama na kuanza kuisema sijui CCM sijuio serikali juu ya kufika 2030 bila kuwa na katiba mpya kwani toka 1977 Tanzania imeendelea kuwepo kwa kutumia katiba gani? Yaani katiba ya sasa haifai kwa kuwa tu haiwafurahishi wapinzani? HAO wapinzani kipindi wanashinda vitiu vya ubunge na kuapa kuwa wabunge walikuwa wanashika katiba ipi kuapa nayo ? Au walishawahi kuikana wakiwa wabunge au katiba hii ni mbaya sana pale ambapo wanakuwa siyo wabunge? #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media10,616 Aufrufe • vor 1 Monat

WARIOBA HATAKI KUSTAAFU SIASA Ni bahati mbaya sana huyu mzee hataki kustaafu siasa na anadhani anaweza kuwa muamuzi wa mambo ya hii nchi!.. Warioba ulishamaliza muda wako kuwa kiongozi wa hii nchi! Ukapewa hukumu la kusimamia kuandika katiba mpya ukaja na rasimu ya kipumbavu na hovyo kuliko maelezo mpaka bunge likaamua kuandika upya! Watu wengi hawakujui ndiyo maana wanapoteza muda kusikiliza ujinga na upumbavu wako unaoongea kila siku! Huku ndiyo kuwashwawashwa sasa! #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media22,143 Aufrufe • vor 1 Jahr

Kadinali Pengo ashauriwe kupumzika kwa sababu yeye ni sehemu ya historia chungu na mbovu sana ya utawala wa Magufuli. Kadinali Pengo hakuwahi kunyanyua kinywa chake pale kampuni ya Magufuli ilipopewa tenda ya kujenga uwanja Chato, hakunyanyua mdomo pale watu walipokuwa wanapewa kesi na kuporwa mali zao, hajawahi kunyanyua mdomo kuongelea mkataba wa hovyo wa TICTS kwa zaidi ya miaka 25 , hajawahi kuongea unufaikaji wa kanisa lake kupitia Askofu Kilaini kwenye hela za rushwa za ESCROW, hajawahi kutoa kauli pale chaguzi zilipoibwa na kuharibiwa na watu kuuwawa wakati wa Magufuli. Huu uchungu na watanzania kaanza kuupata leo kusikia DP World wanakuja kuwekeza ? Au kwa kuwa siyo wakatoliki? Kadinali Pengo ndiye aliyemsaidia Kakoko asiende jela hata baada ya kukutwa na magunia ya fedha nyumbani kwako akiwa mkurugenzi wa bandari. Au anataka tuanze kusema amenufaikaje na uwepo wa Kakoko pale bandarini? Ni vyema Kadinali Pengo akashauriwa ajikite kwenye kupigania afya yake kwa sasa kwa sababu anaonekana hana kumbukumbu ya mambo mengi sana kiasi kwamba anaongea mambo ya nadharia na yasiyo na maana kama vile bandari ya Dar Es Salaam imeanza leo. Ni vyema kanisa lake likamshauri asilitie kabisa kwenye mikingamo na tukaanza kuhoji uwezo wake wa afya ya akili kwa umri alio nao kwa sababu anaongea vitu havieleweki. Masuala ya kuwa na utaalamu wa kuendesha bandari mbona hakuyasema wakati wa Mkapa, Mwinyi,Nyerere au Mkapa? Au sasa hivi ndiyo anaona umuhimu wa uwezo wa watanzania kuendesha bandari kwa kuwa anayekuja kuwekeza siyo mkatoliki kama Karamagi? Kama ni watanzania ,basi Karamagi na TICTS yake ni watanzania na walichofanya kwa miaka 30 ni wazi na kukaribia kuuwa bandari wakishirikiana na akina Kakoko ambao ni maswahiba wakubwa wa Kadinali Pengo angewakemea hao kwanza au hana kumbukumbu? Tunajua kuwa Kadinali Pengo ni mnufaika mkubwa wa bandari wakati wa Kakoko na kwa sasa anataka kutumia kanisa kuleta mikingamo kwenye jambo hili la uwekezaji wa DP World. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media32,013 Aufrufe • vor 3 Jahren

😁😁😁 tukiwaambia hawa watu wamechanganyikiwa na wanaugua akili muwe mnaelewa!.. Tuliwaambia hawa wamelipwa kufanya haya mauzau muwe mnajipa muda kutuelewa! Kitu niko na uhakika nacho ni kuwa tuwe wavumilivu tutasikia mengi kukiko mnavyodhani!.. Yaaani mara mia majeshi ya nje yaje kutawala Tanzania! Kweli? Kwani Open Society hamuwezi kurudisha hela zao? Maana ni kama wamewabana mpaka mmekoa uwezo wa kufikiri tena 😁😁 Trump aje afanyeje? 😁😁🤓
Kigogo Media12,369 Aufrufe • vor 10 Monaten

(✍🏿 na wachambuzi wetu wa mambo ya vitita vya NHIF) MHESHIMIWA Rais Samia Suluhu ni mwenye busara na ustahimilivu sana na mwenye kwenda polepole na mawaziri wake na watendaji wa serikali ambao kwa kweli hawatakiwi kuwamo ndani ya serikali hata hivi sasa kwa madudu wanayoyafanya na kukosa uwajibikaji. LAKINI Rais Samia ni mama na anachukulia mambo kwa utaratibu na uangalifu mkubwa sana na upole kama mama lakini siyo kwamba hajui uozo unaofanywa na watu hasa mawaziri wa serikali yake. Ametumia mfano wa uwajibikaji wa Hayati Mzee Mwinyi kwa kuwa watu ndani ya serikali hasa mawaziri hawataki kuwajibika na dhana ya kuwajibika kwao ni msamiati mgumu sana. Hivi Waziri Ummy Mwalimu unawezaje kutowajibika kwa mauozo yanayofanywa na NHIF na vurugu mnazofanya kwenye sekta ya afya na ukaona ni sawa tu. Unawezaje kujiona wewe siyo sehemu ya tatizo wakati wewe ni moja ya watu mlioamua kupeleka wazee wote wastaafu na walioko kwenye pensheni kwenye NHIF na leo hii serikali inadaiwa 17bn TZS na NHIF na hamtaki kulipa hiyo hela mpaka NHIF inakaribia ku collapse? Wewe kama waziri upo tu huku ukiona NHIF ina matumiza ya ajabu toka 40bn TZS mpaka 70bn TZS kwa mwaka ndani ya miaka miwili iliyopita? Unaendeleaje kuwa waziri wakati unajua wewe ni sehemu ya mamilioni ya fedha za NHIF zilizokwenda kununua ndege za ATCL? Unahangaikaje na mambo madogo ya vitita wakati hayo hata mfanyeje hayawezi kuunusuru huu mfuko kwa sababu unakwenda kufa? Ziko wapi 40bn TZS walizojikopesha wakurugenzi wa NHIF? WAKATI ujumbe huu unalenga mawaziri wa aina ya Ummy Mwalimu ni muhimu sana tukatafakari na kujiuliza maswali haya ya msingi sana, Nimekuwa nikifuatilia mjadala mkali unaoendelea kwa sasa kuhusu NHIF na ‘dhamira yao ya kulinda afya za wanachama wao na kudhibiti njama za watoa huduma za afya kujitajirisha’. Mjadala huu ulikuja kufuatia uamuzi wa NHIF kufanya mapitio ya gharama za vifurushi mbalimbali vya huduma zao, ikidaiwa kuwa bei za sasa ni ‘kandamizi’ kwa wanachama. Waziri amekuwa akitema cheche akibagaza pia hatua ya watoa huduma kuweka sitisho la huduma mpaka hapo utata wa mabadiliko haya utakapomalizwa kwa mazungumzo. Yaliyofuata baada ya hapo ni historia kwa sasa. Wapo wakaosema kuwa Waziri Ummy ana wajibu wa kulinda maslahi ya Watanzania na hasa wanachama wa NHIF na kulinda Mfuko huu ambao ni bayana sasa kwamba unachechemea. Lakini ni kweli kinacholindwa hapa ni Watanzania hawa wanyonge na huduma wanazopata kutoka NHIF? Jibu la uhakika hapa ni *hapana*. Kwa kujua au kutokujua, Waziri Ummy amebeba msalaba wa kutetea waliozalisha tatizo lililopo sasa. Hawa ndiyo wanaoichonganisha Serikali na wanachama na Serikali na watoa huduma. Hawa ni Wajumbe wa Bodi na Menejimenti inayoongozwa na *Bilionea Bernard Konga*, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF. Bodi na Konga ndiyo waliopewa dhamana hii ambayo sasa imeingia kwenye sintofahamu kwa sababu ya ubabe wao wa kushughulikia maoni na malalamiko ya wateja wao, wakiwemo watoa huduma. Ndiyo hawa akina Konga ambao waliruhusu kuchotwa kwa mabilioni mengi sana (bilioni 41) na kukopesha watumishi na baadae kutoa msamaha kupitia uamuzi wao wa kutowakata watumishi hao kutoka kwenye mishahara, posho na mafao yao. Ni huyu huyu Konga wa Waziri Ummy ambaye hata taasisi zilizoingia makubaliano maalum na kulipa fedha nyingi ili huduma zao ziwe za kiwango cha juu sasa wanalazimishwa kupata huduma katika mfumo wa punguzo hili la lazima. Ni huyu huyu Konga ambaye amesimamia wizi ulifanywa kwa kughushi nyaraka, ukihusisha Mkurugenzi wa Fedha na kuchota zaidi ya bilioni 3 kule mkoani Mara. Kuna kila dalili kuwa wizi huu umefanyika kote nchini uchunguzi wa kına utagundua madudu makubwa sana. Bernard Konga wa Waziri Ummy ni mtumishi wa umma ambaye maslahi yake ya utumishi ni kama ya wengine, lakini yeye anaogelea kwenye ukwasi na utajiri mkubwa sana uliompa kiburi cha #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media25,265 Aufrufe • vor 2 Jahren

(✍🏿 na mwandishi wetu wa mambo ya misiba ya viongozi) Wana familia mtu huyu mwambieni tu aendelee na mambo yake kuruhusu kuja msibani kwa ndugu yenu ni kama anakuja kumdhihaki marehemu Nape alifanya haya hadharani kwenye majukwaa na alitumwa na Kinana na Kikwete kumtukana na kumkejeki mzee Lowassa kwa sababu tu hawakutaka awe Rais wakati yeye alimsaidia sana Kikwete kuwa Rais kwa haki na mali! Matusi na kejeli zao na mambo yao yalizidi kiwango cha kibinadamu na yalimuumiza sana Lowassa na kumuachia makovu makubwa sana ambayo amekwenda nayo kaburini. Njia pekee ya nyie kama familia kulinda heshima ya hayati Lowassa hapa dubiani ni kutoruhusu kejeli hizi zikapata kibali kwa mtu mshenzi wa kiwango hiki kuja kwenye msiba. Ifike mahali kwa ujasiri kabisa mseme "Nape,Kinana na Kikwete" wasije msibani na wajue hivyo kuwa familia hamtaki UNAFIKI wao. Na nyie huko Monduki watu hawa mkiwaona msibani , njia nzuri ya kuwafedhehesha ni kuwazomea mwanzo mwisho yaani Watu hawa ni WANAFIKI. Wanimdhalilisha na kumtusi sana Lowassa leo hawawezi wakawa na uchungu na kifo chake #KigogoMediaUpdates #HawaNiWanafiki #NapeNiTakataka
Kigogo Media25,493 Aufrufe • vor 2 Jahren

Wanagomea show za wasanii huku! Yaani jana show ya Mario haikuwa na watu kabisa
Kigogo Media11,624 Aufrufe • vor 10 Monaten

(✍🏿 na mwandishi wetu) Mwenezi wa CCM Paul Makonda anapaswa kujitafakari sana baada ya kusikia kauli hii ya Katibu Mkuu wa CCM. Kauli hii ina mwangwi mkali sana na kwa kuwa Makonda hana akili hawezi kujua kama ujumbe huu ni wa kwake na ataendelea kupuyanga tu kwa kudhani kudhalilisha viongozi wa serikali na kuwatukana ndiyo kufanya kazi kama mwenezi. Makonda anapokosoa mawaziri na wakurugenzi ajue wazi anamkosoa Rais ambaye amewateua na anahoji umakini wa Rais aliyewateuwa kama wanafanya kazi sawasawa! Narudia kitendo cha Makonda kudhalilisha wateule wa Rais ni kuwa anamdhalilisha Rais na anahoji umakini wa Rais kwenye kuteuwa watu hao!.. Kwa ukomavu wa Dokta Nchimbi kwenye siasa za CCM na kwa uzoefu alio nao nina uhakika hiki chama atakirudisha kwenye mstari na kuwa na viongozi wenye maadili na wanaojua kufanya siasa za kistaarabu na zisizo dhalilisha watumishi wa serikali kama ambavyo anafanya Makonda na wakiomtuma kufanya kazi ya kutukana watu na kuwadhalilisha. Makonda ni “project” ya watu fulani waliofanikiwa kurubuni na kudanganya mamlaka za uteuzi kuwa atawasaidia sana kwenye kampeni za uchaguzi ujao na kuthibiti makundi ya uasi ndani ya chama kwa kuwatukana na kuwadhalilisha. Kichekesho kilikuwa ni kuwa wanataka na wakitaka apatikane mtu wa version kama ya “MUSIBA MULAGA” lakini bahati mbaya sana wamepata bomu na kwa mwendo huu silioni bomu hili likiendelea kukaa muda mrefu bila kulipuka kwa kukipaka kinyesi chama kizima. Kinachoendelea ni lazima kutakuwa na malalamiko ya jumla ya viongozi ndani ya serikali juu ya uzalilishaji unaofanywa na Makonda na matendo yake ya kuvunja sheria na taratibu na kuingilia utendaji wa viongozi wa serikali na hili lazima litalazimu uteuzi wake kuangaliwa upya. CCM haiwezi kuendelea kuwa na mwenezi anayedhalilisha viongozi wa serikali kama waziri mkuu,mawaziri,wakuu wa mikoa,wakurugenzi,wakuu wa mikoa na watu wengine kwa kigezo cha kusikiliza kero. MAKONDA hana mamlaka ya kumhoji waziri yoyote kuhusu chochote ni vile tu mawaziri wetu ni waoga na wanafanya kazi kinafiki lakini Makonda ni mtu wa kumwambia AKOME KUSUMBUA WATU kwa kuwa hawaripoti kwake. Akahangaike na watu wake chamani huko na siyo serikalini. Huwezi kushauriwa wa wajinga na makanjanja wa uandishi wa habari walioko Sinza Makaburini halafu ukadhani unafanya mambo ya maana!.Lazima utakwama tu na ndicho kinachomkuta Makonda, kazungukwa na wajinga ndiyo maana anafanya ujinga kila kukicha. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media23,591 Aufrufe • vor 2 Jahren

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Dar Es Salaam) "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza na chaguzi za serikali za mitaa kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwahiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitogeza," - Rais Samia Rais Samia amelitaka jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujipanga kwa kuwa kuna watu wanaotaka kueleta chokochoko kwenye chaguzi hizi. Wako ndani ya CCM na wengine wako nje ya CCM. Kauli hii ya Rais Samia ni kauli safi sana na ya kimamlaka ili kuhakikisha nchi inavuka salama kwenye chaguzi hizi ambazo akina Mbowe wanapanga kuvuruga utulivu wa nchi hii na wale wanaotaka urais wa 2030 ndani ya CCM hasa kundi la akina Nape, January(vijana wa Msoga hawa) na Bashe wanajipanga kufanya uasi mara baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Tunashukuru sana Rais wetu kwa kuweka hili wazi sasa kazi kwenu JWTZ maana wale wazee wa kaunda suti ni maboya tu na wanashirikiana na vikundi vya akina January kumhujumu Rais. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media20,165 Aufrufe • vor 2 Jahren

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Arusha) HII NI AIBU KUBWA!! Hakuna mtalii atakuja kurudi na kutembelea tena Serengeti kwa hali hii. Hii ndiyo highway ya kwenda Serengeti national park kilometa 10 tu kutoka Naabi Gate hali iko hivi. Hali hii inasikitisha na inafadhaisha sana Tunajiuliza hela wanazokusanya TANAPA zinakwenda wapi? Haya ndiyo mafanikio ya Royal Tour? Tunawezaje kama taifa kutumia mabilioni ya fedha kutangaza utalii na watalii wakaamini na kuanza kuja kwa wingi. lakini wanapokuja wanakutana na hali hii? Yaani tuna lengo gani? Au hizi ni zile juhudi za kikundi kile kumfelisha mheshimiwa Rais Samia kwenye mambo ya kuleta maendeleo kwenye hii nchi? Waziri wa Utalii upo? Unajua haya yanatokea? Tunajua TANAPA hela yote wanakusanya wanapeleka hazina na mlishawakataza kutumia hela mpaka muwape kibali. Hivi waziri huoni haja ya kubadilisha huu utaratibu ? Hivi kwenye baraza la mawaziri huwa mnajadili nini nyie watu? Sitaki kuandika sana lakini kaeni mkujua hakuna mtalii mwenye akili timamu atakuja kupoteza muda wake na hela kwenye hali hii. Haya mambo ndiyo maana wakenya wanatuzidi sana na watalii wanapenda kwenda Kenya kuliko kuja Tanzania kwa sababu tunashindwa kuwa siriazi na mambo madogo madogo kama haya. Kwa haya mauzauza na mateso wanayopata watalii hawa kaeni mkijua nguvu zote tulizotumia kama taifa kwanye Royal Tour ni bure na hakuna kitu tunakwenda kufaidika kwa kuwa watalii hawa watakwenda kutangaza ubovu wa barabara zaidi kuliko mazuri waliyoyaona na hii ni uzembe wa TANAPA na wizara na serikali kutokuwa makini na kutengeneza barabara hizi. Hakuna mtalii duniani anayesafiri kwenda mahali kwa ajili ya kupata shida au kuteseka. Kwa hiyo kama mmeanzisha utalii wa kuteseka kwa watalii ni bora mseme ili wajue na sisi tutawasaidia kuutangaza kwa nguvu zote! #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media19,938 Aufrufe • vor 2 Jahren

( ✍🏻 na mchambuzi wetu) CHADEMA HIYOOO INAELEKEA KABURINI... LILIKUWA ni suala la muda tu kwa kikundi hiki kufika hapa kilipo sasa. Lilikuwa ni suala la muda tu kikundi hiki kuanza safari ya kuelekea kaburini kama ilivyokuwa kwa NCCR Mageuzi na TLP na vyama vingine vya kisiasa vya wachaga. KAULI za Lissu kuwa kuna fedha chafu ndani ya kikundi hiki ni kauli ngumu sana na inayoonyesha ile njia waliwahi kupita TLP na NCCR Mageuzi na wao sasa wameanza kuipita na kwa kweli siwaoni wanavuka 2025 salama bila kuwa na vipande vipande vya hiki kikundi. Tulipokuwa tunawaambia wajenge chama na kuacha kutukanatukana watu mitandaoni kama kwamba hiyo ndiyo sera ya kikundi chao hawakuwa wanasikia na waliota mapembe,sasa ule muda wa kugeuza matusi kuwa kura ndiyo huu na sisi kazi yetu ni kuwakumbusha tu kuwa kwa teknolojia ya sasa mbona matusi yanaweza kugeuzwa kuwa kura na wakiyageuza wanashika dola 2025 mapema sana. Malalamiko ya Lissu kuwa kuna fedha chafu ndani ya chaguzi za hiki kikundi ni dalili na ushahidi kuwa siku zote kikundi hiki cha Mbowe kimekuwa kinafanya ujasiriamali wa siasa na kwao siasa ni kazi na wala siyo huduma kwa watanzania. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media16,257 Aufrufe • vor 2 Jahren

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Dar Es Salaam) Sasa nimeanza kuelewa kwa nini JWTZ wamewekwa kuwa tayari kwa ajili ya kushughulikia watu wenye nia ovu nyakati za uchaguzi. Masaa machache yamepita toka Rais awasihi JWTZ kuwa tayari kwa lolote na kauli hiyo imepata majibu! CHADEMA ni chama cha kihuni na kinaongozwa na watu wahuni wa waliojaa hila na uongo na hadaa sana kwa watanzania. Hadaa ni tabia ya viongozi wababaishaji kama ambavyo walisema Lowassa ni fisadi lakini kwa sababu ya fedha wakauza nafasi na akawa mgombea wao.! Inatia kinyaa sana kuwa na chama cha hivi na viongozi wa hivi wanaotoka kwenye vikao na kuja kusambaza uongo kwa nia ya kupotosha kwa manufaa yao ya kisiasa! CHADEMA ni kikundi cha wahuni waliojificha kwenye siasa kwa kujifanya wanasiasa lakini ni watu wa hovyo sana kwenye siasa za upinzani Tanzania. Jeshi la polisi tunawasihi sana kupiga marufuku huu upuuzi wa maandamano kwa sababu tayari watu na kikundi chao wanachoita chama wanaonekana wana ajenda iliyojificha ambayo watanzania wengi hawaijui. Wanawezaje kufanya upotoshaji wa kiwango hiki baada ya kikao chenu? #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media11,391 Aufrufe • vor 2 Jahren

DP World ambayo akina Mbowe hawaijui imewekeza kiasi cha dola za kimarekani $23m kwenye bandari ya Santos huko Brazil ili kuwa ya kisasa na yenye tija na manufaa. Maboresho hayo na uwekezaji huo unachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji ambao ni muhimu sana kwa uchumi wa Brazil na ni njia muhimu sana kupeleka bidhaa za Brazil kwenye soko la dunia. Ni nani asiyetaka uwekezaji wa aina hii kwenye bandari zake? Ni nchi gani itamkataa mwekezaji mwenye uwezo mkubwa kama DP World? Mbowe haijui DP World anachofanya ni ukasuku anaotumwa na akina Karamagi. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media10,189 Aufrufe • vor 3 Jahren
Keine weiteren Inhalte verfügbar