
Kigogo Media
@kigogo2014 • 1,496,684 subscribers
Official X handle of Kigogo Media I The uncensored,unfiltered and unbiased online news in East Africa I Email: [email protected]
Shorts
Videos

TULIWAPA ANGALIZO MUDA SANA MKAWA KICHWA NGUMU NA WAJUAJI 📌 TULIWAPA angalizo muda sana kuhusu umuhimu na nguvu iko kwenye taasisi ya Urais na tukawasihi sana kuwa msimuangalie nani amekaa kwenye kiti cha urais bali tazama neno lenyewe urais. HAMKUWA wasikivu mkawa mnaendeshwa na mihemko na makasiriko mkidhani taasisi ya urais ni kitu chepesi chepesi tu na kinaweza kuchezewa na kudharauliwa WENGINE mkaanza kuleta kejeli hapa kuwa oooh Katoliki ndiyo kila kitu wanaamua nani awe nani nchi hii ba blah blha zingine za kutosha tu.. SHIDA yenu ni kuwa mlikuwa mnatazama urais kama mtu na siyo taaisis. HAYA majibu ya ukubwa na umuhimu wa taasisi ya urais haya hapa na mmeambiwa kwa kirefu nani alitaka kikao kile na walikwenda kufanya nini huko Ikulu. ACHENI kupumbazwa na kudanganywa na maneno ya wanaharakati na wapinzani waliochanganyikiwa ambao hawana agenda inayoeleweka zaidi ya kulalamika na kulaumu kila kitu.. TEC na Kitima bado mnataka kushindana na taasisi ya Urais ? Bado mnataka kufanya harakati kwenye mambo ya dini yenu? Bado mnataka kuwa mouthpiece ya CHADEMA na wahalifu wao walioko gerezani na mikesi ya ugaidi na uhaini? NAWAPA ANGALIZO tu kuwa huyu anayetoa hili tamko hapa ni Bwana Kitima kinara wa kuitukana serikali na dola na mtu aliyetumia TEC kwa muda mrefu sana kuisambulia serikali na mtu aliyefanya mambo ya hovyo sana dhidi ya Rais kwenye msiba wa Kadinali Pengo. KUWENI NA HESHIMA NA MAMLAKA MTAFIKA MBALI 📌 #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media26,523 次观看 • 23 天前

😁😁😁 tukiwaambia hawa watu wamechanganyikiwa na wanaugua akili muwe mnaelewa!.. Tuliwaambia hawa wamelipwa kufanya haya mauzau muwe mnajipa muda kutuelewa! Kitu niko na uhakika nacho ni kuwa tuwe wavumilivu tutasikia mengi kukiko mnavyodhani!.. Yaaani mara mia majeshi ya nje yaje kutawala Tanzania! Kweli? Kwani Open Society hamuwezi kurudisha hela zao? Maana ni kama wamewabana mpaka mmekoa uwezo wa kufikiri tena 😁😁 Trump aje afanyeje? 😁😁🤓
Kigogo Media12,369 次观看 • 8 个月前

WARIOBA HATAKI KUSTAAFU SIASA Ni bahati mbaya sana huyu mzee hataki kustaafu siasa na anadhani anaweza kuwa muamuzi wa mambo ya hii nchi!.. Warioba ulishamaliza muda wako kuwa kiongozi wa hii nchi! Ukapewa hukumu la kusimamia kuandika katiba mpya ukaja na rasimu ya kipumbavu na hovyo kuliko maelezo mpaka bunge likaamua kuandika upya! Watu wengi hawakujui ndiyo maana wanapoteza muda kusikiliza ujinga na upumbavu wako unaoongea kila siku! Huku ndiyo kuwashwawashwa sasa! #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media22,143 次观看 • 1 年前

(✍🏿 na mwandishi wetu wa mambo ya misiba ya viongozi) Wana familia mtu huyu mwambieni tu aendelee na mambo yake kuruhusu kuja msibani kwa ndugu yenu ni kama anakuja kumdhihaki marehemu Nape alifanya haya hadharani kwenye majukwaa na alitumwa na Kinana na Kikwete kumtukana na kumkejeki mzee Lowassa kwa sababu tu hawakutaka awe Rais wakati yeye alimsaidia sana Kikwete kuwa Rais kwa haki na mali! Matusi na kejeli zao na mambo yao yalizidi kiwango cha kibinadamu na yalimuumiza sana Lowassa na kumuachia makovu makubwa sana ambayo amekwenda nayo kaburini. Njia pekee ya nyie kama familia kulinda heshima ya hayati Lowassa hapa dubiani ni kutoruhusu kejeli hizi zikapata kibali kwa mtu mshenzi wa kiwango hiki kuja kwenye msiba. Ifike mahali kwa ujasiri kabisa mseme "Nape,Kinana na Kikwete" wasije msibani na wajue hivyo kuwa familia hamtaki UNAFIKI wao. Na nyie huko Monduki watu hawa mkiwaona msibani , njia nzuri ya kuwafedhehesha ni kuwazomea mwanzo mwisho yaani Watu hawa ni WANAFIKI. Wanimdhalilisha na kumtusi sana Lowassa leo hawawezi wakawa na uchungu na kifo chake #KigogoMediaUpdates #HawaNiWanafiki #NapeNiTakataka
Kigogo Media25,493 次观看 • 2 年前

(✍🏿 na mwandishi wetu) Mwenezi wa CCM Paul Makonda anapaswa kujitafakari sana baada ya kusikia kauli hii ya Katibu Mkuu wa CCM. Kauli hii ina mwangwi mkali sana na kwa kuwa Makonda hana akili hawezi kujua kama ujumbe huu ni wa kwake na ataendelea kupuyanga tu kwa kudhani kudhalilisha viongozi wa serikali na kuwatukana ndiyo kufanya kazi kama mwenezi. Makonda anapokosoa mawaziri na wakurugenzi ajue wazi anamkosoa Rais ambaye amewateua na anahoji umakini wa Rais aliyewateuwa kama wanafanya kazi sawasawa! Narudia kitendo cha Makonda kudhalilisha wateule wa Rais ni kuwa anamdhalilisha Rais na anahoji umakini wa Rais kwenye kuteuwa watu hao!.. Kwa ukomavu wa Dokta Nchimbi kwenye siasa za CCM na kwa uzoefu alio nao nina uhakika hiki chama atakirudisha kwenye mstari na kuwa na viongozi wenye maadili na wanaojua kufanya siasa za kistaarabu na zisizo dhalilisha watumishi wa serikali kama ambavyo anafanya Makonda na wakiomtuma kufanya kazi ya kutukana watu na kuwadhalilisha. Makonda ni “project” ya watu fulani waliofanikiwa kurubuni na kudanganya mamlaka za uteuzi kuwa atawasaidia sana kwenye kampeni za uchaguzi ujao na kuthibiti makundi ya uasi ndani ya chama kwa kuwatukana na kuwadhalilisha. Kichekesho kilikuwa ni kuwa wanataka na wakitaka apatikane mtu wa version kama ya “MUSIBA MULAGA” lakini bahati mbaya sana wamepata bomu na kwa mwendo huu silioni bomu hili likiendelea kukaa muda mrefu bila kulipuka kwa kukipaka kinyesi chama kizima. Kinachoendelea ni lazima kutakuwa na malalamiko ya jumla ya viongozi ndani ya serikali juu ya uzalilishaji unaofanywa na Makonda na matendo yake ya kuvunja sheria na taratibu na kuingilia utendaji wa viongozi wa serikali na hili lazima litalazimu uteuzi wake kuangaliwa upya. CCM haiwezi kuendelea kuwa na mwenezi anayedhalilisha viongozi wa serikali kama waziri mkuu,mawaziri,wakuu wa mikoa,wakurugenzi,wakuu wa mikoa na watu wengine kwa kigezo cha kusikiliza kero. MAKONDA hana mamlaka ya kumhoji waziri yoyote kuhusu chochote ni vile tu mawaziri wetu ni waoga na wanafanya kazi kinafiki lakini Makonda ni mtu wa kumwambia AKOME KUSUMBUA WATU kwa kuwa hawaripoti kwake. Akahangaike na watu wake chamani huko na siyo serikalini. Huwezi kushauriwa wa wajinga na makanjanja wa uandishi wa habari walioko Sinza Makaburini halafu ukadhani unafanya mambo ya maana!.Lazima utakwama tu na ndicho kinachomkuta Makonda, kazungukwa na wajinga ndiyo maana anafanya ujinga kila kukicha. #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media23,591 次观看 • 2 年前

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Arusha) HII NI AIBU KUBWA!! Hakuna mtalii atakuja kurudi na kutembelea tena Serengeti kwa hali hii. Hii ndiyo highway ya kwenda Serengeti national park kilometa 10 tu kutoka Naabi Gate hali iko hivi. Hali hii inasikitisha na inafadhaisha sana Tunajiuliza hela wanazokusanya TANAPA zinakwenda wapi? Haya ndiyo mafanikio ya Royal Tour? Tunawezaje kama taifa kutumia mabilioni ya fedha kutangaza utalii na watalii wakaamini na kuanza kuja kwa wingi. lakini wanapokuja wanakutana na hali hii? Yaani tuna lengo gani? Au hizi ni zile juhudi za kikundi kile kumfelisha mheshimiwa Rais Samia kwenye mambo ya kuleta maendeleo kwenye hii nchi? Waziri wa Utalii upo? Unajua haya yanatokea? Tunajua TANAPA hela yote wanakusanya wanapeleka hazina na mlishawakataza kutumia hela mpaka muwape kibali. Hivi waziri huoni haja ya kubadilisha huu utaratibu ? Hivi kwenye baraza la mawaziri huwa mnajadili nini nyie watu? Sitaki kuandika sana lakini kaeni mkujua hakuna mtalii mwenye akili timamu atakuja kupoteza muda wake na hela kwenye hali hii. Haya mambo ndiyo maana wakenya wanatuzidi sana na watalii wanapenda kwenda Kenya kuliko kuja Tanzania kwa sababu tunashindwa kuwa siriazi na mambo madogo madogo kama haya. Kwa haya mauzauza na mateso wanayopata watalii hawa kaeni mkijua nguvu zote tulizotumia kama taifa kwanye Royal Tour ni bure na hakuna kitu tunakwenda kufaidika kwa kuwa watalii hawa watakwenda kutangaza ubovu wa barabara zaidi kuliko mazuri waliyoyaona na hii ni uzembe wa TANAPA na wizara na serikali kutokuwa makini na kutengeneza barabara hizi. Hakuna mtalii duniani anayesafiri kwenda mahali kwa ajili ya kupata shida au kuteseka. Kwa hiyo kama mmeanzisha utalii wa kuteseka kwa watalii ni bora mseme ili wajue na sisi tutawasaidia kuutangaza kwa nguvu zote! #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media19,938 次观看 • 2 年前

(✍🏿 na mwandishi wetu wa Dar Es Salaam) Sasa nimeanza kuelewa kwa nini JWTZ wamewekwa kuwa tayari kwa ajili ya kushughulikia watu wenye nia ovu nyakati za uchaguzi. Masaa machache yamepita toka Rais awasihi JWTZ kuwa tayari kwa lolote na kauli hiyo imepata majibu! CHADEMA ni chama cha kihuni na kinaongozwa na watu wahuni wa waliojaa hila na uongo na hadaa sana kwa watanzania. Hadaa ni tabia ya viongozi wababaishaji kama ambavyo walisema Lowassa ni fisadi lakini kwa sababu ya fedha wakauza nafasi na akawa mgombea wao.! Inatia kinyaa sana kuwa na chama cha hivi na viongozi wa hivi wanaotoka kwenye vikao na kuja kusambaza uongo kwa nia ya kupotosha kwa manufaa yao ya kisiasa! CHADEMA ni kikundi cha wahuni waliojificha kwenye siasa kwa kujifanya wanasiasa lakini ni watu wa hovyo sana kwenye siasa za upinzani Tanzania. Jeshi la polisi tunawasihi sana kupiga marufuku huu upuuzi wa maandamano kwa sababu tayari watu na kikundi chao wanachoita chama wanaonekana wana ajenda iliyojificha ambayo watanzania wengi hawaijui. Wanawezaje kufanya upotoshaji wa kiwango hiki baada ya kikao chenu? #KigogoMediaUpdates
Kigogo Media11,391 次观看 • 2 年前
没有更多内容可加载