
Mdude Nyagali
@mdudenyagali • 158,227 subscribers
Political Activist in Tanzania focusing on Civil Rights and Good Governance. 🇹🇿. #Author- #FiveYearsOfPain. - To buy my Book, please click the link below.
Shorts
Videos

Continue to torture, kill and kidnap us because of our political positions. We will never stop condemning your evil because nothing that has a beginning has no end. There will be a day when everyone who has done us evil will be held accountable for their actions. The book "The Story of My Suffering" is now available in bookstores in Europe and the USA as well as in the following online bookstores.👇 Amazon - Olympia Publishers Waterstones - Barnes & Noble - WHSmith- Everything is possible with God.🙏
Mdude Nyagali152,525 Aufrufe • vor 1 Jahr

Sijapenda dharau, kejeli na matusi ya huyu Chawa kwa hawa askari Magereza. Sidhani kama wangekuwa askari polisi au askari wa JWTZ huyu chawa angatoa kejeli za namna hii. Jeshi la Magereza ni sehemu ya majeshi ya nchi yetu ni vema tukawapatia heshima kama majeshi mengine.
Mdude Nyagali112,364 Aufrufe • vor 1 Jahr

Ujumbe wangu kwako Rais baada ya tukio la polisi kuteka watu juzi.
Mdude Nyagali71,549 Aufrufe • vor 1 Jahr

Ndugu zangu hawa ni watekaji ambao Samia Suluhu na serikali yake wanasema hawajulikani. Leo walifanya jaribio la kumteka mtu katika ya Hotel ya Rovvenpec Resort Dar es salaam wakashindwa. Inadaiwa hawa ndio waliomteka na kumua Kibao, tusaidieni tupate picha zao kupitia video hii.
Mdude Nyagali82,404 Aufrufe • vor 1 Jahr

Huu ujumbe wa Zitto MwamiRuyagwa Kabwe tufanye tuwezavyo umfikie Samia Suluhu hata kwa njia ya WhatsApp. Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba kwa sasa vyombo vya dola ndivyo vinavyoongoza siasa na sio siasa kuongoza vyombo vya dola. Huko nyuma vyama vya siasa ikiwemo ccm yenyewe vilikuwa na nguvu kuliko vyombo vya dola lakini kwa sasa vyombo vya dola ndio vina nguvu kuliko vyama vya siasa. Kwa sasa vyombo vya dola ndio vinapanga nani awe kiongozi ccm na 80% ya vyama vya upinzani. Vyombo vya dola vinaweza kumuondoa kiongozi yoyote kwenye vyama vya siasa wanavyoviendesha ikiwemo chama tawala na vingine kama walivyowaondoa akina Chongolo, Polepole, Kinana, Mbatia na wengine. Vyombo vya dola wanaweza kufanya hivyo kwa sababu wanamumdu Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala . Sasa vyombo vya dola ndivyo vinavyoamua nani awe mbunge au diwani wala sio wananchi tena wanaoamua. Yani kwa sasa kura za wananchi haziamui tena nani awe mbunge bali dola ndiyo inayoamua. Zamani ulikuwa ukisikia ccm wakijitapa kwamba ccm imeshika dola lakini kwa sasa dola ndiyo iliyoishika ccm. Kwamba kwa sasa ccm imebakia kama rubber stamp tu ya dola. Viongozi wa ccm hawana uhuru wa kutoa maoni na fikra zao kama zamani na wote wanalazimishwa kusifia tu serikali hata kama wakulima huko wamedhulumiwa na serikali. Muasisi wa hali hii ya kuifanya vyombo vya dola kuwa na nguvu kuliko siasa ni Magufuli na Samia amefanya kuiendeleza. Zitto amezungumza kitu cha kweli kama hali itaendelea kuwa hivi basi siku sio nyingi ccm wataondolewa na dola. Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Mdude Nyagali53,000 Aufrufe • vor 1 Jahr

Ikitokea tumepata serikali mpya nje ya chama cha mbogamboga jeshi la polisi lote linapaswa kufanyiwa overhaul. 1- Idara ya Field Force Unit - FFU ni ya kufuta kabisa waende nyumbani kwa sababu hawana kazi yoyote. Mara nyingi wanatumika vipindi vya uchaguzi kupiga mabomu na risasi na wakati mwingine kuvuruga mikutano ya upinzani. Baada ya hapo ni kurudi kambini kucheza draft na bao wakisubiri kipindi cha uchaguzi au mikutano ya upinzani wakapige mabomu. Yani askari zaidi ya elfu 15 wa FFU wanalipwa mshahara kwa ajili ya kazi hiyo tu. Hii ni hasara kwa taifa. Jambo lingine askari waliopo FFU ni adhabu baada ya kufanya makosa makubwa kwenye idara zingine za polisi. Kwa hiyo ukweli ni kwamba FFU yote imejaa vibaka waliopaswa kufukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya kwenye idara zingine. Ndio maana unaona hawana nidhamu wala heshima na wanaendeshwa tu kama robot wanavunja watu miguu, kudhalilisha watu, kuwang'atisha mbwa watu na kuua watu kama walivyofanya majuzi pale Kisutu. Na walivyo bumunda utasikia inamisha vichwa chini msituangalie sura. Yani wanaamini kuwainamisha vichwa chini watu wanaowafanyia unyama ni salama kwao kutotambulika. Kumbe kutambulika ni suala la muda tu, mkibadilisha serikali anabanwa mkuu wakikosi analeta orodha ya askari wote waliohusika na oparesheni husika. 2 - Tunaweza kuanzisha idara mpya ya upelelezi nje ya polisi kama ilivyo FBI. Hii idara ya upelelezi inayojitegemea nje ya polisi tunaweza kuipa jina la Tanzania Top Bureau of Investigation - TTBI. Idara hii mpya haiitaji watumishi wengi. Inahitaji watumishi wasiozidi elfu 6 tu na wanahitaji ofisi moja kila mkoa na watumishi wasiozidi 300 kila mkoa. Zile Camp za FFU tunaweza kugeuza kuwa ofisi za idara hii. Kazi yao kubwa ni kila mkoa ni kufanya upelelezi wa makosa makubwa makubwa kama vile mauaji, human trafficking, ufisadi serikalini, ugaidi na mengine yanayofanana na hayo. Sare zao zinaweza kuwa nyeusi. Polisi wanaweza kubakia na upelelezi wa kesi ndogo ndogo kama wizi wa kuku, baiskel na vikesi vingine vya aina hiyo. Hii itasaidia kukomesha mateso na utekaji. Ukweli ni kwamba vikosi kazi Task force vinavyotumiwa kuteka watu vinaundwa na ma-RCO vina askari kanzu ambao mafunzo yao ya kufanya upelelezi ni madogo mno. Ndio maana hawana njia nyingine zaidi ya kupiga na kutoa mateso mengine kwa watuhumiwa wakiwalazimisha watoe majibu wanayotaka wao. Ikitokea mtuhumiwa ameamua kusema uongo ili kuwarilidhisha wasimpige basi wakigundua wamedanganywa humuua na kwenda kutupa mwili wake huko alikootwa SIR TIVA au mto Ruvu kwenye masalia ya mamba na maeneo mengine. Kumbe tunaweza kuwa na idara ambayo inaweza kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi bila kuteka na kuua watu. Tukiwa na idara ya upelelezi ya viwango vya namna hii inaweza kupata sifa hadi nje ya nchi yetu. Kwamba waombaji wa nafasi za kazi wawe na fani mbalimbali zinazoweza kusaidia kufanya upelelezi mfano Cyber, udaktari, ukemia, sheria na fani zingine zinazoweza kusaidia upelelezi. Mafunzo yao yawe ya hali ya juu na vifaa vya kusaidia uchunguzi vya kisasa kabisa. Kwa hatua za kwanza tunaweza kutafuta wakufunzi FBI na mashirika mengine makubwa kwenye nchi ambazo ni rafiki wa Tanzania. Kwamba wanafunzi kwenye chuo hicho wanafundishwa na kuivushwa namna ya kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi bila kumuumiza au kumlazimisha mtuhumiwa. Lakini pia idara hii inakuwa na askari ambao wanafundishwa namna ya kudhibiti vurugu bila kuua au kuvunja viungo watuhumiwa kama wanavyofanya hawa vibaka wenu. Tukianzisha idara hii itasaidia sana kwenye nyakati hizi ambazo technology imekua na watu hawaibi tena kwa bunduki na badala yake wanaiba kwa kutumia akili na technology. Huu ushauri kwa undani zaidi upo katika kitabu changu lakini pia ulishawahi kuchapishwa kwenye baadhi ya magazeti. Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Mdude Nyagali39,829 Aufrufe • vor 1 Jahr

Ukiacha ukatili wa Magufuli kuuwa, kuteka na kufunga jela wapinzani wake kwa sababu ya uoga wa kukosolewa na kushindana lakini alikuwa mzalendo. Fikiria mpaka Kibaka Ole Sabaya anahoji kwani Magufuli alikuwa analeta mvua? Kwanini wakati wake kulikuwa hakuna mgao wa umeme?
Mdude Nyagali50,809 Aufrufe • vor 2 Jahren

Mnamo 7 March 2021 Jaji Ntemi aliwatafuta CCM kuwataka wapeleke orodha ya mawakili ambao hawana maadili ili awafute uwakili. Kwamba ccm ndio pekee wana kipimo cha kupima maadili ya mawakili? Jaji huyu si tu kwamba hafai kuwa mwenyekiti wa maadili lakini pia hafai kuwa jaji.
Mdude Nyagali43,076 Aufrufe • vor 2 Jahren

Nawapongeza sana ACTWazalendo kwa kuunga mkono slogan ya No Reform No Election. Lengo letu ni kurudisha heshima ya kura za wananchi kuheshimika. Ili tuweze kuingia kwenye uchaguzi huru na haki serikali ikubali kufanya marekebisho yafuatayo; 1. Kama muda uliobakia hatuwezi kupata katiba mpya basi katiba iliyopo ifanyiwe reform kwenye ibara zinazohusu uchaguzi. Katiba ipige marufuku viongozi na watumishi wa tume kuteuliwa na Rais kuanzia ngazi ya taifa mpaka chini. 2. Vyama vinavyounda TCD kila chama kiwe na uwakilishi wa kuteua mjumbe mmoja wa tume huru ya uchaguzi. 3. TLS na tasisi za kidini waislamu kwa wakristo nao watoe angarau wajumbe watatu wanaounda tume huru. 4. Mwenyekiti wa tume na makamu wenyeviti bara na Zanzibar wapatikane baada ya nafasi kutangazwa halafu TCD na taasisi za kidini na TLS wafanye usaili. 5.Wasimamizi wa uchaguzi, Mkurugenzi wa tume na maafisa wa uchaguzi wapatikane kwa usimamizi wa tume huru itakayopatikana hapo juu. 6. Watumishi wa tume wasitokane na serikali wala wasiwajibike kwa Rais. Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Mdude Nyagali23,017 Aufrufe • vor 1 Jahr

Wakati Rais wa Ufaransa akipokelewa kwa baiskeli huko Denmark na mwenyeji wake, huko Mbeya ziara ya waziri mkuu ina msafara wa gari 50 pamoja na helicopter iliyokuwa juu kutwa nzima ikimlinda. Halafu kesho 🇹🇿 inawakopa hawahawa wanaobana matumizi kwa kutembelea baiskel. Upumbavu.
Mdude Nyagali42,311 Aufrufe • vor 3 Jahren

Kesi ya kupinga mkataba wa bandari ni kesho mahakama kuu Mbeya. Na huyu anayezungumza anaitwa wakili Boniface Mwabukusi A.K.A Mayweather na ndio ataongoza jopo la mawakili upande wa wananchi. Endeleeni kutuma michango kuwezesha kesi hii kwa M.Pesa 0753353030 IRENE B. MHANDO.
Mdude Nyagali35,092 Aufrufe • vor 3 Jahren