
millardayo
@millardayo • 3,138,054 subscribers
Award winning TV/Radio Personality | Hosting Amplifaya on CloudsFM |Journalist from Tanzania covering East Africa and beyond | Bookings [email protected]
Shorts
Videos

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaonya Watu wanaojiita Wanaharakati huku akisisitiza kuwa vitendo vyovyote vya ugaidi havitavumiliwa Nchini. Akizungumza leo Julai 9, 2026 Zanzibar wakati wa hafla ya kushuhudia Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa na utiaji saini wa makubaliano kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo, Rais Samia amesema baadhi ya Watu hujisitiri kwa sura ya uzalendo na uanaharakati huku wakifuata maslahi yao binafsi. “Nitumie fursa hii kuwaonya wote wanaojiita Wanaharakati ili watambulike duniani lakini matendo yao ni ya kigaidi,” amesema Rais Samia. Ameongeza kuwa baadhi ya Watu au Makundi huonekana kuwa na sura ya kizalendo lakini ndani yake wakawa na maslahi binafsi ambayo hayaendani na ustawi wa Taifa. “Watu wanavaa sura za uzalendo lakini ndani yake wana maslahi binafsi, nawasihi Watanzania tushikamane kwa maendeleo yetu na si kuwa kundi la watu fulani,” amesema. #MillardAyoUPDATES
millardayo83,358 Aufrufe • vor 5 Tagen

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa licha ya kuwa na mamlaka ya kusaini utekelezaji wa hukumu ya kunyongwa kwa mujibu wa Sheria, hajawahi kutumia mamlaka hayo tangu aingie madarakani. Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na Wakuu wa Sheria Jijini Arusha, ambapo amesisitiza kuwa kalamu za Mawakili na Maafisa wa Sheria zina nguvu kubwa na zinaweza kuwa na athari kubwa endapo zitatumika vibaya. Amesema Mawakili na Maafisa wa Sheria wa Serikali ni walinzi wa rasilimali na maslahi ya Taifa kupitia matumizi sahihi ya Sheria na ushauri wa kisheria, hali iliyowapa sifa ya kuitwa “Maaskari wa Sheria”. “Kalamu ya Mwanasheria ikitumika vizuri inaweza kuzuia hasara kabla haijatokea na inaweza kuiongoza Serikali kufanya maamuzi yenye maslahi kwa Taifa,” amesema Rais Samia. Ameongeza kuwa ingawa kalamu yake kama Rais ina mamlaka makubwa, kalamu za Mawakili na Maafisa wa Sheria zina uzito mkubwa zaidi kutokana na nafasi yao katika mchakato wa haki na maamuzi ya kisheria. “Kalamu yangu ina hatari, lakini zenu ni hatari zaidi, hatari ya kalamu yangu ni kusaini Mtu kunyongwa, jambo ambalo sijawahi kufanya,”. #MillardAyoUPDATES
millardayo16,899 Aufrufe • vor 1 Tag

Mkazi wa Lemara Njiro, Mkoani Arusha, Paul Salim ambaye ni Baba wa Watoto saba na Babu wa Mjukuu mmoja, amesema yeye na familia yake wamekuwa wakiishi katika nyumba ya mabati tangu mwaka 2011 wakilinda kiwanja kilichonunuliwa na Mwanamke mmoja ambaye hawajawahi kumuona tena. AyoTV imezungumza na Paul ambapo amesema waliwekwa kama Walinzi wa eneo hilo baada ya Mmiliki kulinunua, lakini tangu mwaka 2011 hadi sasa hawajawahi kukutana naye wala hawana mawasiliano yake. “Hili ni eneo la Dada mmoja aliyelinunua, sisi tuliwekwa hapa kama Walinzi lakini tangu mwaka 2011 mpaka leo hatujawahi kumuona wala hatuna hata namba zake za simu, tumeendelea kuishi hapa kama Walinzi wa eneo hili, tukilala pamoja na mifugo,” amesema Paul. “Watoto wangu ni saba na tunaishi kwenye chumba kimoja, msaada tunaouhitaji ni kwa ajili ya Watoto hawa, hasa kwenye elimu na changamoto za kiafya,” amesema Paul. #MillardAyoUPDATES
millardayo78,064 Aufrufe • vor 8 Tagen

Hali ya taharuki imetawala katika Mtaa wa Mabibo Sahara Jijini Dar es salaam baada ya Watu zaidi ya 30 wakidai kupangishwa chumba kimoja na Mtu anayetajwa kuwa Mmiliki wa nyumba, ambaye kwa sasa anadaiwa kutoweka na hajulikani alipo. Camera za AyoTV zimefika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wanaodaiwa kuwa waathirika, ambao wamesema kila mmoja alilipa fedha za upangaji akiamini ndiye mpangaji pekee wa chumba hicho. Hata hivyo, walipofika kuhamia walikuta Watu wengine wengi wakidai kuwa nao walipangishiwa chumba hicho hicho. “Kila mmoja wetu alilipia chumba hiki akiamini amepanga yeye peke yake, lakini cha kusikitisha kwa sasa hapa tayari tupo zaidi ya Watu 30, kuna taarifa kuwa mwenye nyumba ametutapeli,” amesema mmoja wa wanaodaiwa kuwa waathirika ambaye ni Mwanafunzi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sahara, Nasib Mangushi amesema alipokea taarifa kutoka kwa Wanafunzi hao na kuwashauri kutoa taarifa Polisi. “Hatua ya kwanza niliwaambia waende Polisi kwa sababu hiyo ni dhuluma, pia nilizungumza na Polisi, wote wamefungua RB na taarifa tulizonazo zinaonesha kuwa mwenye nyumba na Watu wa nyumba hiyo wameondoka,” amesema Mangushi. #MillardAyoUPDATES
millardayo48,701 Aufrufe • vor 7 Tagen

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kutoa bima za afya kwa Wasanii wote watakaotumbuiza katika Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva litakalofanyika Julai 10, 2026 Mlimani City, Jijini Dar es salaam. Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale amesema bima hizo zitalenga kuwasaidia Wasanii kukabiliana na changamoto za kiafya wanazokutana nazo pamoja na kutoa ulinzi wa afya kwa familia zao. Hatua hiyo inalenga kutambua mchango wa Wasanii katika kukuza sanaa na utamaduni wa Tanzania sambamba na kuimarisha ustawi wao kupitia huduma bora za afya. Akizungumza kwa niaba ya Wasanii wenzake, Afande Sele amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Sekta ya Sanaa Nchini. #MillardAyoUPDATES
millardayo32,895 Aufrufe • vor 6 Tagen

Msanii wa muziki Nchini Tanzania, Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva, amethibitisha kushiriki katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Bongo Fleva yanayotarajiwa kufanyika Julai 10, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam. Akizungumzia tukio hilo, Lulu Diva amesema anaamini tamasha hilo litarejesha kumbukumbu nyingi kwa wapenzi wa muziki wa zamani na kuwaunganisha Wasanii pamoja na Mashabiki wao katika kusherehekea miaka 30 ya Bongo Fleva. “Nilitamani siku moja hawa Wasanii wa zamani waandae tamasha kama hili, ni Wasanii ambao tumekuwa tukiwasikiliza tangu zamani, hivyo nawasihi Watu wajitokeze kwa wingi kwenye tamasha lao Julai 10, Mlimani City.” #MillardAyoUPDATES
millardayo42,983 Aufrufe • vor 8 Tagen

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Kigoma imeanza kusikiliza kesi ya uchaguzi inayopinga ushindi wa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM, Clayton Chipando maarufu Baba Levo. Kesi hiyo imefunguliwa na Wananchi wanne wa Jimbo la Kigoma Mjini, Johary Kabourou, Loum Mwitu, Pendo Kombolela na Luma Akilimali ambao pia wameishtaki Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakipinga matokeo ya uchaguzi huo. Baba Levo alitangazwa mshindi wa kiti cha ubunge cha Jimbo la Kigoma Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 baada ya kumshinda mgombea wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe. Katika kesi ya uchaguzi namba 28949 ya mwaka 2025, wadai hao wanaojitambulisha kuwa Wapiga Kura wa Jimbo la Kigoma Mjini, wanadai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro mbalimbali ambazo kwa mujibu wao, ziliathiri uhalali wa matokeo yaliyotangazwa. Shauri hilo linasikilizwa na Jaji Victoria Nongwa ambapo awali lilipangwa kuanza Juni 18, 2026, lakini likaahirishwa baada ya Walalamikaji kushindwa kuwasilisha kwa wakati maelezo ya maandishi ya mashahidi wanaotarajiwa kutoa ushahidi mahakamani, kama zinavyoelekezwa na Kanuni za Mashauri ya Uchaguzi wa Wabunge za Mwaka 2025. Leo, pande zote zimeanza kuwasilisha hoja zao mbele ya Mahakama huku shauri hilo likiendelea kufuatiliwa kwa karibu na Wananchi wa Kigoma na Wadau wa Siasa kutokana na umuhimu wake katika kuamua uhalali wa matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini. #MillardAyoUPDATES
millardayo42,453 Aufrufe • vor 8 Tagen

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema changamoto anazopitia zina mwisho, akizungumza na Viongozi na Wafuasi wa chama hicho waliofika katika Mahakama ya Rufani kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo leo Julai 3, 2026. Kauli hiyo imekuja baada ya Mahakama ya Rufani kusikiliza maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuahirisha shauri hilo, ikieleza kuwa itatoa taarifa baadaye kuhusu tarehe ya kutolewa kwa uamuzi. #MillardAyoUPDATES
millardayo33,619 Aufrufe • vor 11 Tagen

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Gambo amesema kuwa maridhiano yanayohubiriwa Nchini yanapaswa kuwa na ukweli, nia thabiti na dhamira ya kulirejesha Taifa katika misingi ya upendo, mshikamano na amani. Gambo amesema hayo wakati alipokuwa Mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa la Pentecoste Revival Church la Jijini Arusha, akisema haki ikitendeka kwenye Jamii, kazi ya kuridhiana itakuwa rahisi kwasababu Wahusika wataelewa lengo la kutaka kuridhiana kwao. Katika harambee hiyo jumla ya shilingi 116, 206,000 zilipatikana huku Mwanasiasa huyo akichangia shilingi milioni 10 pamoja na Shirika la Hifadhi ya Taifa likichangia shilingi milioni kumi katika kufanikisha ujenzi wa Kanisa hilo. "Mtu yoyote anayehubiri amani lazima aanze na haki, mahali ambapo kuna haki, hapatakuwa na manung'uniko, amani ni tunda la haki” Gambo amesisitiza kuwa ujenzi wa Taifa ni jukumu la kila mwananchi, akionya kwamba Taifa likiharibika hakuna mtu atakayenufaika, akisema Taifa haliwezi kujengwa kwa ujanjaujanja, bali kwa misingi ya ukweli, haki na uwajibikaji ili kudumisha amani na umoja Nchini. #MillardAyoUPDATES
millardayo63,132 Aufrufe • vor 22 Tagen

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya Watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani iliyofanyika Mei 2026 ikiwemo kutumia ChatGPT ambayo ni programu ya Akili Bandia (AI). Akizungumza leo Julai 6, 2026 Jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Mohamed amesema katika udanganyifu uliofanyika wapo walioingia na notisi, waliokamatwa na simu kwa kutumia ChatGPT na kusaidiana majibu. Kwa mujibu wa NECTA, Watahiniwa waliofutiwa matokeo ni 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita (36 wa shule na 8 wa kujitegemea) pamoja na Watahiniwa 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE). Prof. Mohammed amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani, Sura ya 107, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za Mwaka 2016. Aidha, amesema imekifungia Kituo cha Mitihani cha Excellency Open School (P5584) kilichopo Mkoani Manyara kuendelea kutumika kama Kituo cha Mitihani ya Taifa, baada ya kubainika kukiuka miongozo ya uendeshaji wa mitihani ambapo Kituo hicho kitabaki kufungwa hadi Baraza litakapojiridhisha kuwa kinafaa kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Katika taarifa hiyo, NECTA pia imezipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri, Wakuu wa Shule, Wasimamizi, Wasahihishaji wa mitihani pamoja na Watahiniwa wote waliozingatia taratibu za mitihani. Baraza limeeleza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) na mitihani ya Ualimu iliyofanyika Mei 2026 yanapatikana kupitia tovuti yake rasmi. #MillardAyoUPDATES
millardayo22,834 Aufrufe • vor 8 Tagen

Mbunge wa Baraza la Uwakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said amesema licha ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini kuna ‘Yuda’ ndani ya Serikali. Simai ameyasema hayo leo Juni 2, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026. “Dotto Biteko aliwahi kusema Binadamu ni walewale, nataka niwaambie hawa walewale nambatiza mmoja aliyekuwepo ndani ya Serikali basi ni Yuda, nasema hivyo kwa sababu tunataka maendeleo ya Nchi yetu, je Mama kakosea wapi ? Kwa sababu ya kumwamini Mtu kumbe ni Yuda ambaye amesaliti ndugu zake hata ile familia iliyomlea” “Yuda tumeona ameanza kuibuka kwenye Nyumba za Ibada kutafuta huruma za Wananchi na Watu mbalimbali lakini nataka niseme Wabunge wenzangu na Serikali iliyopo hapa tuamkeni, leo anapita anataka kutuaminisha kwamba Rais Magufuli alimpenda,” amesema Simai. Kwa mujibu wa Biblia, Yuda Iskariote ni mmoja wa Wanafunzi 12 wa Yesu Kristo anayejulikana kwa kumsaliti Yesu kwa Vipande 30 vya fedha. #MillardAyoUPDATES
millardayo92,240 Aufrufe • vor 1 Monat

Jeshi la Magereza Tanzania limemkabidhi shilingi milioni mbili, Saimon Juma baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha miezi miwili kilichotokana na kosa la kutumia lugha isiyofaa wakati wa kikao cha familia. Akizungumza na AyoTV leo Juni 23, 2026 Jijini Arusha, Juma amesema kipindi alichokaa gerezani kimemsaidia kujifunza mambo mbalimbali, ikiwemo ujasiriamali jambo ambalo amedhamiria kulitumia kujikwamua kiuchumi. “Kosa langu ni kwamba nilikuja gerezani baada ya kutukana kwenye kikao cha familia, sikuiba wala sikumdhuru Mtu na nimetumikia kifungo cha miezi miwili na siku 16, sikujua kama ningeweza kujifunza ujasiriamali gerezani, nilifungwa baada ya kumtukana Kaka yangu na kumuita ‘Shilawadu’,” amesema Juma. Akizungumza wakati wa kumkabidhi fedha hizo, Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Jeremiah Katungu amesema Jeshi la Magereza linaendelea kuwawezesha wafungwa na Wafungwa waliomaliza vifungo vyao kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea baada ya kurejea katika Jamii. “Jeshi la Magereza linaunga mkono jitihada zake na litatoa kiasi cha shilingi milioni mbili kama mtaji wa kuanzia shughuli zake za ujasiriamali,” amesema Katungu. #MillardAyoUPDATES
millardayo46,784 Aufrufe • vor 21 Tagen

Mkazi wa Lemara Njiro, Mkoani Arusha, Paul Salim ambaye ni Baba wa Watoto saba na Babu wa Mjukuu mmoja, amesema yeye na familia yake wamekuwa wakiishi katika nyumba ya mabati tangu mwaka 2011 wakilinda kiwanja kilichonunuliwa na Mwanamke mmoja ambaye hawajawahi kumuona tena. AyoTV imezungumza na Paul ambapo amesema waliwekwa kama Walinzi wa eneo hilo baada ya Mmiliki kulinunua, lakini tangu mwaka 2011 hadi sasa hawajawahi kukutana naye wala hawana mawasiliano yake. “Hili ni eneo la Dada mmoja aliyelinunua, sisi tuliwekwa hapa kama Walinzi lakini tangu mwaka 2011 mpaka leo hatujawahi kumuona wala hatuna hata namba zake za simu, tumeendelea kuishi hapa kama Walinzi wa eneo hili, tukilala pamoja na mifugo,” amesema Paul. “Watoto wangu ni saba na tunaishi kwenye chumba kimoja, msaada tunaouhitaji ni kwa ajili ya Watoto hawa, hasa kwenye elimu na changamoto za kiafya,” amesema Paul. #MillardAyoUPDATES
millardayo17,140 Aufrufe • vor 7 Tagen

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewataka Wamiliki wa Hoteli, Lodge na Guest house Nchini kuhakikisha wanawasajili Wageni wote wanaofikia katika maeneo yao kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa (NIDA), ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usalama. Katambi ameyasema hayo leo Juni 26, 2026, Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali kuhusu hali ya usalama Nchini. “Wageni wote wanaoingia kwenye Majiji wajisajili, tutakapoenda kwenye hoteli yako tukakuta kuna watu wasioeleweka, tutakuchukulia hatua,” amesema Katambi. Amesema hatua hiyo inalenga kusaidia Vyombo vya Ulinzi na usalama kuwabaini watu wanaotumia maeneo ya malazi kujificha au kufanya shughuli zinazohatarisha usalama wa Wananchi na Nchi kwa ujumla. #MillardAyoUPDATES
millardayo37,414 Aufrufe • vor 18 Tagen

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makond amewasili katika eneo la pembezoni mwa Mnara wa Eiffel Tower, Paris nchini Ufaransa, kwenye Usiku wa Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yatakayofanyika Julai 7, 2026. AyoTV ipo hapa Paris kukuletea matukio yote ya tamasha hilo linalofanyika leo Julai 5, 2026, likipambwa na maonesho ya vyakula vya Kiswahili, bidhaa za uchongaji, pamoja na burudani kutoka kwa Sholo Mwamba, Ramadhan Brothers, Patricia Hirary, maonesho ya ulimbwende na vivutio vingine vingi vya Utamaduni. Makonda, ambaye ni mgeni rasmi wa hafla hiyo, anatarajiwa kuhutubia wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo akiwa ameambatana na Viongozi wengine wa Serikali. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema tamasha hilo ni ishara kwamba lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na kuimarisha nafasi yake katika mataifa mbalimbali duniani. #MillardAyoUPDATES
millardayo18,433 Aufrufe • vor 8 Tagen

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema Balozi wa Urusi Nchini Tanzania, Andrey Avetisyan kuwa chini ya ardhi iliyopo maeneo ya Mlima Kilimanjaro kuna udongo wenye rutuba nzuri unaofaa kurutubisha mimea ya kutengeneza mvinyo ‘wine’ Kitanzania. Makonda amesema hayo usiku wa kuamkia leo wakati alipoalikwa kuwa ni mgeni rasmi kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 25 ya ushirikiano wa urafiki mwema kati ya China na Urusi zilizofanyika katika Jumba la Urusi Jijini Dar es salaam, zikipambwa pia na utazamaji wa filamu iliyowakutanisha pamoja Waigizaji wa Urusi na China. Waziri Makonda amesema “Nilikuwa naongea na Balozi wa Russia akaniambia kwenye Mlima kilimanjaro pale chini pale kuna udongo wenye rutuba nzuri unaofaa kutumika kwenye kilimo cha kutengeneza wine, tuna wine yetu ya Dodoma kumbe na Mlima Kilimanjaro chini ile ardhi ina rutuba nzuri ya kupanda aina ya mimea tukatengeneza wine sisi wenyewe Watanzania” “Ameniambia yupo tayari kushirikiana na sisi kuwachukua Vijana wa Kitanzania kwenda Russia kujifunza namna ya kulima namna ya kutengeneza wine waje watumie hyo fursa ya kutengeneza wine, vilevile kwa Ndugu zetu wa China kuna fursa nyingi” #MillardAyoUPDATES
millardayo38,778 Aufrufe • vor 19 Tagen

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema baadhi ya Viongozi wanapokuwa Serikalini hujikuta wakijisahau na kufikia hatua ya kujiona kuwa wao ndio kila kitu. Sirro ametoa kauli hiyo leo Juni 26, 2026 wakati wa kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (SACP), Richard Abwao aliyefariki dunia Juni 20, 2026. “Kwetu ni faraja sana kwamba mlituletea kijana mchapakazi ambaye siku zake zimefika, lakini amekwenda kwa heshima kubwa.” “Niwashukuru sana Viongozi wetu wa dini, sisi wakati mwingine tunajisahau tukiwa Serikalini, tunaona sisi ndio kila kitu hata wenzangu ni mashahidi, nilikuwa navaa magwanda kama Wambura.”Amesema Sirro. #MillardAyoUPDATES
millardayo35,796 Aufrufe • vor 18 Tagen

Vijana wawili wa Kitanzania wanaofanya kazi katika mradi wa ujenzi wa minara ya kusambaza umeme kupitia Kampuni ya TBEA wameiomba Serikali kuchukua hatua dhidi ya raia wa China wanaodai kuwashambulia wakati wakiwa kazini. Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, vijana hao ambao ni Mbaraka Ally (18) na Stephen Mwampaka (44) wamesema tukio hilo lilitokea Juni 19, 2026 katika Kitongoji cha Sokoine Ranchi, Kata ya Dakawa, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro. Kwa mujibu wa maelezo yao, siku ya tukio Stephen Mwampaka alidai kuvamiwa na kuanza kushambuliwa na baadhi ya raia wa China wanaosimamia mradi huo. Mbaraka amesema alipojaribu kuingilia kati na kutaka kufahamu chanzo cha tukio hilo baada ya kumuona mwenzake akishambuliwa, naye alijikuta akipigwa na wasimamizi hao wa kigeni. Awali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Juni 20, 2026, lilisema linamshikilia Mtuhumiwa mmoja, Zhou Zhi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo huku Mtuhumiwa mwingine aliyefahamika kwa jina la Yung Lu akiendelea kusakwa. #MillardAyoUPDATES
millardayo40,249 Aufrufe • vor 21 Tagen

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema licha ya Serikali kutumia zaidi ya shilingi bilioni 54 kujenga Stendi ya Magufuli, baadhi ya maeneo ya Jiji yameendelea kugeuzwa kuwa stendi zisizo rasmi za mabasi, hali inayochangia ongezeko la foleni na kuvuruga utaratibu wa usafiri. Akitoa mfano wa eneo la Shekilango, Chalamila amesema baadhi ya mabasi yamekuwa yakipaki kwenye hifadhi za barabara na kuyageuza maeneo hayo kuwa stendi, jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara. Chalamila ameyasema hayo leo, Juni 29, 2026, wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Pwani, kilicholenga kujadili mikakati ya kudhibiti na kupunguza tatizo la foleni katika Dar es salaam. “Ukienda Ubungo kuna Stendi ya Magufuli iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 54, lakini leo tumeruhusu karibu kila eneo la mkoa kuwa stendi, Watu wa Uhamiaji hawawezi kufanya kazi yao kwa ufanisi, vyombo vya dola navyo haviwezi kutekeleza majukumu yao ipasavyo na katika miji mingi iliyoendelea duniani, unaweza kupandisha abiria na kuwapeleka hadi stendi kuu, lakini huwezi kupeleka basi hadi nyumbani kwa kila abiria,”amesema Chalamila. #MillardAyoUPDATES
millardayo27,263 Aufrufe • vor 15 Tagen

Usiku wa leo Juni 27, 2026 Camera za AyoTV zimeshuhudia foleni kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam, ikiwemo Ubungo- River Side ambapo magari yanayotokea Mwenge kuelekea Mabibo yamekwama kwenye foleni ndefu iliyofika hadi juu ya Daraja la Kijazi (Flyover). Hali kama hiyo pia imeshuhudiwa kwenye Barabara ya Morogoro, ambapo magari yanayotoka katikati ya Jiji kuelekea Kimara na Mbezi yamekwama kwenye foleni kubwa. #MillardAyoUPDATES
millardayo29,241 Aufrufe • vor 17 Tagen