
millardayo
@millardayo • 3,143,346 subscribers
Award winning TV/Radio Personality | Hosting Amplifaya on CloudsFM |Journalist from Tanzania covering East Africa and beyond | Bookings [email protected]
Shorts
Videos

Mwanzilishi wa Kampuni ya Teknolojia ya NALA MONEY Benjamin Fernandes, ameibua hoja mbele ya Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba kuhusu changamoto zinazowakabili Watanzania ikiwemo kuingia Nchini Marekani hata kama ni kwa sababu za kibiashara au za kimasomo. Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba katika mkutano na Watanzania London Uingereza, Fernandes amesema licha ya kuwa Mtanzania anayejivunia Nchi yake, amekuwa akikumbana na changamoto zinazohusiana na hati ya kusafiria ( passport) katika safari zake za kibiashara za Kimataifa, hali ambayo amesema inaweza kuwa kikwazo kwa Watanzania wanaotafuta fursa nje ya Nchi. Fernandes ameeleza kuwa kupitia biashara yake amefanikiwa kupata uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 50 kutoka Marekani lakini kwa sasa anapata wakati mgumu kwenye biashara yake kwakuwa kuna zuio la Watu wenye passport za Tanzania kuingia Marekani kwa visa za B1 au B2. #MillardAyoUPDATES
millardayo87,150 views • 5 days ago

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemzawadia usafiri wa Bajaji, Muimbaji wa nyimbo za Uzalendo mwenye ulemavu, Issa Musembe Bugondo, aliyeshiriki matukio ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 katika Mikoa mbalimbali. Muimbaji huyo, alitoa ombi la kupatiwa bajaji alipokutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi wakati akitembelea Soko Kuu la Sumbawanga kuwasalimia Wafanyabiashara katika eneo hilo, Oktoba 14, 2026. Akikabidhi Bajaji hiyo, Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mukrim Makame amesema Rais Dkt. Samia amefurahishwa na kujitolea kwa Muimbaji huyo, ambaye licha ya ulemavu amekuwa akisafiri maeneo mbalimbali na kutoa ujumbe wa amani kupitia muziki wake. Kwa upande wake, Bugondo amemshukuru Rais Samia kwa msaada huo, na kumuombea heri katika uongozi wake huku akisema ataendelea kuwa Balozi wa amani Nchini na kusisitiza uzalendo kwa Watanzania. #MillardAyoUPDATES
millardayo21,574 views • 2 days ago

Mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, Damas Mgaya (38) amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba chake, huku ikielezwa kuwa alijinyonga kwa kutumia kamba ya kiatu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga amethibitisha tukio hilo lililoripotiwa leo, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa Marehemu alikutwa akiwa na kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha. Kwa mujibu wa Kamanda Banga, tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na msongo wa mawazo uliotokana na mgogoro wa kifamilia kati ya Marehemu na Mkewe, ikiwemo kutokubaliana kuhusu kushiriki tendo la ndoa, ambapo inadaiwa Mkewe alikuwa akikataa kwa sababu za imani ya dini. Aidha, Kamanda huyo ametoa wito kwa Viongozi wa dini kuendelea kutoa mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na Jamii. #MillardAyoUPDATES
millardayo33,534 views • 3 days ago

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda amewataka Wataalamu, Wakandarasi na Wazabuni wanaohusika na ujenzi wa vivuko Mkoani Mwanza kuhakikisha kazi zote zinakamilika na kukabidhiwa kabla ya mwisho wa mwaka 2026. Akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza, Makonda amesisitiza kuwa vivuko vinavyojengwa, ikiwemo MV Bukondo na MV Ukerewe, vinapaswa kukamilika bila visingizio ili Wananchi waanze kupata huduma za usafiri wa majini. “Kama mwezi huu utaisha hajaja Mtu kuzindua Mheshimiwa Mwenyekiti na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa chukua kivuko peleka kwa Wananchi," amesema Makonda. Ameonya dhidi ya tabia ya kukamilisha miradi lakini kuiacha bila kuanza kutoa huduma kwa sababu ya kusubiri uzinduzi rasmi. “Serikali yetu haiwezi kutoa pesa alafu Mkandarasi au Mzabuni akamaliza kazi alafu kivuko kinabaki kimesubiri kuzinduliwa,” amesema. #MillardAyoUPDATES
millardayo39,853 views • 5 days ago

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema hali ya El Niño inaweza kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027, huku akiwataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu ailinde Tanzania. Akizungumza na AyoTV, Dkt. Chang’a amesema hali hiyo inaendelea kuimarika na kuelekea katika hatua ya kukomaa, jambo linaloweza kusababisha athari mbalimbali zinazohusiana na hali ya hewa. Amesisitiza kuwa Mamlaka inaendelea kushirikiana na Wataalamu wa Sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa Serikali katika kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa na maelekezo sahihi ya kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza. “Masuala ya kiimani yana nafasi muhimu katika maisha ya Mwanadamu, hivyo tunaendelea kusisitiza umuhimu wa Wananchi, pamoja na Viongozi wetu wa dini, kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili atujaalie kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na changamoto hii ya hali ya hewa,” amesema Dkt. Chang’a. #MillardAyoUPDATES
millardayo36,890 views • 5 days ago

Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, leo Septemba 29, 2026 amemuomba radhi Msanii mwenzake, Omary Nyembo “Ommy Dimpoz”, kutokana na kauli aliyoitoa dhidi yake. Akizungumza kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Dudu Baya amesema, “nilitumia jina la Ommy Dimpoz ili ujumbe ufike dunia nzima kwa sababu wewe ni maarufu, wewe ni Mdogo wangu na tunaheshimiana sana najua nilikukera, nilikuudhi, naomba uniwie radhi, nisamehe sana.” Dudu Baya alitoa kauli hiyo dhidi ya Ommy Dimpoz wakati wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Arusha. #MillardAyoUPDATES
millardayo115,044 views • 18 days ago

Mwanamke aitwaye Lorraine Wilkerson (67) kutoka Indiana, Marekani amekamatwa baada ya mamlaka kudai kuwa alikutwa akiendesha gari kwa kufanya mizunguko ya duara maarufu kama “donuts” nje ya jengo la Mahakama akiwa amelewa. Video iliyotolewa na Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Jennings inamuonyesha Wilkerson akiendesha gari kwa kufanya mizunguko midogo mfululizo mbele ya jengo la Mahakama ya Kaunti ya Jennings. Baada ya kukamatwa, Wilkerson alipelekwa katika Gereza la Kaunti ya Jennings akikabiliwa na tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa, ikiwemo kuwa na kiwango cha pombe kwenye damu (BAC) cha asilimia 0.08 au zaidi. #MillardAyoUPDATES
millardayo48,068 views • 10 days ago

Rapa na Mfanyabiashara kutoka Marekani, Rick Ross, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia, huku akisema muziki, vipaji na nguvu inayotoka Nchini vinastahili kupewa nafasi kubwa zaidi Kimataifa. Kupitia mtandao wake wa Instagram, Rick Ross amesema Tanzania imekuwa akilini mwake kutokana na ukuaji wa muziki na vipaji vilivyopo nchini, akieleza kuwa yuko tayari kuja Tanzania, kutumia muda na Watanzania na kujionea mwenyewe vivutio mbalimbali, ikiwemo Serengeti na Zanzibar. “Heshima kubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiweka Tanzania kwenye jukwaa la dunia,” amesema Rick Ross. Staa huyo pia amesema ana mipango mikubwa inayohusisha kufanya kazi na baadhi ya Wasanii wakubwa wa Tanzania pamoja na kuwafikia Wasanii wa kizazi kipya wanaochipukia, akisema kuna vipaji vikubwa ambavyo anataka dunia ivione. Rick Ross amesema yuko tayari kuja Tanzania, kuungana na Watu na kujifunza zaidi kuhusu utamaduni na mazingira ya Nchi, huku akisisitiza kuwa mipango hiyo ni mwanzo wa mambo makubwa anayotarajia kuyafanya nchini. #MillardAyoUPDATES
millardayo115,831 views • 24 days ago

Mtoto Amour Abdulrazak, aliyeripotiwa kupotea Oktoba 10, 2026, na baadaye kupatikana akiwa amefariki dunia, amezikwa leo Oktoba 13, 2026 katika Makaburi ya Kwa Dunga, Mbagala Kingugi, jijini Dar es salaam. Leo, Oktoba 13, 2026, AyoTV imefika nyumbani alipokuwa akiishi Mtoto huyo, ambako shughuli za msiba zimeendelea, na kuzungumza na Mjumbe wa Nyumba Kumi wa Mtaa wa Beach Boy, Mbagala Kingugi, ambaye ameelezea tukio hilo. #MillardAyoUPDATES
millardayo18,441 views • 4 days ago

Wamiliki wa nyumba katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam, wamesema wanakusudia kwenda Mahakamani kupinga rasimu ya Mpango Mpya wa Maendeleo wa Sinza wa mwaka 2026–2046, unaotarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya mwaka huu. Mpango huo, unaosimamiwa kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, unalenga kuliendeleza eneo la Sinza kuwa eneo jumuishi litakalohusisha ujenzi wa majengo ya Biashara na Makazi. Wakizungumza katika mkutano wao uliofanyika Septemba 5, 2026, Wamiliki hao wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kudai kuwapo kwa kasoro katika rasimu ya mpango huo wa miaka 20. Wamedai kuwa utekelezaji wa rasimu hiyo unaweza kuathiri haki zao za umiliki pamoja na stahiki zao endapo watahitajika kuhamishwa ili kupisha utekelezaji wa mpango huo. Mwenyekiti wa Kamati ya Wamiliki wa Nyumba Sinza, Lumuli Mwaipopo, amesema hayo wakati wa kikao cha kuwapa Wamiliki mrejesho na kujadili namna ya kukamilisha taratibu za kufungua kesi mahakamani. #MillardAyoUPDATES
millardayo123,124 views • 1 month ago

#VIDEO Mtandao wa ZBC News Nchini Zimbabwe umeonesha video ya eneo ilikopata ajali Helikopta iliyokuwa imembeba Mfanyabiashara wa Zimbabwe Wicknell Chivayo na Mkewe Lucy ikielezwa kuwa walikuwa wakitoka kwenye Jumba lao la kifahari wanalojenga Kijijini kurudi nyumbani kwao Harare. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijatajwa lakini imeelezwa kuwa Helikopta hiyo ilipata ajali saa kumi na moja jioni ikiwa ni dakika 40 tangu ipae kutoka kwenye Kijiji walichokwenda ambapo Mamlaka zimesema ililipuka baada ya ajali na kusababisha miili ya Marehemu kutotambulika kwa urahisi kwenye eneo la tukio. Msemaji wa Familia ambaye amenukuliwa akisema waliofariki katika ajali hiyo ni Chivayo na Mkewe Lucy, hakutaja Watoto wao kama miongoni mwa Abiria wengine waliofariki. #MillardAyoUPDATES ( 📹 ZBC News )
millardayo45,112 views • 16 days ago

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amependekeza kuku wanaofugwa katika Mikoa ya Dodoma na Singida watambulike kwa jina la Kuku wa Kanda ya Kati badala ya kuitwa kuku wa kienyeji, akisema hatua hiyo itaongeza utambulisho na thamani ya bidhaa hiyo sokoni. Dkt. Mwigulu ametoa pendekezo hilo Agosti 1, 2026, wakati akifungua Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Malecela Jijini Dodoma, ambapo amesema kuku hao ni zao la kipekee la Kanda ya Kati na wanapaswa kutambulishwa kwa jina linaloakisi asili yao. Amesema bidhaa nyingi za kilimo hutambulishwa kwa majina ya maeneo zinakotoka, jambo ambalo huongeza ushindani na thamani yake sokoni, hivyo ni muhimu utaratibu huo utumike pia kwa kuku wa Dodoma na Singida. “Tunapotaja mchele tunaambiwa ni wa Shinyanga au wa Kyela, na tukizungumzia ndizi tunaambiwa ni za Bukoba au Moshi. Lakini tukifika kwenye kuku wa Singida na Dodoma tunaambiwa ni kuku wa kienyeji. Hilo linapunguza utambulisho wao, hivyo waitwe Kuku wa Kanda ya Kati,” amesema Dkt. Mwigulu. #MillardAyoUPDATES
millardayo153,835 views • 2 months ago

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amesema kupendekezwa kwa Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni “chenga ya mwili” aliyoipiga Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema Watu wengi hawakutarajia uteuzi huo. Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge leo Agosti 27, 2026 Waitara amesema “Katika eneo ambalo Watu wamepigwa chenga ya mwili ni uteuzi wa Ndejembi kuwa Makamu wa Rais, Watu wengi walikuwa hawafikirii kama atapata nafasi hiyo.” “Lakini pia amefanikiwa kwa sababu ni Mtu ambaye ameishi maisha ya kawaida siyo Mtu wa kujikweza na tumekaa naye, tunaongea naye kawaida kama kuna mambo ya Wizara yake alikuwa anasimamia na anakushauri ufanye hiki au kile.” #MillardAyoUPDATES
millardayo92,718 views • 1 month ago

Kikao cha Robo ya Nne cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya limewasimamisha kazi Watumishi wawili akiwemo mmoja aliyechagua kutunza ndoa badala ya kazi. Akizungumza katika kikao hicho, leo Agosti 21, 2026 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Aida Haule amesema sababu zilizochangia kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya Watumishi hao ni pamoja na masuala ya kinidhamu. Aida amesema miongoni mwa Watumishi hao, mmoja alichagua kutunza ndoa yake badala ya kutekeleza wajibu wake wa kazi, jambo lililochangia kuchukuliwa kwa hatua dhidi yake. Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma, huku akisisitiza umuhimu wa kila Mtumishi kutimiza wajibu wake na kuzingatia taratibu za kazi. #MillardAyoUPDATES
millardayo98,011 views • 1 month ago

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Kawaida amesema aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amefukuzwa CCM kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kuitwa na Chama lakini akakataa kufika katika Kamati ya Maadili. Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari, “ninazungumza haya kwa sababu najua Watu wengi watamani kujua kilichotokea lakini kama Tawi la Mashariki kwa kushirikiana na NEC, ndilo lililotoa maelekezo kwa Kiongozi aliyepita kuitwa katika Kamati ya Maadili” “Yeye, kwa sababu ya kiburi, kutokuona umuhimu na kudharau maelekezo ya Chama, akasita kufika hapo ndipo tulipofikia hatua ya kuchukua uamuzi wa kumfukuza chamani,” “Lakini hili ni funzo la kwanza tunalolipata sisi Vijana kwa kuendelea kuheshimu Chama, kuheshimu Katiba, kuheshimu kanuni na taratibu za Chama cha Mapinduzi.” #MillardAyoUPDATES
millardayo81,655 views • 1 month ago

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Elkiroa, Kata ya Lemara Mkoani Arusha, wamefanya sherehe za kupika vyakula kusherehekea kuondoka kwa Mama Rashid, Mwanamke aliyekuwa akiishi kwa kupanga katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 17. Hatua hiyo inakuja baada ya baadhi ya Wakazi kumtuhumu kuhusika na vitendo vya ushirikina na kung’ang’ania nyumba zinazodaiwa kuwa mali ya marehemu. AyoTV imefika eneo la tukio ambapo imeshuhudia, majirani katika Mtaa huo wakisheherekea kwa kupika vyakula baada ya Mama Rashid kuhama. Itakumbukwa kwamba, hivi karibuni AyoTV ilizungumza na Mama Rashid ambaye alidai kuwa alikataa kuondoka kwa sababu alikuwa akimdai Msimamizi wa mirathi kiasi cha shilingi milioni saba. #MillardAyoUPDATES
millardayo113,195 views • 2 months ago

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania wanaotoa zawadi za fedha taslimu katika sherehe mbalimbali kuacha utaratibu wa kutupa noti na badala yake kutumia mifumo ya malipo ya kidigitali ili kulinda ubora wa fedha zinazotumika Nchini. Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2026 na Meneja Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania Victoria Msina wakati akizungumza na AyoTV katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea Mkoani Dodoma. Msina amesema noti na sarafu hutengenezwa kwa gharama kubwa hivyo zinapaswa kutunzwa kwa uangalifu na kuwa kila noti ina namba maalumu ya utambulisho na Benki Kuu hufuatilia muda wake wa matumizi hivyo kitendo cha kuzitupa chini kuzikanyaga au kuzishika kwa mikono yenye jasho na unyevu hupunguza ubora na maisha ya fedha hizo. Aidha amesema matumizi ya mifumo ya malipo ya kidigitali ni njia salama na ya kisasa ya kutoa zawadi katika sherehe badala ya kutumia fedha taslimu kwa namna inayoweza kuziharibu, pia amefafanua tofauti ya sarafu zinazovutwa na sumaku na zile zisizovutwa akieleza kuwa hali hiyo hutokana na aina ya metali zinazotumika kuzitengeneza. “Kweli pesa ni ya kwako umetafuta kwa jasho lako lakini kiustaarabu unaweza kutumia njia nyingine mbadala kama kutumia mifumo ya malipo ukaingiza kwenye benki yake halafu ukumbini ukapeleka risiti ya malipo” amesema Msina. #MillardAyoUPDATES
millardayo108,704 views • 2 months ago

Mama mzazi wa Msanii Zuchu, Khadija Kopa amesema baadhi ya maneno yanayotolewa na Watu yamekuwa yakichochea kutaka kuvunja ndoa ya Diamond na Zuchu. Akizungumza wakati wa hafla ya Babe Shower, Bi. Kopa amesema wapo baadhi ya Watu wanaokuza mambo madogo yanayotokea kati yao badala ya kutoa ushauri au kumtia moyo anayepitia changamoto. “Mara nyingi namtetea Diamond kuliko Zuchu hadi analalamika, kwani hata vikombe vinagongana na kwa sababu ya umaarufu wao kitu kidogo kinakuwa kikubwa, kuna Watu washakunaku wanaotia chumvi na kuumiza Watu,” amesema Khadija Kopa. #MillardAyoUPDATES
millardayo100,094 views • 2 months ago

Upande wa Jamhuri umefunga ushahidi wao kwa Shahidi wa 17 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Akizungumza leo Agosti 17, 2026 Mahakamani, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga amesema msimamo huo umefikiwa baada ya Jamhuri kufanya tathmini ya kina ya ushahidi na hoja zote zilizowasilishwa katika kesi hiyo. Hata hivyo, Katuga ameomba Mahakama iruhusu Jamhuri kuwasilisha hoja za ziada kueleza sababu zinazowafanya waone Lissu ana kesi ya kujibu, ombi ambalo Lissu amepinga akieleza kuwa sheria tayari inaweka utaratibu unaopaswa kufuatwa katika hatua hiyo. Iwapo Mahakama itaamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, atapewa nafasi ya kuanza kujitetea kwa kuwasilisha ushahidi na Mashahidi wake na endapo Mahakama itaamua kuwa hana kesi ya kujibu, kesi hiyo itafikia mwisho. Kesi hiyo inaendelea mbele ya jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru. #MillardAyoUPDATES
millardayo75,616 views • 2 months ago




