
millardayo
@millardayo • 3,140,741 subscribers
Award winning TV/Radio Personality | Hosting Amplifaya on CloudsFM |Journalist from Tanzania covering East Africa and beyond | Bookings [email protected]
Shorts
Videos

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Kawaida amesema aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amefukuzwa CCM kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kuitwa na Chama lakini akakataa kufika katika Kamati ya Maadili. Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari, “ninazungumza haya kwa sababu najua Watu wengi watamani kujua kilichotokea lakini kama Tawi la Mashariki kwa kushirikiana na NEC, ndilo lililotoa maelekezo kwa Kiongozi aliyepita kuitwa katika Kamati ya Maadili” “Yeye, kwa sababu ya kiburi, kutokuona umuhimu na kudharau maelekezo ya Chama, akasita kufika hapo ndipo tulipofikia hatua ya kuchukua uamuzi wa kumfukuza chamani,” “Lakini hili ni funzo la kwanza tunalolipata sisi Vijana kwa kuendelea kuheshimu Chama, kuheshimu Katiba, kuheshimu kanuni na taratibu za Chama cha Mapinduzi.” #MillardAyoUPDATES
millardayo76,043 görüntüleme • 2 gün önce

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amesema kupendekezwa kwa Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni “chenga ya mwili” aliyoipiga Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema Watu wengi hawakutarajia uteuzi huo. Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge leo Agosti 27, 2026 Waitara amesema “Katika eneo ambalo Watu wamepigwa chenga ya mwili ni uteuzi wa Ndejembi kuwa Makamu wa Rais, Watu wengi walikuwa hawafikirii kama atapata nafasi hiyo.” “Lakini pia amefanikiwa kwa sababu ni Mtu ambaye ameishi maisha ya kawaida siyo Mtu wa kujikweza na tumekaa naye, tunaongea naye kawaida kama kuna mambo ya Wizara yake alikuwa anasimamia na anakushauri ufanye hiki au kile.” #MillardAyoUPDATES
millardayo86,814 görüntüleme • 4 gün önce

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesimulia ukaribu wake na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, akisema licha ya kuwa rafiki yake wa karibu anayemchukulia kama Kaka yake, cheo kipya cha Ndejembi kilimfanya ampokee kwa heshima ya kiitifaki. Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mavunde amesema wakati akimpokea Ndejembi katika Uwanja wa Ndege Dodoma, alizingatia heshima ya nafasi yake mpya, lakini Makamu huyo wa Rais alimtoa katika mstari wa kawaida wa kiitifaki na kumkumbatia. “Tukio lile limebaki kuwa ni kumbukumbu kubwa sana kwa sababu sio rahisi katika hatua ambayo amefikia Mheshimiwa Makamu wa Rais kumpa heshima ile ya kunitoa kwenye mstari wa kawaida wa kiitifaki kuweza kunikumbatia,” Ameongeza kuwa Kwa busara, weledi, hekima na uwezo mkubwa alionao kiuongozi, hana mashaka na utendaji wake. #MillardAyoUPDATES
millardayo30,536 görüntüleme • 2 gün önce

Kikao cha Robo ya Nne cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya limewasimamisha kazi Watumishi wawili akiwemo mmoja aliyechagua kutunza ndoa badala ya kazi. Akizungumza katika kikao hicho, leo Agosti 21, 2026 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Aida Haule amesema sababu zilizochangia kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya Watumishi hao ni pamoja na masuala ya kinidhamu. Aida amesema miongoni mwa Watumishi hao, mmoja alichagua kutunza ndoa yake badala ya kutekeleza wajibu wake wa kazi, jambo lililochangia kuchukuliwa kwa hatua dhidi yake. Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma, huku akisisitiza umuhimu wa kila Mtumishi kutimiza wajibu wake na kuzingatia taratibu za kazi. #MillardAyoUPDATES
millardayo92,523 görüntüleme • 9 gün önce

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimeomba kukutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba ili kujadili changamoto zinazowakabili ikiwemo kuongeza gharama za nauli. Akizungumza Jijini Dar es salaam, leo Agosti 22, 2026 Katibu Mkuu wa TABOA, Priscus Joseph amesema Chama hicho kinaunga mkono maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na kwamba Wanachama wake wameitikia kwa asilimia 100 kwa kuhamia Stendi ya Magufuli. “Tumemwomba Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa zile changamoto zetu zifanyiwe kazi, hasa ada kubwa ya kupiga debe na Wamiliki wa tiketi zifanywe kazi, tukamwandikia barua tukutane, lakini bado hatujapata jibu.” Amesema utekelezaji wa agizo hilo umeibua pia gharama mpya kwa Wamiliki wa mabasi, hasa kutokana na ulazima wa kutumia shuttle kuwapeleka Abiria kutoka Stendi ya Magufuli kwenda maeneo mbalimbali ya Jiji pamoja na kutumia malori kwa ajili ya mizigo. #MillardAyoUPDATES
millardayo66,306 görüntüleme • 9 gün önce

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi amesema atawatumikia Watanzania wote bila kuangalia itikadi za Vyama vya siasa na kuhakikisha anapigania maendeleo ya Wananchi. Ndejembi ameyasema hayo wakati akiwasalimu wananchi wa Jimbo la Chamwino waliojitokeza kumpokea nje ya Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma mara baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais. “Wananchi sitawazingua na Mama sitamzingua, nilizungumza jana Bungeni na leo ninazungumza tena ya kuwaambia kwamba nitawatumikia Watanzania wote bila kujali Vyama vyetu, kila mmoja anahitaji maendeleo,” #MillardAyoUPDATES
millardayo17,067 görüntüleme • 2 gün önce

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amependekeza kuku wanaofugwa katika Mikoa ya Dodoma na Singida watambulike kwa jina la Kuku wa Kanda ya Kati badala ya kuitwa kuku wa kienyeji, akisema hatua hiyo itaongeza utambulisho na thamani ya bidhaa hiyo sokoni. Dkt. Mwigulu ametoa pendekezo hilo Agosti 1, 2026, wakati akifungua Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Malecela Jijini Dodoma, ambapo amesema kuku hao ni zao la kipekee la Kanda ya Kati na wanapaswa kutambulishwa kwa jina linaloakisi asili yao. Amesema bidhaa nyingi za kilimo hutambulishwa kwa majina ya maeneo zinakotoka, jambo ambalo huongeza ushindani na thamani yake sokoni, hivyo ni muhimu utaratibu huo utumike pia kwa kuku wa Dodoma na Singida. “Tunapotaja mchele tunaambiwa ni wa Shinyanga au wa Kyela, na tukizungumzia ndizi tunaambiwa ni za Bukoba au Moshi. Lakini tukifika kwenye kuku wa Singida na Dodoma tunaambiwa ni kuku wa kienyeji. Hilo linapunguza utambulisho wao, hivyo waitwe Kuku wa Kanda ya Kati,” amesema Dkt. Mwigulu. #MillardAyoUPDATES
millardayo152,150 görüntüleme • 1 ay önce

Upande wa Jamhuri umefunga ushahidi wao kwa Shahidi wa 17 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Akizungumza leo Agosti 17, 2026 Mahakamani, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga amesema msimamo huo umefikiwa baada ya Jamhuri kufanya tathmini ya kina ya ushahidi na hoja zote zilizowasilishwa katika kesi hiyo. Hata hivyo, Katuga ameomba Mahakama iruhusu Jamhuri kuwasilisha hoja za ziada kueleza sababu zinazowafanya waone Lissu ana kesi ya kujibu, ombi ambalo Lissu amepinga akieleza kuwa sheria tayari inaweka utaratibu unaopaswa kufuatwa katika hatua hiyo. Iwapo Mahakama itaamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, atapewa nafasi ya kuanza kujitetea kwa kuwasilisha ushahidi na Mashahidi wake na endapo Mahakama itaamua kuwa hana kesi ya kujibu, kesi hiyo itafikia mwisho. Kesi hiyo inaendelea mbele ya jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru. #MillardAyoUPDATES
millardayo69,341 görüntüleme • 14 gün önce

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Ikulu. Akizungumza leo Agosti 12, 2026 na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kilosa Mjini, Mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano. Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa Vyama vya Siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo. Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo. “Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA, Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi. #MillardAyoUPDATES
millardayo78,801 görüntüleme • 19 gün önce

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Elkiroa, Kata ya Lemara Mkoani Arusha, wamefanya sherehe za kupika vyakula kusherehekea kuondoka kwa Mama Rashid, Mwanamke aliyekuwa akiishi kwa kupanga katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 17. Hatua hiyo inakuja baada ya baadhi ya Wakazi kumtuhumu kuhusika na vitendo vya ushirikina na kung’ang’ania nyumba zinazodaiwa kuwa mali ya marehemu. AyoTV imefika eneo la tukio ambapo imeshuhudia, majirani katika Mtaa huo wakisheherekea kwa kupika vyakula baada ya Mama Rashid kuhama. Itakumbukwa kwamba, hivi karibuni AyoTV ilizungumza na Mama Rashid ambaye alidai kuwa alikataa kuondoka kwa sababu alikuwa akimdai Msimamizi wa mirathi kiasi cha shilingi milioni saba. #MillardAyoUPDATES
millardayo112,351 görüntüleme • 28 gün önce

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania wanaotoa zawadi za fedha taslimu katika sherehe mbalimbali kuacha utaratibu wa kutupa noti na badala yake kutumia mifumo ya malipo ya kidigitali ili kulinda ubora wa fedha zinazotumika Nchini. Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2026 na Meneja Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania Victoria Msina wakati akizungumza na AyoTV katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea Mkoani Dodoma. Msina amesema noti na sarafu hutengenezwa kwa gharama kubwa hivyo zinapaswa kutunzwa kwa uangalifu na kuwa kila noti ina namba maalumu ya utambulisho na Benki Kuu hufuatilia muda wake wa matumizi hivyo kitendo cha kuzitupa chini kuzikanyaga au kuzishika kwa mikono yenye jasho na unyevu hupunguza ubora na maisha ya fedha hizo. Aidha amesema matumizi ya mifumo ya malipo ya kidigitali ni njia salama na ya kisasa ya kutoa zawadi katika sherehe badala ya kutumia fedha taslimu kwa namna inayoweza kuziharibu, pia amefafanua tofauti ya sarafu zinazovutwa na sumaku na zile zisizovutwa akieleza kuwa hali hiyo hutokana na aina ya metali zinazotumika kuzitengeneza. “Kweli pesa ni ya kwako umetafuta kwa jasho lako lakini kiustaarabu unaweza kutumia njia nyingine mbadala kama kutumia mifumo ya malipo ukaingiza kwenye benki yake halafu ukumbini ukapeleka risiti ya malipo” amesema Msina. #MillardAyoUPDATES
millardayo101,986 görüntüleme • 27 gün önce

Fabiano Mkeza ambaye ni Baba wa familia ya Asha Lukonge na Hashim Fabiano ameibua simanzi wakati wa mazishi ya Mke na Mtoto wake, wanaodaiwa kuuawa kwa kunyongwa na Ndugu wa familia hiyo, Anderson Bosco. Mazishi hayo yamefanyika leo Agosti 18, 2026 katika Makaburi ya Azimio, Kilosa Mjini baada ya tukio hilo kutokea Agosti 15, 2026 katika Kijiji cha Ilakala, Kata ya Mhenda, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Fabiano akiwa safarini, ambapo Anderson ambaye awali alifika katika familia hiyo kwa lengo la kufanya vibarua, anadaiwa kumuua Asha pamoja na Mtoto wake kwa kuwanyonga, kisha kuwafukia nyuma ya nyumba yao. Baada ya tukio hilo, Mtuhumiwa huyo anadaiwa pia kuuza magunia nane ya mahindi yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa ajili ya chakula kwa shilingi 300,000, ambapo Jeshi la Polisi limesema linaendelea na msako wa kumtafuta Bosco ambaye anadaiwa kukimbia baada ya tukio hilo na hadi sasa hajulikani alipo. #MillardAyoUPDATES
millardayo45,847 görüntüleme • 13 gün önce

Mama mzazi wa Msanii Zuchu, Khadija Kopa amesema baadhi ya maneno yanayotolewa na Watu yamekuwa yakichochea kutaka kuvunja ndoa ya Diamond na Zuchu. Akizungumza wakati wa hafla ya Babe Shower, Bi. Kopa amesema wapo baadhi ya Watu wanaokuza mambo madogo yanayotokea kati yao badala ya kutoa ushauri au kumtia moyo anayepitia changamoto. “Mara nyingi namtetea Diamond kuliko Zuchu hadi analalamika, kwani hata vikombe vinagongana na kwa sababu ya umaarufu wao kitu kidogo kinakuwa kikubwa, kuna Watu washakunaku wanaotia chumvi na kuumiza Watu,” amesema Khadija Kopa. #MillardAyoUPDATES
millardayo99,478 görüntüleme • 1 ay önce

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imewashauri Wananchi kutumia mifumo ya malipo ya kidigitali katika kufanya malipo mbalimbali ikieleza kuwa njia hiyo ni salama inaokoa muda na pia inapunguza gharama za uchapishaji wa noti Nchini. Ushauri huo umetolewa na Afisa wa Benki Kuu kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa Fredrick Mwakuu, wakati akizungumza na Wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu katika Maonesho ya 33 ya Nanenane yanayoendelea katika Uwanja wa Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma. Mwakuu amesema Benki Kuu imeendelea kuimarisha mifumo ya malipo ya kidigitali kwa kuwaunganisha watoa huduma mbalimbali za kifedha, huku ikiendelea kusimamia mifumo hiyo kwa karibu ili kuhakikisha Wananchi wote wanapata huduma kwa usalama na ufanisi. Aidha, ameeleza kuwa moja ya majukumu ya Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa ni kusimamia watoa huduma wote wa malipo ya kifedha Nchini ambapo kupitia mifumo hiyo Wananchi wanaweza kutuma fedha kutoka Mtu mmoja kwenda kwa mwingine kufanya malipo ya biashara pamoja na kulipia huduma mbalimbali za Serikali kwa usalama na urahisi. #MillardAyoUPDATES
millardayo74,142 görüntüleme • 26 gün önce

Baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu leo Agosti 21, 2026 anasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam kuhusu iwapo ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini namba 19605/2025. Jamhuri ilifunga ushahidi wake baada ya kuwasilisha mashahidi 17 kati ya 30 waliokuwa wameorodheshwa ambapo baada ya hatua hiyo, Lissu aliwasilisha hoja akiomba Mahakama itamke kuwa hana kesi ya kujibu, akidai ushahidi wa Jamhuri haujafikia kiwango cha kuunda prima facie case dhidi yake. Kwa upande wake, Jamhuri imepinga hoja hizo na kueleza kuwa ushahidi wa mashahidi 17 umeonyesha vipengele muhimu vya kosa la uhaini, hivyo Lissu anapaswa kupewa nafasi ya kujitetea dhidi ya Mashtaka yanayomkabili. Iwapo Mahakama itaamua kuwa Lissu hana kesi ya kujibu, anaweza kuachiwa huru katika shauri hilo, lakini iwapo itaamua kuwa hana kesi ya kujibu, kesi itaingia hatua inayofuata ambapo Lissu atatakiwa kujibu ushahidi uliowasilishwa na Jamhuri. #MillardAyoUPDATES
millardayo30,406 görüntüleme • 10 gün önce

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete, amesema ni wakati wa Wafugaji Nchini kuachana na ufugaji wa jadi na kuhamia kwenye ufugaji wa kisasa unaotumia sayansi na teknolojia ili kuongeza ubora wa mifugo na uzalishaji wa nyama bora Akizungumza wakati alipotembelea Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt John Samuel Malecela Jjini Dodoma, ambapo alikuwa mgeni rasmi na kushuhudia paredi la wanyama Ridhiwani amesema Watanzania wengi hawali nyama yenye ubora unaotakiwa bali wanakula misuli kutokana na mifugo mingi kufugwa kwa njia za jadi. Aidha, amesema maonesho ya Nanenane yanapaswa kuwa fursa kwa Wafugaji kujifunza teknolojia mpya na mbinu bora za ufugaji zitakazowawezesha kuongeza tija na kuzalisha mifugo yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko. Ridhiwani amesema mifugo isiyo na ubora hutoa nyama na mazalia yasiyokidhi viwango vinavyohitajika hivyo uwekezaji katika mifugo bora utaongeza upatikanaji wa nyama yenye ubora na kuimarisha sekta ya mifugo Nchini pamoja na kuongeza kipato cha Wafugaji. Pia amesisitiza kuwa ufugaji wa kisasa unapaswa kufanywa kwa mtazamo wa kibiashara na kuwataka Wadau wote wa sekta ya mifugo kushirikiana kuwahamasisha Wafugaji kupokea mabadiliko kwa kuwekeza katika mifugo bora ili kuongeza uzalishaji na mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya Taifa. #MillardAyoUPDATES
millardayo60,483 görüntüleme • 25 gün önce

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ameagiza kukamatwa kwa Mmiliki na Mjenzi wa jengo lililopo Masaki baada ya kubainika kuwa limejengwa kwa ghorofa 13 tofauti na kibali cha ujenzi kilichoruhusu ghorofa sita. Akizungumza leo Agosti 6, 2026 wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria na taratibu za ujenzi, Chalamila amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi wa kitaalamu kuhusu usalama wa jengo hilo. Amesema Wataalamu wanapaswa kujiridhisha kama msingi wa jengo hilo unaweza kuhimili idadi ya ghorofa zilizojengwa, ambazo ni zaidi ya zile zilizoidhinishwa kwenye kibali. “Sheria zimekiukwa, ghorofa zipo 13 wakati kibali ni cha ghorofa sita, Wataalamu wanapaswa kujiridhisha kuhusu msingi uliyojengwa kama inaweza kuhimili ghorofa 13 ambazo hazina vibali, Mmiliki na Mjenzi wakamatwe wawekwe ndani,” amesema Chalamila. Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa Serikali haitamvumilia Mtu yeyote anayekiuka Sheria za Ujenzi, akieleza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaobainika kuhatarisha usalama wa Wananchi kwa kujenga kinyume na vibali walivyopewa. #MillardAyoUPDATES
millardayo59,449 görüntüleme • 25 gün önce

Ng’ombe dume wa mbegu anayefahamika kwa jina la Maro amegeuka kivutio kikubwa katika Maonesho ya 33 ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Dodoma baada ya kufahamika kuwa ana thamani ya Shilingi milioni 30. Maro ana umri wa miaka miwili na miezi mitatu na ana uzito wa kilogramu 847, ni ng’ombe asili ya Friesian kutoka Afrika Kusini ambapo Wataalamu wa mifugo wanasema mama yake ana uwezo wa kuzalisha hadi lita 50 za maziwa kwa siku. Ng’ombe huyo ameletwa katika maonesho hayo kupitia Banda la Jiji la Dodoma na mfugaji Boniphace Mariwa ambaye ni Mkazi wa Jiji la Dodoma. Mbali na kuvutia kutokana na ukubwa na thamani yake Wataalamu wa mifugo wanasema ng’ombe wa mbegu huhitaji mazingira tulivu ili kudumisha uzalishaji mzuri wa mbegu, wanaeleza kuwa wanapopata msongo wa mawazo uzalishaji wa mbegu hupungua na pia hawapendi kelele. #MillardAyoUPDATES
millardayo63,863 görüntüleme • 29 gün önce

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, leo Julai 21, 2026 amemwambia Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kuwa idadi ya Watu waliojitokeza mahakamani kufuatilia shauri la Kikatiba kuhusu haki ya faragha ilikuwa ndogo. Lissu ametoa kauli hiyo kabla ya kuanza kwa usikilizwaji wa Shauri la Kikatiba Na. 7300 la mwaka 2026, lililofunguliwa na Mawakili wake dhidi ya Kamishna Jenerali wa Magereza. Akiwa ameketi nje ya kizimba, Lissu alisikika akisema: “Katibu Mkuu, Watu ni wachache humu, maana yake mobilization ni ndogo.” Shauri hilo linasikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dar es salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu ambao ni Jaji Amir Mruma, Jaji Dkt. Angelo Rumisha na Jaji Dkt. Evaristo Longopa. #MillardAyoUPDATES
millardayo87,811 görüntüleme • 1 ay önce

Msemaji wa Timu za Taifa, Haji Manara amewataka Wanasiasa kuacha kuingilia masuala ya soka, akisisitiza kuwa michezo inapaswa kubaki kuwa chombo cha umoja na si sehemu ya mvutano wa kisiasa. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Julai 30, 2026 Manara amesema kauli yake inafuatia baadhi ya Wanasiasa kudai kuwa wataiandikia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuomba Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) isifanyike Nchini Tanzania. #MillardAyoUPDATES
millardayo62,692 görüntüleme • 1 ay önce