
Maulid Kitenge
@mshambuliaji • 1,833,365 subscribers
CROWN MEDIA
Shorts
Videos

Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, leo Agosti 28, 2026, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi. Kwa sasa, mchakato wa kikatiba unaendelea, huku jina la Ndejembi likitarajiwa kuwasilishwa Bungeni leo kwa ajili ya kuidhinishwa na Wabunge kupitia kura. Iwapo atathibitishwa, Ndejembi atachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa Dkt. Emmanuel Nchimbi. #KitengeUpdates
Maulid Kitenge22,562 görüntüleme • 5 gün önce

Breaking: Meli ya Mafuta inateketea kwa moto muda huu katika Bandari ya Kigoma ya Ziwa Tanganyika huku Chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika. Inasemekana Meli hiyo ya Mafuta ilikuwa ikijiandaa kuelekea nchini Congo. Endelea kufuatilia #kitengetv_tz kwa taarifa za kina zaidi juu ya tukio hilo #KitengeUpdates
Maulid Kitenge19,928 görüntüleme • 4 gün önce

Yanga wameshamalizana na Feisal Salum, lolote linaweza kutokea✍🏼
Maulid Kitenge68,480 görüntüleme • 23 gün önce

Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema haoni uwezekano Tanzania kupata Katiba mpya ifikapo mwaka 2029, licha ya kuwepo kwa matarajio ya wananchi kuhusu mchakato huo. Akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia leo Agosti 28, 2026, Warioba amesema Serikali inapaswa kutafuta njia mbadala za kushughulikia changamoto zilizopo, akionya kuwa kuendelea na uchaguzi bila kuzitatua kunaweza kulisababishia taifa madhara makubwa. Amesema wananchi bado wanaomboleza kutokana na yaliyotokea Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa majeraha na madhara yaliyotokea ni makubwa na hayawezi kupuuzwa au kuachwa yakisahaulika huku taifa likiendelea na maisha ya kawaida. #KitengeUpdates
Maulid Kitenge15,835 görüntüleme • 5 gün önce

Leonard Thadeo ambaye alitangazwa Mshindi wa Urais katika Uchaguzi uliokuwa na ‘utata’ wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo. Akizungumza Jijini leo, Thadeo amesema ameamua kujiuzulu baaada ya kuona uchaguzi huo uliofanyika Julai 5 mwaka huu kuwa uligubikwa na viashiria vingi vya uvunjwaji wa Katiba ya TOC hivyo kwa tafakuri yake aliyoifanya leo amekuja na tamko la jumla la kujiuzulu nafasi hiyo. #KitengeUpdates
Maulid Kitenge35,967 görüntüleme • 18 gün önce

Kwani wana Simba Ahmed Ally anawachukuliaje Nyie ? #KitengeSports
Maulid Kitenge37,563 görüntüleme • 21 gün önce

Mwalimu Kaona apishane na aibu ndogondogo msimu huu #KitengeSports
Maulid Kitenge33,983 görüntüleme • 22 gün önce

Hivi umeshawaza hiyo Burj Khalifa mpya ya Dubai itakuwaje?
Maulid Kitenge20,054 görüntüleme • 13 gün önce

“Mimi sipendi kuzungumzia mambo ambayo yapo kwenye mkataba kwa sababu hizi ni Siri baina yangu na Simba, sipendi kuongea jambo likachukuliwa tofauti hivyo hayo mambo ya kiwanja tuyaache,” Mkurugenzi wa Kampuni ya Jayrutty, Joseph Rwegasira #KitengeSports
Maulid Kitenge34,992 görüntüleme • 27 gün önce

Klabu ya Simba imelazimika kutoa ufafanuzi wa Sakata la Mchezaji aliye kwa Mkopo kwao Selemani Mwalimu ikisema wao waliongea na Uongozi wa Wydad Casablanca juu ya Mkopo huo lakini kilichotokea Uongozi wa Klabu hiyo ya Morocco umebadilika umeingia Uongozi mwingine. Msemaji wa Simba Ahmed Ally amezungumza na Kocha Mchezaji Maulid Kitenge na kumueleza kuwa wamesikia madai ya Wydad na watakachofanya sasa wao ni kuwasiliana na Uongozi mpya wa Wydad. #KitengeSports
Maulid Kitenge49,558 görüntüleme • 1 ay önce

Roman Reigns ameendelea kutawala katika WWE baada ya kumshinda Seth Rollins kwenye pambano kuu la SummerSlam na kufanikiwa kutetea taji lake la World Heavyweight Championship. Baada ya pambano hilo kumalizika, Roman Reigns na Seth Rollins walifanya ishara maarufu ya The Shield (fist bump), hatua iliyowagusa mashabiki wengi na kuibua kumbukumbu za enzi za kundi hilo lililowahi kutikisa WWE. Muda mfupi baadaye, Rollins aliweka barakoa ya The Shield katikati ya ulingo, tukio lililozua hisia na tafsiri mbalimbali kuhusu urithi wa kundi hilo na heshima kati ya wapinzani hao wawili. #KitengeSports
Maulid Kitenge36,400 görüntüleme • 1 ay önce

Mmiliki wa timu ya Azam FC Jamal Bakhresa amefanya mahojiano na Kocha Mchezaji Maulid Kitenge na kusema Azam FC haitendewi haki kwenye Ligi Kuu, huku akienda mbali zaidi kuwa licha ya uwezekaji mkubwa wao lakini imekuwa kazi bure kwa kutotendewa haki Uwanjani. Jamal Bakhressa amesema kama TFFB na Bodi ya Ligi hawawataki ni bora wawaambie ili watafute Ligi nyingine ya kushiriki. #KitengeSports
Maulid Kitenge63,808 görüntüleme • 1 ay önce

Ukiona huwezi kushindana nao, ungana nao tu, Shalulile ni wa kila mtu 😂 #KitengeSports
Maulid Kitenge32,493 görüntüleme • 29 gün önce