ROYAL TELEVISION PLUS's banner
ROYAL TELEVISION PLUS's profile picture

ROYAL TELEVISION PLUS

@Royaltv_plus781,290 subscribers

Media Coverage

Shorts

Breaking News: Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Alhamisi Mei 28.2026, Mahakama imeifuta rasmi na kuindoa Mahakamani Hati ya kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, iliyokuwa inahusu usawa kwenye mgawanyo wa mali za chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar Katika uamuzi wake uliotolewa muda mfupi uliopita Mahakamani hapo kupitia kwa Jaji D. Ngunyale imeeleza kuwa wadai (waliofungua kesi) hawakuonesha -kifungu chochote kwenye hati y madai kinachoonesha kwamba uvunjifu huo (unaolalamikiwa na wadai) ulianza lini, jambo lililopelekea Mahakama kushindwa kujiridhisha kama ina mamlaka au la ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo Jaji Ngunyale amesema hati ya madai ilikuwa ina mapungufu makubwa, hivyo pingamizi lililowekwa na CHADEMA lina msingi. NB: Royal TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na maamuzi hayo ya Mahakama.

Breaking News: Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Alhamisi Mei 28.2026, Mahakama imeifuta rasmi na kuindoa Mahakamani Hati ya kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, iliyokuwa inahusu usawa kwenye mgawanyo wa mali za chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar Katika uamuzi wake uliotolewa muda mfupi uliopita Mahakamani hapo kupitia kwa Jaji D. Ngunyale imeeleza kuwa wadai (waliofungua kesi) hawakuonesha -kifungu chochote kwenye hati y madai kinachoonesha kwamba uvunjifu huo (unaolalamikiwa na wadai) ulianza lini, jambo lililopelekea Mahakama kushindwa kujiridhisha kama ina mamlaka au la ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo Jaji Ngunyale amesema hati ya madai ilikuwa ina mapungufu makubwa, hivyo pingamizi lililowekwa na CHADEMA lina msingi. NB: Royal TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na maamuzi hayo ya Mahakama.

10,352 views

Videos

Royaltv_plus's profile picture

Mmoja wa viongozi na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Same Andrew Mchome amelaani kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche kutangaza kwamba ataandikia barua FIFA ili wasitishe mashindano ya AFCON nchini Tanzania kwa madai ya kuwepo kwa vikundi vilivyopanga kufanya vitendo vya kigaidi. Hatua hiyo imekuja kufuatia Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuwakamata watuhumiwa kadhaa katika maeneo mbalimbali ya nchi wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi licha ya kwamba bado vitendo vyao havijathibitishwa Mahakamani Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Julai 29, 2026 Jijini Dar es Salaam Mchome amesema kauli ya Heche ni ya kupingwa kwa sababu inachafua taswira ya nchi kimataifa, na kuongeza kuwa hakuna chama chochote cha siasa kinachopinga maendeleo ndani ya nchi yake hivyo kitendo cha Heche kujitokeza hadharani na kudai ataiandikia FIFA barua kupinga kufanyika kwa AFCON si cha kiungwana "Juzi nimemsikia akizungumza anasema kwamba tutaandika barua FiFa kuzuia mashindano ya AFCON kutokana na kuwepo kwa viashiria vya UGAIDI, kilichopo kwenye nchi yetu sasa hivi ni kwamba, Kuna watu ambao wana tuhuma ya kupanga vitendo hivyo lakini hakuna Mahakama iliyohukumu mtu kutokana na vitendo vya UGAIDI" amesema mchome Ameongeza kuwa Kauli ya Makamu mwenyekiti huyo sio ya kizalendo kwa taifa na yaweza kutia hofu wageni wanaotamani kuja kuwekeza nchini lakini pia kutembelea vivutio vya utalii. Mchome amemtaka Heche kuacha kukigombanisha chama chao na wananchi kwani anaamini kupitia mashindano hayo ya AFCON watanzania wataenda kunufaika kwa namna moja ama nyingine kupitia ugeni mkubwa utakao kuwa nchini. "Mpenda maendeleo yeyote hawezi kuwa na roho kama hiyo ya kupinga Maendeleo, ugeni utakaoingia nchini utasaidia hadi mamalishe kupata ridhiki zao, pia utafungua ukurasa mwingine kwenye sekta ya utalii" amesema mchome

ROYAL TELEVISION PLUS

21,125 views • 29 days ago

Royaltv_plus's profile picture

VIDEO: Watanzania wameaswa kuacha kusikiliza wanaharakati na wanasiasa wanaochochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini, kwa kuwa watu hao hawana nia njema kwa Taifa Rai hiyo imeitolewa leo, Alhamisi Juni 04. 2026, Jijini Dar es Salaam na Mwanafalsafa wa Pan-Afrika kutoka Zimbabwe, Dkt. Joshua Maponga wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu uzinduzi wa makala inayozungumzia Matukio yaliyotokea Nchini kabla na baada ya Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu), makala ambayo imeandaliwa na kampuni ya African Spear Head Media Katika maelezo yake, Dkt. Maponga amedai kuwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) yamekuwa yakipokea fedha kutoka mataifa ya nje kwa lengo la kuhamasisha vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili na amani ya nchi, ikiwemo vurugu na migawanyiko kati ya wananchi na viongozi wao, ambapo amesema hali hiyo ni hatari kwa ustawi na usalama wa Taifa, hivyo kushauri serikali kuchukua hatua za kufanya uhakiki wa mashirika hayo ili kubaini vyanzo vya fedha wanazopata na namna zinavyotumika Aidha, amedai kuwa watu wanaochochea vurugu mara nyingi huishi nje ya nchi katika mazingira mazuri, huku wananchi wanaoshiriki machafuko hayo wakikabiliwa na madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, mali, uharibifu wa makazi yao nk Sambamba na hilo ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za maandamano yasiyo ya amani na vurugu, akisisitiza kuwa matukio kama hayo yanaweza kuathiri maendeleo na rasilimali za Taifa Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa African Spear Head Media David Hundeyin amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja ya nchi muhimu kiuchumi barani Afrika kutokana na nafasi yake ya kimkakati, hususani kupitia Bandari ya Dar es Salaam inayotumiwa na mataifa mbalimbali katika shughuli za biashara na uchumi Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kulinda amani na rasilimali za nchi yao, kwani machafuko yanaweza kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi na kuathiri maendeleo ya Taifa ...“Vurugu na mauaji yaliyotokea Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu) yalikuwa na athari kubwa kwa jamii, hata hivyo bado kuna baadhi ya watu wanaoendelea kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu, wananchi wanapaswa kuwa makini na watu wa aina hiyo kwa kuwa hawana nia njema kwa Taifa lao" -Hundeyin.

ROYAL TELEVISION PLUS

49,677 views • 2 months ago

Royaltv_plus's profile picture

VIDEO: Mvutano ndani ya CHADEMA umechukua sura mpya baada ya viongozi watatu wa chama kutoka Morogoro na Tanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, wakipinga hatua zilizochukuliwa dhidi yao walipopaza sauti kuhusiana na tuhuma za ubadhirifu wa pesa za michango ya wadau kwa chama hicho unaodaiwa kufanywa na makamu mwenyekiti wao John Heche na kudai zilikiuka Katiba na Kanuni za chama . Viongozi hao ni Barnabas Okola, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, Mathias Cosmas, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kilindi, na Joseph Mwakidasi, Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Muheza. Katika taarifa yao kwa umma ya Julai 21, 2026, wamesema hawakupewa taarifa rasmi za tuhuma zinazowakabili, hawakuitwa kusikilizwa wala kupewa nafasi ya kujitetea kabla ya maamuzi yaliyotangazwa. Wamedai kuwa hatua zilizochukuliwa dhidi yao ni batili kwa kuwa hazikufuata utaratibu uliowekwa na Katiba na Kanuni za CHADEMA, hivyo bado wao ni viongozi halali wa chama hadi taratibu za kikatiba zitakapokamilika. Kupitia barua yao, viongozi hao wameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutumia mamlaka yake kuhakikisha Katiba na Kanuni za CHADEMA zinazingatiwa, kuchunguza madai ya ukiukwaji wa taratibu za ndani ya chama na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo inaongeza orodha ya migogoro ya ndani ya CHADEMA inayofikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, huku ikitarajiwa kufungua mjadala mpya kuhusu ufuataji wa taratibu za kikatiba ndani ya chama hicho. Jitihada za kumpata Msajili wa Vyama vya Siasa ili kuzungumzia malalamiko hayo na kueleza hatua zinazoweza kuchukuliwa zinaendelea.

ROYAL TELEVISION PLUS

19,172 views • 1 month ago

Royaltv_plus's profile picture

VIDEO: Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Hamisi Said Liunde, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, kuunda tume maalumu ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche. Pia, Liunde amemtaka Heche kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanachama wa CHADEMA kwa kutumia lugha ya udhalilishaji iliyowafananisha na mbwa. Akizungumza katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Kata ya Masoko, Mjini Kilwa, Liunde amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa kitaifa kuchukua hatua za haraka ili kulinda taswira ya chama na kuondoa mashaka miongoni mwa wanachama. "Tumekuja kuongea kuhusu tuhuma za kifedha zinazomkabili Heche. Tunaomba chama kijitokeze mara moja na Heche akae pembeni kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo zote zinazoendelea," amesema Liunde. Akihoji matumizi ya lugha yaliyofanywa na Makamu Mwenyekiti huyo, Liunde ameeleza kuwa maneno hayo yameumiza hisia za wanachama, hasa jamii ya Kiislamu. "Suala la Makamu Mwenyekiti kufikia hatua ya kutuita mbwa ni udhalilishaji, hususan kwetu sisi Waislamu. Ukimuita Muislamu mbwa unakuwa umemkosea sana, kwa sababu yule ni mnyama ambaye akikugusa tu kuna taratibu ndefu za kisheria na kidini za kujisafisha ili uwe twahara tena. Heche atumie lugha ya staha, lugha aliyotumia ni ngumu mno; kiongozi anapaswa kuwa na kifua cha kuvumilia," ameongeza. Mbali na hayo, Liunde ametoa wito kwa Serikali na Rais kuweka mazingira ya maridhiano ya kisiasa ili kusaidia kuachiwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, aliye gerezani, akisisitiza kuwa maridhiano ya kweli hayawezi kukamilika ikiwa Mwenyekiti wao bado yupo ndani.

ROYAL TELEVISION PLUS

16,629 views • 1 month ago