
ROYAL TELEVISION PLUS
@Royaltv_plus • 781,290 subscribers
Media Coverage
Shorts
Videos

VIDEO: Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya kuchunguza matukio ya Kijinai yaliyotokea Nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29.2025, Jaji Shaban Lila amesema Tume hiyo ni Huru kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi Nchini, na kwamba hakuna mamlaka wala mtu yeyote anayeweza kuingilia majukumu na kazi za kila siku za Tume husika, hata 'Rais mwenyewe' aliyeunda hana mamlaka hayo Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Agosti 24.2026, Jaji Lila ameeleza lengo kuu la Tume hiyo kuwa ni kuchunguza na kubainisha wahusika wa ghasia na ukiukwaji wa sheria katika matukio ya ghasia za wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.2025 Ameongeza kuwa Tume huyo pia itachunguza waliosababisha madhara yaliyotokana na ghasia hizo, wakati wa kudhibiti ghasia hususani kuhusu vifo, majeruhi na watu waliopotea wakati na baada ya uchaguzi.
ROYAL TELEVISION PLUS30,484 просмотров • 4 дней назад

VIDEO: Philipo Mwakibinga amesema mjadala wa demokrasia nchini unapaswa kuangalia pia namna viongozi wanavyoendesha vyama vyao na misimamo yao kisiasa. Mwakibinga amesema amelinganisha kauli za Tundu Lissu na John Heche kuhusu uchaguzi, akisema kauli zao zinafanana lakini mazingira wanayopitia ni tofauti. Amedai hali hiyo inazua maswali kuhusu kwa nini Lissu yuko ndani huku Heche akiwa nje, pamoja na msimamo wa Heche kutotaka maridhiano wakati Lissu akitajwa kuwa tayari kwa maridhiano. Mwakibinga amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa makini, akidai kuna uwezekano Heche anatumiwa na CCM kumweka Lissu katika mazingira ya kubaki ndani, huku akisisitiza kuwa madai hayo ni mtazamo wake na hana uhakika nayo.
ROYAL TELEVISION PLUS16,420 просмотров • 4 дней назад

VIDEO: KOCHA wa YANGA SC ameonesha amewapiga mkwara mzito JKT Tanzania wakati huu ambao timu yake inajiandaa kuchuana na maafande hao kweye mchezo wa NBC Premier League unatakaopigwa KMC Complex, hapo kesho Katika hali isiyokuwa ya kawaida, KOCHA huyo raia wa Afrika Kusini ametaja kikosi KIZIMA cha maafande hao katika mkutano wake na Waandishi wa Habari leo
ROYAL TELEVISION PLUS13,186 просмотров • 5 дней назад

VIDEO: Msikilize Lumola akitangaza maamuzi ya kurejea kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) alikokuwa awali, Licha ya kuwa miongoni mwa wagombea Ubunge wa CHAUMMA katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Nchini Oktoba 2025, Lumola anadai hakuwahi kuwa mwanachama halisi wa chama hicho, kwakuwa hakuwahi kuchukua kadi ya uanachama wa chama hicho Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Jumapili Agosti 16.2026, Lumola anasema alitangaza kuondoka CHADEMA kupitia tamko lake aliloweka kwenye mitandao ya kijamii, na kwamba leo amejitokeza kutangaza kulifuta tamko hilo Amesema Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Tundu Lissu ni mtu imara, aliyekuwa tayari kuumia kwa ajili ya Watanzania, na kwamba anamuunga mkono akiamini kwamba yeye na viongozi wenzake ndani chama hicho wamebaki imara bila kukubali 'kupiga magoti' licha ya magumu yote wanayopitia.
ROYAL TELEVISION PLUS26,771 просмотров • 12 дней назад

VIDEO: "Wanawaambia tuandamane huku wao wakiwa wameweka Passport mfukoni ili kikinuka anapanda zake Bodaboda anakula Boda anaenda zake Kenya kesho unamsikia yupo Canada, Ubelgiji na maeneo mengine, mimi nimefanya nao kazi nawajuwa, au kuna mtu ana shaka na hilo?, hapa Tunduma nilikuja tukakinukisha, uwongo -kweli?, kwani Katambi (Patrobas Katambi ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi; kabla ya kutimikia CCM, wakati akiwa CHADEMA aliwahi kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa) mmemsahau?, nilikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa kutisha, na huyu (John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, na Mwenyekiti wa zamani wa BAVICHA Taifa) ambaye leo anasema ameniachia nafasi HAKUTAKA hata niwe Mwenyekiti kwasababu alikuwa anajuwa NAMZIDI AKILI..." -Katambi Ni sehemu ya yale aliyozungumzwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi alipofanya ziara ya kikazi Tunduma, Mkoani Songwe hivi karibuni #SiasaZetuTZ
ROYAL TELEVISION PLUS35,625 просмотров • 17 дней назад

VIDEO: "Asilimia kubwa huku tunakoleta mizigo rushwa imetawala kwasababu unaweza kuona mtu anafika leo akaanza kushusha kwa sababu tu ametanguliza chochote kitu, lakini yule aliyemkuta ambaye anafuata utaratibu akashusha nje ya wakati" -Elias "Sisi hapa watu wote ukiangalia tunaichukia sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaichukia kwasababu watendaji wengi wa serikali wanajikumbatia wao, na sisi wengine ni kama vile hatuhusiki na hii Nchi" -Elias Elias Jonas Mwang'ingo ni Dereva wa Lori anayesubiri kupakia au kushusha mizigo katika Bandari Kavu iliyopo eneo la Mchicha -Sandali, Temeke, Jijini Dar es Salaam Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila hivi karibuni, Elias ametaja changamoto kadhaa zinazowasibu kwenye eneo hilo ikiwemo mrundikano wa mizigo mingi kupita uwezo, suala la rushwa na kukosekana kwa choo.
ROYAL TELEVISION PLUS18,284 просмотров • 10 дней назад

VIDEO: Mwanaharakati na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Martin Maranja Masese (MMM) amewashukia wale wote wanaobeza mwenendo wa uongozi wa sasa wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa Tundu Lissu Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mitandao yake binafsi ya kijamii, MMM amehoji, kwamba wakati Freeman MBOWE akiwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa wale wasiokitakia mema chama hicho walikuwa wanaikashfu CHADEMA kuwa haina demokrasia ndani yake, na wengine walienda mbali zaidi na kukiita kuwa 'Chama cha MBOWE' Hata hivyo, MMM anasema baada ya Tundu Lissu kuingia madarakani kama Mwenyekiti Mpya watu walewale wamegeuka tena na kusema bora uongozi wa MBOWE.
ROYAL TELEVISION PLUS28,676 просмотров • 22 дней назад

VIDEO: Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara imemuhukumu Mtoto mwenye umri wa miaka 16 adhabu ya kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwenzake Hata hivyo, uamuzi huo wa Mahakama umezua mjadala 'mkali' miongoni mwa wadau wa sheria na ustawi wa jamii kuhusu uhalali wa adhabu hiyo kwa mtoto Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Boniface Lyamwike, ambapo imeelezwa kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 23.2026 kijijini kwao, Mkoani Manyara
ROYAL TELEVISION PLUS20,338 просмотров • 23 дней назад

VIDEO: "Mama (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan) amekubali (kutupeleka kwenye maridhiano, na wale wanaosema eti bila CHADEMa hakuna kitakachofanyika, mnatakiwa kujuwa kwamba CHADEMA ni chama kama vilivyo vyama vingine, kitendo chao cha kutofika kwenye kikao cha Mheshimiwa Rais, hiyo ni sawasawa na mtoto mmoja anapopotoka na kuwa mvuta Bangi..." -Shani Ally Kitumbua Shani Ally Kitumbua ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Chama cha Wakulima (AAFP), na hayo yote ameyasema katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Agosti 05.2026
ROYAL TELEVISION PLUS19,972 просмотров • 23 дней назад

VIDEO: Katibu wa CHADEMA Jimbo la Sumve mkoani Mwanza, Samuel Richard Malimi, amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche, kuwaomba radhi wanachama kwa kutoa kauli iliyowafananisha na mbwa baada ya kumtaka apishe uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili. Kadhalika, Malimi amemwomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuingilia kati kile alichokiita "fukuzafukuza" inayoendelea ndani ya chama hicho dhidi ya wanachama wanaojihoji masuala ya msingi. Akizungumza na wanahabari mkoani Mwanza, Malimi ameeleza kusikitishwa kwake na utaratibu wa kuwafukuza uongozi na uanachama watu wanaojaribu kuhoji matumizi ya fedha ndani ya CHADEMA. "Unapewa majibu mengi utaambiwa msaliti, umehongwa, na kila anayehoji kuhusu fedha anaitwa mbwa. Ina maana Makamu Mwenyekiti Heche anaongoza mbwa? Ndugu zetu Waislamu hata mbwa akikunusa hurusiwi kwenda msikitini; kwa hiyo Makamu Mwenyekiti amekosea, atoke hadharani awaombe watu msamaha kwa maneno aliyoyatoa," amesema. Aidha, kiongozi huyo wa Jimbo la Sumve amemsihi Heche kutoendesha chama kama taasisi ya kifamilia na badala yake arusu maridhiano ya kisiasa ili kumsaidia Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu aliyeko gerezani.
ROYAL TELEVISION PLUS23,973 просмотров • 1 месяц назад

Mkaguzi na Madhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Professa Mussa Assad amesema ni muhimu kuwepo na ukaguzi na ufuatiliaji wa maisha ya wanasiasa au viongozi wanaoteuliwa kwa nafasi mbalimbali na tathmini iwe inafanyika mara kwa mara sio kwa viongozi tu bali hata ndugu na jamaa zao. Prof. Assad amesema hayo alipohojiwa na Clouds TV na kueleza kuwa hilo litatoa taswira juu ya uadilifu na kujulikana kwa uhalali wa umiliki wa mali hizo wakati wa utendaji wa viongozi hao. Ameongeza kuwa yupo kijana mmoja anamfahamu ni Waziri kwa kipindi cha miaka mitano anamiliki magari ya kifahari ikiwemo Landcruiser LC 300 matatu, Range Rover na maisha ya gharama anayoishi kiongozi huyo jambo ambalo linaleta maswali juu ya namna alivyopata mali hizo kwa miaka mitano.
ROYAL TELEVISION PLUS43,403 просмотров • 2 месяцев назад

Mmoja wa viongozi na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Same Andrew Mchome amelaani kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche kutangaza kwamba ataandikia barua FIFA ili wasitishe mashindano ya AFCON nchini Tanzania kwa madai ya kuwepo kwa vikundi vilivyopanga kufanya vitendo vya kigaidi. Hatua hiyo imekuja kufuatia Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuwakamata watuhumiwa kadhaa katika maeneo mbalimbali ya nchi wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi licha ya kwamba bado vitendo vyao havijathibitishwa Mahakamani Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Julai 29, 2026 Jijini Dar es Salaam Mchome amesema kauli ya Heche ni ya kupingwa kwa sababu inachafua taswira ya nchi kimataifa, na kuongeza kuwa hakuna chama chochote cha siasa kinachopinga maendeleo ndani ya nchi yake hivyo kitendo cha Heche kujitokeza hadharani na kudai ataiandikia FIFA barua kupinga kufanyika kwa AFCON si cha kiungwana "Juzi nimemsikia akizungumza anasema kwamba tutaandika barua FiFa kuzuia mashindano ya AFCON kutokana na kuwepo kwa viashiria vya UGAIDI, kilichopo kwenye nchi yetu sasa hivi ni kwamba, Kuna watu ambao wana tuhuma ya kupanga vitendo hivyo lakini hakuna Mahakama iliyohukumu mtu kutokana na vitendo vya UGAIDI" amesema mchome Ameongeza kuwa Kauli ya Makamu mwenyekiti huyo sio ya kizalendo kwa taifa na yaweza kutia hofu wageni wanaotamani kuja kuwekeza nchini lakini pia kutembelea vivutio vya utalii. Mchome amemtaka Heche kuacha kukigombanisha chama chao na wananchi kwani anaamini kupitia mashindano hayo ya AFCON watanzania wataenda kunufaika kwa namna moja ama nyingine kupitia ugeni mkubwa utakao kuwa nchini. "Mpenda maendeleo yeyote hawezi kuwa na roho kama hiyo ya kupinga Maendeleo, ugeni utakaoingia nchini utasaidia hadi mamalishe kupata ridhiki zao, pia utafungua ukurasa mwingine kwenye sekta ya utalii" amesema mchome
ROYAL TELEVISION PLUS21,125 просмотров • 1 месяц назад

VIDEO: Watanzania wameaswa kuacha kusikiliza wanaharakati na wanasiasa wanaochochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini, kwa kuwa watu hao hawana nia njema kwa Taifa Rai hiyo imeitolewa leo, Alhamisi Juni 04. 2026, Jijini Dar es Salaam na Mwanafalsafa wa Pan-Afrika kutoka Zimbabwe, Dkt. Joshua Maponga wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu uzinduzi wa makala inayozungumzia Matukio yaliyotokea Nchini kabla na baada ya Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu), makala ambayo imeandaliwa na kampuni ya African Spear Head Media Katika maelezo yake, Dkt. Maponga amedai kuwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) yamekuwa yakipokea fedha kutoka mataifa ya nje kwa lengo la kuhamasisha vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili na amani ya nchi, ikiwemo vurugu na migawanyiko kati ya wananchi na viongozi wao, ambapo amesema hali hiyo ni hatari kwa ustawi na usalama wa Taifa, hivyo kushauri serikali kuchukua hatua za kufanya uhakiki wa mashirika hayo ili kubaini vyanzo vya fedha wanazopata na namna zinavyotumika Aidha, amedai kuwa watu wanaochochea vurugu mara nyingi huishi nje ya nchi katika mazingira mazuri, huku wananchi wanaoshiriki machafuko hayo wakikabiliwa na madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, mali, uharibifu wa makazi yao nk Sambamba na hilo ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za maandamano yasiyo ya amani na vurugu, akisisitiza kuwa matukio kama hayo yanaweza kuathiri maendeleo na rasilimali za Taifa Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa African Spear Head Media David Hundeyin amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja ya nchi muhimu kiuchumi barani Afrika kutokana na nafasi yake ya kimkakati, hususani kupitia Bandari ya Dar es Salaam inayotumiwa na mataifa mbalimbali katika shughuli za biashara na uchumi Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kulinda amani na rasilimali za nchi yao, kwani machafuko yanaweza kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi na kuathiri maendeleo ya Taifa ...“Vurugu na mauaji yaliyotokea Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu) yalikuwa na athari kubwa kwa jamii, hata hivyo bado kuna baadhi ya watu wanaoendelea kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu, wananchi wanapaswa kuwa makini na watu wa aina hiyo kwa kuwa hawana nia njema kwa Taifa lao" -Hundeyin.
ROYAL TELEVISION PLUS49,677 просмотров • 2 месяцев назад

VIDEO: Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA Prof. Lwaitama, viongozi na makada wengine wamejitokeza kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumatano Agosti 05.2026 kwaajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi inayohusu usawa kwenye mgawanyo wa mali za chama hicho iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohammed na mwenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA KESI hiyo iliyoletwa kwa mara ya pili Mahakamani hapo, inahusu usawa kwenye mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar
ROYAL TELEVISION PLUS16,109 просмотров • 23 дней назад

VIDEO: Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Mkoani Iringa Mchungaji Peter Msigwa leo, Jumatano Julai 22.2026 ni miongoni mwa wadau waliofika kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia mwenendo wa shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mkuu wa Gereza Ukonga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tundu Lissu Shauri hilo la Kikatiba lililofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma inayoketi Dar es Salaam, linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) linaloongozwa na Jaji Amir Mruma Waleta maombi katika shauri hilo waliojitambulisha kuwa ni Mawakili wa Tundu Lissu wanalalamikia kuzuiliwa na/ au kunyimwa faragha ya kuzungumza na mteja wao wanapomtembelea Gerezani
ROYAL TELEVISION PLUS23,393 просмотров • 1 месяц назад

Waziri wa mambo ya ndani Nchini Tanzania Mhe. Patrobas Katambi ameonya kuwa Vyama vya siasa visipotumika vizuri na kutekeleza wajibu wake kisheria ni tishio kubwa kwa usalama wa Nchi, hasa pale viongozi wa Vyama hivyo watakapotumia ndimi na machapisho yao kuhamasisha vurugu badala ya mapatano. Waziri Katambi ameeleza hayo leo Jumatatu Mei 25, 2026 Bungeni Mjini Dodoma wakati akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani kwa mwaka 2026/27, akisema Wizara yake itaendelea kusimamia na kukumbusha kuhusu taratibu, miongozo na sheria za Tanzania. "Vyama vya siasa visipotumika vizuri Mhe. Spika ni tishio kubwa la usalama hasa pale Viongozi wa vyama hivi watakapotumia ndimi na kauli zao, maandiko na machapisho kuhamasisha vurugu na sio mapatano, pale watakapohamasisha wananchi kwenda kufanya mambo ambayo yanapelekea uvunjifu wa amani. Mhe Spika tutazidi kukumbushana na kusimamia taratibu kwasababu Wizara ya mambo ya ndani ni kitovu cha masuala yote ya amani, usalama na nidhamu ya Taifa kwenye utekelezaji wa sheria. Tutasimamia na kukumbusha wajibu wetu kila mmoja." Amesisitiza Waziri Katambi. Amekosoa pia kuhusu baadhi ya wanasiasa kujificha kwenye mgongo wa haki za binadamu bila kutekeleza msingi wa wajibu wao, badala ya kulaumu na kukosoa serikali pale ambapo sheria zinapochukua mkondo wake, akisema wajibu wa Vyombo vya usalama ni kutafsiri sheria na kusimamia utii wa sheria Nchini
ROYAL TELEVISION PLUS48,696 просмотров • 3 месяцев назад

VIDEO: Mwanaharakati na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Martin Maranja Masese (MMM) amewashukia wale wote wanaowatuhumu viongozi na makada wa chama hicho kuwa wananufaika na kufurahia uwepo wa Mwenyekiti wao wa Taifa Tundu Lissu gerezani, akiwataka kumuachia mara moja ili kile wanachonufaikanacho mrija wake ukate Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mitandao yake binafsi ya kijamii, MMM amedai kuwa uzushi huo unaenezwa na watu aliowaita kuwa ni 'Ma-CCM' ambapo ameenda mbali kabisa na kuwataka kutekeleza kile kilichopo ndani ya uwezo wao ikiwemo kumuachia Tundu Lissu, au la wawaze namna bora ya kuendelea kukabiliana Mahakamani
ROYAL TELEVISION PLUS14,062 просмотров • 25 дней назад

VIDEO: Mvutano ndani ya CHADEMA umechukua sura mpya baada ya viongozi watatu wa chama kutoka Morogoro na Tanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, wakipinga hatua zilizochukuliwa dhidi yao walipopaza sauti kuhusiana na tuhuma za ubadhirifu wa pesa za michango ya wadau kwa chama hicho unaodaiwa kufanywa na makamu mwenyekiti wao John Heche na kudai zilikiuka Katiba na Kanuni za chama . Viongozi hao ni Barnabas Okola, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, Mathias Cosmas, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kilindi, na Joseph Mwakidasi, Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Muheza. Katika taarifa yao kwa umma ya Julai 21, 2026, wamesema hawakupewa taarifa rasmi za tuhuma zinazowakabili, hawakuitwa kusikilizwa wala kupewa nafasi ya kujitetea kabla ya maamuzi yaliyotangazwa. Wamedai kuwa hatua zilizochukuliwa dhidi yao ni batili kwa kuwa hazikufuata utaratibu uliowekwa na Katiba na Kanuni za CHADEMA, hivyo bado wao ni viongozi halali wa chama hadi taratibu za kikatiba zitakapokamilika. Kupitia barua yao, viongozi hao wameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutumia mamlaka yake kuhakikisha Katiba na Kanuni za CHADEMA zinazingatiwa, kuchunguza madai ya ukiukwaji wa taratibu za ndani ya chama na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo inaongeza orodha ya migogoro ya ndani ya CHADEMA inayofikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, huku ikitarajiwa kufungua mjadala mpya kuhusu ufuataji wa taratibu za kikatiba ndani ya chama hicho. Jitihada za kumpata Msajili wa Vyama vya Siasa ili kuzungumzia malalamiko hayo na kueleza hatua zinazoweza kuchukuliwa zinaendelea.
ROYAL TELEVISION PLUS19,172 просмотров • 1 месяц назад

VIDEO: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Handeni, kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche, akae pembeni ili kupisha uchunguzi kufuatia uwepo wa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili. Akiongea na Waandishi wa Habari mkoani Tanga leo Julai 20, 2026, Katibu wa CHADEMA Jimbo la Handeni Mjini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Kombo Mohamed Matulu, amesema “Kutokana na sintofahamu zinazoendelea ndani ya Chama chetu ni kubwa na leo tulikuwa tufanye maandamano makubwa sana yanayolenga malalamiko, Wanachama hawana majibu juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwenye Chama na Viongozi wetu wakuu wa Chama ambao ndio dira ya Chama, tulipanga kuandamana kwasababu tuhuma zipo ila hatujapata majibu hadi sasa” “Kinachonisikitisha Mh. Heche tunamtegemea kama nguzo na yeye tuhuma zote zinamuelekea, sasa kwanini asitujibu au asitupishe pembeni ili tuhuma hizi zichunguzwe, badala yake anaongea na Waandishi na kuwaita hawa Wanachama tunaowategemea anawaita Mambwa, na sisi baada ya hapa tutaitwa Mambwa, sasa hizi sio kauli za Viongozi, tunasikia sikia akina Lema ndio wameibua hizi tuhuma kwenye Kamati Kuu lakini mpaka leo hawajitokezi kusema kuhusu hilo”.
ROYAL TELEVISION PLUS19,242 просмотров • 1 месяц назад

VIDEO: Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Hamisi Said Liunde, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, kuunda tume maalumu ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche. Pia, Liunde amemtaka Heche kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanachama wa CHADEMA kwa kutumia lugha ya udhalilishaji iliyowafananisha na mbwa. Akizungumza katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Kata ya Masoko, Mjini Kilwa, Liunde amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa kitaifa kuchukua hatua za haraka ili kulinda taswira ya chama na kuondoa mashaka miongoni mwa wanachama. "Tumekuja kuongea kuhusu tuhuma za kifedha zinazomkabili Heche. Tunaomba chama kijitokeze mara moja na Heche akae pembeni kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo zote zinazoendelea," amesema Liunde. Akihoji matumizi ya lugha yaliyofanywa na Makamu Mwenyekiti huyo, Liunde ameeleza kuwa maneno hayo yameumiza hisia za wanachama, hasa jamii ya Kiislamu. "Suala la Makamu Mwenyekiti kufikia hatua ya kutuita mbwa ni udhalilishaji, hususan kwetu sisi Waislamu. Ukimuita Muislamu mbwa unakuwa umemkosea sana, kwa sababu yule ni mnyama ambaye akikugusa tu kuna taratibu ndefu za kisheria na kidini za kujisafisha ili uwe twahara tena. Heche atumie lugha ya staha, lugha aliyotumia ni ngumu mno; kiongozi anapaswa kuwa na kifua cha kuvumilia," ameongeza. Mbali na hayo, Liunde ametoa wito kwa Serikali na Rais kuweka mazingira ya maridhiano ya kisiasa ili kusaidia kuachiwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, aliye gerezani, akisisitiza kuwa maridhiano ya kweli hayawezi kukamilika ikiwa Mwenyekiti wao bado yupo ndani.
ROYAL TELEVISION PLUS16,629 просмотров • 1 месяц назад