
Shaffih Dauda
@shaffihdauda1 • 997,504 subscribers
Head of Programs at @CloudsMediaLive | Sports Analyst at CLOUDSFM Radio and CLOUDS TV | Tweets are my own
Shorts
Videos

FOOTBALL 🤝MAISHA Juzi niliandika kidogo kuhusu mpira wa miguu na tafsiri ya moja kwa moja ya maisha , kwenye video alikuwa Ahmed Ally na vijana wenye changamoto ya utindio wa Ubongo kwa pamoja walikuwa wakifanya hamasa na kaulimbiu ni #HiiTunavuka Huko nyuma Ziliwahi kuwekwa slogan nyingi sana lakini hazikuweza kuwafikisha Simba walipo leo , zilifanywa hamasa hasa lakini hazikuwafikisha walipofika leo 2024/25 ni mwaka wa bahati kwa Semaji , mapema tu mwezi August alitupa msemo wa #UbayaUbwela kwenye Pre Season imetoboa na ndio msemo bora wa kimichezo nchini consistently tangu alipoutamka , kwenye leo LeoTena ya CloudsFM alisema yeye ni mtoto wa Yombo na huo msemo ameutoa huko kitaa well Nchi imeupokea na sasa inauishi. Juzi baada ya kupoteza kwa bao 2 , akaacha Fadlu na vijana wake wafanye wanachojua mazoezini yeye akawaambia mashabiki hii haijaisha na Jumatano Tunavuka nchi nzima ikaanza kuimba #HiiTunavuka Jioni ya April 9 , Shomari Kapombe kwenye panati ya Maamuzi , Jukwaa limesimama kelele kwa mbaaaali , jukwaani Semaji amejikunja kama kinda la Ndege usoni chozi likimdondoka Oooooh Yes , Goaaaaaaal na Mnyama amefuzu Nusu Fainali 🙌 Kwenye kilele cha furaha semaji anashindwa kujizuia sura imemaliza tabasamu lote kilichokuwa karibu ni machozi tu Mwanaume amelia , kwa sababu ya mpira Ahmed amedondosha chozi , kwa sababu ya mpira kila nyumba ya mwanasimba leo ni sikukuu Kaka nakukubali 👊 unawaheshimisha wanasimba , unawafanya wauishi mpira 👊
Shaffih Dauda103,266 views • 1 year ago

AFCON 2025 | MOROCCO 🇲🇦 Nimeleta hapa video inayoonesha mzozano kati ya Osimhen na Lookman , lakini pia chanzo cha mzozano huo Kwenye video Osimhen aliamini Lookman amemnyima pasi makusudi , na wakati huo Osimhen alikuwa tayari na mabao mawili alihitaji pasi pengine afunge Hattrick Lakini Lookman pia ni kama hakuwa na nia mbaya ndio maana hapo mwisho unaona anapambana kuupeleka mpira kwa Osimhen akiwa chini . Kwa upande wako Osimhen alikuwa sawa kulalamika _____? Maana sauti ya Osimhen inasikika akimwambia. lookman tunacheza kama timu 😄 asiwe mbinafsi
Shaffih Dauda42,360 views • 5 months ago

AFCON 2025 | MOROCCO 🇲🇦 Hii Nigeria mbele yeyote atafunga tu kwa kutegemea nani yupo eneo husika kwa muda sahihi , lakini hapa nyuma hapa , kila mkate kabla ya kuliwa lazima upakwe siagi na mtaalamu Iwobi na ndio utarudi kwenye mtazamo wangu nilioutoa jana asubuhi kuwa Nigeria ni Iwobi na Ademola Lookman Sasa wewe angalia hii TRIVELA chana msamba 😄🙌wenyewe wanamuita IWOBINHO
Shaffih Dauda35,829 views • 4 months ago

Jana niliweka post yenye title CHAMBUA kutoa nafasi ya kila mmoja atoe maoni yake kuhusu Simba vs Mashujaa . Wengi wamemuhukumu Mwamuzi kwa makosa makubwa mawili 1.Kuongeza dakika 15 2.Kutoa penati 2 Hili la penati tutalielezea wakati mwingine lakini kwa sasa tubaki hapa kwenye dakika 15 za nyongeza Mimi na wewe tunapoenda uwanjani au kulipia visimbuzi lengo letu ni kutazama mchezo ( ndio burudani yetu) huu mchezo kitaratibu ni wa dakika 90 Yanapotokea matukio ya kupunguza dakika / kupoteza muda ni sawa na kwenda Bar kuuziwa mvinyo ukiwa nusu chupa kwa bei ile ile Je ni sahihi…? Jibu sio sahihi tutakubaliana hapa Tunazoziita dakika za nyongeza msingi wake sio dakika za nyongeza ni dakika za kufidia ili zikamilike 90 , kama timu imepoteza dakika 10 zikiongezwa 3 kama watu wanavyotamani maana yake mechi imechezwa dakika 83 vipi hizo 7 zimeenda wapi na sisi tumetoa kiingilio na kulipia kisimbuzi …? Ndio maana mwamuzi anafidia hapo Kuna picha hapo juu ni mechi ya Ligi ya Ujerumani unaweza kuitumia kama mfano kwenye vikao vya hapo kijiweni kuwa haya ni mambo ya kawaida duniani kote na kwenye hili Mwamuzi alikuwa sawa tu. Zipo mbinu nyingi za kupoteza muda bila kuharibu starehe , kama unaongoza jitengee eneo piga pasi hata Milioni ndio mpira ila sio kujidondosha na kulala uwanjani Namaliza kwa swali lingine kwenu, Je kwenye huo mchezo husika kulikuwa na mazingira ya kupoteza muda______? DIGALA was here
Shaffih Dauda76,640 views • 1 year ago

Kutoka Jamhuri ya watu wa TikTok wakitoa maoni yao kuelekea mwisho wa msimu 2024/25
Shaffih Dauda71,076 views • 1 year ago

Hivi karibuni kuna video imesambaa ikionesha mabomba ya sindano yaliyotumika huku na inaelezwa yamekutwa kwenye moja ya vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Azam Complex, jambo ambalo limezua mijadala mingi kwa wadau wa soka nchini. Wapo wanaodai kuwa pengine mabomba hayo yalitumika kuchoma wachezaji sindano za kuongeza nguvu kitu ambacho kinapingwa vikali kwenye michezo. Kasongo amefafanua pia kuhusu hilo na hatua ambazo wanazichukua juu ya jambo hilo.
Shaffih Dauda83,192 views • 1 year ago

Achana na sauti za content creator zitakutoa kwenye reli 😂 Binafsi mechi hii nimeiongeza kwenye orodha ya mechi ambazo Waarabu wametupunja burudani ya dakika 90 kutokana na kutumia dakika nyingi kulala uwanjani. Lakini pia mechi hii naiongeza kwenye orodha ya mechi zilizonionesha ni kwa namna gani alama moja ina thamani sana na inaweza kufanya ukatili wa kihisia kuamini nisemacho ongea na shabiki wa Yanga muda huu muulize ni kwa namna gani ameumia kwa matokeo yale. Kwenye video hii hakuna cha kujifunza hasa vitendo vya kulala uwanjani vinawapunja watazamaji burudani ya dakika 90 Zaidi tu niwapongeze MC Alger walishinda mechi kwenye saikolojia na kwa bahati mbaya Yanga wakaingia kwenye mtego wakamuongza Refa kama mpinzani wao wa pili uwanjani
Shaffih Dauda70,621 views • 1 year ago

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemtangaza rasmi Bw. Rashid Mijuza kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kumhamisha na kumpeleka Makao Makuu ya Wizara hiyo aliyekuwa Meneja wa Uwanja huo Bw. Malinde Mahona ambaye atakuwa msimamizi wa viwanja vyote nchini. Waziri Kabudi amesema hayo Mei 10, 2025 alipofanya ziara maalumu ya ukaguzi wa Kiwanja hicho na viwanja vya Mazoezi ya CHAN 2024 akiongozana na Katibu Mkuu Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa jijini Dar es salaam.
Shaffih Dauda54,077 views • 1 year ago

VIDEO 🎙️ Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi TPLB, Steven Mguto amewaomba Mashabiki wawe na subira, wasiende uwanjani kwa sasa watulie kusubiri taarifa rasmi ya Bodi ya Ligi. Clouds Sports imezungumza nae saa nne hii na ameahidi saa Tano asubuhi au zaidi taarifa rasmi itakuwa imetoka
Shaffih Dauda60,388 views • 1 year ago

Match Highlights Matukio yaliyotokea kwenye mchezo kati ya Yanga Sc dhidi ya MC Alger
Shaffih Dauda64,849 views • 1 year ago