
Swahili Times
@swahilitimes • 1,642,352 subscribers
Habari | Elimu | Burudani | [email protected] | Maoni ya wasomaji si maoni ya Swahili Times | Simu/WhatsApp/Telegram: +255 743 778 779
Videos

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itaanza safari za moja kwa moja kwenda Moscow kuanzia Julai 2026. Aidha, amesema shirika la Azur Air linatarajiwa kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Moscow kwenda Zanzibar, hatua inayotarajiwa kuimarisha zaidi biashara na sekta ya utalii kati ya nchi hizo mbili.
Swahili Times17,964 Aufrufe • vor 3 Tagen

Rais Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kwa kutambua uongozi wake, mageuzi katika sekta ya elimu, juhudi zake za kuimarisha diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa.
Swahili Times22,867 Aufrufe • vor 4 Tagen

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa kwa mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambaye amekuwa akipinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya TZS milioni 500 ikiwemo kutajwa kwa majina yao hadharani, jambo ambalo amesema linaashiria kuwepo kwa mtandao unaolenga kuwalinda wahusika.
Swahili Times18,559 Aufrufe • vor 8 Tagen

Rais Samia Suluhu Hassan amemzawadia gari mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni ombi la mama huyo kwa Rais baada ya kueleza changamoto ya usafiri inayomkabili. Aidha, zawadi hiyo imetolewa kwa kuthamini mchango wa marehemu Kanumba katika kukuza tasnia ya filamu nchini.
Swahili Times78,540 Aufrufe • vor 3 Monaten

"Sisi kama familia, kwa niaba yake [William Lukuvi] tunaomba msamaha na upatanisho kwa wale wote ambao amewahi kuwakosea katika harakati zake za kisiasa na maisha yake kwa ujumla, na wale wote ambao pengine waliwahi kumkosea, sisi kama familia tunawasamehe kwa niaba yake." - Mosi Lukuvi, mdogo wa marehemu William Lukuvi
Swahili Times60,496 Aufrufe • vor 2 Monaten