#bajetiyawakulima

Salaam Ndugu Zangu. #BajetiYaWakulima IMEPITA ✅ Awali ya wote nichukue fursa hii kuwashukuru Viongozi wenzangu na Menejimenti na Taasisi mbali mbali za Wizara ya Kilimo kwa kufanikisha kwa uweledi na umahiri mkubwa uwasilishaji wa hoja ya Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Maonyesho ya ‘From Farm To Lab’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Dodoma. Niwashukuru wadau wote walioitikia wito wa kuhudhuria na kuwa na sisi kwenye Bajeti hii ya Kihistoria ya Wizara ya Kilimo. Pamoja na Vipaumbele vyetu 6 tunajivunia kuwa #BajetiYaWakulima imejikita kwenye mabadiliko yatakayoleta tija kwenye 1)Korosho 2)Sukari 3)Tumbaku na 4) Kahawa reforms Shukrani za dhati ziende kwa Waheshimiwa Wabunge wenzagu kwa kuwa na imani na Wizara na kazi zake kwa mara nyingine, tunashukuru mapendekezo na ushauri wote tuliopokea na tunaahidi kufanyia kazi kwenye utekelezaji. Tunawasihi msichoke kutufikishia mawazo yenu pale mnapoona tunaweza kuboresha utekelezaji wa bajeti hii na mipango yake. Kwa nafasi ya kipekee Nimshukuru Dkt Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza kwenye Sekta Ya Kilimo. Hii imani uliyotupa, hakika hatutokuangusha. Tunaahidi kusimamia utekelezaji kwa umahiri na uzalendo ili kuleta tija kwenye maendeleo ya Taifa hili na kufanikisha maono mapana ya Maendeleo na Mapinduzi kwenye Sekta ya Kilimo. Taifa Letu, Kesho Yetu. Kazi Iendelee
Hussein M Bashe16,913 Aufrufe • vor 2 Jahren

Here we go. BBT component 2- BBT Financing ☑️ tunaendelea #BajetiYaWakulima
Hussein M Bashe15,382 Aufrufe • vor 2 Jahren
Keine weiteren Inhalte verfügbar