Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

82,895 views • 4 months ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

. Wizara ya Afya Tanzania 🇹🇿 na NBTS TANZANIA Mama mjamzito amejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala – Amana Regional Referral Hospital. Anapatikana katika wodi No. 09, ambapo katika kipindi hicho cha kujifungua aliongezewa damu chupa 12. Familia ya mama mjamzito, imelipa gharama stahiki za huduma ya kujifungua, baadae wakaletewa gharama ya mzazi huyo kuwekewa damu ambayo wamepewa risiti ya malipo ya damu. Pia, wamelipa malipo yote. Mama aliyejifungua amekuwa discharged (ameruhusiwa kutoka hospitalini), lakini amenyimwa ruhusa ya kuondoka hospitalini hadi alete watu 12 wa kuchangia damu (replacement donation) iliyotumika. Maagizo hayo ya kumzuia mama aliyejifungua yametolewa na Muuguzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala (Amana Regional Referral Hospital), ambaye anapatikana chumba Na. 15 katika hospitali hiyo Je, utaratibu huo ni sahihi kisheria? Kwanini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ilala inautumia kama sharti la kumzuia (dention) mgonjwa? Je, kumzuia mgonjwa kuondoka baada ya kuruhusiwa siyo false imprisonment? Kisheria, chini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja na Wizara ya Afya, hospitali hairuhusiwi kumshikilia mgonjwa aliyesharuhusiwa kuondoka (discharged) kwa sababu tu hajapata wachangiaji wa damu wa hiari. Sera hii ililetwa kwa sababu ya tatizo la kihistoria katika hospitali nyingi ambapo wagonjwa au familia zao waliambiwa wapeleke “wachangiaji damu” kabla mgonjwa hajaruhusiwa kuondoka hospitalini. Sera inaweka msimamo: Damu inayochangiwa ni ya hiari na bure. Wagonjwa hawapaswi kulazimishwa kulipa au kuleta wachangiaji kama sharti la kupata huduma ya damu. Hairuhusiwi kuuza au kununua damu. Gharama inayolipwa hospitalini ni vifaa vya maabara, vipimo vya usalama wa damu, uhifadhi wa damu, na huduma ya kuongezewa damu, lakini siyo malipo ya damu yenyewe. Wagonjwa wasibebeshwe mzigo. Kwamba wagonjwa wanatakiwa kuleta wachangiaji wa damu (replacement donors) ndiyo waruhusiwe kuondoka wodini? Je, wakikosekana hao replacement donors? Mgonjwa atashikiliwa kwa muda gani hospitali?

Martin Maranja Masese

39,829 views • 3 months ago