Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

Mayai kwa afya ya akili!

71,323 views • 1 year ago •via X (Twitter)

11 Comments

Silent Whisper's profile picture
Silent Whisper1 year ago

Usije ukakanyaga juu ya mayai ukadhani jukwaa la sisiemu....

公式:ちぃたん☆広島's profile picture
公式:ちぃたん☆広島2 years ago

I'm Chiitan Japanese crazy mascot☺️Chiitan loves death metal💀💕

Alfred Tarimo's profile picture
Alfred Tarimo1 year ago

Mbona wewe huonekani kama unayatumia sasa🤣🤣. Sijasema huna akili

Cactus KIlindu🌵's profile picture
Cactus KIlindu🌵1 year ago

Nnacho kukubali unauheshimu uongozi wa lisuu Safi Sana pastor

𝑴𝒂𝒌𝒂𝒗𝒆𝒍𝒊 's profile picture
𝑴𝒂𝒌𝒂𝒗𝒆𝒍𝒊 1 year ago

Juzi nilikuona Benjamini pale umeweka wa mbuzi balaa nikaona noma kuja kukusalimia bwana😂

Nyasbo 5G's profile picture
Nyasbo 5G1 year ago

Boni Yai Kawafumbua Watu Wengi Sasa Kuhusu Kufuga Kuku Wa Mayai!😂Hivi Mna Uhakika Gani Kwamba Mayai Ndo Yamejanga Ghorofa Lake?😂😂

KITASA🔑🧥's profile picture
KITASA🔑🧥1 year ago

Huyo jamaa ana ujasiri sana kupiga mlege mbele ya mchungaji😂😂

Mwl.Keberenge wa nyasaricho's profile picture
Mwl.Keberenge wa nyasaricho1 year ago

Siasa hailipi . Hongera kwa mradi mzuri sana . Serikali ya CCM ingewapa vijana mitaji wakawekeze kwenye ufugaji badala ya kununua MV8

Elon Michael's profile picture
Elon Michael1 year ago

Unauza mayai lakini mbona wewe hakusaidii akili,,, maana siku zinapo zidi kusonga unaonyesha dalili za wazi kuwa afya yako ya akili haipo sawa

Donald Maziku's profile picture
Donald Maziku1 year ago

Hiyo inaweza kuwa na maana kuliko kujaribu kuipamba ccm na bi kizimkazi

Lucas E. Malembo's profile picture
Lucas E. Malembo1 year ago

Hongera sana #KilimoNiAjira

Related Videos

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Jijini Dodoma imesema zipo tabia nyingi kwenye Jamii ambazo Watu huzifanya zinazoashiria wana changamoto ya afya akili au magonjwa ya akili ikiwemo ku-bet, kunywa pombe na kutumia simu kupita kiasi, kutoridhika na kukosoa kila kitu, kuona kila Mtu ni mbaya na hakupendi, kutukana na kucomment vibaya mitandaoni, kuogopa kupanda ndege, lift n.k ambapo imesema Mtu akijiona na viashiria hivi anapaswa kuwahi Mirembe ili apewe ushauri au dawa badala ya kusubiri hadi apelekwe akiwa amefungwa kamba. Akiongea na AyoTV , Mtaalamu Bingwa wa Saikolojia na Afya ya Akili amesema “Kuhusu ku-bet Watu wanataka kuongeza kipato lakini Wataalamu wa Afya ya Akili tunajiuliza iweje Mtu afikirie maisha yake anaweza kumudu kwa kubahatisha?, Mtu huyu tunaanza kutilia mashaka akili yake, Mtu anachukua hela ya ada, mshahara wake wote kwenda kubet, kubobea kwenye ku-bet ni uraibu (addiction) na hawa pia tunawahudumia kama Warahibu wa dawa za kulevya” “Pombe kupita kiasi ni tatizo mpaka Mtu akikosa pombe anatetemeka, Mtu kupata furaha kupita kiasi na akiwa na hela ananunua hata asivyohitaji na kutoa ofa kwelikweli ni tatizo, kuna Mtu kila Mtu ni mbaya anaona kila Mtu hampendi ofisini hadi nyumbani, una haja ya kuchunguzwa” “Magonjwa ya akili yanazidi 300, kuna magonjwa ya wasiwasi ikiwemo Mtu ghafla anapata mshtuko moyo, kuogopa kusimama mbele za Watu kuzungumza, kuna Watu wanaogopa kupanda lift au kukaa vibaraza vya maghorofa pekee yao, uoga kupanda ndege, Mtu akipoteza hali ya kupenda vitu alivyokuwa akivipenda siku za nyuma mfano outing na ghafla anajitenga au kujiona hana thamani na hata kufikiria bora kufa, huu ni ugonjwa wa akili” “Mtu anapojiona ana changamoto ni vizuri akaja Mirembe kuliko kufikiria wewe ni mzima ukabaki Mtaani halafu ukaletwa siku umefungwa kamba, kuhusu ubalozi tunatumia Watu wenye ushawishi kama Mh. Jokate ambao afya zao za akili zipo vizuri ili watusaidie kupeleka elimu kwenye Jamii kwahiyo sio kweli Mtu tunayemtumia akawa ana tatizo na hata walio-comment vibaya kuhusu ubalozi wa Mh.Jokate nao wanafaa kuchunguzwa afya yao ya akili, lindeni afya zenu za akili” #MillardAyoAUPDATES

millardayo

41,510 views • 2 years ago

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu ameishauri Serikali kuanzisha mfumo wa kuchangia Bima ya Afya kwa wote kupitia miamala ya simu, ambapo kila Mtanzania angechangia kiasi kidogo cha fedha katika kila muamala anaoufanya. Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/27, May 11, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, Kingu amesema Tanzania ina idadi kubwa ya miamala ya simu inayoweza kutumika kama chanzo cha uhakika cha kugharamia huduma za afya bila kuongeza mzigo mkubwa kwa Wananchi. “Nimefanya statistics kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kusoma ripoti za Benki Kuu ya Tanzania, Tanzania kwa mwaka mmoja inarekodi miamala bilioni 6.3 kwa Watu wanaofanya miamala kwenye mitandao ya simu na miamala mingine, Mchengerwa mnasubiri nini kuja na platform kwenye hii Nchi, sio mkalete tozo mpya zitakazowapa Watanzania mzigo, mimi nawapa mawazo, njooni na ‘coding system’ ambayo itatumia teknolojia ya kisasa Watanzania wako tayari kuchangia Bima ya Afya kwa wote, wanachosubiri ni kupewa mwelekeo,” amesema Elibariki Kingu. Aidha amesisitiza kuwa hata mchango mdogo wa shilingi 10 au 30 kwa kila muamala unaweza kusaidia Serikali kukusanya fedha nyingi zitakazowezesha Wananchi kupata huduma bora za afya bila kuambiwa kwenda kununua dawa nje ya Hospitali. “Kwa hesabu hizi mnaweza mkakusanya trilioni nne mkafadhili Bima ya Afya kwa wote Watanzania wakienda Hospitali wasiambiwe dawa nenda kanunue kwa Mtu fulani,” amesema Elibariki Kingu. #MillardAyoUPDATES

millardayo

27,442 views • 3 months ago