Loading video...

Video Failed to Load

Go Home

Reflection on Oct 29 protests When security forces started shooting protestors it infuriated the youth to the extent that they attacked and burnt police stations and CCM offices starting late afternoon Oct 28 and Oct 30 onward! Let us be clear that the aggression started from the State by...

28,412 views • 4 months ago •via X (Twitter)

0 Comments

No comments available

Comments from the original post will appear here

Related Videos

Askofu wa Kanisa la Matendo Makuu ya Mungu nchini Tanzania kutoka Ushirika wa Wachungaji wa Kipentekoste, Askofu Pius Ikongo, amesema Kanisa Katoliki nchini Tanzania chini ya Baraza la Maaskofu TEC, wanahusika na uratibu na ufadhili wa ghasia na uvunjifu wa amani uliojitokeza wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025. Askofu Ikongo amebainisha hayo alipozungumza na Watanzania kupitia Vyombo vya habari Mkoani Kilimanjaro siku chache baada ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki kutoa waraka wao, waraka ambao Baba Askofu Ikongo anasema umedhihirisha mahusiano ya TEC na uvunjifu huo wa amani wanaouita maandamano. "Mnayaita maandamano lakini sisi hatutambui kama yalikuwa maandamano na nyie mmehusika kuratibu na kusimama yaliyotokea Oktoba 29, kwa asilimia 90 na kumi iliyobaki ni ya wanasiasa wakiwemo wa Chadema na Waraka wenu unathibitisha wazi kuwa kilichofanyika Oktoba 29 kilikuwa ni maelekezi yenu ninyi Maaskofu 41." Amesisitiza Askofu Ikongo. Aidha katika msisitizo wake, Baba Askofu Ikongo ameitaka TEC kuliomba radhi Taifa la Tanzania, akisema anaamini kuwa Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla watawasamehe Maaskofu hao, akisema Mungu ameshafichua maovu yao na hivyo ni muhimu kuomba radhi. "Tumeshajua adui yetu ni ninyi TEC, Mmeratibu vurugu hizi kwa njia nyingi na mmekiri na kudanganya umma kuwa yale yalikuwa maandamano na zipo taarifa kuwa wapo Vijana kutoka nje ya nchi waliokuwa wamefichwa kwenye majengo yenu." Amesema Askofu huyo. Katika hatua nyingine, ameitaka TEC kuwaeleza Watanzania ikiwa kwenye yaliyotokea yalikuwa maandamano, akiwataka wale wote wenye ushahidi wa Video za maandamano kuzitoa hadharani, nje ya Video na picha mnato za uhalifu, wizi na uharibifu wa mali za umma na za watu binafsi ikiwemo magari na vitega uchumi.

ROYAL TELEVISION

60,485 views • 7 months ago

Katika orodha ya watu wote waliokamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za makosa ya uhaini na makosa mengine kutokana na maandamano ya 29/10/25 hakuna raia wa kigeni hata mmoja katika hati ya mashtaka Hii dhana kwamba walioandamana walikuwa wageni inatoka wapi? Wageni gani ambao wamekamatwa na kushatakiwa kwa mambo ambayo yanatokana na maandamano yaliyofanyika tarehe 29/10/25? Kwamba walioshiriki maandano hawakuwa wanazungumza kiswahili. Hao waliokamatwa na kushtakiwa wote wanazungumza kiswahili. Hao wasioweza kuzungumza kiswahili wapo wapi? Je, waandamanaji hao ambao hawazungumzi kiswahili ni kati ya hawa waliokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini au wale waliouwawa kwa kupigwa risasi na wengine miili yao haijulikani ilipo hadi sasa? Kwamba waandamanaji walikuwa na silaha za moto? Kwamba waandamanaji wameuana wenyewe kwa wenyewe? Hii mnataka kumdanganya nani? Washirika na wadau wa maendeleo kutoka nje au Watanzania? Katika waandamanaji waliokamatwa na kushtakiwa katika mahakama mbalimbali hakuna hata mmoja amekamatwa na bunduki. Hizo silaha za moto walizokuwa nazo ninyi mmezitunza wapi sasa? Bila kujua, mnalidogodesha Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao tangu siku ya kwanza ya maandamano askari wake walikuwa barabarani. Kwamba wakiwa barabarani walishindwa kudhibiti watu wenye silaha za kivita? Mnataka kusema kwamba, hao watu waliokuwa na silaha za moto walikuwa wanavuka vizuizi vya JWTZ wakiwa na silaha hata baada ya kutangazwa amri ya kutokutoka ndani? Hivi mnajisikiliza kweli? Unasema hakukuwa na maandamano kwa kuwa waandamanaji walikuwa na silaha za kivita. Halafu unasema wengine wamepoteza maisha bila kushiriki. Kwanini mmewaua ambao hawakuwa na silaha? Hata hivyo, mnajaribu kutuonesha wananchi kwamba mipaka ya nchi yetu haipo salama hadi kuruhusu watu kutoka nchi jirani kuvuka na kuingia na silaha za moto? Idara ya uhamiaji ivunjwe na kufutwa mara moja. Kwamba watu hao waliingia nchini wakiwa na silaha za moto na kusababisha madhara kwa binadamu, walitumia mipaka na Airports? Serikali ipo? Intelejensia yenu ya kuzuia mikutano ya kisiasa mliuza wapi? Kujaribu kutupa hizi lawama kwa majirani ni kutafuta mgogoro wa kidiplomasia usiokuwa na lazima. Lipo tatizo, litatuliwe. Wasikilizeni wananchi, hususani kundi hilo la vijana. Msiendelee kukaa kwenye denial.

Martin Maranja Masese

46,467 views • 6 months ago